CSSA 2-3-10 - JUDGMENT UPON THE HOUSE OF AHAB

Swahili

185. HUKUMU JUU YA NYUMBA YA AHABU

"Ambaye Yezebeli mke wake alimshawishi?"

 

Ahabu ni mtu ambaye aliyefahamu neno ambalo ni la haki, lakini alikosa nguvu za kutimiza kusudi ili kuuweka ufahamu wake katika matendo. Eliya amempelekea onyo la Mungu kwa Ahabu na akalithibitisha onyo hilo kwa ishara za miujiza, kama vile njaa (1 Wafalme 17) na dhabihu ile aliyoitoa pale Mlima Karmeli (1 Wafalme 18). Na ijapokuwa alitambua nguvu za BWANA katika miujiza hii na wala hakupinga kuuawa kwa manabii wa Baali, hata hivyo wakati Yezebeli alipotaka kumwua Eliya, yeye hakufanya jitihada yoyote ya kupinga tendo hili. Hakuweza kupokea maonyo ya Mungu na mambo yake yakazidi kuharika zaidi wakati alipomriuhusu mke wake kumwua Nabothi, mtu ambaye maisha yake ya haki yalidhihirisha imani yake ya kina kuhusu dini. Kitendo cha Yehu kuiangamiza kwa haraka nyumba ya Ahabu inaonyesha kanuni ya kuwa Mungu hadhihakiwi, bali atawaadhibu watendao maovu.

 

1 Wafalme 19:21; 2 Wafalme 9:10

 

ELIYA ANAHAKIKISHIWA USALAMA - 1 Wafalme 19:1-2

Eliya bila shaka alikuwa amefikiri kuwa baada ya uthibitisho mkuu wa nguvu za Mungu pale juu ya mlima Karmeli (1 Wafalme 18), asingekuwepo mtu yeyote ambaye angevumilia kuabudu tena ibada ya uongo kamwe. Hata hivyo, imani ya tumaini lake ilikuwa ya muda mfupi. Ahabu alipomwambia Yezebeli mambo yote yaliyotokea mlima Karmeli na jinsi Eliya alivyowaua manabii wa Baali, alighadhabika sana na kumpelekea Eliya ujumbe akisema, "miungu inifanyie hivi na kuzidi, nisipokufanyie roho yako kesho panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao" (1Wafalme 19:2). Kwa ajili ya kuhofia usalama wa maisha yake, Eliya alikimbia na hatimaye akafika Mlima Horebu. Nabii alitamani heri afe. Hakuweza kuona jinsi ambavyo angefanikiwa katika agizo kuu la kuwageuza watu mioyo yao itoke katika ibada ya sanamu. Wakati Eliya alipokuwa amepumzika ndani ya pango Mungu alisema naye na kumwuliza "Unafanya nini hapa Eliya?" (mstari 9).

 

Eliya akajibu kwamba amefanya kila linalowezekana kufanya uamsho katika Israeli, lakini hawakutaka kusikia, "Nami nimesalia, mimipeke yangu, nao wanitafuta roho yangu waiondoe" (mstari 10). Mungu akamwambia Eliya asimame juu ya mlima, "Na tazama BWANA akapita, upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwemo katika upepo ule; na baada ya upepo tetemeko la ardhi; na baada ya tetemeko la ardhi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwemo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu" (mstari 11-12). Kazi ya Eliya ilikuwa kama ile ya upepo mkali sana, ngurumo na moto, kila kimoja kilidhihirisha nguvu za Mungu katika hukumu na kuangamiza. Lakini Mungu alikuwa anajaribu kumwonyesha Eliya kuwa kuna jambo fulani ambalo hakulifamu, na jambo hili lilikuwa ni la muhimu sana sawasawa na hukumu. Lililotakiwa ni ilke sauti ndogo tulivu ya maelekezo katika Neno la Mungu. Bado walikuwepo watu 7000 katika Israeli wasiopiga goti kwa Baali ambao Eliya hakuwafahamu. Eliya aliulizwa, "Unafanya nini hapa, Eliya?". Akimaanisha kuwa kuna watu wengi sana waliosalia ambao anatakiwa awafundishe ile "sauti ndogo, ya utulivu" ya Neno lake BWANA ili kwamba imani yao na ujasiri wao uimarike. Siku hizi hitaji kubwa ni, "kuyaimarisha mambo yalisalia" (Ufunuo 3:2). Jambo hili linatendwa na walimu waaminifu katika eklesia zetu na katika shule zetu za Jumapili kwa kuziimarisha imani zetu ili kwamba kila mmoja wetu aweze kuzishinda tamaa za watu wasiomcha Mungu katika siku za hatari.

