198. NABII MALAKI
"Ni nani awezaye kuikabili siku ya kuja kwake?"
Kazi ya kufanya upya Hekalu ilitiwa nguvu na manabii Hagai na Zekaria. Nehemia alikuwa ameazimia kujenga upya ukuta. Alikuwa ameishi Yerusalemu kwa miaka 12 (kumi na mbili) na kisha akarudi kwa Arthashasta (Nehemia 13:6). Alipokuwa mbali nguvu za kiroho zilipungua naye aliporudi akaanza mlolongo (mfululizo) wa masahihisho (mageuzi) (Nehemia 13). Matatizo ambayo ilibidi akabiliane nayo ni yale yale yaliyotajwa katika unabii wa Malaki, kwa hiyo ni jambo la kawaida kutarajia kuwa Malaki alitabiri kipindi hiki.
Malaki 1-4
UTARATIBU WA MAANDIKO YA MALAKI
Katika unabii huu kuna kuna aina ya kufurahisha ya maandiko ya nabii Malaki, wakati akijaribu kuwaamsha watu wake kuhusu wajibu wao. Nabii kwanza alisema tamko ambalo lilinung`unikiwa na watu. Ndipo Nabii akaendelea kubainisha dhambi zao.
KWA MFANO
1. Tamko la nabii: "Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humheshimu Bwana wake; iko basi Mimi ndiye Baba, ipo wapi heshima yangu? Na iwapo Mimi ni Bwana, iko wapi hofu yangu anasema BWANA wa Majeshi kwenu" (Malaki 1:6). Manung`uniko ya watu: "Ni kwa vipi tumelidharau Jina lako?"
2. Nabii anasema wazi dhambi yao: "Mnatoa mkate uliotiwa unajisi (ulioharibika) kwenye madhabahu yangu..." (mstari 7).
Yapo masawali na majibu nane ya aina hii hii. Soma unabii huu wote na utambue yote yaliyopo na hili litasaidia ufahamu wako. Nabii ilimbidi kutumia njia hii ya usemi kwa sababu iliwaelezea wazi Israeli dhambi zao. Kama Laodokia, "hawakujua" ya kuwa walikuwa "fukara na wanyonge, na wasiojiweza, na vipofu, na uchi" (Ufunuo 3:17). Siyo tu kwamba walikuwa wamezama katika ndani ya msimamo na matendo maovu kama vipofu, lakini pia walijifanya kuwa wenye haki. Dhambi hudanganya, na ni kwa kujichunguza wenyewe mara kwa mara kuhusiana na haki ya Mungu na ukosefu wetu kama Neno la Mungu linavyoonyesha ambapo litatuwezesha kukwepa kuangukia ndani ya mtego ule ule.
"MTUMISHI MJUMBE WANGU"
Jina Malaki linamaanisha "Mtumishi wangu" (au Mjumbe wangu). Anawakilisha sauti ya BWANA kwa Israeli; na kwa kadri alivyowaonya watu, alisema juu ya Mjumbe wa pili angekuja - ambaye ni Bwana Yesu Kristo (Malaki 3: 13; 4:16).
MANENO YA HUKUMU NA SIFA
Siyo maneno yote ya nabii huyu kuwa yalikuwa ya hukumu na maonyo. Yalikuwemo ndani ya Israeli wakati huu ambao hawakufuata matendo maovu na ni uovu ambao ndiyo ilikuwa njia ya wengi. Hawa wachache wachache wangekutana pamoja kila mara kuzungumza "mmoja na mwingine" kuhusiana na mambo ya BWANA na kujiimarisha katika tumaini tukufu lililowekwa mbele yao (Malaki 3:16). Lakini walikuwapo watu ambao walisema "ni ubatili kumtumikia Mungu". Walikuwa ni watu wasioridhika na imani yao ilidhoofika kwa sababu hiyo. Kwa upande wao ilionekana kuwa ni watu wenye majigambo na wao walikuwa wenye furaha wakatii wnye haki ndio walionekana wenye huzuni. Kwamba waovu walionekana kuwa wenye mafanikio, na ambapo wale wenye haki walikuwa katika umasikini (Malaki 3:14-15). Lakini Malaki alikuwa mwepesi wa kuwakumbusha kuwa ipo siku inakuja wakati wale wote wanaomjaribu Mungu watakatiliwa mbali, bali wenye wataokoka (Malaki 4:1-2).
