188. YONA
Kufuatia utawala wa Yelu, Mfalme wa Israeli, Kiti cha enzi kilikuwa kimekaliwa na Yelwahazi, Yehoazi (alijulikana kama Yoashi pi) na kisha Yeroboam 11. Wakati wa utawala wa yeroboam manabii wame Yona, Isaya, Hosea na Amon ndiyo waliokuwa tabiri kwa ajili ya Taifa. Wakati akijaribu kuwageuza Israeli kuacha njia za uovu, Yona alipigwa na Mungu kuwaonya waashuru watubu na waache uovu wao. Yona alifikiria kuwa kama ikiwa waashuru watatubu watafanikiwa na kusitawi hatimaye watakuwa tishio kubwa kwa usalama wa Israeli watu wake wapendwa. Kwa hiyo, alijaribu kujiepusha kuitii amri ya Mungu, Lkini hatimaye alijifanya kama sisi wote tunavyotakiwa kujifanya kuwa hakuna mtu anaweza kwenda kinyume na kusudi la Munguau kupinga njia za haki ya Mungu. Hukumu ya Mungu huletwa na wasi lakini toba huleta rehema ya Mungu.
YONA 1 - 4
MTU MWENYEWE YONA - Yona 1:1
Yona mwenyewe alikua mwana wa Amitai. Ambaye alitokea Gath-Hefa, Kijiji kidogo katika Galilaya, Kiko umbali yapata maili tatu Kaskazini Mashariki mwa Nazarethi (2 Wafalme 14.25). Alikuwa ni miongoni mwa watu walionyesha kujali sana maisha jamii ya ndugu zake ni ambayo ni tabia inayopaswa utawariwa na kila mfuasi wa kweli wa Mungu. Katika hili, hata hivyo bidii yake ilipita kiasi ya kuwa jail ndugu zake ilipita kiasi sana kwa kujaribu kuwaepusha Israeli na hukumu ya haki ya Mungu.
UJUMBE WA YONA - Yona 1, 2
Ingawaje Israeli walikuwa kwa nje wamefanikiwa lakini kwa ndani hali yao kiroho ya taifa ilikuwa imeshuka sana ingawaje Yona alikuwa akijitahidi sana kuzuia hali hiyo. Ni wakati huu ambao Yona alitumwa kwenda kuhubiri toba kule Ninawi, Mji mkuu a Ufalme wa Ashuru. Alitakiwa awaonye watu kuwa mji huo utapinduliwa kwa muda siku 40 kama hawatatubu kwa ajili ya mji zao mbaya.
YONA ANAMKIMBIA BWANA - Yona 1:3–16
Ingawaje Israeli walimwacha Mungu, lakini waashuru walikuwa waovu zaidi – siyo tu kuwa walikuwa hawamchi Mungu, pia walikuwa na kiburu, washirikina na wakatili mno. Kwa hito Yona hakuona sababu ya kuwa hubiria msamaha na akajaribu kujiepusha na agizo la Mungu kwa kukimbilia Yona na kupanda meli iliyokuwa inakwenda Tarshishi (Mstari 1-3) Labora alifiiri kuwa kama toba ya Ninawi itachelewashwa kwa muda siku 40, basi Mungu atauharibu mji. Hakutambua kuwa rehema ya Mungu kuweza kuongezwa kwa watu wote. Hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kupunguza wema wa Mungu na neema yake (Mathayo 20:15). Ilimpasa Yona kujifunza kuwa Mungu anapenda watu wote wakirie toba, hata kama Israeli walipewa fursa (Upendeleo) maalumu (1 Timotheo 2:4). Wakati meli ilipoanza safari.Yona alikwenda chini ya meli akijilaza. Wakati alipokuwa amesinzia tufani kubwa ya kutupiana ikaanza, hata meli ikawa haribu na kuvunjika kutokana na mawimbi makubwa ya bahari (1: 4) Mabaharia wakatupa