 

AHADI YA KULIPA MALIPO YAYOSITAHILI - 1 Wafalme 19:14-18

Majibu ya Mungu kwa Eliya, BWANA pia anamwimarisha kwa kumpatia ujumbe kuhusu hukumu itakayokuja juu nyumba ya uovu ya Ahabu. Mungu anetumia upanga wa Hazaeli, mfalme wa Israeli, Yehu mfalme wa Israeli na mwishowe Elisha nabii (1 Wafalme 20 :17). Wafuasi waaminifu wa BWANA, siku hizi wanahakikishwa kwamba uovu utakwisha wakati ujao ambapo Falme za wanadamu zitakapoangamizwa na badala yake kusimama Ufalme wa Mungu (Zaburi 149; 1 Wakorintho 15 :24-28; Danieli 2 :44-45).

 

UOVU WA AHABU – 1 Wafalme 21

Ahabu alipenda anasa, na raha, na hata hivyo alilitaka shamba ambalo lilipakana na (makao makuu) ikulu yake huko Yezreeli. Shamba hilo lilikuwa ni mali ya Nabothi, Myezreeli. Ahabu, akamwambia Nabothi, "Nipe shamba lako la mizabibu nilifanye shamba la mboga, maana lipo karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake" (mstari 2).

 

Lakini Nabothi alikataa, maana alikuwa mtu wa haki na ambaye alizitii sheria za Mungu. Sheria ilimkataza mtu kuuza urithi isipokuwa kama kulikuwa na sababu maalumu ambazo zilimlazimisha kuuza (Hesabu 36: 7, Mambo ya Walawi 25: 23). Hata hivyo ardhi ya urithi iliyouzwa ilitakiwa irudishwe kwa mwenye nayo katika mwaka wa Yubile (miaka wa 50) (Mambo ya Walawi 25: 13). Ndiyo maana, hata Nabothi akakataa kuuza na Ahabu akaghadhabika sana kuwa na moyo mzito. Ahabu hakuweza kuelewa ni kwa nini Nabothi alikataa kumwuzia na kama vile mvulana mwenye umri mdogo "akajilaza kitandani pekee yake, akageuza uso wake, akakataa kula" (mstari 4).

 

MPOANGO MWEREVU WA YEZEBELI – 1 Wafalme 21:5-16

Yezebeli alipoona hali ile ya Ahabu akamwambia, "Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ulke chakula moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi" (mstari 7). Ndipo Yezebeli akapanga mpango wa uovu wa kumwaga damu isiyo na hatia ya Nabothi. Akaziandika barua kwa kutumia jina la Ahabu, na kuwaandaa wazee wa mji wawatangazie watu ili kufunga, na wamweke Nabothi mbele ya watu wote. Na wakati hilo linafanyika mashahidi wa uongo watokee na kumshitaki Nabothi kuwa amemkufuru Mungu na kumtukana mfalme, ndipo Nabothi angechukuliwa nje ya mji na kupigwa mawe hadi kifo. Tendo hili la mauaji ya kutisha lilifanyika, naye Yezebelipo alipopata taarifa kwamba Nabothi na wanawe wamekufa (2 Wafalme 9:26), ndipo akamwambia Ahabu, "Inuka utamalaki shamba la mizabibu la Nabothi, maana Nabothi, hayuko hai, lakini amekufa" (mstari 15).

 

Tabia ya udhaifu wa Ahabu na tabia ya ukatili ya mke wake mwovu ni tabia ambazo zimetofautiana waziwazi na haziwezi kupatana kabisa. Ahabu hakuweza hakumjali kabisa maskini Nabothi, mawazo yake yote yalifikiria shamba la mizabibu kuwa sasa ni la kwake, na kwa furaha alikwenda kudai kuwa ni la kwake.

 

ELIYA ANAMLAUMU AHABU – 1 Wafalme 21: 17-24

Mungu hawezi kufichwa jambo lolote (1 Petro 3: 12; Waebrania 4: 13; Zaburi 139: 1-4). Mungu akamwambia Eliya, "Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, ukamwambie, ukisema, BWANA asema hivi, je! Umeua, ukatamalaki ... mahali pale mbwa wa walipoiramba damu ya Nabothi, mbwa watairamba damu yako" (mstari 18, 19). Hivyo Eliya akaenda na kukutana na mfalme Ahabu katika shamba la mizabibu la Nabothi na akamwambia ujumbe wa Mungu. Pia akasema kwamba Mungu ataiangamiza kabisa nyumba yake. Ahabu aliposikia maneno hayo akatambua ukubwa wa uovu alioufanya. Akazirarua nguo zake na kuvaa magunia na kufunga (mstari 27).

 

YEHU ANATUMIWA KULETA MALIPO YA MUNGU YANAYOSTAHILI JUU YA NYUMBA YA AHABU

2 Wafalme 9, 10

 

Ilikuwa Yehu ndiye atumike kuiangamiza kabisa nyumba ya Ahabu. Ahabu aliuawa vitani, na mbwa waklaramba damu yake, sawasawa na jinsi Elivyokuwa ametabiri (1 Wafalme 22:37-38). Yehu alikuwa mtu katili kabisa na alikuwa anajulikana kuwa kichaa na aliendesha gari lake kwa mwendo mkali mno (2 Wafalme 9:20). Yehu kwa hiari alitimiza maagizo ya Mungu (2 Wafalme 10: 30).

