CSSA 2-3-24 - JOHN THE BAPTIST: HIS BIRTH AND MISSION

Swahili

199. YOHANA MBATIZAJI: KUZALIWA NA UJUMBE WAKE

"Nawe, mtoto, utaitwa nabii wa aliye juu sana, kwani utamtangulia Bwana kumtengenezea njia zake".

 

Malaki aliwaambia watu wa siku yake kuwa "Mungu wa hukumu anakuja, atawaonya kwamba wachache wangekuwa tayari kumpokea wakati atakapokuja. Kwa sababu ya hali hii ya uovu, ilikuwa ni muhimu sana Mungu kumtuma mjumbe mwingine kwanza, kwa ajili ya kutayarisha njia" (Malaki 3:1). Kwa miaka mia nne amabyo Mungu aliyamaza kimya wakati Israeli wakiharibu njia yao kwa kutokujali Neno lake. Ukimya huo ulivunjwa na kutokea malaika Gabrieli ghafla kwa Zakaria. Matokeo ya kuzaliwa kwa Yohana mbatizaji, ambaye aliashiria kuja kwa masihi, yalileta mageuzi ya dini wakati utashi wa taifa uliguswa na umahili wa huyu nabii wa jangwani. Kwa njia hii mioyo ya watu iliandaliwa kumpokea yule "mjumbe wa agano", Mwana pekee wa Mungu.

 

Luka 1:1-27; 57-80

 

HALI KATIKA ISRAELI WAKATI YOHANA ALIPOZALIWA:

Kwa sababu ya uovu wa Israeli, Mungu alikuwa ameruhusu mataifa maovu kama Babeli, Uajemi, na Uyunani kuiteka na kuitawala na sasa Rumi, baada ya kuishinda dola ilivunjika ya Uyunani, na ikawa Bwana wa dunia "kumbuka jinsi Mungu alivyokuwa ametabiri hili kupitia kwa Danieli” (sura 2 :31-40). Wayunani walikuwa ni taifa lenye lenye kujiona ambao walichukiwa kutawaliwa na wageni nao walitazamia siku ambayo wangekuwa huru tena. Wayunani siyo tu waliwaona watawala wa Kirumi kuwa wakuchukiza, bali pia walikuta chini ya uongozi wa wageni. Herode mkuu aliyekuwa mtu wa Edomu alikuwa meoa malkia mrembo Myahudi na "kongoka" kuwa na dini ya Kiyunani naye alikuwa ameteuliwa na Warumi kuwa mfalme wa Uyahudi.

 

Kilichoonyesha Wayahudi kuwa wana tofauti ni sheria ambayo Mungu alikuwa amewapatia kupitia kwa Musa, sheria hii ndiyo ilkuwa msingi wa maisha ya taifa. Ingawa Rumi ndiyo iliyotawala nchi, lakini waliwaruhusu Wayahudi kuongoza mambo ya Hekalu mjini Yerusalemu, wakati wa nyakati hizi kulikuwa na vikundi vingi vya dini. Walikuwepo Mafarisayo wenye kujiona na kujikinai, na Masadukayo waliokuwa makuhani matajiri, walikuwepo wanasheria na waandishi ambao wote walishika imani tofauti ambazo hata mmoja hakishika sheria kama Mungu alivyokuwa amekusudia.

 

Katikati ya mchanganyiko huu wa kidini kulikuwa na watu wa kawaida, waliohitaji uongozi na bila mafanikio walikuwa wakitafuta mchungaji wa ambaye angewaongoza katika kweli. Lakini kwa watu wale waliofuata maandiko ya Agano la Kale na maneno ya manabii, kilikuwa kizazi cha matumaini. Ingawaje manabii hawa walikuwa wameishi mamia ya miaka iliyokuwa imepita zamani. Maneno yao waliyosema yalikuwa yamehifadhiwa katika vitabu vilivyotamkwa kwa majina yao navyo havikusahaulika. Kwa mfano Isaya aliandika kuhusu wakati Israeli kwa mara nyingine ingekuwa taifa kuu (Isaya 9:6-7; 11:1-10). Danieli alitabiri kuja kwa masihi (Danieli 9:24-27).