MALAKI ANAONYA-NEHEMIA ANATENDA - Malaki na Nehemia 13:7-31
Ujumbe wa Malaki ulisikika na malalamiko na maonyo kabla Nehemia hajaonekana kwenye eneo na kufanya kwa nguvu zaidi matendo ya mabadiliko. Angalia ulinganisho kati ya maneno ya Malaki na njia ambayo Nehemia alitenda:
1. Ndoa na watu wasio katika Kweli
2. Ufisadi juu ya agano uliofanywa na Walawi
3. Sheria za zaka kusahaulika
NDOA NA WATU WASIO KATIKA KWELI - Malaki 2:10-16
Kwa ajili ya kumheshimu ilitamkwa "... Hamtafanya ndoa nao... Kwani watawageuza wana wenu katika kunifuata, ili watumikie miungu mingine..." (Kumbukumbu la torati 7:3-4; Yoshua 23:12-13). Kulikuwa na mifano mingi ya hatari ya kushindwa kutokana na ndoa zilizofanywa na watu wasio katika kweli ili kukubaliana na onyo la nabii. Mfano mmoja ulio wazi ni ule wa mfalme Sulemani (somo la 7). Katika siku za Malaki wengi waliwaacha wake zao wa Kiyahudi nakuoa wanawake wageni (wasiokuwa wana wa Israeli). Mungu mwenye upendo na mwenye huruma alisikitishwa na huzuni ya wanawake hao Wayahudi, ambao walifika na kulia kwenye madhabahu yake. Na kwa hiyo akasema na wale wanaume wakatili ya kwamba wasipoonyesha upendo na upole (wema) kwa wake zao, asingepokea dhabihu zao (Malaki 2:11-17). Malaki anatamka waziwazi msimamo wa Mungu kuhusu talaka (kuacha mke) (au kuvunja ndoa). "Analichukia !” (mstari 2:16).
Katika siku za Malaki, hata makuhani walikuwa wamevunja sheria hii. Kulikuwepo ndoa nyingi za mchanganyiko hata ikawa watoto waliozaliwa katika aina hii ya ndoa hawakuweza kuzungumza lugha ya sheria na matokeo yake hawakuifurahia kweli (Nehemia 13:24). Wale watoto amabo walikuwa "uzao wa Mungu" walikuwa wamechanganyikiwa katika ufahamu wao wa kiroho hata wakawa katika hatari ya kufanyika kama Wasamaria (linganisha 2 Wafalme 17:33-41).
UFISADI WA AGANO UNAFANYWA NA WALAWI - Malaki 2:1-9
Ukuhani unashughulikiwa moja kwa moja - "Nanyi ee makuhani, agano hili ni kwa ajili yenu". Mungu alitishia kuzigeuza baraka za makuhani kuwa laana kama wasingesikiliza maneno yake (Malaki 2:2). Mungu aliwakumbusha (hususani Walawi) kuhusu jinsi alivyowachangua wao kuheshimiwa kwa ajili ya ukuhani na kwa njia yamzunguko akataja matukio mawili yaliyoleta uchaguzi huu (mstari 5-6).
(a) Pale Sinai walipo "mwogopa" na kukataa kuiabudu ndama ya dhahabu (Kutoka 32:26-29).
(b) Pale Shitimu wakati Finehasi alipogeuka kinyume cha mwenendo wa Israeli kule Baali-peori na kupokea agano la amani na ukuhani wa milele (Hesabu 25: 12-13).
