CSSA 2-3-02 - DAVID'S SIN AND ITS CONSEQUENCES

Swahili

177. DHAMBI YA DAUDI NA MATOKEO YAKE:

“Jambo alilolifanya Daudi lilimchukiza BWANA”

Katika masomo ya nyuma tuliyoyasoma tumekuwa tukifuatilia maisha ya Daudi.

Tumefikia mpaka kupendezwa na imani yake kwa Mungu na sisi tumeona jinsi Mungu alivyombariki kwa kumpatia ile ahadi nzuri sana ya ajabu ya ule uzao, yaani Bwana Yesu kristo, Tumeona akiokolewa kutoka kwa maadui zake, na sasa tumefikia sehemu ya Biblia ambayo kwa mara ya kwanza tunaposoma, inatufanya kusimama kwa mshangao na kujiuliza swali, “Ni kwa jinsi gani Daudi aliweza kufanya kitu cha namna hii?” Lakini tutakopolipata jibu sahihi la swali hili, ni hapo ndipo tutakuwatumejifunza somo la muhimu sana, fundisho ambalo kila mmoja wetu wetu inampasa kujifunza. Ni fundisho litakalotunyenyekeza katika ufahamu wetu na kutufanya tuweze kutambua kwamba ni kwa njia ya rehema ya Mungu tu pekee tunaweza kutumaini kupata uzima wa milele.

2 Samweli 11 na 12.

ADUI MKUU WA DAUDI :
Kwa kweli adui mkuu wa Daudi hakuwa Sauli au, maadui yaliyoizunguka Israeli, au mtu yeyote au mnyama kwa maana Mungu angeweza kumwokoa Daudi kutokana na maadui wote hawa. Adui mkuu wa Daudi alikuwa ni adui aliyejificha katika majaribu yaliyo ndani ya moyo wake – dhambi ya mwili au tamaa ambayo kama itafuatwa, huongoza kwenye dhambi .Tamaa hii, ambayo kila mmoja wetu anayo; ndiye adui wetu mkubwa sana ambaye inatubidi tumshinde, kwani tusipomshinda, basi tutaongozwa kutenda mambo yasiyompendeza Mungu, na kwa sababu hiyo sisi wenyewe tutajiletea aibu na majuto na kwa familia zetu.

DHAMBI YA DAUDI

2 Samweli 11
Jeshi la Isreli chini ya uongozi wa Yoabu lilikuwa nje kupigana na wana wa Amoni, lakini Daudi alibakia nyumbani huko Yerusalemu. Siku moja jioni Daudi alikuwa akitembelea darini nyumbani kwake, ambapo alimwona mwanamke mzuri, akioga. Alikuwa ndiye Bathsheba, mke wake Uria, mmojawapo wa asakari jasiri wa Daudi ambaye alikuwa pamoja na Yoabu kwenye uwanja wa vita wakipigana vita.

Daudi akatamani ampate Bathsheba ili awe mke wake naye Daudi akamkaribisha nyumbani kwake na akazini naye. Mungu alikuwa amekataza hili alipowapatia zile amri kumi. Kwani ilikuwa ni uovu kwa mtu kuchukua mke wa mtu mwingine (Kutoka 20: 14-17). Mithali hueleza wazi wazi kuhusina na tabia hii ya hatari ambayo Daudi alikuwa ameanza

“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika' (Mithali 6: 32-33)

DHAMBI MOJA INAONGOZA KUTENDA DHAMBI NYINGINE:
 Ingawaje Daudi tangu kudhamilia kutokumtii Mungu, ndipo sasa akatambua ya kuwa ametenda dhambi. Je alipaswa kufanya nini? Alijaribu kuzificha njia zake ili mtu yeyote asifahamu kamwe dhambi aliyoitenda. Akapeleka barua kwa Yoabu, akimwomba amweke Uria kwenye eneo la hatari vitani ili auawe. Akasababisha Uria kuuawa ili kwamba ampate Bethsheba kuwa mke wake. Na sasa Daudi alikuwa na hatia kwa kuvunja Amri tatu: kumtamani mke wa jirani yake, uzinzi na pia kuua (kutoka 20: 13-17). Lakini BWANA, aonaye yote na ajuaye mambo yote, alijua kuhusu uovu huu na jambo hili lakutisha alilolitenda Daudi (2 Sam.11: 27). Kamwe sisi tusijaribu kuzificha.
 
Dhambi zetu, bali tuzitubu dhambi waziwazi kwa Mungu, kwani kufanya hivyo tutajiokoa maumivu ya moyo na mateso.