 

ZAKARIA NDANI YA HEKALU - Luka 1:6-22

Kuhani mmoja mwaminifu na mtumishi wa Mungu, aliyeitwa Zakaria, na mkewe Elizabethi walikuwa kati ya watu waliosubiri "kuja kwa masihi”, Neno la Kiebrania "Masihi lina maanisha mtiwa mafuta" (katika Kiyunani neno hili ni "Kristo") nalo linaelezea kuhusu mfalme ambaye angekuja kama kiongozi wa watu wake. Zakaria na Elizabethi wote walikuwa "wenye haki mbele ya Mungu, walioenenda katika amri zote na kanuni za Mungu pasipo lawama" (Luka 1:5). Lakini maisha yao yalileta chukizo moja kuu - hawakuwa na watoto, ingawa waliomba mara nyingi ili kupata watoto (Luka 1:13).

 

Bila wao kufahamu kuwa wangekuwa wazazi wa nabii mkuu kuliko wote ambaye angemtengenezea njia Mwana wa Mungu. Akiwa kuhani, "zamu ya Zakaria ilikuwa kufukiza uvumba " ndani ya Hekalu. Tendo hili lilifanywa subuhi na jioni, na wakati kuhani alipoingia mahali patakatifu pa patakatifu ukimya ulijaa katika mkusanyiko wa waabudu nje ya. Moshi wa uvumba wenye harufu ya kunukia ambao ulipanda kutoka kwenye madhabahu ya dhahabu ulikuwa kama sala ya watakatifu ambamo sifa na shukrani hupanda kwa Mungu (soma Zaburi 41:2; Ufunuo 5:8; 8:3). Wayahudi walikuwa wamejifunza umuhimu wa harufu ya uvumba, kwani tunasoma kwamba walikuwa, "huko nje walikuwa wakisali wakati wa kufukiza uvumba" (Luka 1:10). Wakati Zakaria alipokuwa akiendelea na wajibu maalumu ghafla alihisi kuwa mtu mmoja alikuwa amesimama upande wa kulia wa madhabahu wa uvumba. Alikuwa ni malaika wa BWANA, akimurikwa na nuru ya vinara saba vya taa. Inaonekana kuwa alihisi kuwa yule mtu ni malaika, kwa maana alitetemeka kwa hofu. Ukimya wa miaka mia nne ulikuwa unakaribia kuisha na sauti ya Mungu ilisikika tena, "Usiogope Zakaria, kwani sala yako imesikiwa, naye mkeo Elizabethi atazaa mtoto (mwanamume), nawe utamwita jina lake Yohana". Ilikuwa ni vigumu kuyaamini masikio yake wakatimaneno ya faraja na ya muhimu yakitoka katika mdomo wa malaika aliyemtembelea, Jina Yohana linamaanisha "neema ya BWANA". Huyu atakayezaliwa angeleta enzi mpya ambayo neema ya Mungu ingewaongoza watu kwenye toba, na kifo (Warumi 2:4; Yohana 1:17). Ni mwana aliye wa namna gani! Ni sehemu tukufu jinsi gani ambayo angetekeleza.

