141. UFUNUO KWENYE KICHAKA
Katika somo hili tutagundua jina la ajabu la Mungu wa Israeli. Ni jina ambalo lina maana kamili na alipewa Musa katika kipindi cha mwafaka sana katika historia ya watu wake Musa mwenyewe alihitaji kuhisi kuwa hakika Mungu alikuwa pamoja naye. Matukio ya utukufu wa kichaka chenye kuwaka moto na sauti ya Mungu iliyotokea katikati yake yaliwezesha kurejesha tena imani ya Musa kwa Mungu na yeye mwenyewe Musa bado alikuwa mwenye mashaka ya kuwa kiongozi, na kwa hiyo Mungu akampa Haruni, kaka yake, awe msemaji wake. Musa na Haruni walirudi pamoja Misri kukamilisha ukombozi wa wana wa Israeli.
KUTOKA 3
KATIKA MIDIANI (Kutoka 3:1-12)
Karibu miaka arobaini ilikuwa imepita tokea Musa alipokimbilia huko Midiani. Mungu sasa alikuwa tayari kuwaokoa watu wake kufuatana na mpango wake aliokuwa amempatia Ibrahimu muda mrefu zamani (Mwanzo 15:13-16).
Musa alikuwa amepeleka kuchunga makundi ya kondoo wa baba-mkwe wake mpaka eneo la kuzunguka mlima Sinai. Palikuwa mahali pa upweke penye utukufu wa asili, panapofaa kwa ufunuo kutoka kwa Mungu.
Hapa, kuna vilele virefu vinavyoinuka ki-wima kutoka uwanda na ukimya wa kina huongeza ukuu wa utukufu wa Mwuumbaji ikilinganishwa na hali duni ya mtu.
Musa katika tukio hili aliona maono ya kushangaza- kichaka kikiwaka moto lakini pasipo kuteketea! (Kutuka 3:1-2). Musa akasogea karibu zaidi. Malaika akasema naye kutoka katikati ya kile kichaka (mstari 3-4). Akaambiwa avue viatu vyake kwa maana mahali alipokuwa amesimama palikuwa patakatifu (mstari 5) na kuwa malaika huyo alisema kwa niaba ya Mungu wa baba zake (mstari 6).
Musa mwenye kujaa hofu ndipo aliposikia maana ya kichaka kinachowaka! Mungu alikuwa amesikia kilio cha mateso ya wana wa Israeli katika Misri, naye alikuwa ameshuka kuwakomboa. Kwa lengo hilo alikuwa amemteua Musa kuwa mkombozi wao (Mstari 7-10, linganisha Kutoka 2:23-25). Musa aliagizwa kuliongoza taifa ili waende kumwabudu Mungu kule mlima Sinai. Kwa ajili ya dalili ya jambo hili, Mungu alimpatia ishara ya kichaka kinachowaka (Mstari 11,12).
Kuwaka kichaka bila kutekea kulielekeza kwenye historia ya baadaye ya watu wa Mungu. Wangeteseka sana pamoja na kupata “majaribu mengi mazito” lakini Mungu angewahifadhi (linganisha Yeremia 30:11). Jina lake, likiwa karibu kufunuliwa kwa Musa, aliwahakikisha kuwa wataendelea kuishi kama taifa, ukweli ambao unatambuliwa na manabii (Malaki 3:6; Isaya 43:1-2). Mungu angejifunua mwenyewe kwao, angewapitisha kwenye mateso mengi na mwishowe wangedhihirisha utukufu wake katika Ufalme watakapokuwa kichwa cha mataifa yote (Zekaria. 2:15)
JINA LA MUNGU (Kutoka 3:13-16)
Majina ya Waebrania mara nyingi huelezea juu ya tabia au kusudi. Jina lake Mungu nalo pia halina tofauti na lina maana yake. Jina lake lina maana na linatueleza wakati ujao wakati dunia yote itakapojawa na utukufu wa Mungu.
Musa aliomba Mungu amwambie Jina lake aweze kurudi kwa watu wake na kuwaonyesha kwamba alikuja kwa amri ya Mungu ili kuwaongoza Israeli kutoka Misri.