TOBA NA MSAMAHA  - 2 Samweli 12: 1-14.
Baada ya miezi kadhaa, Nathani nabii alikwenda kwa Daudi Akasema kwa mfano kuhusu mtu fulani tajiri aliyekuwa na mifugo mingi kupita kiasi aliyeacha kuchukua mwana – kondoo katika kundi la mifugo yake ili kumwandalia chakula mgeni wake aliyemfikia nyumbani kwake ila badala yake akachukua mwana - kondoo mmoja wa pekee wa mtu masikini ambaye alimpenda sana.

Hisia ya haki ya Daudi iliamshwa mara moja. Akatamka hukumu juu ya tendo hilo batili, mtu huyu aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa; naye atamrudishia mara nne …” Lakini katika kutamka hivyo akawa ameshajihukumu yeye mwenyewe. Nathani akamjibu, “Wewe ndiwe mtu huyo” Maneno haya yalikuwa ufunuo wa kutisha.

Daudi alihuzunika sana, Nathani akamwambia “Kwa nini umelidharau neno la BWANA … umemwua Uria …nawe umemtwaa mkewe awe mke wako … basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako” (mstari  9,10). Daudi alikuwa amefanya hivyo kwa siri (mstari 12) na kutenda kama kwamba Mungu hakuwapo, na kwa sababu hii adhaabu yake ilipaswa kuwekwa wazi .

Daudi hakukwepa lawama wala kujihesabia haki mwenyewe akatubu na kusema “Nimemfanyia BWANA dhambi” Nathani akamwambia Daudi “BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa” (mstari 13).Chini ya sheria, Daudi alifahamu kuwa alistahili kifo. Ingawaje BWANA alikuwa amemsamehe dhambi yake, lakini dhambi hiyo ilimletea masikitiko kwa miaka mingi. Daudi kutoka siku ile alihisi kwamba asingeliweza kuwahukumu wengine, hata kama wangestahili hukumu hiyo.

Nathani akaendelea kusema, “Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa” (mstari 14). Kwa sababu ya dhambi ya Daudi watu wote wangemdhihaki BWANA. Inatupasa tuwe waangalifu tusiwapatie watu sababu ya kusema maovu juu ya Kweli. Mtoto aliyezaliwa na Bathsheba alikufa.

Daudi akafunga na kulia kwa tumaini la kwamba Mungu angemwokoa mtoto uhai wake, lakini mtoto alifariki baada ya siku 7. Ni katika muda huu Daudi aliandika Zaburi mbili – Zaburi 32 na 51.

Katika Zaburi 32 Daudi anasema kuhusu maumivu na mateso aliyoyahisi alipojaribu kuficha dhambi yake na kukaa kimya (mstari 3-4) na hali ya faraja aliyoipata alipotubu na Mungu akamsamehe (mstari 5).
 
Inatupasa tuzingatie kwamba katika 2 Sam.12: 4 dhambi inaelezwa kuwa kana kwamba “ni msafiri” au “mtu mtembezi” Daudi hakuwa mzoefu wa kufanya dhambi kwani anaelezwa na Mungu kuwa “mtu anayeupendeza moyo wangu” (Matendo 13: 22). Dhambi yake ilikuwa kujitenga kwa muda kutoka kwenye njia za maisha ya ki-mungu. Hili halikupunguza uovu wa dhambi ambayo aliitenda Daudi lakini ilimpatia BWANA msingi wa msamaha wa dhambi ambao haukuwapo kwa Sauli.

Msamaha wa Mungu kwa Daudi unalo fundisho kubwa Hapakuwa na jambo lolote lingine ambalo angelifanya, wala asingeweza kutoa dhabihu ya aina yoyote (Zaburi 51: 14-17) ili kumwepusha na adhabu ya kifo kufuatana na sheria. Ingawaje Daudi alikuwa mkosaji aliokolewa kutoka katika kifo. Hapa lipo tumaini kwa wote wanaotenda dhambi – iwapo wanatubu. Mungu kwa neema yake ametupatia tumaini la wokovu kupitia ubatizo katika Kristo (Waefeso 2: 8-9).

MATOKEO YA DHAMBI YA DAUDI:
Ingawaje dhambi halisi ya Daudi ilisamehewa madhara yake yalifikia kuwa na upeo mpana. Mtoto wa kwanza ambaye Daudi na Bathsheba walimpata, alikufa sawasawa na maneno ya Nathani, yule nabii (2 Sam. 12: 15-23). Halafu wakapata mwana wa kiume mwingine ambaye walimwita Sulemani, ingawa BWANA alimwita Yedida ikimaanisha “Apendwaye na BWANA”. Nathani alimwambia Daudi kwamba BWANA angeruhusu maovu kuja juu yake kutoka katika nyumbani mwake mwenyewe (mstari 11) na hili lilitokea. Miongoni mwa wanawe, watatu walimletea maumivu makubwa akilini mwake Amnoni, Absalomu na Adoniya, na hawa wote waliuawa kwa ajili ya maovu yao.

