CSSA 2-3-17 - THE PROPHET JEREMIAH — THE KINGDOM OVERTHROWN

Swahili

192. NABII YEREMIA - UFALME UNAANGUSHWA

"Neno lako lilikuwa shangwe kwangu na furaha ya moyo wangu"

 

Maisha ya nabii Yeremia yanadhihirisha mfano wa kushangaza wa uvumilivu unaoendelea katika utendaji-mzuri. Alibeba majukumu makubwa na kuteswa na wapinzani wake wengi wenye nguvu akiwa kijana; na kwa hiyo thawabu nzuri sana inamngoja katika ufalme, pamoja na waaminifu wengine wa Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa njia nyingi huduma yake ilikuwa ni kivuli cha yale aliyoyatenda Bwana Yesu Kristo. Pamoja na jitihada hizi zote alizokuwa nazo na matumaini ya ufalme uliokuwa mbele yake, hatimaye aliweza kutamka kwamba: “Ni vyema mtu autarajie wokovu wa BWANA na kuungojea kwa utulivu. Ni vema mwanadamu aichukue nira yake wakati wa ujana wake." (Maombolezo ya Yeremia 3: 26-27).

 

Yeremia 1, 2 Wafalme 24:25; 2 Mambo ya Nyakati 36; Ezekieli 21:24-27

 

YEREMIA

Huduma ya unabii wa Yeremia ilianza katika mwaka 13 wa Yosia kuendelea kwa miaka 40 hadi ya utawala wa Sedekia mfalme wa mwisho wa Yuda. Kazi ya Yeremia iliendelea wakati wa mabaki waliokuwa wameachwa katika nchi mpaka kufikia muda wa kuondoka kwao kwenda Misri. Yeremia 40:2, 4, 6; 43:7,8. Yeremia alionyesha mfano, imani yenye kustahimili na ya kudumu, na msimamo imara mbele ya wapinzani wake na kuteswa. Wakati huu Yuda walikuwa katika hali ya uovu wa maadili na wenye kutenda mabaya (23:14). Yeremia alikuwa ni kijana mdogo alipoitwa kuwa nabii kwa katika Yeremia 1:6 anajiita "mtoto" (Kiebrania "Naar" inayomaanisha mtoto, mtumishi, kijana mdogo). Kwa hiyo tunao vijana wawili Yosia na Yeremia ambao kwa pamoja walijaribu kuletaa uamsho mkubwa.

 

UJUMBE WA YEREMIA NA TABIA YAKE

Ujumbe wa Yeremia ulikuwa ni kuhubiri ujumbe wa hukumu inayokuja kuwapata watu wa Yuda. Alijaribu kwa njia yoyote iliyowezekana kulizuia taifa lisielekee kwenye hatari. Akiwa mtiifu sana wa BWANA, Yeremia aliteseka sana kwa mambo mengi - alichukuwa na kudharauliwa na watu (Yeremia 12: 6), alipigwa (Yeremia 20: 2), aliyupwa kwenye shimo la matope ya mavi (Yeremia 38: 6), na alifungwa gerezani (Yeremia 38 :13). Lakini licha ya chuki zote hizi ambazo alirudindikiwa juu yake, Yeremia aliwapenda watu wake na ilimsononesha sana kuwaona watu wakiendelea katika dhambi zao. Kwa njia hii inaonyesha tabai ya ajabu inayofanana na ya Bwana Yesu Kristo, kwa mfano anagalia Yeremia 11: 19; Isaya 53: 7; 1 Petro 2: 23. Mtu huyu wa ajabu aliyeomboleza kwa ajili ya watu wake, hakuweka masharti kwa ajili ya ujumbe aliohubiri. Hii ilitokana na upendo wake kwa watu wake hata aliweza kuendeleza juhudi zake za kuwarejesha. Ingawaje Yeremia alipata dhihaka nyingi kutoka kwa wapinzani wake, Upendo wa Yeremia wa Neno la Mungu ulikuwa wa kina kirefu moyoni mwake na usingeweza kuzimwa. Ulikuwa ni kama: "moto uwakao uliofungwa ndani ya mifupa yangy ... nami nimechoka kwa kustahimili" (Yeremia 20:9). Hili hapa ni fundisho kubwa kwa ajili yetu. Wakati kosa linapofanyika, maadili yakawa yameharibika, basi hapo ndipo upendo unataka tusimame katika Neno kama Yeremia na kuisema Kweli.

