CSSA 2-3-25 - THE MESSIAH IS BORN

Swahili

200. MASIHI ANAZALIWA

"Yesu akaongezeka katika hekima na kimo, na katika kumpendeza Mungu na watu."

 

Somo hili linaweka kumbukumbu ya tukio kuu katika historia kufikia leo hii. Kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu kulileta mwisho wa ahadi zote ya kwamba mwokozi angeletwa. Huyu ndiye angeleta baraka za Mungu kwa mataifa yote, ulimwengu ulikuwa umelaaniwa kutokana na dhambi utatukuzwa hatimaye, na kurejeshwa kwenye upendo wa Mungu.

 

Luka 1: 26-56; 2 Mathayo 1 na 2.

 

MALAIKA ANASEMA NA MARIAMU

Katika mji wa Nazarethi, aliishi binti mdogo aliyeitwa Mariamu, alikuwa ni ukoo wa Daudi, aliyekuwa ameahidi kuolewa na mtu aliyeitwa Yusufu. Miezi sita baada ya Gabrieli kumtokea Zakaria, Mungu alimpeleka kumwambia Mariamu kwamba alikuwa amechaguliwa kuwa mama wa mtoto ambaye angekuwa mwokozi wa dunia, "Usiogope Mariamu" malaika alisema kwa kuwa umepata neema kwa Mungu "kwa unyenyevu", alisikiliza kwa makini kuhusu ujumbe huu wa ajabu sana . "Utamzaa mtoto mwanamume nawe utamwita jina lake Yesu, Atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana aliye juu sana; naye BWANA Mungu atampatia kiti cha enzi cha baba yake Daudi; naye atatawala juu ya Nyumba ya Yakobo milele; na ufalme wake haukutakuwa na mwisho" (Luka 1:31-33). Linganisha hili na ahadi ya Mungu aliyompatia Daudi katika 2 Samweli 7: 12-16, ambapo Masihi anatabiriwa waziwazi kuwa vile vile mwama wa Mungu na mzao wa Ibrahimu ili kutimizwa ahadi alizoahidiwa Ibrahimu (Mathayo 1:1). Malaika alimwambia Mariamu kuwa mtoto huyu angezaliwa kwa nguvu za Roho mtakatifu, na kwa hiyo angeitwa Mwana wa Mungu (Luka 1:35). Mariamu alielewa kuwa binamu yake Elizabethi alikuwa ana mimba, "kwani kwa Mungu hakuna lisilowezekana" (Luka 1:37). Maneno haya yalimkumbusha Mariamu kuhusu uhakikisho aliopewa Sara kwamba angemzaa mtoto wa ahadi. Jinsi Mariamu alivyofurahi, lakini pia jinsi alivyokuwa mnyenyekevu, alipotambua kuwa heshima kuu na wajibu wa kumtunza Mwana wa Mungu, yule ambaye unabii na ahadi zote zilizomhusu Masihi.

 

MALAIKA ANASEMA NA YUSUFU - Mathayo 1: 18-24

Siyo kwamba malaika alijitokeza kwa mariamu, lakini alimtokea pia Yusufu, akamwambia kuwa Mariamu angezaa mtoto kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kwamba, jina la mtoto huyo litakuwa Yesu, kwa kuwa angewaokoa watu wake kutoka dhambini (Mathayo 1: 21). Jina Yesu lina maanisha "BWANA ataokoa" na kwa hiyo kwa jina lake tuna unabii wa kazi ambayo wa kazi ambayo Mungu aliiandaa kwa ajili yake kuifanya. Na kwa hiyo Yusufu, fundi seremala wa Nazarethi akamchukua Mariamu kuwa mke wake, na wao kwa pamoja wakawa na wajibu wa kumtunza Yesu na kumlea katika njia ya kweli, na kwa hiyo kumwandaa kwa ajili ya kazi kuu ya ukombozi.

 