Wakiwa wao ni mdomo wa Mungu walikuwa wamewafundisha wengi, lakini kwa sababu sasa "walikuwa wamekwenda njia ya kando, walisababisha watu wengi kujikwaza katika sheria" na kuliharibu agano la Lawi" (Malaki 2:8). Vizazi vilivyofuata vilishindwa kuzingatia mafundisho ya mababu zao. Kuna haja kubwa kwa watoto wa wazazi wa Wakristadelfia ili kuthamini urithi wa kweli; kwa bahati ya kuona kuwa ni bahati ya thamani kuujua ukweli na kudhamiria kuidumisha kweli isiangukie katika uharibifu (soma Zaburi 78:1-8).
UHARIBIFU WA UKUHANI - Malaki 3:8-18
Nehemia alipotoka Babeli, aliona kwamba Eliashibu, kuhani mkuu alikuwa na urafik na Tobia na kuwa alikuwa amempa mahali pa kulala kwenye nyumba ya Mungu (soma Nehemia 4:3). Pia akafahamu kuwa mmoja wa wana wa Eliashibu alikuwa amemwoa binti Sanbalati (Nehemia sura 4). Kwa hakika, ikiwa kulikuwepo uharibifu katika ngazi za juu za ukuhani, kwa hiyo ilikuwa ni lazima kwamba jambo hili lingewahusu hata makuhani wengine, kiasi kwamba utekelezaji wa sheria haikutekelezwa. Fungu la kumi (zaka) haikutolewa kwa walawi (Nehemia 13:10; Malaki 3:8).
Kufanya biashara, iliruhusiwa siku ya sabato (Nehemia 13:15-22) na ndoa na watu wasiokuwa Wayahudi hazikuwa tatizo (Nehemia 13:23-30; Malaki 2:10-16). Katika mambo yote walitakiwa kuitii sheria, mfano wao mbaya ulikuwa umewageuza watu wengi wakaacha kumtumikia BWANA (Malaki 2:8).
HUKUMU INAYOKUJA - Malaki 2:17-13; 4:3
Watu wakaona kuwa hukumu ya Mungu haikuwajili watu wale waliotenda maovu, kwa hiyo walifikiri kuwa bidii zao zote za kutenda haki hazikuwa na maana. Ilionekana kana kwamba wale waliomjaribu Mungu waliokolewa kutoka katika maovu na ambapo watu walionyenyekea mbele za Mungu walionekana kuendelea kuteseka (Malaki 3:15). Hata walifikia kuuliza, kama kweli alikuwepo Mungu wa haki "Yuko wapi yule Mungu wa hukumu?" (Malaki 2:17), walisema. Ingawaje Mungu hakuleta hukumu juu ya watu waliotenda maovu wakati wa nabii Malaki, hii haina maana kwamba alikuwa ameicha hukumu. Kusudi lake linahusu siku ambayo wenye haki na waovu watashughulikiwa kulingana matendo yao jinsi yalivyokuwa kwa mjumbe wa agano (Malaki 3:1), ambaye ni Bwana Yesu Kristo. Jambo muhimu ambalo hawa watu wa nyakati za Malaki iliwapasa kujiuliza wao wenyewe ilikuwa, wako tayari kwa ajili yake "Lakini, nani watasimama siku ya kuja kwake?" Ndani yake (Bwana Yesu Kristo) BWANA "atakuja karibu na hukumu na kuwa shahidi mwepesi" kwa wale waliotenda maovu (Malaki 3:5).
