CSSA 2-3-15 - HEZEKIAH—JUDAH'S GREATEST KING

Swahili

190. HEZEKIA-MFALME MKUU KULIKO WAFALME WAOTE WA YUDA

"Mungu ndiye kimbilio na nguvu yetu, msaada uliokaribu wakati wote"

 

Baba yake Hezekia alikuwa Ahazi, ambaye alikuwa mfalme mwovu. Alilifunga Hekalu na akasababisha kuanzishwa kwa ibada ya uovu ya kipagani katika Yuda. Ina burudisha kusoma habari Hezekia. Kama vile Ahazi alivyotenda maovu, hivyo hivyo Hezekia naye akatenda yaliyo ya haki mapachoni pa BWANA. Alifuata mfano wa kiroho wa mmoja wa baba zake, mfalme Daudi hata ikasemwa kuhusu Hezekia kwamba, "akafanya aliyo mema machoni pa BWANA, mfano wa aliyoyatenda Daudi, baba yake" (1 Wafalme 18:3). Pia imeandikwa kuwa "katika kazi aliyoanza kwa utumishi wa nyumba ya Mungu, na kwa torati na kwa amri; ili kumtafuta Mungu wake aliifanya kwa moyo wake wote, akafanikiwa" (2 Mambo ya Nyakati 31 :20-21).

 

2 Mambo ya Nyakati 29-32; 2 Wafalme 18-19

 

KAZI YA KWANZA YA HEZEKIA-KULIFUNGUA HEKALU 2 Mambo ya Nyakati 29: 1-19

Hezekia alikuwa na umri wa miaka 25 alipoanza kutawa na jambo la kwanza alilofanya, katika mwezi wa kwanza wa kutawala kwake kama mfalme, ilikuwa "kuikufungua - milango ya nyumba ya BWANA na kuitengeneza (mstari 3).

 

Lakini kufungua milango tu haikutosha, kwani hilo lisingewaleta watu kwa Mungu. Kwa ajili ya hili walihitajika, kwa hiyo Hezekia akawaoita Walawi pamoja na makuhani ambao ndio waliokuwa walimu wa dini katika Israeli. Aliwaambia wajitakase na waitakase nyumba ya BWANA kwa kuisafisha na kuiandaa ili watu waweze kuabudu. Makuhani wakatii na katika siku ya nane nyumba ilikuwa imetakaswa na katika siku ya 16 kila kitu kilikuwa tayari kwa ibada.

 

HEZEKIA AKATOA SADAKA YA DHAMBI KWA AJILI YA TAIFA - 2 Mambo ya Nyakati 29: 20-36

Hezekia alitambua kuwa taifa zima walikuwa wametenda dhambi, kwa hiyo akakusanya kwanza watawala na kwenda Hekaluni. Hezekia akawaambia watawala na kusanyiko lote la wana wa Israeli washiriki wao wenyewe katika sadaka ya dhambi, ili watambua kuwa walikuwa wametenda dhambi kwa kugeuka na kumwa cha Mungu. Baada ya sadaka ya dhambi (dhabihu ambayo taifa lilikubali kuwa wametenda dhambi mbele ya BWANA). Hezekia akatoa dhabihu ya kuteketezwa kwa moto (mstari 27). Dhabihu ya kuteketezwa kwa moto ilielezea kujikabidhi kwa ukamilifu kabisa kwa Mungu. Wakati dhabihu ya kluteketezwa ilipotekezwa kabisa juu ya madhabahu, Walawi wakaanza kuimba, ikifuatiwa na vyombo vya muziki vilivyotengezwa na mfalme Daudi. Ndipo wote waliokuwepo wakaimarisha vichwa na kuabudu na kwa furaha wakamsifu BWANA. Pamoja na watu kutambua tena kwa mara nyingine jinsi Mungu alivyokuwa mwema kwao na ambavyo angeweza kubariki ikiwa watamtumikia Mungu peke yake, ndipo wakaleta sadaka za shukurani au "dhabihu za hiari" kuonyesha shukurani zao kwa Mungu (mstari 3).