baharini shehena ili kupunguza uzito wake (1:5). Nawote wakiwa wamesha kata tama kila mtu akaomba msaada kwa Mungu wake. Lakini wakamkuta Yona bado yeye amesinzia, wakamwamsha ili na yeye amwombe Mungu wake (1:6). Warifikiri kuwa inawezekana kuna mtu ndani ya meli aliyesababisha hayo mabaya yawapate, kwa hiyo walipiga kura, na ikathibitika kuwa Yona ndiye aliye sababisha matatizo hayo (1: 7). Na walipomwuliza Yona (mstari 8) aliwaeleza kuwa yeye ni Mwebrania na anamcha bwana (BWANA), Mungu aliyeziumba bahari na Nchi kavu. Na ya kuwa ndiye atawalaye vitu vyote nay eye ndiye atulizaye mawimbi ya bahari (Zaburi 65:7, 89:9; 107:25-30). Na zaidi ya hayo pia aliwaeleza kuwa ameukimbia uso wa BWANA. Watu wale waliposikia ndipo wakaogopa mno, wakamwuliza wafanye nini ili bahari ipate kutulia (1: 9-10) wakati alipowaambia kuwa wanatakiwa wamtupe baharini, waliogopa sana. Lakini Yona alielewa kuwa tufani ile ilitokea kwa sababu yake, na kwa sababu hiyo alikuwa anajiandaa kuutoa uhai wake dhabihu kwa ajili ya watu wale waliokuwa ndani ya meli. Na kwa njia hii angeweza pia kujiepusha na ujumbe wa kupeleka rehema ya Mungu kwa watu wa Ninawi, na kutokana na kifo chake Israeli wangeweza kupona! Baada ya mabaharia kujitahidi kwa juhudi zao zote ili kuipeleka meli pwani kwa kutumia kasia kushindikana (1:13), ndipo wakaamua kuwa njia pekee ya kuokoa maisha yao ilikuwa ni kutokana na kifo cha Yona, ingawaje hawakutaka kuwa na hatia ya kifo chake (1: 14). Wakishakumtupa Yona baharini ndipo bahari ikatulia (1: 55) na ndipo watu wale walipotambua nguvu za BWANA. Walimtolea dhabihu Mungu wa kweli na wa pekee na kuweka nadhiri ya kumtumikia yeye.
UHAI WA YONA UNATUNZWA - Yona 1:17; 2
Yona alizama haraka sana ndani ya tufani ile ya bahari na vilindi vya bahari vikamfuniak kichwa chake (sura 2: 5), alipokaribia kifo, akamwelezea Mungu mawazo yake na akaweka nadhiri kwamba ikiwa Mungu atamwokoa bari atatenda mapenzi yake (sura 1: 6-9). Samaki mkubwa maalumu ambaye alikuwa ameandaliwa na Mungu, alimmeza. Yona akawa ndani ya ya tumbo la samaki yule kwa muda wa siku 3 mchana na usiku, na kisha samaki yule akamtapika pwani (mstari 10). Akiwa mwenyefuraha nyingi, Yona akatunga au akaandika Zaburi nzuri sana ya kumshukuru Mungu (sura 2). Akiwa amekwisha kata tama kabisa ya kuishi “kutoka ndani ya tumbo la yule samaki (Kiebrania “Sheol”)”. Kaburu alimlilia Mungu naye Mungu, akawaokoa. Hiki “Kifo, mazishi na ufufuo wa Yona” ulikuwa uwe ni mfano ni enacted mfano. Naye Yesu aliuzungumzia mfano huo kuwa ni ishara ya nabii Yona. Kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la Nyangumi hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa Nchi 9 (Mathayo 12:40, Yona 1:17) kwa hiyo kilikuwa kifo cha ajabu sana kuhusu kifo, mazishi na kufufuka kwa Kristo.