Jina la Mungu kama lilivyofunuliwa katika Kutoka 3:14 ni “MIMI NIKO AMBAYE NIKO” lakini tafsiri hii katika Biblia za kiingereza siyo sahihi. Maneno hayo yanatakiwa yatafsiriwe kuwa ya kinabii nayo yasomeke “Nitakuwa mimi nitakaye kuwa”. Wakati Musa atakaposema kwa niaba ya Mungu kwa Israeli angesema “ Yeye atakayekuwako” na maana ifananayo kwa ukaribu katika matamko ya kiingereza kuhusu neno la Kiebrania ni “ YAHWE”. “ YAHWE” ndilo hasa Jina la Mungu na tunaona kwa kawaida limeandikwa katika Biblia zetu “BWANA” au “MUNGU”. Tunatakiwa kila wakati kulitamka Jina la Mungu kwa heshima kabisa. Ndilo Jina lake takatifu, na ni kutokana na jina hili tunawezeshwa kulifikiria kusudi la Mungu la wakati ujao kwa dunia na watu wake. Jina lake linaunganishwa na Ibrahimu, Isaka na Yakobo (mstari 15) kwa kuwa waatakukuwa wenye nguvu ( Malaika) kama sehemu ya kutimiza sehemu ya agano lake ambalo aliwaahidi.
Mungu sasa anawaita watu kutoka katika mataifa kwa ajili ya Jina Lake (Matendo ya Mitume 15:14). Wale watakaostahili wakati Yesu Kristo atakapokuja mara ya pili watapewa uzima wa milele na watamsaidia katika Ufalme. Kisha kusudi la Mungu litakuwa kuwaelimisha na kuwabariki mataifa yote ili kwamba dunia ijawe na utukufu wa Mungu na Mungu ataweza kukaa nao watu wale ambao “watakuwa” na uzima wa milele.
Wataonyesha tabia zote za kushangaza zinazopatikana katika –Jina la Mungu (Kutoka 34:6,7). Jina lake Mungu “Mimi Nitakuwa ambaye Nitakuwa” ndipo hasa litakapokamilika (linganisha Hesabu 14:21; Isaya 11:9; Habakuki 2:13; 1Wakorintho 15:28; Uf. 21:3).
TABIA YA MUNGU (Kutoka 34: 6-7)
Jina BWANA linafafanua zaidi kuliko kusudi. Linatufundisha sisi kuhusu tabia ya Mungu. Mungu anapenda haki na kuchukia uovu ( soma Warumi 11:22). Wakati tunapobatizwa, tunabatizwa “katika jina la Baba ……” (Mathayo 28:19). Hii ina maana ya kuwa maisha yetu yanatakiwaa yaonyesha wema wake. Mfano mmoja wa jinsi hili linavyotendeka linaonekana katika maisha ya Yesu.
Alisema “ Jina lako nimewadhihirishia”, yaani alionyesha tabia ya Mungu katika mambo yote aliyoyafanya. Alisema, “Nami naliwajulisha Jina lako”, maana yake alifundisha injili ya Ufalme wa Mungu au alifundisha kusudi la BWANA (linganisha Yohana 17:6,26). Muumini inampasa, kuiacha dunia na kutembea kwa uaminifu na kwa utiifu kuelekea ufalme ujao. Tunaangalia kwenye mfano wake Kristo kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku, tujifunze kutoka kwake ili tuonyeshe tabia ya Baba yake nyakati hizi za uovu wa kimataifa.
Jina hili linatimizwa:-
-
Katika akili, tabia na kutukuzwa katika uzima wa Bwana wetu Yesu Kristo
-
Katika kukuza tabia ifananayo na ya BWANA ndani ya wanaume na wanawake wenye imani kwa njia ya utiifu wao wa injili.
-
Katika hao watakaokuwa wake Kristo atakapo kuja mara ya pili; na hatimaye, mwisho wa millennia (miaka elfu moja) wakati Mungu atakapokuwa “yote katika wote”.
MAAGIZO ALIYOPEWA MUSA (Kutoka 3:16-22)
Mungu alimwagiza Musa kwa kina jinsi atakavyotenda ili kufanikisha ukombozi wa Israeli. Alitakiwa kuwa jasiri mbele ya uso wa Farao na kukata maagizo Mungu angeleta juu ya mfalme na taifa lake adhabu ambayo walistahili. BWANA angeweza kuogopwa na kuheshimiwa na wote wawili Wamisri na watu wa Mungu, Waebrania. Wakati wa kipindi cha mapigo yangaliyokuja angekuja kujulikana machoni mwa watu wote.