FUNDISHO KWETU
Tumekwisha kusikia sasa habari ya kusikitisha na ya kutisha, lakini ni habari ambayo ni lazima tuisimulie watu wengine kwa sababu ya onyo kubwa tunalopewa ikiwa tunataka kuwa wafuasi wa Kristo. Daudi alijiletea mwenyewe juu yake adhabu ya kutisha na huzuni kwa wengine kwa kuwa kwa muda hakuweza kufikiria matokeo yake. Aliruhusu akili yake isiweze kufiria na mawazo yake yakajitenga kutoka kwenye njia za Mungu. Mawazo ya dhambi yalimdanganya na kumfanya atende dhambi.

Inatupasa tufahamu kuwa dhamabi inasababishwa na kutenda kwa kufuata tamaa mbaya zinazotoka ndani ya mioyo yetu wenyewe (Marko 7: 21-23). Ni lazima tuzielekeze akilin zetu kwenye Neno la Mungu, na kila wakati tutende lile linalompendeza Mungu. Inatupasa kujibidiisha katika kufanya kazi zinazohusu Kweli ya Mungu. Kama tukifanya hivi hapo hatuchukuliwa kutoka kwenye njia za Mungu na mawazo dhaifu yanaweza kutuongoza kwenye dhambi. Na muda mfupi wa tendo la dhambi unaweza kutuletea miaka mingi ya huzuni Imetamkwa kwamba dhambi huchafua, huvuruga, huleta makovu katika maisha ya mtendaji dhambi na kumdangania visigino vyake kana kwamba anafukuzwa kwa juhudi. Tunaelezwa wazi kabisa, “ikimbie zinaa” (1 Wakorinto 6: 18, 9 -10).

Fundisho kutokana na dhambi ya Daudi ni kuwa “Mtu ajidhaniaye amesimama ajiangalie asianguke” (1 Wakorintho 10: 12). Tuanaishi katika katika sehemu zenye uovu na katika dunia ya uzinzi ambapo dhambi ya Daudi ni mojawapo ya uovu wao, maisha ya kupenda anasa. Enyi vijana jihadharini. Hata kama ni vijana ambao hawaoa au kuolewa wanaotuzunguka pande zote wanaweza wakawa na maadili kidogo au hakuna maadili kabisa yoyote yaliyobakia, inatupasa “tumwogope Mungu na kuzishika amri zake” kiakili na kwa uadilifu tukiyapinga majaribu hayo na kwa mawazo safi na mioyo safi na kwa nguvu kudhamiria kuzikimbia tamaa za ujana na badala yake tumfuate utauwa.
 Daudi aliitwa “mtu aupendezaye moyo wa Mungu” (1 Sam 13: 14). Ingawaje Daudi alitenda dhambi lakini alimpenda Mungu na kujibidiisha katika kutumia muda wake mwingi katika kuandika Zaburi na kufundisha watu wengine njia za Mungu. Mungu alimhurumia Daudi kwa sababu Daudi alitubu na kuwahurumia wengine kumbuka mafundisho kuhusu Sauli – mara mbili Daudi alimwokoa Sauli uhai wake (1 Samweli 24 na 1 Samweli 26 ). Hii ndiyo maana Mungu alimsamehe Daudi. Ni jambo la muhimu sana kwetu sisi kuwahurumia wengine. Tunasali, “utusamehe makosa yetu kama na sisi tunavyowasamehe wanaotukosea” – ikiwa tunawasamehe wengine ndipo Mungu atatusamehe na sisi (Mathayo 6: 12, 14,15).

REJEA KATIKA MAKTABA:
“Mtu Daudi” (H .Tennant) – Sura 7.
“Historia ya Biblia” (H .P. Mansfield) Kitabu cha 4, Namba 3.
“ Njia za kutosheleza” (R. Roberts) –Sura 17 .

MASWALI YA FUNGU
1. Dhambi ni nini – na tunawezaje kuishinda?
2. Ni kwa jinsi gani Daudi alivunja amri zile kumi za Mungu Pamoja na Bathsheba?
3. Ujumbe wa Nabii Nathani kwa Daudi ulikuwa ni upi baada ya Daudi kutenda dhambi?

MASWALI YA INSHA:
1. Ni kwa vipi Daudi aliteseka kwa sababu ya dhambi yake?
2. Ni mafundisho gani tunayojifunza kutokana na Msamaha wa Mungu kwa dhambi ya Daudi?
 

Swahili Title
177 DHAMBI YA DAUDI NA MATOKEO YAKE
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type