CSSA 2-1-09 - THE HOPE OF THE PROMISES MADE UNTO THE FATHERS

Swahili

134. TUMAINI LA AHADI WALIZOPEWA MABABA
Tumejifunza maelezo ya historia ya maisha ya Ibrahimu. Na sasa tutaangalia mafundisho kutokana na ahadi kubwa na za thamani alizopewa mtu huyu mkubwa mwenye imani, na akapewa Isaka na Yakobo.

Kusudi la somo hili ni kuona umhimu wa ahadi hii kwa Ibrahimu ikiwa ni ya pili kati ya maagano matatu ambayo katika haya ndiyo msingi wa makusudi ya Mungu. Agano la kwanza lilifanyika katika bustani ya Edeni ambapo ahadi ilitolewa ya uzao wa mwanamke ambaye atashinda dhambi na kifo (Mwanzo 3:15).

Agano la tatu baadaye Mungu alilifanya na Mfalme Daudi kuhusu uzao ule ule ambaye atakuwa Mwana wa Daudi na Mwana wa Mungu ambaye atatawala akiwa mfalme katika kiti cha enzi cha Daudi milele katika dunia yote (2Samweli 7:12-16; Luka 1:30-35)

Mwanzo 12:1-3; 7; 13:14-17; 15:8-21; 22:16-18; Wagalatia 3

UMUHIMU WA AHADI KWA IBRAHIMU
Ibrahimu ametamkwa, mara sabini katika Agano Jipya peke yake, mara nyingi kwa sababu ya imani yake na uthabiti wake kwa ahadi za Mungu. Yeye ni mfano wetu mzuri wa kufuata (angalia maelezo ya Paulo katika Warumi 4).Na zaidi hasa Paulo alifundisha ya kwamba INJILI ilihubiriwa kwanza kwa Ibrahimu katika ahadi hizo muhimu ambazo Mungu alimwahidi yeye yapata miaka elfu mbili kabla ya Kristo kuzaliwa. ?Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu INJILI zamani,kusema?katika wewe Mataifa yote yatabarikiwa? (Wagalatia 3:8). Neno Injili lina maana ya ?Habari Njema? na kwa kweli kusudi la Mungu la kuyabariki Mataifa yote kupitia kwa Ibrahimu ni habari njema hakika.

Mtume Paulo pia alionyesha ya kwamba ahadi kwa Ibrahimu zilimnena yeye ambaye ni uzao mmoja maalumu, ambaye ni Bwana Yesu Kristo ndiye atatimiza ahadi hizo (Wagalatia 3:16; Warumi 15:8). Hapa tena kuna ahadi zinazosema kuhusu Ufalme na urithi wa milele wa nchi ya Israeli unaothibitishwa na ufufuo wa Kristo.

Tumaini hili linashikiliwa na watu wote ambao watakuwa ''wana'' wenye imani ya Ibrahimu. Ahadi hizi zitakapotimia, mataifa yote yatabarikiwa.

Huo ndio msingi wa ?Injili? na ni tofauti iliyo wazi kutokana na kosa la kanisa linalodhani ya kwamba roho zinaenda mbinguni baada ya kufa. Inahuzunisha kuwa hawaelewi ?tumaini? hili la Injili linalofundisha kwamba Ufalme wa Mungu utakuwa duniani.

MAELEZO YA KINA YA AHADI
Ibrahimu alikuwa ni ?mgeni na mpitaji katika nchi?, akitarajia siku zitakazokuja wakati uzao wa ahadi, Bwana Yesu Kristo atakaposimikwa kuwa mtawala juu ya ufalme wa Mungu. Ibrahimu aliamini ya kwamba hata kama yeye na wanawe wangekufa, Mungu angewafufua kutoka kwa wafu na kumwona Kristo katika Ufalme wake. Watairithi nchi waliyoahidiwa (Waebrania. 11:39,40; Matendo ya Mitume 7:1-3). Hakuwazia kwamba vitu vingi alivyokuwanavyo kuwa vilikuwa vyenye thamani sana ukilinganisha na ahadi ya kuimiliki nchi katika Ufalme wa Mungu. Wala hakukatishwa tamaa hata kama ingechukua muda mrefu kutimizwa kwa ahadi za Mungu kwa Ibrahimu na Sara.

