CSSA 2-3-22 - NEHEMIAH — MAN OF FAITH AND ACTION "Let us rise up and build"

Swahili

197. NEHEMIA MTA WA IMANI NA MATENDO

"Hebu tusimame na tujenge"

Baada ya kundi la kwanza kurudi chini ya uongozi wa Yoshua na Zerubabeli, palikuwa na makundi mengine zaidi yaliyorudi chini ya Ezra mwandishi. Miaka kumi na mbili baadaye Nehemia alirudi Yerusalemu akiwa mtawala wa Jimbo. Wakazi walikaa pasipo kuwa na mpangilio mzuri wa kujenga nyumba na walikuwa ni walikuwa katika hali ya kukata tamaa. Hali hii ilihitaji mtu mcha Mungu, mwenye imani na matendo ili kuliweka sawa taifa hili dogo na kuwatia moyo watu wake katika hofu ya BWANA. Nehemia akajitolea kuwa ndiye mtu wa aina hiyo. Tutajifunza masomo ya maana kutoka kwake ambayo yanaweza kutusaidia kushinda matatizo yetu.

 

Nehemia 1-6

 

HABARI MBAYA KUTOKA YUDA - Nehemia

Nehemia alikuwa na cheo cha heshima cha mshika - kikombe kwa mfalme Arthashasta, mfalme wa Uajemi. Hanani nduguye, na wengine walikuwa wa kutoka Yuda na Nehermia akawauliza habari kuhusu taifa changa lililoanzishwa. Angalia, ya kwamba hilo ndilo lilikuwa swali lake la kwanza alilowauliza ndugu zake.

 

HABARI MBAYA KUTOKA YUDA - Nehemia

Nehemia alikuwa na cheo cha heshima cha mshika - kikombe kwa mfalme Arthashasta, mfalme wa Uajemi. Hanani nduguye, na wengine walikuwa wa kutoka Yuda na Nehermia akawauliza habari kuhusu taifa changa lililoanzishwa. Angalia, ya kwamba hilo ndilo lilikuwa swali lake la kwanza alilowauliza ndugu zake, ingawaje alikuwa akifanya kazi katika Ikulu huko Shushani, lakini moyo wake ulikuwa Yerusalemu. Alijishughulisha sana kwa ajili ya watu zake kule Yerusalemu, naye alisikitika zaidi alipopata habari, "mabaki ... wako katika mateso makubwa na lawama; ukuta wa Yerusalemu nao umevunjika, na malango yake yamechomwa moto" (mstari 3). Aliposikia maneno haya alikaa na kulia, na kuomboleza kwa muda wa siku nyingi, kipindi chote ambapo alifunga na kumwomba BWANA.

 

SALA YA NEHEMIA - Nehemia 1: 4-11

Baada ya siku nyingi za kufunga na kusali, Nehemia alikuwa tayari kumkaribia BWANA, na kuomba kwa ajili ya kurudi Yerusalemu na watu wake. Akamsihi BWANA kukumbuka agano lake kwa watu wake, na ahadi ya kuwa Sayuni palikuwa ndipo mahali pa utukufu wake. Kwa kumalizi a, Nehemia alimsihi BWANA, kusika sala yake, na ile ya watumishi wake waaminifu "wanatamani kuliogopa Jina lako". Akaitafuta baraka ya Baba kwa ajili yake mwenyewe akiwa mnyweshaji wakati wa kukaribia mbele ya Arthashasta.

 

SALA INAJIBIWA - Nehemia 2:1-8

Miezi minne ilikuwa imepita tangu Nehemia alipopata habari za kusikitisha kutoka kwa Hanani, naye kwa mara nyingine ilikuwa ni zamu yake kushughulika kama mnyweshaji wa mfalme. Alikuwa mwenye huzuni sana na mawazo mengi wakati huo, hatimaye aliposimama mbele ya mfalme. Akitambua badiliko la sura yake, mfalme alimwuliza, kwa nini sura yako ina huzuni, wakati wewe siyo mgonjwa? Hili siyo kitu kingine ila sikitiko la moyo (mstari 2). Nehemia sasa akaogopa na akajibu kuwa sababu ya huzuni yake ilikuwa ukiwa na maangamizo ya mji alioupenda Yerusalemu. Ghafla nafasi ya ajabu ikafunguliwa kwake wakati mfalme alipojibu, "Naye mara moja Nehemia, akitambua njia zote za BWANA (Mithali 3:6), akatamka sala fupi, kimya kimya kwa Mungu wake, ili abariki ombi lake ambalo alikuwa karibu kulimwomba mfalme, na ampatie kibali machoni pa mfalme. Nehemia akaomba ruhusa ili kwenda Yuda kujenga upya Yerusalemu, sala yake ilijibiwa kwa jinsi ya ajabu. Mfalme akamkubalia ombi lake na kumwekea muda wa kurudi Uajemi (mstari 6). Nehemia akaomba kibali kwa ajili ya usalama wake na kumruhusu kupata mbao katika msitu wa mfalme (mstari 7, 8). Akawa mtu wa sala na matendo. Nehemia akatambua kuwa "mfalme alinipa kibali kutokana na mkono mwema wa Mungu wangu juu yangu" (mstari 8). Nehemia akiwa na uhakikisho ule, akakaza moyo kuwasaidia ndugu zake kule Yerusalemu. Mtume Paulo anaeleza msingi kwa ajili ya shauku kuwa "kama Mungu yu pamoja nami, ni nani anaweza kuwa kinyume chetu?” (Warumi 8: 31-39).