KUZALIWA KWAKE YESU - Luka 2:1-7

Nabii alitabiri miaka 700 kabla sehemu ambayo Yesu angezaliwa kuwa ingekewa Bethelehemu (Mika 5:2), lakini Yusufu na Mariamu waliishi Nazarethi. Hata hivyo Neno la Mungu halishindwi na muda hii ikatimizwa kwa njia ya ushangaza. Mariamu na Yusufu ambao wote walikuwa wa jamaa ya ukoo wa Daudi, iliwabidi kusafiri wakitokea Nazarethi kwenda Bethelehemu, mji wa Daudi, kwa sababu mfalme wa Rumi alikuwa ameagiza kuwa raia wake waandikwa sensa kwa ajili ya kulipa kodi. Ili waweze kuandikwa ilbidi waende kuandikwa katika mji wa kwao. Safari ilikuwa ya karibu kilometa 100, ilikuwa ni ndefu sana, ngumu, na Marimamu alikuwa amekaribia kujifungua mtoto. Walipofika Bethelehemu hawakuweza kupata nafasi, sehemu pekee waliyoweza kupata ilikuwa ni kwenye banda la kulishia ng`ombe. Katika banda hilo, mtoto Yesu alizaliwa usiku. Mazingira ya ndani ya hilo banda yalikuwa ni duni sana, yaliyokuwa ya umasikini, ndani ya banda hilo sauti ya Mwana wa Aliye juu sana, alitoa sauti yake ndogo. Kwa uangalifu mama yake alimfunika nguo na kumweka kumlaza ndani ya hori hilo la kulishia ng`ombe. Kutoka katika mwanzo, huu duni, katika mji ambao Mungu alimtia mafuta Daudi mfalme wa Israeli, kilembwe wa Daudi alizaliwa. Hakika angemtuykuza Mwanaye, na watu wote wale "wote wasiodharau siku ya mambo madogo" (Soma Zakaria 4:19; Luka 1:52; 1 Wakorintho 1:27).

 

WACHUNGAJI WA BETHELEHEMU - Luka 2:8-20

Mashambani karibu na Bethelehemu, wachungaji walikuwa wakilisha mifugo yao ya kondoo; ghafla wakati wa usiku, malaika wa BWANA akawatokea na anga zikajazwa na nuru ya mng`ao wa utukufu wa Mungu nao wakashikwa na mshangao, wakaogopa sana. Malaika akawahakikishia: Msiogope kwa kuwa ninawaletea habari njema za furaha kuu, ambayo itakuwa kwa watu wote; kwa kuwa kwa ajili yenu mtoto amezaliwa katika mji wa Daudi, mwokozi, ndiye Kristo Bwana, na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto amefunikwa nguo za kitoto kichanga, na amelazwa katika hori ya kulishia ng`ombe (Luka 2:10-12). Wale wachungaji wa kondoo walisikiliza kwa makini. Kwa mshangao, utukufu wa kuzaliwa kwa Mwana wa Aliye juu sana ulionyeshawa kundi la malaika wakisherekea kuzaliwa kwake, ghafla kulitokea kundi kubwa la malaika waliokuwa wakimtukuza Mungu, wakisema; "Utukufu uwe kwa Mungu juu, na ulimwenguni kuwe na amani, furaha kwa watu wote" (mstari 4). Wachungaji wa kondoo walishtuka mno kwa haraka wakawaacha kondoo zao na wakaenda Bethelehemu kumwona mtoto. Wakamkuta vile vile kama malaika alivyosema nao wakamsifu Mungu, "kwa mambo yote waliyoyasikia na kuyaona, kwa kadri ya walivyoambiwa" (mstari 20).

 

MTOTO MCHANGA YESU ANAPELEKWA HEKALUNI - Luka 2:21-39

Alitakiwa kufuata sheria ambayo Mungu aliitoa kupitia Musa, ambayo ilimtaka kila mtoto mwanamume ilimpasa atahiliwe siku ya nane. Mariamu na Yusufu walitii sheria hii na jina lake aliitwa Yesu, ambalo lilitamkwa na malaika (Luka 2:21; Mathayo 1:21). Siku ya 40 Mariamu na Yusufu walikwenda huko Yerusalemu ili kutoa sadaka kwa mzaliwa wa kwanza na kumfikisha kwa Mungu. Walipokuwa Hekaluni, mtu mmoja mzee sana aliyeitwa Simoni, aliyeongozwa na Roho Mtakatifu, alimwona mtoto na kumchukua mikononi mwake, Simoni alikuwa ameahidiwa kuwa hatakufa mpaka atakapomwona Kristo Bwana. Kwa heshima na upole Simoni alivuviwa na kusema "sasa wamruhusu mtumishi wako aondoke kwa amani, kufuatana na neno lako kwa kuwa macho yangu yameuona ukombozi wako, ambao umeutayarisha mbele ya watu wote; Nuru kuwaangazia Mataifa, na utukufu wa watu wako Israeli" (Luka 2:29-32). Wakati huo huo, Ana, nabii mke, aliyekuwa mzee sana alikuja Hekaluni, naye alipomsikia Simioni, na kuliona tukio, alimshukuru Mungu na akasema kuhusu Yesu "kwao wote ambao walitazamia wokovu katika Yerusalemu" (Luka 2:38). Ni maneno ya neema jinsi gani na kutokana na ushuhuda huu uliosemwa na wazee wa Yerusalemu ambao mioyoyao ilikuwa na shauku kwa ajili ya "faraja ya Israeli". Imani yao ilikuwa imegeukia katika kuona, kutimia kwa unabii mwingi katika uso wa huyu mtoto mdogo.