YONA ANAHUBIRI NINAWI – Yona 3
Akiwa Pwani, BWANA akasema na Yona mara ya pili usema; Ondoka, uende Ninawi, Mji ule mkubwa ukaihubiri habari nitakayo kuamuru (Mstari 1-2). Wakati huu alitii, na kwenda mji wa Ninawi akaondoka ambao ulikuwa ni mkubwa sana kwa kuwa ilimchukua mwendo wa siku tatu kuweza kuuzunguka mji wote yamkini ni kama Km 100 za mzigo (mzunguko) wake (3:1-3). Akiwa katikati ya mji alipaza sauti yake, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa. (3:4). Akawaambia watu wageuke waache kuabudu miungu na waache uovu wao na wamtumikie BWANA. Ujumbe huu ambao ni wa wazi wazi ulisababisha watu wasadiki na mwitikio wa watu kwa ujumbe huu ukaenea haraka sana na katika sehemu zote za mji watu wote tangu aliye mdogo mpaka mfalme aliyekuwa akitawala katika kiti cha enzi, ambaye alipiga mbiu na akatangaza habari hii katika mji kwa amri ya mfalme akiwaita wau wote ili wafanye toba ya kitaifa na kuyaacha maovu yote na uykatili (3: 6-9). Mungu akaona matendo yao ya tendo akaghairi au akabadilisha kusudi lake dhidi yao akaokoa mji wa Ninawi (3: 10). Mungu anawatendea watu wote kwa namna moja na kuwshughulikia watu wote kwa njia ya namna moja (soma Yeremia 18: 6-10). Wakati mtu anapojiandaa kutubu kutoka katika njia mbaya, rehema ya Mungu inakuwa nyingi zaidi. Lakini mtu anapokataa rehema ya Mungu hukumu ya Mungu kumjilia ghafla, kama vile ilivyowajilia watu wa Ninawi wakati wa Nakumuu nabii.
YONA ANAKATISHWA TAMAA - Yona 4:1-5
Yona alikuwa amehubiri ujumbe wa Mungu kule Ninawi lakini kwa uchungu alikasirika sana na alikatishwa tama na majumuiko ya kazi yake (4:1). Kwa kweli moyo wake ulikuwa kwa Israeli, ambao kwao alikuwa amefanyakazi ya matengenezo kwa bidii sana (4:2). Ndipo akasafiri kutoka magharibi na kwenda upande wa mashariki wa mji wa Ninawi na alipofika nje ya mji akaketi ili kuona matokeo yake ya kuwahubiria watu (4:5). Toba yao ya unyenyekevu ili kuwalete rehema ya Mungu na msamaha, lakini ilisababihsa akasirike sana. Alimlalamikia BWANA, akasema ni heri aje kuliko kuona Ninawi ikiwa imetubu, hii ilikuwa ni sababu iliyomkimbiza kwenda sehemu ya kwanza. Yona alikuwa based kwamba hakuelewa jinsi Mungu angeweza kushughulika na Taifa lingine kwa kuliruhusu Taifa pekee ambalo lilikuwa adui wa Israeli, kwa macho yake Israeli lilikuwa na hali ya pekee kwa rehema ya Mungu. Alitakiwa kuelewa kuwa BWANA aliziumba bahari na nchi kavu (1:9) alikuwa ni Mungu wa Mataifa kama vile alivyokuwa Mungu wa Wayahudi (Warumi 3:29)
YONA ALIJIFUNZA SOMO – MFANO WA MTANGO - Yona 4:6-9
Akiwa nje ya mji, Yona alijifanyia kibanda (kibanda cha muda kilichotengenezwa kwa miti – ni mfano wa vibanda vilivyotengenezwa na Israeli wakati wa sikukuu za vibanda, Mambo ya Wlawi 23:41-44) na akasubiri ili aone jambo litakaloipata Ninawi. Ndipo Mungu akachipusha mtango au mti mkubwa ukaota na kukua kando ya Yona na huu ulimwezesha kupata kivuli cha ziada ambacho alikifurahia kuwa nacho. Lakini usiku mtango ukaliwa na buu na ni Mungu aliye lituma buu lile maalum. Na siku ya pili jua likachomoza na Mungu akaleta upepo wa mashariki nao ukavuma sana. Yona akanung’unika sana kwa ajili ya kuliowa kwa mtango ule ambao uliweza kumpa kivuli wakati ule, akatamani ni heri kuona angekuja. Yona akapatikana tena akiwa amekasirika na akiwa hana toba, Mungu tena akamwuliza, “Je, unafanya vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Yona kwa ukaidi aliendelea kushikilia msimamo wake,” Ndiyo ninafanya vema kukasirika hata kufa. Swali la Mungu linaonyesha kwamba Yona alikosea na alipaswa kubadili mawazo yake. Alikuwa ameleta toba kwa watu wa Ninawi lakini yeye mwenyewe hakuwa mwenye toba linganisha na (1 Wakorintho 9:27). Upumbavu katika nafasi yake unasi yake unathibitishwa mbele yake na kauli ya Mungu ambayo inahitimisha kitabu. “Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja; na mimi je! Hai kuikunipasa kuhubiri Ninawi, nyie ule mkubwa; ambamo ndani yake amo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kumbana katika mkono wa kulia wa mkono wao wa kushoto; tena wamewagawa wa kufungwa wengi sana”. Yona aliwahurumia mimea kuliko wanadamu! Mtu alikuwa ndiye kiumbe wa mwisho katika uumbaji wa Mungu, aliyeumbwa kwa sura ya Mungu wa kwa mfano wake. Yona kwa matokeo haya alikuwa akimhurumu Mungu kwa kumwokoa mtu aliyemwumba! Mtango ambao Yona hakuufanyia kazi, na ambao, tofauti na mtu unaodumu kwa muda mfupi, alipenda sana kuuona huo ukitunzwa fundisho hapa lipo waziwazi. Mungu ni mwokozi wa watu wote. Mungu hapendi mtu yeyote apotee bali wote wangie yeye kwa njia ya toba, kama vile Ninawi walivyofanya, nao wakaishi (1 Timotheo 2:2:4; 2 Petro 3; 9; Ezekieli 23:32).