 

HUKUMU YA MUNGU INAANZA

Kwa ajili ya kifo cha Yosia hukumu za Mungu zililishukia haraka na kwa uzito taifa hili lililokosa. Yosia aliacha wana watatu ambao wote walitawala, lakini wote walifanya maovu mbele ya macho ya BWANA. Mfalme wa Misri alimchukua mfalme wa kwanza Yehoahazi, na akawatoza watu wamlipe kodi. Halafu Nebukadreza, mfalme wa Babeli akawashinda Wamisri naye akamchukua mfalme wa Yehoakimu hadi Babli. Mwana wa Yehoakimu akatawa kwa muda, lakininaye pia alichukuliwa kwenda utumwani hdi Babeli. Hatimaye mwana wa tatu wa Yosia, Zedekia akatawala, lakini yeye naye alilazimishwa kuitii Babeli.

 

YEREMIA ALIENDELEA KUWAONYA WATU - Yeremia 27: 12-22

Hadi kufikia rehema ya BWANA ikawa bayana katika kuwapeleka manabii wake kuwaonya na kuwasisitizia watu wa Yuda. Kwa kuwa Mungu aliwahurumia watu wake na makao yake. Lakini “waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA kwa watu wake, hata kusaiwe na kuponya” (2 Mambo ya Nyakati 36: 15-16). Katika tukio moja, Yeremia alivaa nira ya ubao shingoni mwake na kuwaambia watu kuwa inawapasa kujisalimisha kwa Wakalidayo na kuwa chini ya nira ya Babeli au la wangekufa kwa "upanga, na kwa njaa na kwa tauni" (Yeremia 27: 8). Lakini Hanania nabii wa uongo, akasimama na kuivunja nira iliyokuwa katika shingo la Yeremia na kuwaambia watu kuwa BWANA alimwambia awaambie watu kuwa nguvu ya Babeli ingevunjika hivi karibuni na kuwarudisha mateka wote waliohamishwa! (Yeremia 28: 1-4). Bila shaka watu walitaka kuamini unabii huu badala ya unabii wa Yeremia, ambao kwa kweli ni ujumbe uliotoka kwa BWANA.

 

SEDEKIA MFALME WA MWISHO KATIKA YUDA

Sedekia alipoanza kutawala aliahidi kuwa atakuwa mtii kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Hata hivyo, muda ulipoendelea, manabii wa uwongo wa Yuda walidai kwamba Mungu angeiangamiza Babeli na kwamba na watu wote katika Yuda wangekuwa salama. Sedekia akaziamini taarifa hizi za uongo, badala ya kusikiliza Neno la BWANA alilosema Yeremiaa, na akaamua kuungana na Misri na mataifa mengine yakliyowazunguka kmwasi mfalme wa Babeli. Ilikuwa ni katika kitendo hiki Yeremeia, akaivaa ile nira, kwa kumwonya mfalme kuwa watu wote wangekufa iwapo hawataendelea kuitumikia Babeli. Sedekia akamsikiliza Yeremia naye hakuasi. Hata hivyo miaka kadhaa baadaye, Sedekia alivunja ahadi ahadi yake aliyomwahidi Mfalme wa Babeli (Ezekieli 17). Akafanya mapatano na Misri na kwa wazi wazi akaiasi Babeli, akitumaini kuwa Misri wangekwenda kumsaisadia kupigana vita. Nebukadreza alikasirika sana, na alikwenda haraka na jeshi lake kuelekea Yerusalemu. Na Nebukadreza aliposikia kuwa jeshi la Misri lilikuwa linakuja kuisaidia Yuda, Nebukadreza alipita Yerusalemu kwenda kupigana na Misri kwanza na akawashinda. Na sasa Sedekia alibakia bila ya kuwa na msaada wowote, naye Nebukadreza akarudi na kuuzingira mji wa Yerusalemu.