Katika kila hatua ufafanuzi wa kina zaidi na zaidi ulionekana hadi picha kamili ilipofunuliwa. Na sasa tulitazamie kusudi la jumla la ahadi alizopewa Ibrahimu na tutaona Mungu alikusudia nini:-

Mwanzo 12:1-3 - Pale URU na HARANI ahadi ya kwanza na wito ulitolewa:-
    1. Abramu aliahidiwa kwamba atakuwa taifa kubwa na kuwa jina lake litakuwa kuu.
    2. Mungu atawabariki wanaombariki Abramu, na angewalaani wanaomlaani;
    3. Mungu alimwahidi kwamba katika yeye mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.

Mwanzo 12:7 ? pale SHEKEMU, baada ya Abramu kuvuka mto Frati akiiacha nchi ya kwao na nyumba ya baba yake, Mungu alimwahidi ?uzao? na ?nchi?.

    4. Mungu alimwahidi Abramu ?uzao? ambaye angeiriithi nchi ya Kanaani.

Mwanzo 13:14-17 ? Pale BETHELI baada ya Lutu kuondoka na kwenda Sodoma, Mungu alimwahidi kuwa uzao wa Abramu watakuwa wengi ambao wataimiliki nchi milele. Hapa kuna kielelezo cha kwanza cha ufufuo.

    5. Abramu na ?uzao? wake wangeirithi milele nchi ambayo alitembea ndani yake
    6. Anaambiwa kwa mara ya kwanza kwamba uzao wake watakuwa wengi, hawatahesabika.

Mwanzo 15- Ingawaje hakuwa na mtoto, Abramu aliamini ahadi ya Mungu ya kusanyiko kubwa sana la uzao wake alipokuwa huko HEBRONI

    7. Mungu akafanya Agano na Abramu;
    8. Abramu aliambiwa mipaka ya nchi aliyoahidiwa.

Mwanzo 22: 16-18 ? Alipokuwa amejitayarisha kumtoa Isaka kuwa sadaka kwa ajili ya kutii amri ya Mungu, Ibrahimu alipewa thawabu ya ahadi kubwa ambayo ilithibishwa kwa mhuri wa kiapo cha Mungu

    9. Uzao wa Ibrahimu unajumuisha pamoja na uzao ambaye ataimiki milango ya adui zake maana yake atawashinda maadui zake
    10. Na katika uzao wake mataifa yote watajibarikia;
    11. Ahadi ilithibitishwa kwa kiapo, ?Nimeapa kwa nafsi yangu?.

UFAFANUZI KUHUSU AHADI
    1. Umoja wa uzao wa Ibrahimu (umoja = mmoja).
Bwana Yesu Kristo ndiye kiini katika ahadi ya uzao aliyeahidiwa kwa Ibrahimu. Ni yeye ambaye baraka zitakuja kupitia kwake. (Mathayo. 1:1; Wagalatia 3:16). Ibrahimu aliahidiwa ya kwamba yule ambaye ?atamiliki lango la adui zake? ndiye atakaye yabariki ?mataifa yote ya dunia?. Kwa hili ili liwezekane ni lazima Mungu ayaweke mataifa yote chini ya utawala wa Kristo. Yesu Kristo atatawala mataifa yote (1 Wakorintho15:25; Danieli 2:44). Yesu Kristo mwenyewe anatueleza sisi kwamba Ibrahimu aliamini katika yale ambayo Kristo angeyatenda aliposema, ?Ibrahimu, baba yenu alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu;naye akaiona, akafurahi? (Yohana 8:56).

    2. Wingi wa uzao wa Ibrahimu (wingi= zaidi ya mmoja).
Vifungu vingi husema kuhusu uzao wa Ibrahimu mwingi usioweza kuhesabika ukiwa uliobarikiwa. Uzao huu ulitoka kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Lakini ili mtu ahesabiwe kuwa wa uzao wa Ibrahimu siyo lazima awe Myahudi kwa kuzaliwa.Siyo wale waliozaliwa na Ibrahimu kwa jinsi ya mwili wanaohesabika. Bali wana wa Ibrahimu ni watu wale wanaoishiriki imani ya Ibrahimu (Yohana 8:33-40; Warumi 9:6-13). Kwamba imani na utiifu ndiyo vinajulikana kuwa ?familia moja? (Wagalatia 3:7-9). Ambaye ni Mkuu kuliko wote katika ?familia? ni Bwana Yesu Kristo.