ISHARA YA NABII YOHA - Mathayo 12: 38 – 41
Wakati mafarisayo walipotaka Yesu athibitisha kwa ishara kama yeye ndiye Masihi wa Israeli aliwajibu, “kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara ila ishara ya nabii Yona” aliendelea kuonyesha nji mbili ambazo Yoha alikuwa ishara kwa kizazi hicho. Mstari 40; siku tatu za Yona mchana na usiku katika tumbo la nyangumi ilikuwa ni ishara ambayo nay eye, pia angekuwa katika moyo wan chi kwa muda kama huo huo soma sehemu, “maisha ya Yona yanahifadhiwa”. Mstari 41; toba ya watu wa Ninawi lilikuwa ni fundisho kwa Israeli ili waweze kutubu pia pia na kumtafuta Mungu katika kweli, kabla hajaleta adhabu kwao (Mathayo 12:41). Kwa kweli Wayahudi walipewa miaka 40 ya kutubu lakini hata hivyo waliendelea kuonyesha kizazi kibaya na cha zinaa na kwa sababu hiyo waliangamizwa mwaka 70 B.K. Walikuwa na ushahidi mwingi sana wa kumwamini Mungu na kumtumikia yeye kuliko watu wa Ninawi.
FUNDISHO KWETU
Hatuwezi kumkimbia Mungu na tukafanikiwa. Ni upumbavu kufirikiri kuwa tunaweza kubadilisha mapenzi ya Mungu; Yona alijaribu, lakini alijikuta katika matatizo makubwa, kwamba “naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuuliza, unafanya nini wewe?” Danieli 4:35. Mungu alimwumba mtu na anataka watu wote watabu. Wala hakuna mtu aliye na haki na kuzuia wingi wa rehema wa mkono wa mungu. Tunatakiwa tuhubiri Neno liokoalo watu wote bila upendeleo wa watu na mwingine (Marko 16:15-16).
MAKTABA REJEA.
Historia ya Biblia (H. P. Mansfield) – Sehemu ya S Kitabu cha 8 Wema na ukali wa Mungu (H. P. Mansfield) ukurasa 2-50.
VIFUNGU VYA MASWALI
-
Ni kwa nini Yona hakutaka kwenda kuhuburi watu wa Ninawi? Na ni jinsi gani alivyojaribu kujiepusha na jukumu hili?
-
Ni jambo gani la kutisha lililompata Yona alipojaribu kunkimbia Mungu na jinsi gani alivyookolewa?
-
Wakati Yona alipohubiri Ninawi, ni nini matokeo yake kwa
-
Watu wa Ninawi na,
-
Yona mwnyewe, wakati alipoona mwitikio wa watu wa Ninawi?
-
Je? Yesu alikuwa ana maanisha nini aliposema “Ishara ya nabii Yona”.
MASWALI YA INSHA
-
Eleza historia ni kwa nini Yona aliyoka kumkimbia Mungu na ilitokea nini wakati Mungu alipomwambia mara ya pili kwenda kuhubiri Ninawi.
-
Fafanua jinsi Yona alivyofundishwa somo kuwa watu wote wanaweza kuokoka na onyesha matumizi ya fundisho hili?