 

Ndipo ilipofuata miezi 18 ya maisha ya kuitisha kwa watu wa Yerusalemu. Wakati huo jeshi la Babeli lilipokuwa likiudhoofisha ukuta kwa nje, watu ndani ya mji wakateseka kwa njaa na magonjwa, kwa kuwa chakula chao kiliisha haraka. Kwa hiyo unabii wa Yeremia (Yeremia 27:8) ukawa hakika umetimia-walikuwa wamemwasi Babeli nao sasa walikuwa wakifa kwa "upanga, kwa njaa, na kwa tauni". Na kwa mara nyingine tena Sedekia akamwendea Yeremia kwa ajili ya msaada, lakini nabii alipomshauri kuitii amri ya Mfalme wa Nebukadreza, wana wa mfalme wakakasirika wakamtumbukiza Yeremia katika shimo (gereza). Hata Yeremia alipoachiwa alimshauri tena mfalme, kujisalimisha na kulitii jeshi la Babeli kwa kuwa kwa kufanya hivyo angeiokoa nafsi yake mwenyewe na kuuponya mji usiteketezwe (Yeremia 38:17-23). Lakini Sedekia akasita-sita. Alihofia zaidi upendeleo wa wakuu wenzake. Hatimaye askari waliokuwa wamedhoofika hawa kuulinda tena ukuta.

 

Aduii wakavunja ukuta na kuingia ndani na kuanza kuwaangamiza watu, kuuteketeza mji na kulibomoa Hekalu. Hazina zote na samani za Hekalu zikachukuliwa mpaka Babeli (yapata mwaka 586 KK). Mfalme Sedekia akakamatwa na kuburuzwa mbele ya Nebukadreza, na wanawe wakauawa mbele ya macho yake, naye macho yakatobolewa, na akachukuliwa hali amefungwa minyororo mpaka Babeli. Kwa hiyo kwa kugeuka na kumwacha Mungu na kuacha kusikiliza Neno lake, watu hujiletea juu yao hukumu ya kutisha. Majeshi ya Babeli yakamtafuta Yeremia - ili kumtoa gerezani! Wakamtoa gerezani na kumfungua kamba, wakamtunza na hata kumpatia zawadi (Yeremia 39:11-14; 40:1-6). Mfalme Nebukadreza alikuwa ameamrisha akaisema "Mtwae, umtunze sana, wala usimtendee neno baya lolote, lakini umtendee kama atakavyokuambia" (Yeremia 39:12). Jinsi ulinzi wa BWANA ulivyokuwa wa ajabu kwa Yeremia ili kuhakikisha kwamba kazi yake inakamilika.

 

"NITAKIPINDU...HADI ATAKAPOKUJA "

Kuhusu huku kupinduliwa nabii Ezekieli alikuwa amewaonya watu waziwazi na kumwambia mfalme Sedekia, "Ewe mtu mwovu mfalme wa Isreali, ambaye siku yako imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho; BWANA Mungu asema hivi; kiondoe kilemba ivue taji, haya hayatakuwa tena kama ilivyokuwa; kikweze kilicho chini, kakishushe kilichoinuka. Nitakipindua, nitakipindua, nitakipindua, hiki nacho hakitakuwa tena, hata atakapokujaa YEYE AMBAYE NI HAKI YAKE; nami nitampa (Ezekieli 21:24-27). Na hatimaye Ufalme wa Yuda ukafikia maangamizi ya kutisha. Tangu kupinduliwa kwa Sedekia hakutokea tena mfalme alitoka katika ukoo wa Daudi, aliyetawala juu ya ufalme wote wa Israeli. Huyu mmoja "yeye ambaye ni haki yake" ni Bwana Yesu Kristo, ambaye ni Mwana mkuu wa Daudi (2 Samweli 7:12-14) ambaye bado hajarudi na kuitawala dunia akiwa mfalme na kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi.