 

MAMAJUSI KUTOKA MASHARIKI - Mathayo 2:1:12

Mariamu na Yusufu wakarudi Bethelehemu ambapo walikaa kwa muda, mbali kabisa, katika nchi ya Mashariki, watu wenye hekima walikuwa wakingojea ishara ya ambayo ingewaongoza kule alikozawa Masihi. Walipoiona nyota mpya angani, wakatambua kuwa wakati ulikuwa umewaandia. Mtayarisho makuu kwa ajili ya kuanza safari yalifanyika, safari ambayo ilikuwa ndefu. Zawadi zilipakiwa nao wakaanza safari kwenda Yerusalemu, walifika mji wa Yerusalemu kwa matazamio makubwa na wakaanza kuuliza "Yuko wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa, kwa kuwa tumeiona nyota yake kule mashariki nasi tumekuja kumsujudia!". Habari za jambo hili zilimfikia mfalme mwovu Herode, ambaye kwanza aliwaita kwake makuhani wakuu na waandishi na akawauliza wamweleze ni wapi Kristo ingempasa kuzaliwa. Wakamwambia kwamba Bethlehemu ndiyo mahali anayotakiwa kuzaliwa kutokana na unabii wa Mika (Mika 5:2). Herode aliwaita wale mamajusi kwake na kuwapeleka Bethelehemu kwa ujanja, akawaomba wamtafute mtoto mchanga ili naye aende kumsujudia. Herode kwa kweli alianza kuwaua wato wachanga, siyo kwamba aliulinda ufalme wake kwa wivu naye hakumhitaji mfalme ambaye angekuwa mshindani wake. Kama walivyoiona ile nyota, ghafla waliiona ile nyota ambayo iliwaongoza mpaka mahali ambapo mtoto mchanga alikuwepo. Huko walimsujudia Yesu na kumpatia zawaida za thamani, dhahabu na uvumba (ubani) na manemane. Mungu akawaonya aliwaonya mamajusi katika ndoto na wasirudi kwa Herode, bali waende nyumbani kwao kwa kupitia njia nyingine.

 

MAISHA HUKO NAZARETHI - Mathayo 2:13-23

Kisha malaika akamtokea Yusufu katika ndoto akamwambia watoke mara moja akimbilie Misri pamoja na Mariamu na mtoto Yesu, watarudi wakati usalama utakapokuwepo… Muda mfupi ulipopita, Herode akatambua kuwa wale mamajusi hawakurudi, kwa hiyo akaghadhabikika. Ndipo akatenda uovu mkuu na ukatili kwa kuamrisha watoto wa Bethelehemu waliokuwa na umri chini ya miaka ya miwili wauawe, na kwa hiyo kilio kikuu kikatawala katika nchi. Lakini Yusufu, Mariamu na mtoto wa thamani walikuwa mbali upande wa kusini katika nchi ya Misri, mbali ya uwezo wa mfalme. Yusufu na Mariamu walibakia na mtoto Yesu huko Misri hadi Herode alipokufa, ndipo walipoongozwa na Mungu wakarejea Israeli na kuishi Nazarethi, ambapo Yesu alitumia muda mkubwa zaidi ya maisha yake. Huko ndipo Bwana Yesu alipokulia ndani ya jamii kubwa, kwa kuwa watoto wengine baadaye walizaliwa na Mariamu na Yusufu. Nazarethi ulikuwa karibu na barabara nyingi za biashara, na ni mji ambao uko kwenye bonde la milima. Ilikuwa hapa ambapo Yesu alijifunza kuwa na ujuzi wa Yusufu Seremala, wakati ambapo "aliongezeka katika hekima na kimo, na kumpendeza Mungu na watu" (Luka 2:52). Yesu alikua kama kijana yeyote Myahudi, akajifunza kusaidia nyumbani kwake, kwa maana ndiye alikuwa mtoto mkubwa wa ambayo ilikuja kuwa familia kubwa ya ndugu wa kiume na ndugu wa kike (Mathayo 13:55-56).