 

HEZEKIA NA WATU WANAISHIKA PASAKA – 2 Mambo ya Nyakati 30:1-22

Sasa ikawa ibada ilikuwa imeanza tena katika Hekalu, sikukuu zingeweza kufanyika, kwa hiyo Hezekia akaamua kwamba pasaka ni lazima itunzwe. Akapeleka barua siyo tu katika Yuda ambayo alikuwa mfalme wake, bali pia alituma barua kwa Israeli. Katika barua hiyo alimwalika kila mmoja kuja Yerusalemu kuishika sikukuu ya Pasaka, bali kwa kuwa siku ya 14 ya mwezi wa Abibu imeshapita (ambayo ndiyo iliyokuwa siku ya kusherehekea Pasaka) waliwajibika kuiweka sherehe katika siku 14 ya mwezi wa pili. Sheria iliruhusu hili litokee chini ya mazingira furahi (Hesabu 9:10-11). Katika barua Hezekia aliwakumbusha watu wote juu ya dhambi zao na nia yao ya kumrudia BWANA. Wangefanya hivyo ndipo BWANA "mwenye neema na rehema" wala hatawageuzia uso wake mbali. Yote haya hutegemea ikiwa wao kwanza watamrudia BWANA (mstari 9).

 

Wengi katika Israeli walicheka, lakini wengine walinyenyekea na wakafika Yerusalemu (mstari 10,11). Katika Yuda Mungu aliwagusa watu kukusanyika pamoja kama mtu mmoja kuishika Pasaka. Wakati wa kuishika Pasaka Israeli walipaswa kuondoa chachu yote ya nchi. Chachu ni ishara ya uharibifu, kwa hiyo watu walifundishwa kuhusu usafi wa moyo na akili katika kumtumikia Mungu. Wakati Israeli walipokusanyika huko Yerusalemu waliona madhabahu ambazo Ahazi alisababisha zijengwa kwa ajili ya kuabudu sanamu na miungu ya mataifa. Ibada hii ya sanamu ilikuwa kama chachu kwa sababu iliharibu (ilisababisha uovu) tabai halisi ya taifa, kwa hiyo kabla ya sherehe kuanza waliziondoa na kuzitupa nje ya mji katika kijito cha Kedroni (mstari 14). Baada ya kumaliza wakasherehekea Pasaka ambayoilifuatiwa na sherehe ya mikate isiyotiwa chachu ambayo ilifanyika kwa furaha kwa muda siku saba (mstari 21). Hezekia akasema maneno ya kuwafurahisha moyo Walawi, nao "wakawafundisha watu elimu nzuri ya BWANA" (Mstari 22).

 

SHEREHE NYINGINE YAWEKWA KWA SABABU YA KUABUDU – 2 Mambo ya Nyakati 30: 23-27

Wakati wa sherehe ya mikate isiyotiwa chachu ilipokuwa imekaribia kumalizika, watu wakakusanyika pamoja. Wakafurahi sana kwa kuwa waliweza kufika pamoja ili kumwabudu BWANA na kufundishwa na Makuhani njia za BWANA. Kila mmoja alifurahi na kuamua kukaa tena siku zingine saba huko Yerusalemu ili kuendelea kumwabudu na kujifunza njia za BWANA. Kwa hiyo "ikawa furaha kuu huko Yerusalemu" (mstari 26). Mungu akapendezwa sana na juhudi zake kwa kuwa imeandikwa ya kuwa "akatenda yaliyo mema na ya adili, na uaminifu mbele za BWANA, Mungu wake ... alifanya kwa uaminifu wake wote na akafanikiwa" (2 Mambo ya Nyakati 30:20-21).