 

NEHEMIA ANAFIKA YERUSALEMU - Nehemia 2: 9-18

Akiwa anajilinda na kujihami kwa ajili ya askari wa Uajemi, mara moja akanza safari yake ndefu kwenda mji wake alioupenda. Baada ya kufika alitoa vitambulisho vyake kwa watawala waliomzunguka , lakini alipokelewa kwa chuki na ukaidi na maadui wa Wayahudi wakithibitisha chuki na upinzani wao (mstari 10). Afadhari Hekalu lilikuwa limejengwa, haukuwepo ukuta wa kuuzunguka mji, na kwa ajilki ya hiyo wale walioishi ndani ya mji walikuwa rahisi kwa ajili ya ushawishi wowote wa maadui na hatari. Akangojea siku tatu ili aweze kutafakari kazi ya kujenga upya iliyokwa mbele yake. Ndipo, usiku mmoja, akiwa pamoja na wenzake waaminifu, hali akiwa amepanda mnyama wake, alikagua hali ya kuta za mji wake, aupendao. Hata ingawa kuta zake zilikuwa zimevunjika, lakini aliupenda mji, ambamo historia ya zamani ilijionyesha - lakini ukuta ulivunjika na malango yake yaligeuka meusi kwa ajili ya moto. Maeneo yalizungukwa na vifusi vikubwa vya matofari yaliyovunjika, hata ikawa mnyama aliyempanda hakuweza kupita na wala hakupata njia ya kuendelea na safari. Ndipo aliporudi kwa Wayahudi lakini hakutamka neno lolote kuhusu safari hiyo ya ukaguzi mpaka walipokuwa tayari kulipokea. Siku chache baadaye, aliwakusanya watawala wa Wayahudi pamoja na kwa uangalifu kuwafafanulkia hali ya kusikitisha ya mji ulioharibika na aibu ambayo waliyoipata kutokana na hali hiyo kutoka machoni pa wana - wa mataifa yaliyowazunguka (mstari 17). Akajihusisha yeye mwenyewe na matatizo yao yaliyowapata "mnaona dhiki tuliyomo". Akawafurahisha kwa kueleza mkono mwema wa Mungu ulio juu yake na baraka za mfalme wa Uajemi, hata ikawa alipomaliza maelezo yake, watu wote kwa pamoja na kwa moyo wakatamka "Hebu na tusimame kujenga" (mstari 18).

 

NEHEMIA ANAJIBU CHANGAMOTO ZILIZOTOKA KWA WAPINZANI - Nehemia 2: 19-20

Shauku ya Nehemia iliwavuvia watu na wakawa na ari ya kufanya kazi, lakini ilisababisha mapokezi mabaya kutoka kwa maadui zao. Haikuchukua muda mrefu kabla ya wao kufika kwenye eneo kuwacheka kwa dharau watu waliokuwa wanafanya kazi, wakatia fikira kuwa walikuwa wakipanga maasi kwa ajili ya mfalme (Nehemia 2:19). Walakini Nehemia kiongozi mkuu kweli kweli, aliweza kuikabili changmoto hii kwa tamko muhimu la ukweli ambalo liliwanyamazisha maadui zake, "yule Mungu wa mbinguni, Atatufanikisha, kwa hiyo sisi watumishi wake tutasimama na kujenga, lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu katika Yerusalemu" (mstari 20).

