191. MSIMAMO WA YOSIA KATIKA KWELI
"Kabla ya huyu hapakuwa na mfalme kabla yake"
Ingawaje Yosia alianzisha uamsho wa kina na wa nguvu, hata hivyo haukugusa mioyo ya watu, watu walifanya kama mfalme alivyoagiza lakini siyo kwa kuwa walimpenda BWANA, bali kwa sababu walimwogopa mfalme wao kijana aliyekuwa na bidii ya kumtafuta BWANA. Ni kutokana na sababu hii uamsho wa Yosia kwa kweli haukuwa na mafanikio.
2 Mambo ya Nyakati 33-35; 2 Wafalme 22-23
YUDA WANAMWACHA MUNGU NA KUABUDU SANAMU
Kifo cha Hezekia kilimleta mwanaye, Manase kwenye kiti cha enzi .Utawala wake wa miaka 55 ulikuwa ndiyo uliokuwa mrefu kuliko wafalme wote katika Yuda, lakini ulikuwa na sifa mbaya kwa kutotenda haki kuliko muda mrefu wa utawala wake (2 Wafalme 21: 11). Alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili na kuendesha kampeni kwa ajili ya ibada ya sanamu, na wema wote wa baba yake alioufanya (2 Wafalme 21:3; 2 Mambo ya Nyakati 33:15). Na chukizo kubwa zaidi kwa Mungu alilolifanya ilikuwa ni mauaji ya halaiki ya maelfu ya watu wasio na hatia "mji wa Yerusalemu aliujaza" kwa damu zao! Na ni lazima izingatiwe kwamba uovu wa utawala wa Manase haukusahaulika, kwa sababu hiyo miaka 50 baadaye jeshi la Babeli walikuja Yerusalemu na kuuteka tena na ni utawala wa Manase uliolaniwa zaidi kuwa ndiyo uliokuwa chanzo cha uvamizi huo (2 Wafalme 24 :3-4). Na katika miaka yake ya mwisho ya utawala wake Manase alitubu na akajaribu kujinyenyekeza na kuacha uharibifu wake aliokuwa ameufanya (2 Mambo ya Nyakati 33:11- 17). Lakini alikuwa amechelewa mno, kwa kuwa mwanaye, Amoni, alipomrithi, alifuata njia zoote za uovu za alioufanya baba yake katika utawala wake. Baada ya miaka miwili Amoni aliuawa katika maasi. Watu wa nchi waliwaua waasi na kumtawaza Yosia, mwana wa Amoni kuwa mfalme badala yake. Kutokana na tukio hili inapendeza sana kusoma habari za Yosia kwa ufupi: "Naye akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA, akaziendea njia za Daudi baba yake, asigeuke kwa kuume, wala kwa kushoto"
MWANZO MWEMA
Alikuwa mtoto wa miaka minane alipoanza kutawala, na alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita "akaanza kumtafuta Mungu wa Daudi, baba yake" (2 Mambo ya Nyakati 34:3). Imani yake ilimsukuma kufanya kazi ya uamsho. Ni jambo gani lililosukuma Yosia kumtafuta Mungu wa baba yake, Daudi, wakati taifa lote lilikuwa limejiharibu kwa kutenda dhambi mbele ya Mungu? Hakuna shaka kwamba mama yake alikuwa na ushawishi mzuri kwake; na jina la mama yake aliitwa Yededia, lenye maana ya "mpendwa". Na pia walikuwepo manabii-Yeremia, Sefania na Hulda aliyekuwa nabii mke. Kutoka kwa watu hawa mfalme huyu kijana alipata maelekezo ya njia ya Mungu. Katika miaka ya ujana wake alijifunza kujibu swali lililoulizwa na mfalme Daudi: "Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako" (Zaburi 119:9). Kwa njia ya maombi na kutafakari Neno hatimaye alikuja kuona uzuri wa njia za Mungu. Na kisha Yosia akatambua jinsi uovu ulivyokuwa ukitendeka kila mahali katika ufalme wake. Hili lilisababisha msukumo mkubwa sana katika akili ya mfalme huyu kijana. Moyo wake ukapata moto kwa ajili ya kuleta uamsho, na akaona umhimu wa kufanya mabadiliko, na kwa hiyo akiwa na umri wa miaka 20 akaanza mabadiliko makubwa sana na matengenezo (2 Mambo ya Nyakati 34:3).
