182. ONYO LA SULEMANI KATIKA UZEE WAKE:
“Wakati Sulemania alipozeeka... moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA,Mungu wake, kama jinsi ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake.”
Kuanguka kwa Sulemani kutoka kuwa mtu wa imani kulikuwa kwa pole pole, siyo kwamba alianguka ghafla. Hisia ya kujionua maarufu ilianza kuonekana maishani mwake. Ile hali ya unyenyekevu aliyoionyesha kule Gibea, wakati alipojieleza kuwa ni mtoto, ilianza kutoweka. Hakuendelea tena kumtumikia Mungu kwa moyo wake wote. Mambo mengine mhimu yalianza kunyonya wakati wake.
1 Wafalme 10: 24-11: 25
IMANI YA SULEMANI INAANZA KUDHOOFIKA – 1 Wafalme 10: 25-29
Maandiko yanatuambia kwamba Sulemani alikusanya magari ya vita, wapanda farasi na farasi kutoka Misri. Alikuwa anaanza kuwa kama waflme wa mataifa waliomzunguka, na kuzitegemea nguvu za mwili badala ya Mungu. Wakati Sulemani alipoziona hizi akawa kwa hakika akianza kumpa kisogo Mungu, aliye nguvu ya kweli ya Israeli. Isaya miaka mingi iliyofuata alitoa onyo dhidi ya kuziamini farasi, “Ole wao watelemkao kwenda wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangali Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA” (Isaya 31: 1 – tazama pia Zaburi 147: 10;33:17). Lakini Mungu alikuwa amewapatia ushauri wa maalum kwa wafalme wa Israeli. Mungu aliwaonya kupitia kwa Musa aliwaonya kwamba watakao kuwa wafalme wa Israeli asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwe na mali nyingi, wala asiwe na wake wengi. Kila moja kati ya hayo yangemwongoza mfalme kuacha kumtegemea Mungu, na kutuamini katika mwili (angalia kwa makini Kumbukumbu la Torati.17:16 -17). Kila amri, Sulemani alishindwa. Hakuna shaka kwa kweli, kwamba Sulmani angekuwa macho kuitunza amri ya Mungu. Na kila mfalme aliamriwa yeye mwenyewe kuandika nakala ya sheria alipouchukuwa ufalme na kukaa juu ya kiti cha enzi (Kumbukumbu la Torati 17: 18). Licha ya onyo hili hata hivyo Sulemani alishindwa. Iwapo kweli tunajuwa kwamba tunayo dhambi mojawapo inayotudandanya na jinsi mtu anavyoweza kuiacha kweli pole pole, basi tunaona jinsi tunavyokuwa na maisha ya Sulemani ndani yetu. Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kubwa na huenda alifikiri kwamba alikuwa na hekima na nguvu yenye uwezo wa kuyashinda majaribu yoyote ambayo yangetokana na mali hizi alizokuwa nazo. Alifikili kwamba wengine wangeshindwa, lakini yeye angeyaweza kushinda. Hayo ni nia ya mwili. Mara hatua moja inapokuwa imelekea upande wa usiofaa, hatua nyingi zaidi zitafuata na itaonekana kwamba ni sawa sawa tu na “wala hakuna madhara yoyote”. Hivyo tunaweza kunaswa na fikira zetu na tukayaharibu matumaini yetu. Eva kule bustanini ya Edeni aliona kwamba mawazo ya mwili yalimwongoza kwenye hukumu ya kifo, na mawazo ya Sulemani pia, alitambua kuwa mtu anapoongozwa na mawazo ya mwili yanampeleka kwenye kwenye kifo. Ingaliwezekana kuyashinda ikiwa angesema “BWANA asema,” lakini hawakufanya hivyo, na matokeo yao mabaya yameandikwa katika maandiko ili kuwa fundisho kwa ajili yetu sisi wote.
ANGUKO LA SULEMANI – 1 Wafalme 11:1-8
Tamaa ya Sulemani ya kuwa na mali na farasi wengi ilidhoofisha imani yake. Hata hivyo, aliendelea kumtambua BWANA kuwa ndiye Mungu mmoja wa pekee na wa kweli. Lakini alikuwa ameruhusu mwili umtawale na hekima yake ya kipekee haikutosha kuweza kumzuia kuangukia katika kosa lingine la hatari na uchungu. Tunasoma kwamba “Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wa kigeni, pamoja na binti Farao, Wanawake wa Waoabi, na Waamoni, na Waedomi, na Wasidoni na Wahiti” (mstari 1).