 

JIBU LA YUDA DHIDI YA TISHIO LA ASHURU - Isaya 22

Hezekia alikuwa ametawala kwa muda wa miaka sita na alikuwa amewaongoza watu kwa Mungu. Lakini nguvu kubwa ya jeshi la Ashuru ilikuwa ni kuishambulia Israeli sehemu ya kaskazini, lakini jibu la Hezekia ilikuwa ni kuweka imani yake - siyo katika ulinzi wake bali katika BWANA Mungu wake. Aliondoa kifungo cha Ashuru (2 Wafalme 18: 7). Kisha habari zikaja kutokea Kaskazini kwamba mfalme wa Kasakazini kwamba mfalme wa Ashuru na jeshi lake walikuja kupigana na na mfalme wa Israeli na kuwachua Israeli mateka na kuwatawanya katika dola yao (2 Mambo Wafalme 18:9-12). Miaka michache baadaye, katika mwaka wa 14 wa kutawala kwake, jeshi la Ashuru, wakati wakiwa na mfalme wao Senekarebu, wakapanda ili kupigana na ufalme wa Yuda. Wakaitwaa miji ya Yuda, isipokuwa mji wa Yerusalemu ndiyo uliobakia peke yake. Toke hili lilitokea upande wa kaskazini liliwaweka watu wa Yuda katika mashaka mengi na fadhaa. Baadhi walitaka kukimbilia Misri na wengine waliuamini ulinzi wa Yerusalemu. Lakini walimsahau BWANA "yeye aliyeyafanya hayo, wala kumjali yeye aliyeyatengeneza hayo zamani" (mstari 22: 8-11). Na bado lingine walikuwa tayari kusalimu amri wakisema "tule na tunywe, maana kesho tutakufa" (mstari 12-14). Na wengine walijivunia haki yao wenyewe wakiamini kuwa wao wataokoka bal wengine wataangamia. Na mwishowe walikuwepo wengine kama Eliakimu waliokubaliana na uaminifu wa Hezekia. Hawa waliahidiwa ukombozi, na siyo kutokana na uvamizi wa Ashuru, bali pia kuwa watahesabiwa kati ya watu maarufu sana katika nyumba ya Daudi (mstari 20-25). Je, tunaweza kufikiria jinsi watu wa Yuda na Yerusalemu walivyohamishwa na msukumo waliokuwa nao kwa ajili ya imani ya Hezekia katika BWANA? Hata hivyo Hezekia alielewa kuwa Mungu asipokuwa nao, hawataweza kuokoka kamwe katika kuigana vita nna kulishida jeshi la Ashuru lenye nguvu. Kwa hiyo kwa mara nyingine tena akawakusanya watu pamoja na kwamara nyingne tena akazungumza na watu uso kwa uso. Akawaambia kuwa wawe na "nguvu na ujasiri" maneno yale yale aliyomwambia BWANA alipomwambia Yoshua alipowaongoza Israeli kuingia katika nchi ya ahadi (Yoshua 1:9). Aliendelea kusema kuwa umati uliokuwa pamoja na Israeli, pamoja na jeshi la BWANA ambao ni malaika wa mbinguni kuwa walikuwa wengi sana kuliko jeshi la Ashuru (2 Mambo ya Nyakati 32:6-8; Zaburi 34:7). Hezekia aliweza kuona kuwa vita vilikuwa kati ya mkono wa nguvu wa mwili, ambao mwanadamu huuabudu na kuutegemea, na Mungu wa mbinguni. Kwa maneno haya ya imani, watu wakaelewa kuwa wanalo tegemeo, kwa hiyo "wakajiamini (yakawa nguzo) wenyewe kwa kutegemea maneno ya Hezekia".

 