MATENGENEZO YA YOSIA - Wafalme 23: 5-20
Matengenezo ya Yosia yalianza kwa kuwaondoa makuhani waliokuwa wakiabudu sanamu waliojulikana kama "Kemoshi" au makuhani wanaovaa kanzu-nyeusi (Hosea 10: 5 angalia mstari wa pembezoni). Ndipo mfalme akaanza kuteketeza mahali pa juu, vichaka, masanamu na vinyago violivyojengwa katika Yerusalemu na kuzungkka katikaYuda yote. Akayavunja madhabahu ya Baali na kuyasaga masanamu yote kuwa unga. Akaiangusha madhabahu (akaiangamiza) iliyokuwa iliyoitwa Tofethi, mahali ambapo watu waliwatoa watoto wao kama sadakaya kuteketezwa kwa mungu (aliyeitwa) Molek (mstari 10). Alikiwa makini sana, hata ikawa kwamba siyo tu machukizo yaliyowekwa na Amoni na Manase yaliyoondolewa bali hata yaliyokuwa yamesalia tangu enzi ya Ahazi na Selemani. Umahiri wake katika ibada ya Kweli ulimpeleka hadi kwenye miji ya Israeli huko kaskazini. Mapenzi yake kwa BWANA na kwa watu wake ulimfanya aendeleze malengo yake kuelekea kaskazini mpaka huko Naftari. Kamwe hapakuwahi kuepo na jitihada za dhati za kuondoa uovu wa ibada ya vinyago na ushirikina. Yosia, mwenyewe! alisimamia kazi hii, na kazi hii ilipomalizika ndipo aliporudi Yerusalemu (2 Mambo ya Nyakati 32:3: 8).
YOSIA ANATIMIZA UNABII – 2 Wafalme 23: 15-17
Katika safari zake za kutembea katika nchi yote aliisafisha kwa kuondoa ibada za sanamu, Yosia akafika Betheli. Utakumbuka kuwa hapo ndipo Yeroboamu alipoijenga sanamu ya mndama ya dhahabu ili watu waiabudu (1 Wafalme 12: 27-33). Na kwa sababu ya uovu huu aliwakosesha Israeli wakatenda dhambi. Muda mfupi baada ya Yeroboamu kuisimamisha sanamu hii ya ndama ya dhahabu, nabii wa Mungu alikuja Betheli na kumwambia maneno haya Yeroboamu, "Angalia mtoto atazaliwa katika Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako" (1 Wafalme 13: 2). Yosia akaibomoa madhabahu na kupaondoa mahali pa juu, alipokuwa ametengeneza Yroboamu, na akachukua mifupa ya makuhani walioabudu sanamu kutoka katika makaburi na akaiteketeza juu ya madhabahu (2 Wafalme 23: 15-20). Ikawa kwa kufanya hivi Yosia akawa ametimiza unabii ambao ulitabiriwa miaka 360 kabala, na kuonyesha umhimu mkubwa wa mfalme huyu kijana katika malengo ya Mungu katika mwaka wa 18 wa utawala wake, wakati mfalme alipokuwa na miaka 26, aligeukia katika kuanzisha ibada ya kweli. Ujumbe wa watu wanne waaminifu ulitumwa kwa ajili ya kutengeneza nyumba ya Mungu, na gharama ya matengenezo ikitokana na fungu kubwa la fedha ambazo zilichangwa na watu wote wa mataifa mawili; Israeli na Yuda, walipotembelea Hekalu wakati wote wa muda wa matengenezo (2 Mambo Nyakati 34:8-9). Watumishi wenye ujuzi waliitikia kwa moyo wa mfalme na ukaguzi wa fedha haukuwepo kwa kuwa watu hao waliaminiwa (2 Wafalme 22:7). Wakiwa katikati ya matengenezo haya Kitabu cha Sheria ya Musa kikapatikana (2 Mambo ya Nyakati 34:14 angalia mstari wa pembezoni). Shafani, mtu mwenye hekima na mwandishi mwaminifu, akampelekea mfalme kitabu hicho cha thamani. Wakati maneno yake yenye utisho wa hukumu (kwa mfano Kumbukumbu la Tolati 28, Mambo ya Walawi 26) yaliposomwa mbele ya Mfalme, alizilarua nguo zake na kulia kwa huzuni sana. Akajua jinsi watu walivyomwasi BWANA, na akatambua kuwa hukumu ilikuwa imewekwa mbele yao (Mambo ya Nyakati 34:19, 27). Mara moja akamwuliza Hulda nabii mke. Ambaye alidhihirisha kuwa laana zilizoandikwa katika kitabu zingelifikia taifa, lakini kwa sababu ya unyenyekevu wa mfalme mbele za Mungu, hukumu hiyo Mungu angeisogeza mbele. Kwa hiyo uaminifu wa mfalme ulikililinda kizazi katika Yuda. Lakini pamoja na yote haya hawakuitikia kutoka ndani ya mioyo yao. Walimwogopa sana Mfalme kuliko kumwogopa Mungu. Yosia alijaribu kuwalazimisha watu kumpenda Mungu, lakini watu hawakutafuta njia ya kumpenda Mungu na kwa sababu hiyo watu hawakuweza kuwa na upendo wa Mungu ndani ya mioyo yao.