Paulo anaonyesha ya kwamba kama tunaiamini Injili na kubatizwa, tunakuwa tumebatizwa ?katika Kristo? na pia tunahesabiwa kuwa ?uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ahadi? (Wagalatia 3:27-29). Hapa ndipo tunapo jumulishwa katika uzao wa Ibrahimu, ambao wataurithi Ufalme wa Mungu milele (Ufunuo 5:9-10); Mathayo. 5:5; Warumi 4:13-14). Sehemu mojawapo muhimu sana ya ahadi ile inayohusika kwetu, ni ile ahadi ya kwamba dhambi zetu zinaweza kusamehewa kwa njia ya ubatizo (Matendo ya Mitume 3:25-26). Hiyo ni baraka ya moja kwa moja kutokana na ahadi za Mungu kwa Ibrahimu kwa wale wanaofanyika ?wana kwa njia ya imani? na wanaoenenda kwa imani kama ?baba? yao Ibrahimu.

    3. Urithi ni kwa Njia ya Ufufuo;
Ibrahimu atakuwa alivutiwa sana ajabu kwa ajili ya kuhitaji ufufuo iwapo yeye na uzao wake walikuwa warithi wa nchi/au milele. Wao, kama sisi, walikuwa wanaume na wanawake wenye damu na nyama waliokabiliwa na kifo na kaburi. Ili Neno la Mungu liweze kutimia, Ibrahimu na uzao wake ni lazima wafufuke kutoka kwa wafu. Ibrahimu bado hajaingia katika urithi wake (Matendo ya Mitume 7:5). Tunajuaje kwamba watafufuliwa na kisha watapokea urithi wao? Uthibitisho umo ndani ya ufufuo binafsi wa Uzao, Bwana Yesu Kristo. Ufufuo wake ndiyo uthibitisho ya kwamba atarudi,na ya kuwa atafufua wafu na ya kwamba atawapa thawabu wenye haki (Matendo ya Mitume 17:31; 2 Timotheo 4:1,8).Kufufuka kwake yeye mwenyewe kunahakikisha kutimia kwa mambo yote katika ahadi za Ibrahimu (Warumi 15.8).

    4. Ahadi ilithibitishwa kwa kiapo cha Mungu
Mungu alimwonyesha Ibrahimu kwa njia ya fumbo kuhusu ahadi ya kuzidishwa kwa uzao kuwa itakuwa kweli. Akafanya agano na Ibrahimu kwa kupasua sadaka na kupita katikati ya vipande, akifanya iwe ishara ya kuwa ahadi yake ilikuwa imetiwa muhuri na haitabadilika (Mwanzo 15:9-18)

Wakati Ibrahimu alipoonyesha kuielewa imani na utiifu katika kumtoa Isaka kuwa sadaka kwa hiari sawasawa na jinsi Mungu alivyomwagiza alipewa thawabu ikiwa ni pamoja na ahadi nzuri aliyopewa, kwa kiapo cha Mungu. Kwa kuwa Mungu hawezi kuleta shaka kwenye Neno lake bali ili alithibitishe alitia kiapo kwa ajili ya kusimamia uwepo wake mwenyewe, Ibrahimu akapata uthibitisho mkuu kuliko uthibitisho wowote ?Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao,mwanao wa pekee, katika kukubariki nitakubariki?? (Mwa. 22:16-18). Hivyo ahadi zilithibitishwa na kuhakikishwa kwa kuifanya njia iweze kuwezekana.

5. Ahadi inarudiwa kwa Isaka na Yakobo
Ahadi hiyo hiyo moja ilifanyika kwa Isaka na Yakobo, wazawa wa Ibrahimu (Mwanzo 26:3-4; 28:3-4, 13-14)

VITABU REJEA:
"Elpis Israel" (J. Thomas)?Part 2, chapter 2
"Christendom Astray" (R. Roberts)?Lecture 9
"First Principles Bible Marking Course" (C.S.S.S.)?pages 57-62

MASWALI YA AYA
    1. Fafanua uhusiano uliopo kati ya Injili na ahadi ambazo Mungu alimwahidi Ibrahimu
    2. Tunawezaje kutumaini kurithi ahadi alizopewa Ibrahimu?
    3. Ni kwa jinsi gani ufufuo ni muhimu katika kutimiza ahadi alizoahidiwa Ibrahimu ?

MASWALI YA INSHA
    1. Onyesha umuhimu wa ahadi za Ibrahimu katika kusudi la Mungu.
    2. Kuonyesha maendeleo ya kina cha ahadi za Mungu alizopewa Ibrahimu kwa kutumia kalamu weka kivuli cha rangi kwa kila moja ya mistari katika Biblia yako zinazoeleza kwa ufasaha kuhusu ahadi hizo.
    3. Elezea jinsi ahadi kwa Ibrahimu zinavyoelekeza mbele kwa Kristo na kwenye uzao mwingi usioweza kuhesabika.a Mungu ya‘–

Swahili Title
134 TUMAINI LA AHADI WALIZOPEWA MABABA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type