JESHI LA ASHURU- WAKAFIKA YERUSALEMU – 2 Wafalme 18:37, 39

Jeshi la Ashuru lilipoufikia mji wa Lakishi na wakati walipouhusuru (walipouzingira) mji ule, Senekaribu akapeleka sehemu ya jeshi lake huko kuodhoofisha mji tayari kwa vita. Jeshi hili lilipiga kambi kwenye mambonde yanayozunguka Yerusalemu, na kiongozi wao Rabushake akaanza kwa kupiga mayowe ya kiburi kwamba hata mmoja wa miungu ya nchi waliopigana nao hawakuweza kuziokoa nchi zao kutokana na nguvu kuu za jeshi la Ashuru. Na kwa dhihaka akatamka kwamba miji mingine ya Yuda ilikuwa tayari imeshatekwa na kwa sababu hiyo BWANA asingeuokoa Yerusalemu, kwa hiyo akamlinganisha BWANA, Mungu wa mbingu na nchi kuwa sawa na miungu ya mataifa mengine. Hezekia kwa hekima yake akawakataza watu wake wasimjibu Rabushake hata neno moja (mstari 36). Haikuwa na maana ya kumjibu mpumbave sawasawa na upumbavu wake, na tena isingewatuliza watu kutokana na hatari hiyo. Kufuru ya Rabushake kwa BWANA, ilimhuzunisha sana Hezekia, Hezekia akazirarua nguo zake, akavaa magunia, kisha akaingia ndani ya Nyumba ya BWANA na akaomba (2 Wafalme 19:1). Hezekia alifahamu kuwa kama msaada wa BWANA hautakuwepo basi yasingekuwepo matumaini kabisa. Ni mara ngapi tunaamini kuyatatua matatizo yetu kwa kuzitegemea njia zetu wenyewe badala ya kutafuta njia ya Mungu kwa njia ya maombi. Je, tunaweka tegemeo letu kwa BWANA au "kwenye mkono wa mwili?". Ndipo Neno la Mungu likamjia Isaya naye akamwambia Hezekia kuwa Mungu angesababisha habari kuwafikia Ashuru ambayo ingesababisha Ashuru wayaondoe majeshi yao Yerusalemu na kurudi katika nchi yao. Na hilo likatokea. Jeshi lililokuwa chini ya Rabushake likaondoka Yerusalemu. Hata hivyo jeshi la Ashuru hlikuacha kushambulia mji wa Yerusalemu na mfalme wake.

 

BARUA YA KUMKUFURU BWANA - 2 Wafalme 19: 8-19

Wakati Rabushake aliporudi kwao na kuungana na jeshi lote la Ashuru, alituma barua kwa Hezekia ya kumkufuru BWANA akisema kuwa angerudi na kuuteka Yerusalemu, alionyesha kuwa BWANA asingeweza kuwaokoa, akaandika kuwa "Mungu wenu mnayemwamini, asiwadanganye". Hezekia alihuzunishwa mno na barua hii yenye kufuru, na kwa mara nyingine tena akamgeukia Mungu. Akaipeleka barua ile akaingia ndani ya Nyumba ya Mungu na kuikunjua barua mbele ya BWANA, na kisha akasali akamwomba Mungu msaada ili kwamba falme zote za dunia zipate kufahamu kuwa BWANA peke yake ndiye Mungu. Maombi yenye imani ya Hezekia na maombezi yanafundisho kuu. Akatangaza utukufu na nguvu za BWANA, Mwenyezi kwa mataifa yote. Akamwomba Mungu ili asikie kiburi na dhihaka ya Senekaribu. Imani yake mwenyewe inajieleza na ufahamu wake wa kujua kuwa miungu ya Senekaribu ni "kazi ya mikono ya watu". Na hatimaye Hezekia akamwomba BWANA awalinde watu wake, ili kwamba "falme zote za dunia zipate kujua kuwa wewe ndiwe BWANA, Mungu, wewe peke yako".

 

MUNGU ANAMJIBU HEZEKIA - 2 Wafalme 19: 20-36.