Kwa kulinganisha na wale waliotenda maovu, walikuwepo watu wenye haki, wale "ambao walimwogopa BWANA na kuzungumza pamoja mmoja na mwenzake kuhusu Kweli” (Malaki 3:16). Majina yao yameandikwa katika "kitabu cha kumbukumbu" nao katika hukumu siku ya mwisho watapewa uzima wa milele. Nao wakuwa wangu asema BWANA, Mungu wa majeshi, “katika siku ile nitakapofanya johari zangu" (Malaki 3:17). Mungu amewaahidi kuwafanya hazina maalumu katika siku ambayo Kristo atarudi.
KATIKATI YA MALAKI NA MATHAYO
Malaki alipokufa, sauti ya manabii haikusikika tena kwa karibu miaka mia nne, kwa hiyo ikathibitisha maneno nabii Mika aliyesema kuwa kwa sababu ya maovu yanayoendelea "hawatakuwa na maono" (Mika 3:6). Wakati wa kipindi hiki hisoria ifuatayo ikatokea: waajemi walishindwa (walitekwa) na Wayunani Uasi wa Wayahudi, ulioongozwa na Wakabayo. Yuda Makabayo mnamo mwaka 165 K.K (Kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo) aliuteka Yerusalemu akalitasa akasafisha) Hekalu, na kuliweka tena wakfu. Warumi waliingia katika Palestina mwaka 66 K.K - wakiongozwa na Jenerali Pompey. Wapathani waliuchukua Yerusalemu na kumweka Mmakabayo kwenye kiti cha enzi Yerusalemu na kufanywa kuwa "mfalme wa Wayahudi" ndiye aliyekuwa mtawala wa kutisha aliweka amri ya kuwaua watoto wachanga wa Bethlehemu wakati Yesu Kristo alipozaliwa. Herode alipokufa Yesu na wazazi wake walirudi kutoka Misri (Mathayo 2:1,16-23).
FUNDISHO KWA AJILI YETU
Malaki aliwashutumu makuhani kwa kukosa ufahamu na kushindwa kuwafundisha kuudumisha ukweli, sisi tukiwa vijana tunaojifunza kweli tusizionyeshe tabia hizi (1 Timotheo 4:12-13). Kwa mfano tunatakiwa tusikilize onyo la Malaki kuhusu kuoana na watu wasiokuwa Wakristo, tukifahamu kuwa ni kinyume cha amri ya Mungu (2 Wakorintho 6:14-17; 1 Wakorintho 7:39). Ingawa watu watendao maovu wanaweza kuonekana wakipata mafanikio, lakini kumbuka kwamba ni kwa muda tu, Mungu hajasahau hukumu, ameiweka akiba kwa ajili ya siku aliyoteua yule "Mjumbe wa agano" Bwana Yesu Kristo atakuja ghafla, na sisi inatupasa kukesha (kuwa waangalifu) na kusali kila wakati na kuzungumza pamoja kuhusu mambo ya kweli, ili tuhesabiwe kustahili kuepuka hukumu ile (Zaburi 37:1-3; Luka 21:36).
MAKTABA YA REJEA
"Manabii wa makabila kumi ya uhamishoni" (J. Carter)
"Historia ya Biblia" (H.P.Mansfield) - Kitabu cha 7 namba 9,10
"Malaki" (J.Ullman) - Maelezo
MASWALI YA VIFUNGU
1. Jina Malaki lina maana gani, na ni ujumbe upi aliwapatia watu?
2. Ni mambo gani matatu amabyo Malaki aliyatumia kuwaonya watu?
3. Ni nani "mjumbe wa agano" atakayekuja na kazi yake itakuwa ipi?
4. Ni kwa vipi kazi ya Malaki na Nehemia zilifanana?
5. Kwa kutumia matukio ya siku za Malaki kama kielelezo onyesha ni kwa ni kwa nini kuoana na mtu asiye amini
MASWALI YA INSHA
1. Mungu alimpeleka nabii wake Malaki kuwaonya watu-ni katika njia gani Walawi na Makuhani hawakumtii Mungu?
2. Ni nani "Mjumbe wa agano" (Malaki 3:1) na kazi yake itakuwa ni nini?