 

UJENZI MPYA UNAANZA UKIFUATIWA NA UPINZANI ZAIDI - Nehemia 3:4

Maneno yakafanyika kuwa matendo hapo Nehemia alipowaongoza watu wote katika kazi za kuzijenga upya kuta (angalia mchoro wa Yerusalemu katika ukurasa unaofuata). Vikundi vya familia vilifanya kazi pamoja kama vile ilivyokuwa kwa madaraja yote; Makuhani, Walawi, Watumishi, Wafanya biashara, wachanganyao manukato, watawala, wanawake, na wafanya biashara za baharini. Wengi walishughulika katika sehemu ambazoo walikuwa na maslahi zao maalumu. Watu waliowazunguka waliutazama kwa hila ujenzi mpya wa kuta za Yerusalemu. Kiongozi wao alikuwa Sanbalati ambaye alikuwa pamoja na "jeshi la Samaria" (Nehemia 4:2). Yeye na Tobia, Mwamoni waliwachochea kwakusema "Hata hicho wanachokijenga, kama mbweha atapanda juu yake atayabomoa mawe ya ukuta wao" (mstari 3). Alipoyasikia maneno yao ya kutia uchungu pamoja na dharau, Nehemia akautafuta msaada kwa Mungu wake kwa njia ya sala, kuw angewalaani na kutowasamehe dhambi yao kwa kuwa walileta aibu juu ya Mungumbele ya watu wake. Kwa hiyo watu wakatiwa nia "na kuwa na akili ya kazi" (au kuwa na bidii ya kazi) (mstari 13), nao wakaumaliza ukuta uliozunguka mji hadi kufikia nusu ya urefu (kimo) cha mwanzoni. Sasa adui zao wakakasilika "na kujikusanya na kukubaliana kwa pamoja kuja kupigana dhidi ya Yerusalemu, na kuizuia" (Nehemia 4:8), kwa mara nyingine tena, Nehemia akamgeukia Mungu katika sala na kisha akaweka walinzi juu ya kuta mchana na usiku. Lakini sasa matatizo yalidhihirika miongoni mwao wao wenyewe. Baadhi ya watu wa Yuda walikatishwa tamaa, walichoka na kuogopa, na kwasababu hiyo hawakuweza kujenga ukuta. Kunung`unika, kama vile ilivyo ari, kunaambukiza. Uvumi ukaanza kuenea kuhusu shambulio ambalo lilikusudiwa. Nehemia alipoyaona majeshi ya Sanabalati yakiwa yamezunguka mji na yakiwa karibu kushambulia, akawasihi watu kumkumbuka BWANA na kupigana kwa ajili ya koo zao na nyumba zao. Kwa kuona tendo hili la kutojali. Maadui waliondoka kwa sababu "Mungu aliya sambaratisha mashauri yao" (mstari 15). Na kwa hiyo watu wakarudi kazini kwao juu ya kuta. Ndipo Nehemia akafanya mpango ili kwamba nusu ya wale waliokuja naye kutoka Uajemi wasimame juu ya zamu za ulinzi, na nusu nyingine waendelee na kazi ya kujenga upya kuta. Kwa nyongeza, kila Myahudi mtumishi aweke siraha yake karibu-karibu, ili kwamba wakati baragumu itakapolia, mara moja kila mmoja angeweka chini vyombo vya ujenzi na kuchukua siraha yake na kwenda kukusanyikia sehemu ya uvamizi. Na Nehemia mwenyewe alikuwa na yeye ndiye mlinzi mkuu juu ya kuta za mji, na pamoja naye alifuatana na mpiga tarumbeta ili kutoa ishara. Pia aliwafundisha watu kuwa iliwapasa wakae ndani ya Yeresalemu nyakati za usiku, na wasirudi katika vijiji vyao kama vile walivyokuwa wakifanya kabla. Nehemia akaweka mfano wa ajabu wa uthibiti kazini kwa kuwa yeye na watu aliokuwa pamoja nao hawakupumzika kamwe, hata hawakuweza kubadilisha nguo-walifanya hivyo hata wakati wa kuchukua siraha zao wakati walipoenda kupata mahitaji yao ya maji ya kila siku (mstari 23 pembezoni). Kila wakati walikuwepo penye kituo chao, kila wakati walishughulika na kazi ya ukuta au wakisimama kulinda ili kujilinda dhidi ya maadui.

