125. PAULO AKIWA KATIKA MJI WA RUMI
“Kwa maana nimefungwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli”
Shabaha
Kuonyesha namna Mtume Paulo alivyoendelea kuhubiri Kweli, bila kujali matatizo aliyokabiriwa nayo. Safari ile ndefu na yenye hatari kuelekea Rumi ilikuwa imemalizika na Paulo sasa alikuwa ameingia katik mji Mungu na ashukuriwe kwa ajili ya wenzake ndugu na dada waliokwenda kukutana naye na kumtia moyo. Sasa alikuwa apewa nafasi ya ajabu ya kuhubiri Injili katika mji mkuu wa Dola ya Rumi. Ingawa alikuwa mfungwa katika minyororo lakini alifahamu kuwa mateso zaidi yanamsubiri, hata hivyo alikuwa na furaha kwa kuwa yeye alikuwa ni “chombo kiteule” kupeleka Injili kwa watu wengi. Askari aliyekuwa kiongozi wa kuwapeleka wafungwa katika safari ya Rumi, aliwakabidhi kwa mkuu wa walinzi. Wafungwa wale wangine waliwekwa gerazani, lakini Paulo alipewa heshima kubwa kwa aliruhusu kuishi katika nyumba yake mwenyewe ya kupanga. Na askari aliteuliewa kumlinda (mstari 16) na bila shaka alikuwa bado amefungwa mnyororo ili kuhakikisha asitoroke.
Matendo ya Mitume 28: 16 – 31
PAULO ANAHUBIRI INJILI KATIKA RUMI (mstari 16 – 31)
Ingawaje Paulo mwenyewe alikuwa mfungwa, lakini hata hivyo Kweli bado ilihubiriwa. Kama Paulo. asingepeleka Injili kwa Wayahudi, basi angewaalika Wayahudi hao waende nyumbani kwake, ili waisikie Kweli. Siku tatu baada ya yeye kufika Rumi aliwaita Wakuu wa Wayahudi nyumbani kwake na akawaeleza ni kwa nini alikuwa mfungwa katika Rumi. Alieleze kwamba “kwa maana nimefungwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli” (mstari 20). Wayahaudi wakamwambia Paulo kwamba hawakuwa wamesikia tuhuma zozote zilizomhusu yeye. Wakamwambia kuwa wangependa kwenda kusikia kwa nini alikuwa amefungwa na Wayahudi. Siku ilipangwa na watu wengi tena walikusanyika kumsikiliza Paulo. Akajadiliana nao “tangu asubuhi hata jioni” akawaeleza kwa kutumia Maandiko ya Agano la kale (sheria ya Musa na Manabii) akazielezea ahadi nzuri sana kuhusiana na kuja kwa Ufalme wa Mungu na kuonyesha kwamba wokovu ungeweza kupatikana kupitia imani katika Yesu Kristo tu (mstari 23). Baadhi yao waliamini mambo ambayo Paulo aliyasema na wengine waliyaziba masikio yao na kuifanya mioyo yao kuwa migumu. Na pale alipoelewa wazi wazi kwamba baadhi yao hawakuta kumsikiliza akatamka kwamba Isaya alikuwa ametabiri vyema juu ya watu kama hao ambao hawangeelewa mmbo yaliyomhusu Yesu (mstari 25 – 27); linganisha na Isaya 6: 9 – 10). Kwa vile Wayahudi wengi wasingeamini angewageukia watu wa Mataifa, ili wasikie habari njema ya wokovu. Akawageukia Wayahudi wenye moyo mgumu na kusema, “Basi, ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia” (mstari 28). Paulo alikaa Rumi kwa miaka miwili akahubiri “habari njema” za kuja kwa Ufamle wa Mungu na mambo yaliyohusu Bwana Yesu Kristo. Akasema kwa kadiri ya wingi wao kama walivyokuwa wanakuja kumsikia “kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu” (mstari 31).