Chaguo lake la kuwa na wanawake lisingekuwa baya zaidi. Kila mmoja kati ya hao wanamke alitoka katika mataifa “ambayo BWANA aliwaamba wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala waiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao” (mstari 2). Lakini maandiko yanasema “Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda”. Zaidi ya hao wakeze waliorodheshwa katika mstari wa 1, Sulemani pia alikuwa na wake wengine 700 na masuria 300, Katika hili uamuzi wake ulikuwa wamakosa na aliyadharau maonyo ya kweli ya maandiko. Jambo lisiloweza kukwepe mara moja likatokea, kwani tunasoma, “nao wake zake wakamguza moyo wake, maana ikawa Sulemani alipokuwa mzee wake zake wakamguza moyo wake; afuate miungu mingine, na moyo wakle haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake” (mstari 3, 4). Ni jinsi gani inavyo sikitisha namna mfalme wa Israeli mwenye hekima na aliyepewa heshima na manufaa mengi makubwa alivyoanguka kwa kuupenda ulimwengu na kutafuta anasa kuliharibu moyo wake na kumpofusha macho yake.
Mwana wa Daudi mwaminifu badala ya kuonyesha hekima, msimamo imara na uongozi mzuri, alipokuwa mfalme mzee na mpumbavu, Sulemani anaeleka kulijutia hili “Heri kijana maskini na mwenye, kuliko mfalme mzee mpumbavu, ambaye hajui tena kupokea maonyo” (Mhubiri 4:3). Kupitia msukumo wa wake zake ambao walikuwa wapagani, Sulemani akawa mwabudu sanamu, naye akaabudu sanamu za miti na mawe ndani ya Hekelu ambalo alilijenga kwa ajili ya Mungu wa kweli. Maana Selemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni. Ni tukio la kushangaza na la aibu kiasi gani kwa taifa, ukimuacha Sulemani kumwabudu huyu mungu. Sulemani pia akamwabudu mungu Milkomu au Moleki, chukizo la Waamoni. Kwa mungu huyu watoto walitolewa kafara na ngom zilitumiwa kuzuia vilio vyao. Ibada hii ya kuchukiza ikawa ni mojawapo ya kawaida ya ibada katika maisha ya wana wa Israeli, nayo ilifanyikia kwenye bonde la Hinomu. Haikuwaimeondelewa hadi utakaso wa mfalme Yosia miaka mingi baadaye ambapo ndipo dini hizi za machukizo zilitokomezwa kabisa (2 Wafalme 23:10).
HUKUMU YA MUNGU KWA SULEMANI KWA AJILI YA UPUMBAVU – 1 Wafalme 11: 9-25
Amri zilikuwa wazi na hapakuwepo na udhuru kwa upotofu wa Sulemani wa kutokuzifuata amri hizi. Zaidi ya kuwa mwongozo wa wazi wazi kutokana na sheria ya Musa, Mungu alikuwa amemtokea Sulemani mara mbili.
1. Huko Gibea pamoja na ahadi ya baraka kama angeshika amri za Mungu.
2. Huko Yusalemu wakati wa kuliweka wakfu Hekalu, pamoja na onyo la hukumu iwapo yeye na taifa wangefuata na kuabudu miungu mingine (Wafalme. 3: 13 -14, 9: 6-8).
Ni kanuni ya maandiko kwamba yeye apewaye vingi, vingi pia hutazamiwa kutoka kwake. Kwa hiyo ilikuwa ni sawa sawa na muhimu kwake yeye aliye pewa neema nyingi, kwake hukumu ya kutisha ingemwangukia. “Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, kwa kuwa umefanya hayo; wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wao, nami nitampa mtumishi wako.” (mstari 11). Hii kwa kweli ilikuwa ni adhabu ya kuogopesha, naye Suleman bila shaka alikumbuka adhabu ya aina hiyohiyo ambayo Sauli alipewa kwa ajili ya upumbavu wake (1 Samweli 13:13-14). Walakini kwa ajili ya haki ya Daudi, Mungu aliamua kwamba hukumu hiyo haitatekelezwa katika siku za Sulemani, bali katika siku za mwanawe Rehoboamu. Zaidi ya hayo, siyo ufalme wote ungeondolewa kutoka kwa Rehoboamu, ila makabila mawili yangalibakia, kabila moja la (Yuda) kuendeleza utawala wa kifalme na kabila la Benyamini (1 Wafalme 12:21). Rehema ya Mungu isingetoka kabisa katika uzao wa Daudi kama vile ilivyoondolewa kwa Sauli (2 Samweli 7: 15).