 

AHADI YA MFALME MPYA NA KUREJESHWA TENA KWA UFALME - Yeremia 23:1-8

Katikati ya unabii kuhusu mnatatizo yatakayowapata Israeli na Yuda, Yeremia alisema ahadi nzuri mno ambayo ilitoka kwa Mungu (Yeremia 23:5-6). Mungu akasema, "Nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima; naye atafanya hukumu na haki katika nchi. Katika siku zake Yuda atakaa ataokolewa Israeli atakaa salama." Ni mfalme mzuri mno wa tofauti jinsi gani huyu, utakuwa ukilinganisha na wafalme wengi waliowahi kutawala vibaya sana juu bya Israeli. Tunamfahamu huyu mfalme aliyeahidiwa ni Bwana Yesu Kristo, kwa maana wakati wa kuzaliwa kwake malaika alisema maneno haya kuhusu yeye "Na BWANA Mungu atampataia kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo (yaani Israeli na Yuda) milele" (Luka 1:32-33). Sisi pia, tunazamia kuja kwa mfalme huyu ambaye siyo keamba atatawala juu ya Israeli yote tu, bali ataleta hukumu na haki katika dunia yote.

 

FUNDISHO KWETU

Yeremia alikuwa mtu wa imani na hodari ambaye alikuwa mkweli kwa Mungu hata kama watu walimchukia kwa ajili ya hilo. Sedekia alikuwa mtu dhaifu, alikuwa mtu asiye na imani, aliyegeuka na kumwacha Mungu na kuvunja neno lake la ahadi kwa Nebukadreza. Na sisi tuwe kama Yeremia na kuwa na imani thabiti kwa Mungu kila wakati. Tunatazamia wakati ambao Mungu atampatia kiti cha enzi "yeye ambaye ni haki yake", ambaye ni Bwana Yesu Kristo. Na tuzizingatie ishara za siku ya kurudi kwake na kama vile Yeremia mtu mwaminifu, tujitayarishe kwa ajili ya siku ile.

 

MAKTABA YA REJEA:

"Unabii wa Yeremia" (C.C.Walker)

"Historia ya Biblia" (H.P.Mansfield) - Kitabu cha 6, Namba 5-6

 

MASWALI YA VIFUNGU:

1. Yeremia alikuwa akitabiri nini alipokuwa amejivika nira shingoni?

2. Ni baadhi ya mambo ambayo yalisababisha Yeremia ateseke katika mikono ya ndugu zake?

3. Ezekieli nabii alisema kuhusu kupinduliwa kwa ufalme wa Yuda (Ezekieli 21:24-27). Alimaanisha nini katika unabii huu?

 

MASWALI YA INSHA:

1. Fafanua maneno ya unabii ambayo Yeremia aliyatamka kwa neno au kwa matendo wakati wa utawala wa Sedekia.

2. Watu wa Yuda walimdhihaki Yeremia na kuyadharau maneno ya Mungu, mpaka hasira ya Mungu ikainuka kwa ajili ya watu wake:-

(a) Fafanua jinsi Mji wa Yerusalemu hatimaye ulivyopinduliwa

(b) Sedekia ndiye alkiyekuwa mfalme wa mwisho kukalia kiti cha enzi cha Yuda - toa uthibiotisho kuwa ufalme utarudishwa tena Yesu Kristo atakaporudi.

Swahili Title
192 NABII YEREMIA - UFALME UNAANGUSHWA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type