Kwa mara nyingine Neno la Mungu likamjia Isaya na ujumbe wa kumhakikishia Hezekia. Isaya akasema "Basi BWANA asema hivi katika habari ya mfalme wa Ashuru, yeye hataingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa" (mstari 32). Mungu akaendelea kusema, "Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu" (mstari 34). Jinsi yalivyokuwa ya uhakika maneno ya Mungu, maana usiku ule ule malaika wa BWANA alizunguka katika jeshi la Ashuru na kuwaua askari 185,000 kati yao. Na kutokana na adhabu hii ya kudhalilishwa kwa jeshi la Senekaribu, akarudi Ashuru. Habari za ushindi wa BWANA kwa jeshi la Ashuru mara moja zilienea na mataifa yakaleta zawadi kwa BWANA na kwa Hezekia kwa sababu ya mwujiza huu mkuu (Mambo ya Nyakati 32: 23). Na Senekaribu mwenyewe aliuawa na wanaye wakati alipokuwa akiabudu katika Hekalu la Visroki mungu wake (2 Wafalme 19: 36-37). Ni lazima tutambue kuwa wakati huu wa taabu, imani ya Hezekia ilijaribiwa hakika kwa kuwa alipata ugonjwa uliokaribia kumwua (Tazama 2 Wafalme 20:5-6). Lakini BWANA kwa neema yake akamtia nguvu na kumwongezea miaka kumi na tano ya kuishi. Zaburi 46-48 na 120-134 inawezekana ziliandikwa na Hezekia wakati huu wa ukombozi na kuelezwa vyema katika kumbukumbu yake juu ya wema ya Mungu.

 

FUNDISHO KWETU

Tunaona ndani ya mtu huyu Hezekia, tabia zilizokuwa za kumpendeza Mungu. Kwa kuwa katika kumtumikia Mungu, Alitenda hivyo kwa moyo wake wote. Na Mungu anatutaka na sisi tujiweke wakfu kwa ajili ya kumtumikia Mungu, na siyo kwa kutumia sehemu ya muda fulani tu, bali kila wakati. Hezekia, siyo tu kwamba yeye binafsi alimtumikia Mungu bali aliwataia moyo watu wengine katika njia ya Mungu. Tujifunze somo la maisha ya Hezekia ili na sisi tuweze kufurahia ushirikiano na makundi mengine kwa njia ya mammbo yanayopendeza ya ukweli wa Mungu. Wakati matatizo yalipompata Hezekia hakuyumbishwa na kukosa kwa watu wengine imani, akitambua kuwa BWANA peke angeleta ukombozi. Imani yake ilikuwa imara, na alimwomba Mungu bila kukoma kwa ajili ya ukombozi kutokana na mateso yake. Na sisi, vilevile inatupasa kukumbuka kuwa Mungu yupo kila wakati ili kutusaidia katika nyakati zetu za taabu. Mfano wa imani yetu na tumaini letu kwa Mungu itakuwa ni jukumu letu la kuwaimarisha wengine, kama vile alivyofanya Hezekia kwa watu wake walioishi wakati huo.

 

MAKTABA REJEA

Historia ya Biblia (H.P.Mansfield) Kitabu cha 5 Namba 12, ukurasa 188-194

 

Njia za Mu.....

(R.Roberts) ukurasa 179-181

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. (a) Ni jinsi gani Hezekia anavyofafanuliwa katika Biblia?

(b) Ni jambo gani la kwanza alilolifanya alipokuwa baada ya mfalme?

(c) Aliwaagiza makuhani na Walawi wafanye nini?

 

2. Ni jinsi gani Hezekia alivyoandaa Pasaka kutunzwa na watu na watu waliupokeaje ujumbe wake?

3. Wakati mfalme wa Ashuru alipokuja kuipiga Yerusalemu:

(a) Ni jinsi gani Hezekia alivyowaandaa na kuwatuliza moyo watu wakefanya?

(b) Wa Ashuru walisema nini kuhusu Mungu wa Israeli?

4. Eleza maombi ya Hezekia alipopata barua ya Raboshake?

 

MASWALI YA INSHA

1. Eleza kazi ya Hezekia katika kazi ya uamsho wa kurejesha ibada ya BWANA huko Yerusalemu.

2. Fafanua kwa kina mwitikio wa Hezekia aliposikia maneno ya Raboshake na wakati alipopata barua ya Senakaribu. Na jibu la Mungu lilikuwa ni lipi na ni masomo gani tunayojifunza kutokana na msimamo wa Hezekia?