 

Malaika Gabrieli akaendelea kueleza ujumbe maalumu wa Yohana kuwa ni nabii na mtangulizi wa Masihi. Ujumbe wa Yohana ungekuwa sawa na ule wa Eliya , angekwena "katika roho na nguvu ya Eliya kutayarisha mioyo ya watu ili waweze kumkubali Masihi wao (Luka 1:15-17; 1 Wafalme 18:37; Malaki 4:6). Zakaria alitetemeka kwa ajili ya ule mwonekanao wa malaika na yale maneno. Alitaka uthibitisho wa ahadi hiyo, hasa kwa kuwa yeye na Elizabethi walikuwa wazee sana. Malaika alijibu akimjulisha kuwa yeye (malaika) alikuwa ndiye Gabrieli, mwenye umaarufu ambao ulimfanya kusimama "mbele ya Mungu". Zakaria akapewa ishara, ambayo kwa hali yake halisi ilikuwa inakaribia sawa na kukosa imani, angekuwa bubu hadi hapo maneno ya ahadi yatakapotimia (Luka 1:19-20).

 

Huko nje watu walikuwa na shauku, wakihofia kuwa jambo fulani limetokea. Alipojitokeza mlangoni alikuwa na tatizo la kuelezea kuchelewa kwake. Aliwaashiria kwa mikono akijaribu kuwaelezea mambo ya ajabu, na kwa kuwa hakuweza kuzungumza walitambua kwamba alikuwa ameona maono. Watu wakaondoka Hekaluni kwa mshangao, wakifikiria kuhusu tukio hili la ajabu. Zakaria akaondoka kwenda nyumbani baada ya kumaliza hudumu yake, na kufuatana na maneno ya Gabrieli, katika muda uliowekwa, mwana wao alizaliwa.

 

KUZALIWA KWA YOHANA MBATIZAJI - Luka 1:57-80

Gabrieli alikuwa amesema kwamba wangekuwa na furaha na shangwe na kuwa watu wengi wangeshangilia kwa ajili ya kuzaliwa kwake (Luka 1:14). Elizabethi na Zakaria hawakuwa ndio pekee waliokuwa na shauku. Ndivyo ilivyokuwa kwa wenyeji wote mji ule mdogo huko mlimani. Walifahamu jinsi maharusi hawa walivyotamani watoto, na sasa sala zao ilikuwa zimejibiwa. Siku ya nane baada ya kuzaliwa, majirani na wana ukoo (binamu) walikusanyika kushuhudia kutahiliwa kupewa jina kwa mtoto. Watu hao waliokusanyika wakajichukulia madaraka na kumpa mtoto jina la Zakaria. Je, hili halikuwa jina la baba yake na pia jina la Waisraeli, lilionekana kufaa pia. Lakini walipomwuliza Elizabethi jina ambalo mtoto angeitwa, naye akatamka Yohana. Hili lilianzisha mzozo, ambapo kutokana na mzozo huu ilibidi aombe msaada wa Zakaria, walihisi kuwa na hakika angethibitisha chaguo lao, na kwa wakati pekee kabisa, alipata ubao na kuandika "Jina lake ni Yohana" wakashangaa. Dakika ile ile mdomo wake ukafunguka na kusema akimtukuza Mungu (Luka 1:64). Watu walishangaa sana kwa jinsi mambo yalivyokea na bila shaka vituko hivi vilikumbukwa na watu wengi katika miaka iliyofuata. Hivyo tangu akiwa mtoto mchanga, Yohana akawa ni sababu ya udadisi kwa maana watu walijiuliza "ni aina gani huyu mtoto angekuja kuwa" (Luka 1:65-66).

 