Alimwua Yezebeli na kumkanya chini kwa kutumia farasi wake (2 Wafalme 9:31-33). Akawaua wana wa Ahabu 70 (2 Wafalme 10: 7), na akawaangamiza kabisa watu wote wamwabuduo Baari na akaziharibu kabisa sanamu zote (2 Wafalme 10: 18-28). Kwa Yehu akawaua watu wote walisalia wa nyumba ya Ahabu, watu wote waliokuwa wakuu na jamaa zao, na makuhani wake, hadi alipokuwa amewaangamiza wote asisalie hata mmoja (msatari 11).

 

YEHU ANAPIMWA NA ROHO - KUSHINDWA KWAKE - 2 Wafalme 10:29-36

Ingawaje Yehu alitumika kuiangamiza nyumba yote ya Ahabu na wote waliomwabudu Baari, hata hivyo yeye mwenyewe hakuwa mtu ambaye ni mwelekevu. "Lakini Yehu hakuangalia aenende katika sheria ya BWANA Mungu wa Israeli kwa moyo wake wote; hakutoka katika makosa ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli" (mstari 31). Akaibakiza ibada ya sanamu ya ndama iliyoanzishwa na Yeroboamu na kuwakosesha Israeli hata wakaiacha ibada ya kweli ambayo makao yake makuu yalikuwa Yerusalemu.

 

FUNDISHO KWETU

Mtu ambaye ni mcha Mungu anatembea katika Kweli na ndivyo inavyowapasa kutembea watu wote wanaopenda kumpendeza Mungu (Yakobo 1: 5-7). Ahabu aliyumba, ikawa rahisi yeye kuweza kutumiwa na mkewe ambaye alikuwa mwovu na mwabudu sanamu. Ndoa kati ya waamini wa Kweli huepusha uovu huu (Mithali 19:14; Waefeso 5: 25-33). Ndoa ya aina hii huleta uwiano wa kweli kati ya ndugu wanamume na wanawake; kwa maana wanajifunza jinsi ya kila mmoja anavyojitoa dhabihu kwa kujikana mwenyewe kwa ajili ya mwingine, na siyo kama walivyokuwa Ahabu na Yezebeli ambao walitafuta jinsi ya kujifurahisha wao nafsi zao kwa kutumia gharama za watu wengine. Ingawaje waovu huonekana kustawi; lakini hawana mafanikio yao huwa siyo ya milele na wala hawaridhiki (Zaburi 73). Kama tunatafuta makao kwa BWANA kwa njia ya ubatizo katika Bwana Yesu Kristo, ni lazima tutapata dhiki kutokana na waouvu wa ulimwengu huu, lakini mwenendo mzuri utafanyika ambao unakubaliwa na Mungu, ambao ndiyo utakaotuwezesha kustahili kuwa wenyeji wa mji wa Sayuni wakati ujao. Tabia ya BWANA ni kamilifu yenye rehema na haki (Kutoka 34: 6-7; Warumi 11:22). Na kama tukifuata mfano wa Kristo, tutafaidika kwa kupata rehema neema na rehema yake katika utawala wake. Wale wanaoasi njia zake, watapata hasira yake. Fundisho hili hutusaidia kuona msimamo wa Mungu kuhusu dhambi. Havumilii dhambi, ingawaje anawapatia nafasi watenda dhambi ili watubu. Wale wanaokataa rehema yake hakika watapata adhabu haraka na ya haki.

 

MAKTABA REJEA:

Historia ya Biblia (H.R.Mansfield) - Kitabu cha 5; Namba 2-4

Njia ya Mungu ya kutosheleza (R. Roberts) - Sura 20

Mkono wa Mungu unaoonekana (R. Roberts) - Sura 27-30

Eliya Mtishbi (J. Martin) - Sura 7-10

 

MASWALI YA VIFUNGU:

1. Eliya alijifunza kutokana na ile "Sauti ndogo ya utulivu"?

2. Ahabu alikuwa anataka nini na je alipata kwa njia gani?

3. Kwa sababu ya uovu wa Ahabu katika kuchukua shamba la mizabibu ya Nabothi, Mungu alimlaumu kupitia Eliya ... je, hukumu ilikuwa ipi?

4. Ni kwa njia gani Yehu alitimiza hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu?

5. Je, Yehu alikuwa mtu wa aina gani? Ni jinsi gani alivyoshindwa mbele ya Mungu?

 

MASWALI YA INSHA:

1. Je, Ahabu alikuwa anataka nini na Yezebeli alitumia mbinu gani kupata kitu hicho?

2. Je, ni fundisho gani tunalojifunza kutokana na tabia ya Ahabu na namna ya maisha yake?

 

Swahili Title
185 HUKUMU JUU YA NYUMBA YA AHABU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type