 

JARIBIO LA MWISHO LA ADUI LASHINDWA - Nehemia 6

Adui walikuwa wameshindwa katika majaribio yao yote ya kusimamisha kazi ya ujenzi na kwa hiyo wakabadilisha mbinu na wakafanya ujanja. Na mbinu nyingine walifahamu kuwa Nehemia alikuwa kiongozi hodari sana ambaye angewahamasisha na kuwaimarisha wafanya kazi na kwa hiyo wakapanga kumwangamiza. Wakamwomba akutane nao, lakini haraka aligundua nia yao, naye akawajibu (kwa majibu mazuri kwa yeyote ambaye angeingilia kazi ya Mungu), "Ninatenda kazi kubwa, hivi kwamba siwezi kuja huko chini, kwa nini kazi isimame wakati nikiiacha, na kuja kwenu?” (Nehemia 6:3). Walimwomba mara nne, na kila wakati aliwapatia jibu hilo hilo (Nehemia 3). Ombi la mwisho la Sanbalati lilikuja katika muundo wa barua "kwamba ilikuwa ikienezwa pote kwamba ukuta ulikuwa ukijengwa kwa makusudi ya uasi, na kuwa Nehemia alikuwa akiazimia kujiteua kuwa mfalme. Kwa mara nyingine tena Nehemia alitambua kuwa hii ilikuwa mbinu ya kumwangamiza naye akajibu; "Hakuna vitu kama hivyo vinavyofanyika kama unavyobuni kutoka moyoni mwako wewe mwenyewe" (mstari 8). Hatimaye wakaazimia kumwondolea heshima yake kwa kumwonyesha kila mmoja kuwa alikuwa mwoga mwenye hofu. Wakamwambia sheria ya kukutana na Nehemia Hekaluni wakati milango imefungwa, akisema kuwa adui zake walikuwa tayari kumwua usiku ule. Lakini kwa kuwa hakuwa mwoga, watu waliimarika, na kwa hiyo ilikuwa muhimu kwa kuwa hakushindwa na ombi hili. Hivyo akajibu, Mtu kama mimi, nikimbie? ...Sitaingia ndani" (mstari 11).

 

HATIMAYE UKUTA UKAMALIZIKA - Nehemia 6:15-16

Licha ya vikwazo,matatizo (dhiki); mashambulizi, vitisho, hila, na upinzani, ukuta ulimalizika kwa muda mfupi sana kwa siku 52, Sanbalati na rafiki zake walishindwa kwa kila hila na maadui wa Wayahudi waliziona kuta zilizomalizika za Yerusalemu. Kwa hisia za kukata tamaa, nao wakawa na huzuni sana. Walilazimika kutambua kuwa kazi ilifanyika kwa uwezo wa Mungu wa Nehemia. Kwa hakika Nehemia aliweza kutafakari juu ya maneno ya Zaburi 34:19 "Ni mengi mateso ya mwenye haki; lakini BWANA anamwokoa kutokana nayo yote".

 

FUNDISHO KWETU

Nehemia alikuwa na upendo mkuu kwa Yerusalemu na hamu ya dhati ya kurudi Yuda, na kwa hiyo kwa neema ya BWANA akamjibu maombi yake huko Shushani katika Ikulu. Akiwa kiongozi shupavu, hakukosa kukabiliwa na matatizo, lakini alidumu katika kumtafuta msaada wa BWANA nyakati za shida pamoja na kuendelea kufanya kazi na watu. Alikuwa ni mtu wa sala na MATENDO - imani yake ilidhihirika kuwa matendo yake. Inatupasa na sisi tufanye hivyo hivyo leo katika maisha yetu kwa kuwa matendo kwa matendo ya imani tutaamriwa. Ari na kufa moyo vyote huambukiza sana. Tunaweza kuwavuvia wengine katika utumishi wa Bwana ikiwa tutakuwa makini na kujitoa wenyewe. Sisi kama Nehemia, inatupasa tuyafahamu udanganyifu wa wapinzani wanaotuzunguka, na kuutafuta msaada na ulinzi wa BWANA huku tukiendelea kutenda sawasawa na mapenzi yake.

 

MAKTABA YA REJEA

"Historia ya Biblia" (H.P Mansfield) - Kitabu cha 7, Namba 6, 7.

"Nehemia" (R. Abel) - C.S.S.S. Maelezo

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. Ni jinsi gani sala ya Nehemia ya kurudi Yerusalemu ilivyojibiwa?

2. Ni upi ulikuwa mpango wa Nehemia wa kuwalinda wafanyakazi kutokana na mashambulizi wakati wa kujenga upya kuta za Yerusalemu?

 

MASWALI YA INSHA

1. Fafanua matukio yaliyomfanya Nehemia asafiri kwenda Yerusalemu, ukizingatia hisia yake kwa ajili ya mji ule.

2. Eleza jinsi Nehemia alivyoyatatua matatizo yaliyomkabili katika kuujenga upya mji.

3. Tunaweza kupata mafundisho gani kutokana na mfano wa Nehemia aliyekuwa:

(a) mtu wa sala?

(b) mtu wa matendo?

 

Swahili Title
197 NEHEMIA MTA WA IMANI NA MATENDO
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type