Ingawa hukumu kubwa zaidi iliahirishwa, Mungu akamwinua shetani juu ya mfalme, yaani Hadadi, Mwedomi. Hadadi alikuwa amekimbia shambulio lililofanywa na Yoabu kwa Edomu; na akatorokea Misri na aliishi huko wakati Daudi alipokuwa mfalme. Lakini aliposikia kwamba Daudi na Yoabu walikuwa wamefariki, akarudi nchini mwake kwa lengo la kuwashawishi Edomu kumwasi Sulemani. Rezoni naye ametajwa katika mistari 32-25 kuwa (shetani) mpinzani mwingine aliyeinuliwa na Mungu kumsumbua Sulemani. Alikuwa anatawala Syria kutokea Dameski na kutoka huko akaishambulia Israeli. Hata hivyo hukumu kuu kabisa ilikuwa bado mbele, ambapo Yeroboamu, mmoja wa watumishi wa Sulemani, angeasi na kuyaongoza makabila kumi katika uasi. Siku za utukufu, umoja, amani na mafanikio ukiwa ndiyo umefikia mwisho na hayo hayatakuwapo tena mpaka Kristo atakaporudi na ndipo Mungu atampatia kiti (Ezekieli 21: 27, 37: 22).
FUNDISHO KWETU:
Sulemani alijiletea kifo na maangamizo yake mwenyew na kwa ufalme wake pia kwa ajili ya upumbavu wake. Hata hivyo katika maisha ya mtu huyu ambae BWANA alimpenda (2 Samweli 12: 24-25); na ambaye BWANA alijihidhihirisha kwake mara mbili, kuna fundisho la nguvu kwetu.Tunaona mfano wa kanuni ya mfano kwamba “kuwa rafiki wa dunia ni kuwa uadui wa Mungu” (Yakobo 4:4). Marafiki wa Sulemani katika mataifa yaliyomzunguka walitumaina farasi na utajiri na hivyo ndivyo Sulemani pia alivyovitegemea, akijaribu kuwashngaza sana, akakusanya vitu hivi vyote viwili. Moyo wake ulikuwa pale hazina yake ilipokuwa; hapa duniani, na wala siyo mahali ambapo ungepaswa kuwepo, kwa Mungu huko mbinguni (Mathayo 6:19 – 21). Inatupasa kuwa waangalifu sana ili kwamba mambo ya Mungu yachukue nafasi ya kwanza kila wakati maishani mwetu, na ya kuwa hatuvitumainii vitu vya kizazi cha dunia hii mbovu (angalia Luka 21: 34 - 36). Katika ndoa zake na wasioamini moyo wa Sulemani ukageuka kuwafuata katika kuabudu sanamu zao. Kama tukifanya urafiki wa karibu na watu wasiomjuwa BWANA katika tutakuwa tunamgeuzia migongo yetu yeye. Kwa kuwa Mungu amekataza urafiki wa aina hiyo na ndoa na wasiamini (1 Yohana 2: 15 - 16, 2 Wakorintho 6:14-18; 1 Wakorintho 7: 39).
Huu ni mwiko wa busara maana unatuepusha sisi na uchungu wa moyo na huzuninyingi zinazotokana na masikitiko ya kutokufuata amri za Mungu. Inatubidi kutafuta na kuendelea kudumu na marafiki wetu wanaoamini, tukitiana moyo katika njia za haki na kweli ambazo tunasoma katika Biblia.
REJEA KATIKA MAKTABA:
“Historia ya Biblia” (H.P. Mansfield) - Kitabu cha 4 Namba 10.
MASWALI YA VFUNGU:
1. Orodhesha njia alizoshindwa Sulemani na hivyo kusababisha ufalme wake kuanguka.
2. Ni kwa gani tunapaswa kuchagua marafiki zetu ili tusijitenge kujitenga na Mungu kama Sulemani alivyofanyiwa?
3. Mungu alisema kuwa atafanya nini kutokana na matokeo ya kushindwa kwa Sulemani?
MASWALI YA ISHA:
(1) Fafanua mazingira yaliyosababisha Sulemani kuacha njia za Mungu.
(2) Eleza mafundisho tunayoweza kujifunza kutokana na upumbavu wa Sulemani katika miaka yake ya uzee.
(3) Je, ndoa na asiyeamini inaruhusika?Katika jibu lako rejea katika ndoa alizokuwanazo Sulemani.