Yeremia alitabiri katikati ya uamusho wa moyo wa Yosia wa matengenezo na kuwakemea kwa matamshi yenye nguvu kwa ajili ya njia zao mbaya. (Yeremia 2:20; 6: 13-19). Alifahamu kukataa kwa watu kwa ajili ya uamusho, Yosia alikaza nia ya kuondoa machukizo yote katika nchi yote ili watu wamwelekee na kumtumikia BWANA (2 Mambo ya Nyakati 34:33). Aliwakusanya wazee kwa pamoja na akasababaisha wafanye agano na BWANA (mstari 29-32). Lakini pamoja na bidii zote za Yosia, watu hawakuguswa kabisa na mambo hayo yote yaliyokuwa yamefanyika, bali matengenezo yalikuwa ya nje tu, hayakufanyika ndani ya mioyo yao. "Na pamoja na hayo yote dada yake, Yuda mwenye hiana, hajanirudia mimi kwa moyo wake wote, bali kwa unafiki asema BWANA" (Yeremia 3: 6-11).
PASAKA ILIYOKUWA KUBWA - Mambo ya Nyakati 35: 1-19
Hitimisho la kazi yake ya matengenezo ilikuwa ni kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Pasaka iliyo kubwa, sikukuu ambayo ilisahauriwa kwa miaka yote mingi ambayo waligeuka wakaacha kumfuata BWANA. Kila kitu kiliandaliwa kwa usahihi-sadaka zilitolewa kwa kufuata Sheria ya Musa, huduma za Makuhani na Walawi katika Hekalu kwa kufuata utaratibu wa maandiko ya Daudi na Sulemani (Mambo ya Nyakati 35: 2-6, 15). Ombi lake mfalme lilileta watu wengi kwenye sherehe kutoka Kaskazini (mstari 17, 18) na kwa amri yake mwenyewe kila kitu kilifanyika kwa uangalifu (mstari 10,16). Na kamwe hapakuwa kuwa na sherehe maalumu ya Pasaka kama hiyo iliyofanyika katika mwaka wa 18 wa mfalme Yosia.
KIFO CHA MFALME YOSIA – 2 Mambo ya Nyakati 35: 20-27
Farao Neko, Mfalme wa Misri, alipita katika Israeli akienda kupigana vita na Ashuru kule Karkemishi ukingoni mwa mto Frati (2 Wafalme 23:29). Kwa upumbavu Yosia (mstari 21, 22) akaenda Megido kupigana na Jeshi la Wamisri, lakini alijeruhiwa vibaya na mpiga upinde na kurejeshwa Yerusalemu. Huko alizikwa kwa maombolezo makubwa na taifa humkumbuka kwa imani yake yab "uamsho" na uhodari wake walihuzunika na kukata tamaa. Miaka mingi baadaye, nabii Zekaria alitumia tukio hili kulielezea uzito wa maombolezo ambayo yatawapata Wayudi, watakapotambua kwamba walimchoma Mwana wa Mungu (Zekaria 12:9-24).
FUNDISHO KWETU
Tukiwa watu tunaofundishwa na walimu waaminifu wa Neno la Mungu, ni mafundisho makubwa ya jinsi gani tunayojifunza na kutokana na maisha na huyu kijana. Akiwa na umri mdogo sana alikuwa amefundishwa njia za Mungu naye akakaza nia yake kutenda yale yaliyokuwa sahihi mbele za Mungu. Alipokuwa na umri wa miaka 16 alisukumwa na ufahamu wake wa upendo wake kwa Mungu kuitakasa Yuda kwa kuondoa miungu na ibada ya sanamu na kwa juhudi kubwa alijitolea nafsi yake katika kazi hii ngumu.Kamwe wewe usitamke kuwa utakuwa na bidii ya kusoma Biblia utapokuwa mzee. Badala yake chukua maisha ya Yosia, kuwa mfano kwa ajili ya maisha yako mwenyewe na kwa juhudi na unyenyekevu wa kusoma kila siku njia za Mungu, naye atabariki juhudi zako ili umtumikie.
MAKTABA REJEA
Mkono wa BWANA
MASWALI YA FUNGU
1. Eleza hatua za kina ambazo Yosia alijaribu kuzifanya kuondoa ibada za sanamu katika nchi.
2. Nijambo gani lilikuwa la muhimu katika matendo ya Yosia pale Betheli penye madhabahu?
3. Ni kitu gani kilipatikana katika Hekalu na kilimgusa vipi Yosia?
MASWALI YA INSHA
1. Eleza tukio la kupatikana kwa nakala ya kitabu cha Torati wakati Yosia alipokua alilitakasa
Hekalu na matukio nyaliyofuata baadaye.
-
Ni mafundisho gani tunayoweza kupata kutokana na maisha ya mwanzo ya kutawala kwa Yosia katika msimamo wake katika Neno la Mungu?