 

YESU ANAHUDHURIA PASAKA - Luka 2:40-52

Yesu alijua mambo mengi kuhusu sheria ya Wayahudi na manabii naye alikuwa na ufahamu uliokuwa zaidi ya umri wake, kwa kuwa Baba yake alimfanya mwepesi wa kuelewa njia zake (Isaya 11:2-3). Alipokuwa na umri wa miaka kumi na mbili aliachana na familia yake kwenda Yerusalemu ili kusherehekea Pasaka. Hii ilikuwa sherehe iliyofanyika kila mwaka kukumbuka kila mwaka kukumbuka jinsi Mungu alivyowaokoa watu wa Uyahudi kutoka utumwani huko Misri. Kwa upande wa Yesu, akiwa na umri wa miaka kumi na mbili lilikuwa ni tukio kuu. Kulikuwa na dhabihu nyingi zilizotolewa, aliangalia makuhani walipofanya kazi zao, akasikiliza Zaburi zilipoimbwa, na kusikiliza mazungumzo kati ya walioelimika waliokuwa wamehudhuria kwenye Pasaka ile, Yesu alipendezwa, na kwa hali ya kipekee, katika kila jambo aliloweza kulisika kuhusu Mungu, naye alitafakari maana ya maneno yao yote aliyoyasikia na kuona. Baada ya kukaa kwa muda mfupi katika mji wa Yerusalemu, Mariamu na Yusufu, pamoja na watu wengine wengi, walianza kurejea nyumbani kwao, wakifikiri kuwa Yesu alikuwemo katika yale makundi makubwa. Baada ya safari ya siku moja waligundua kuwa Yesu hakuwemo, kwa haraka walirudi tena Yerusalemu, lakini ilikuwa siku ya tatu, ambapo walimkuta ndani ya Hekalu akiwa amekaa na kati ya walimu wakongwe, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Yusufu na Mariamu waliangalia tukio hilo kwa mshangao mkubwa. Walifahamu kuwa kwa sababu Yesu ni Mwana wa Mungu, angeyakabidhi maisha yake kwa ajili ya kutenda mapenzi ya Baba yake, "Ilikuwaje hata mkanitafuta?" akasema "Hamfahamu ya kwamba imenipasa kuwa katika katika nyumba ya Baba yangu?" Kwa upole, Yesu alijaribu kuwaeleza waelewe kuwa tayari alikuwa na ufahamu kuhusu kazi yake iliyokuwa mbele yake. Alifahamu sababu iliyomfanya azaliwe duniani, anye akajitayarisha kutekeleza kusudi hilo. Hata hivyo, Yesu akarudi na Yusufu na Mariamu huko Nazarethi na "akawa mtiifu kwao".

 

FUNDISHO KWETU

Yesu akiwa seremala (Marko 6:3), naye akasikiliza kwa makini katika masomo ya kila siku kutoka kwenye Maandiko Matakatifu kwa pamoja Mariamu na Yusufu walifahamu kwamba Mungu ndiye alikuwa Baba yake, na kwamba alikuwa akiandaliwa kwa kazi siku ya mbele. Kadri ya miaka 18 tangu wakati huo, aliondoka nyumbani kwake kuanza kazi yake aliyokuwa amepewa na Baba yake. Siyo kwamba tunatakiwa kufanya kazi zote alizozifanya Yesu Kristo, lakini, katika kufuata mfano wake, inatupasa tukumbuke jinsi ilivyo muhimu kujifunza kuhusu Mungu na kweli yake wakati tukiwa na mdogo, ili kwamba tutakapokua wakubwa, tuweze kumtumikia yeye kwa njia aliyoiweka. Yesu alikuwa ndiye aliyeahidiwa ambaye angewaokoa wanadamu kutoka katika dhambi zao (Mathayo 1:21). Yeye ndiye mzao wa Ibrahimu aliyeahidiwa na ni yule ambaye atakuwa Mfalme na kuketi katika kiti cha enzi cha Daudi (Mathayo 1:1; Luka 1:32-33). Katika Wagalatia 3:26-29, tunajifunza namna tuwezavyo kuchangia katika mibaraka iliyoahidiwa kutokana na ubatizo katika Kristo.

 

MAKTABA YA REJEA

"Nazarethi inatembelewa" (R.Roberts)-Sura ya 6,7 na 8

"Historia ya Biblia " (H.P. Mansfield)- Kitabu cha 8, Namba 1,2

"Maisha ya Yesu" (M.Purkis)- sura 1

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu wa Nazarethi. Ni ujumbe gani wa ajabu alioupata?

2. Eleza safari ya mamajusi kutoka mashariki kwenda Bethehemu.

3. Eleza kilichotokea wakati Yesu alipokuwa na umri wa miaka 12, alipokwenda Yerusalemu kwa ajili ya Pasaka?

4. Ni ahadi gani kubwa iliyotimizwa kutokana na kuzaliwa kwa Yesu na kazi yake?

 

MASWALI YA INSHA

1. Fafanua kuzaliwa kwa Yesu na habari za furaha ambazo malaika waliwaambia wachungaji wa mifugo.

2. Fafanua safari ya Mariamu, Yusufu na Yesu walipokwenda Yerusalemu wakati wa Pasaka.

 

Swahili Title
200 MASIHI ANAZALIWA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type