 

MATUKIO YALIYOISHIA KATIKA WAKATI WA KUCHUKULIWA MATEKA KWA YUDA:

 

 

MFALME WA YUDA

Mwaka wa kutawala

KK

MATUKIO

Rejea: ya kuja kwa Kristo

Yosia

Miaka 31

 

 

 

 

 

668-608

 

 

 

8

631

Alimtafuta BWANA

2 Mambo ya Nyakati 34:3

 

12

627

Utakaso wa kwanza

2 Mambo ya Nyakati 34:3

 

13

626

Yeremia anaitwa

Yeremia 1: 1-2; 25:3

 

18

621

Kitabu kinapatikana utakaso wa pili - Pasaka.

2 Wafalme 22:14

 

 

609

(Neko, Mfalme wa Misri 609-593)

 

 

 

608

Vita ya Megido - Kifo cha Yosia. Farao Anapigana na Wamedi na wa Babeli

Yuda wa Syria

 

 

2 Wafalme 23:29

2 Wafalme 23: 29,34

Yosephus. Ant. x.v.i

 

Yehoahazi(Shalumu)

mwana wa 2 wa Yosia

 

608

Anapinduliwa na kuchukuliwa hadi Misri Misri-

 

Yehoyakimu

anawekwa mfalme badala yake mwezi mmoja.

 

608-597

Ngariba inalipwa Misri

Yeremia 27 :1 -11

 

 

 

Yehoyakimu (Eliakimu) kutawaliwa na Babeli kwa bashi

2 Wafalme 23:35-36

Mwana wa 1 wa Yosia 2 Wafalme 24 :1, Mika 11

 

 

605

Nebukadneza aiteka Yerusalemu

Danieli 1:1

 

 

 

Sbambulio la 1 la Wababeli

Yeremia 46:2

 

 

 

Miaka 70 ya utupu (ukame )ya bashi

Yeremia 25:1,11

Mwana(Nebukadneza mfalme wa Babeli

 

605-562

 

 

 

 

604-603

Nebukadneza anaota ndoto mwaka wa 2

Danieli

2:1

 

 

603

Saumu ya umina-Biblia inaunguzwa

Yeremia 36:9,23

 

 

602

Anamwasi mfalme Nebukadneza baada ya

2 Wafalme 24 :1

 

 

 

Makundi ya Wakaldayo baada ya miaka 3.

2Wafalme 24:1

Wamoabi,A, na Amoni wanamtesa Yuda.

 

Mfalme wa Yuda Mwaka wa matukio KK Rejea.

 

Utawala Kuja kwa Kristo

 

Yehoyakimu( Eliyakimu)

 

11

597

Shambulio la 2

2 Mambo ya Nyakati 36:5-7

 

 

 

Babeli, Mji unajisalimisha Yos.Anti x,vi,3

Yehoyakimu anauawa mjini

Yeremia 22:18; 36:30

Yerusalemu mateka 3000 wanachukuliwa

Yehoyakimu (Yekonia ,Konia)

Mwana wa Yehoyakimu

 

597

Shambulio la 3 la Babeli

2 Wafalme 24:10-16

 

 

 

Miezi 3 (mitatu)Yehoyakimu anasalimu amri

Ezekieli 1:2

 

 

 

Na kuchukuliwa mateka

Esta 2:6

Hadi mkusanyika

Mkubwa wa mateka na vyombo.

Pamoja na Ezekieli na Mordekai

 

597-586

(Mattania) mwana wa 3 wa Yosia

Miaka 11 4

 

 

594

Alitawazwa na Nebukadneza

 

 

 

 

Nira,utumwa unatabiriwa

Yeremia 51:29 (P suntinki)

 

 

 

 

 

 

 

593 -588

Shambulio 4 la Babeli

Yeremia 32 :1-2

 

 

 

Psammentinki 11 mfalme

Yerusalemu unahusuriwa miezi 11

2Wafalme 25 :8-9 Wamisri

18

 

 

 

Yeremia anafungwa Anunua

Ezekieli 12 :13

 

 

 

Shamba la Hekalu launguzwa

Zedekia achukuliwa utumwa Yeremia

 

Mwaka wa 19 wa Nebukadneza.

Yeremia 52:12-16,29

 

 

 

 

Swahili Title
190 HEZEKIA-MFALME MKUU KULIKO WAFALME WAOTE WA YUDA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type