FUNDISHO KWETU
Maisha ya Paulo yalikuwa ni maisha ya mwanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo. Katika mazingira yaliyosababisha wengine waogope na kutetemeka, yeye alikuwa imara na mtulivu - na ulipofika wakati wa kutenda mapenzi ya Mungu, hakusita kwa kuogopa. Katika mambo yote, alifahamu kwamba mateso huwafundisha watu kumtegemea Mungu. Kumbuka alivyosema. “Imetupasa kupita katika mateso mengi ili tuingie katika Ufalme wa Mungu”. Huenda hatutaweza kufanya sawasawa na Paulo, Mtume mkubwa kwa Mataifa, “chombo kiteule’’ cha Bwana, lakini tutapata msaada kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kufanya mapenzi yake, iwapo kama Paulo, tutabaki imara katika Kweli na kila wakati tupende Mungu atuongoze katika maisha yetu.
MAELEZO YA ZIADA
Ingawaje tumefika mwisho wa Kitabu cha Matendo ya Mitume,lakini kazi ya Paulo haikuishia hapa. Aliendelea kuhubiri na kuandika barua ili kuwaimarisha na kuwasihi waumini walioishi katika miji mbalimbali ya Dola ya Rumi. Kwa mfano, aliandika waraka kwa eklesia ya Wafilipi na kwa Wakolosai. Na kwa nyongeza, Mtume huyu aliendelea kuhubiri kwa wote waliopenda kumsikiliza. Paulo aliwahubiri watumishi wa nyumbani mwa Kaisaria na wakaongoka (Wafilipi 4:22). Alikuwa na kundi la marafiki watu waliokuwa watawala amabao mara nyingi walikuwa naye. Walishirikiana naye katika tumaini tukufu na kumsaidia Paulo kwa kadri alivyotoa msaada na ushauri kwa wote walimjia. Hatimaye Paulo aliachiliwa huru kutoka Rumi. Akaendelea kuhubiri kila mahali katika Dola ya Rumi. Mwisho watawala wakamweka kifungoni tena huko Rumi. Safari hii hakuachiliwa. Na katika baadhi ya maneno yake ya mwisho aliandika akimwambia rafiki yake mwaminifu Timotheo, “kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika”. Kwa hili alimaanisha kwamba angekufa upesi kwa ajili ya mambo aliyoyaamini. Lakini hata hivyo hakuhuzunika, kwa kuwa aliendelea kusema, “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hapo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake” (2 Timotheo 4:6-8). Paulo alifahamu kwamba atapata Taji ya uzima, yaani uzima wa milele, wakati Yesu Kristo atakaparudi. Tufuate mfano wa Paulo, tukitazamia kurudi kwa Kristo na tukiwa tumejiweka tayari kukutana naye. Tumbuke alivyowahi kusema kwa waumini wa Korintho, “mnifuate mimi, kama na mimi ninavyomfuata Kristo” (1 Wakorintho 11:1).
MASWALI
Majibu Mafupi
- Paulo alikaa wapi alipofika Rumi?
- Ni nani aliozumgumza nao kwanza Injili mara tu alipofika?
- Ni lipi “Lile tumaini” alilokuwa akiwaambia?
- Je, ni kila mmoja aliyesikia Injili alimwamini Paulo?
- Ni nani aliowasema Paulo kuwa wangefurahi kuisikia Injili?
- Paulo alijifunza nini kutokana na mateso yake?
Majibu ya Kina
- a) Eleza Mtume Paulo alikuwa anafanya nini katika Rumi kwa maika miwili?
b) Ni watu wa aina gani walikuja kumsikia?
Majibu ya Nyongeza
- a) Jambo gani jingine ambalo Paulo alilitenda alipokuwa mfungwa huko Rumi?
b) Katika waraka wake wa pili kwa Timotheo, alisema kuwa alikuwa akitarajia nini?
|