UJUMBE WA YOHANA MBATIZAJI - Luka 1:15-17, 76-80

Zakaria akijaa roho mtakatifu, akamshukuru Mungu kwa wema wake kwa ajili ya kuwajia watu wake na kuwakomboa kwa kuwa wakatiulikuwa umefika ambapo mzao wa Daudi (mstari 69) na Ibrahimu (mstari 73) angetokea kuwakomboa Israeli waaminifu waliotazamia ukombozi. Ndipo alipomsema mwanaye, "na wewe, mtoto, utaitwa nabii wa Mungu Mkuu sana, kwa kuwa utamtangulia Bwana kutengeneza njia zake" (mstari 76-80). Zakaria aliyafahamu maneno ya Isaya nabii "sauti ya mtu aliye nyikani: Tengenezeni njia ya BWANA" (Isaya 40:3) na sasa ilikuwa wazi kuwa mwanaye ndiye angelifanya kazi hii kuu. Pia aliyafahamu maneno ya Malaki: Tazama, ninamtuma mjumbea wangu atatengeneza njia mbele yangu; na Bwana mnayemtafuta, atakuja katika Hekaluni mwake, ndiye mjumbe wa agano, unayependezwa naye; tazama, atakuja asema BWANA wa majeshi" (Malaki 3:1). Zakaria alifahamu kuwa mtoto ambaye angemzaa angekuwa mtangulizi nakwamba kazi yake ingekuwa "kutengeneza njia" kwa ajili ya Yesu Kristo aliyeelezwa kuwa "Mjumbe wa agano" kama Gabrieli alivyomwambia Zakaria (mstari 15). Yohana angekuwa mkuu mbele ya macho Bwana "kama Mnazarayo asingekunywa mvinyo wala kileo kikali, naye angejazwa roho mtakatifu tangu kuzaliwa kwake." Kwa hiyo huyu mtoto akakua na kujaa moyo mkuu, naye akawa jangwani, mpaka alipojitokeza kwa Israeli (Luka 1: 80). Aliishi katika upweke, akila nzige na asali ya mwitu, akakua na mtu. Alikuwa amejitenga kabisa na aina ya uovu wa watu wa mjini, akajikita kunyonya akili ya roho, Yohana alingoja muda ambao Mungu angempeleka kwenye uwakili wake aakiwa mtangulizi wa Masihi, bila woga angekuwa changamoto ya utashi wa taifa na kuwaongoza watu kumrudia Mungu.

 

FUNDISHO KWETU

Tumejifunza kuwa walikuwepo watu waliokuwa wamesomea Neno la Mungu na walikuwa wakitarajia kuja kwa kiongozi mkuu. Watu wengi katika Israeli kwa wakati huu walikuwa wakiangalia kwa makini ishara za nyakati. Wengine walikuwa walisubiri kwa matumaini kuhusu kuonekana kwa Masihi. Ni vizuri kuwa macho kwa ajili ya ishara za nyakati; lakini subira nyingi zinahitajika ili kungoja kutimia kwake. Tunapokuwa wachanga muda wa kutimizwa kwa nyakati hizo unaonekana kuwa mbali sana na wala hauonekani kuwa wa maana kiasi hicho, lakini mapenzi ya Mungu kila wakati hutimia, nasisi inatupasa kujifunza kumngonjea kwa saburi. Kama vile watu wa siku zile walivyongonjea kwa saburi kwa ajili ya kufika Yohana na Yesu, na sisi sasa tunangonjea kwa saburi, tukiziona ishara za ajabu za kuja Yesu mara ya pili hapa duniani.

 

MAKTABA YA REJEA

1. Huduma ya Manabii (C.C. Walker) - Sura 40

2. Nazarethi intembelewa tena (R.Roberts) - ukurasa 4 na 5

3. "Historia ya Biblia" (H.P.Mansfield) - Kitabu cha 8 Namba 1

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. Elezea hali ilivyokuwa huko Israeli wakati Yohana alipobatizwa.

2. Kwa nini malaika Gabrieli alijidhihirisha pale hekaluni.

3. Ujumbe wa Yohana Mbatizaji ulikuwa ni upi?

4. Eleza jambo lililotokea wakati marafiki walipokusanyika kupewa kuhusu kupewa jina kwa Yohana.

 

MASWALI YA INSHA

1. Eleza kwa kina kufika kwa malaika Gabrieli kwa kuhani Zakaria.

2. Eleza habari ya kuzaliwa kwa Yohana mbatizaji na uanishe na uanishe kwa ujumbew wake

 

Swahili Title
199 YOHANA MBATIZAJI: KUZALIWA NA UJUMBE WAKE
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type