Wakati ulipofika, Farao angewapa ruhusa waende lakini hawangekwenda mikono mitupu (mstari 21). Walitakiwa “waazime” (neno hilo kihalisia lina maana “dai”) vyombo vya fedha na mavazi kutoka kwa Wamisri. Walikuwa wameshughulika kwa miaka mingi wakiwa watumwa kwa hiyo Mungu alidai mishahara yao! Kwa nguvu yake Mungu atawaonyesha kuwa alikuwa Mkuu zaidi kuliko nguvu ya Misri na miungu yake.
KUSITASITA KWA MUSA (Kutoka 4:1-17, 27-31)
Musa alisitasita kutenda. Bila shaka alikumbuka alivyokataliwa na watu miaka arobaini iliyokuwa imepita. Mungu akampatia ishara tatu ili kuonyesha kuwa Mungu atakuwa naye.
-
Fimbo iliyogeuka kuwa Nyoka (mstari 1-5)
-
Mkono ulibadilika kuwa wenye ukoma na ukaponywa (mstari 6-8)
-
Maji ya mto yaliyogeuka kuwa damu (mstari 9)
Hata hivyo, Musa hakutaka kwenda. Jibu la Mungu lilikuwa wazi na lenye kumhakikishia “Enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, kukufundisha utakalolisema” (mstari 11,12). Bado Musa aliendelea kukataa kwenda (mstari 13) kwa hiyo hasira ya Mungu ikawaka (mstari 14). Hivyo Haruni akateuliwa kuwa msemaji wa Musa (mstari 15,16), na Musa akaagizwa kurudi kwa Farao, na fimbo mkononi, kwenda kutenda miujiza (mstari 17).
Haruni akatumwa kwenda kuonana na Musa na wakati wakirudi kwa pamoja wakawafahamisha Israeli kusudi la Mungu na kuwaaminisha ya kwamba wakati wao wa ukombozi ulikuwa umefika. “Watu wakaamini… nao wakainama vichwa vyao na wakasujudu” (mstari 27-31).
MUHTASARI:
-
Kichaka kilichowaka bila kuteketea ilikuwa ni ishara ya nia ya Mungu kuwaokoa watu wake kutoka katika mateso yao na kujidhihirisha mwenyewe kati yao.
-
Ili kwamba Israeli waweze kukumbuka kusudi la Mungu juu yao alijidhihirisha mwenyewe kwa jina la “BWANA” Yeye atakayekuwa.
-
Hukumu za Mungu zilikuwa zimwagwe juu ya Misri ili kwamba watu wote waweze kuliogopa Jina Lake Takatifu- kama vile kama dunia itakavyoliogopa Jina Lake wakati wa Armageddoni)
VITABU REJEA:
"Elpis Israel" (J. Thomas)—Pp. 288-289
"Phanerosis (Australian Edition), Pp. 56-59
"Visible Hand Of God" — Chapters 10 and 11
'The Story Of The Bible" (H. P. Mansfield)—Pp. 237-257
MASWALI YA FUNGU
-
Nini maana ya kichaka kinachokuwa kinawaka?
-
Jina la Mungu ni lipi na lina maana gani?
-
Ni jinsi gani Bwana Yesu Kristo alilidhihirisha Jina la Mungu?
-
Kulikuwa na sababu gani ya kumtuma Musa kurudi Misri?
-
Ni ishara zipi Mungu alimpatia Musa kuonyesha kwamba Mungu atakuwa pamoja na naye? Ni jinsi gani Musa alizitumia ishara hizo?
MASWALI YA INSHA
-
Eleza maana ya jina lenye kumbukumbu la Mungu.
-
Eleza matukio yaliyofanyika wakati malaika wa Mungu alipomtokea Musa kule kwenye kichaka kilichowaka.
-
Musa aliitikiaje wakati alipoambiwa kwenda kuwaongoza Israeli kutoka Misri? Je,alisaidiwaje katika kazi hii?