CSSA 2-4-12 - FEEDING THE MULTITUDE

Swahili

212. KULISHA MKUSANYIKO

“Mimi ndiye chakula cha uzima”

Kuwalisha mkutano (mkusanyiko) na kunyamazisha tufani inaelezwa kuwa “ishara” ya nne nay a tano ya injili ya Yohana inaonyesha ya kwamba Yesu ndiye “mkate wa uzima”  na kwamba anaweza pia kunyamazisha dharuba za maisha zinazokuja juu ya watu wake. Watu wa Israeli walipendezwa na muijuza wa kulisha watu 5000. hakutoa chakula hiki kwa sababu tu ya kuridhisha njaa yao, bali alitaka wanafunzi wake na watu kuelewa ya kwamba alikuwa ndiye “mkate wa uzima” na kwamba kama wangalimwamini na kumpokea kama mwokozi wao wangalipata hatimaye kushiriki uzima wa milele.

Lakini wengi waliona ya kwamba hawangaliweza kumkubali hasa alipokataa haja yao kumfanya mfalme, akiwafunga kumuacha (Mathayo 14:15-33; marko 6: 32-52; Yohana 6)

Kupunzika (pumziko) mahali pa jangwa

Ulikuwa wakati wa Pasaka, miezi kumi na mbili kabla ya kifo cha Yesu, naye alikuwa bado mashuhuri kwa watu (Yohana 6:4).

Bada ya kukataliwa huko Nazarethi Yesu aliwatuma wanfunzi wake 12 wawili wawili kuponya wagonjwa na kuhubiri ya kuwa watu watubbu (Marko 6:6-13). Sasa wanafunzi walikuwa wakirudi Kaperinaumu, wakiwa na hami kumwambia yote waliyoyatenda na kufundisha. Wakti huo huo yesu alikuwa ameshasikia ya kwamba yule mwovu Herode alikuwa amemua binamu yake na rafiki Yohana mbatizaji hili lilikuwa limemhuzunisha yeye na kumkumbusha ya kwamba alikuwa pia karibu kufa.

Kwa hiyo Yesu alihisi kuwepo haka ya kuondoka kutokana na kelele na msukosuko wa Kaperinaumu, naye akasema kw awanafunzi wake “twendeni tujitenge jangwnai, tupumzike kwa muda” (Marko 6:31). Hivyo wakaenda kwa meli kuvukabahari ya Galilaya hadi mahali pa jangw akaribu na bethsaida mbali na makundi.

Kondoo bila mchungaji (Marko 6:33-34)

Walakini watu wengi walimwona akiondoka nma wakikumbuka miujiza aliyokuwa ameifanya wakaharakisha kuzunguka ukiongoni mw abahari kw amiguu, wengine waliongeza kujiunga na kundi wakati wanaendelea. Yesu aliposhuka kutoka mlimani alikokuwa akipumzika pamoja na wanfunzi wake, kundi likawa linamgoja. Akisahau uchovu wake na huzuni “aliguzwa na huruma kwao, kw asababu walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji, naye akaanza kuwafundisha mambo mengi”Marko 6:34.

Wanafunzi wajaribiwa (Marko 6:35-39)

Aliwafundisha hadi jioni, na wanafunzi wakaja kwake kumwomba kuwaruhusu watu kwend azao ili wakanunue chakula kwnai katika haraka yao hawakuwa wameleta chchote, “wape chakula wale” alisema bwana wao “akifhamh ambacho angefanya” (Marko 6:37; 6:6). Kwa yakini wanafunzi hawakuelewa namna wangalivyonunua chakula cha kutisha kwa ajili ya watu wengi hibvyo. Andrea akamwambia Yesu ya kwamba kijana (mvulana) mmoja alikuwa na mikate ya hayiri mitano na samamki wawili wadogo, lakni ni kwa vipi hiyo ingaliwalisha zaidi ya watu 5000?

Kwa amri ya Bwana wale 12 wakawakalisha watu kwa mpango wa makundi ya 10000 na 50 kwneye nyasi, sasa watu na wanafunzi wakamtazama, wakadadisini nini Yesu angalifanya.

Chakula kw aajili ya makundi(Marko 6:40-44)

 Yesu alishukuru na kuanza kumenga mkate, kwa mshangao wao wote chakula kiliendela kuongezeka, hivi kwmaba wakati wote wam,eshakula cha kutosha, wanfunzi walijaza vikapu vikubwa na masalio. Hawakuwa na lingine isipokuw akusema “hii ni kweli ya kwamba yule nabii ajaye duniani amekuja”(Yohana 6:14)

Kule kwa Yesu kumega mkate kuwatukumbusha sisi chakyla cha kukumbukumbu cha jioni, alisema kuwa mkate aliowapa wanafunzi ulisemea mwili wake. Alikuwa nafundisha ya kwamba kwa kule kumenga mwili wake mwenyewe kwa kifo angalitoa mkate wa kweli ambao ungaliwadumisha wengi katika uzima walihubiri injili wakiwapa ujumbe huu kati ya watu. Katika miujiza wa kulisha watu 5000 vikapu kumi n ambili viilijaa masalio, kimoja kwa kila mwanafunzi. Kama vile waliwajibika kuhakikisha kuwa hakuna kinachopotea wakti walikusanya masali

(Vipande), hivyo hivyo Injili ingalipewa tu kwa wale alio na njaa kwa hiyo, kuchanganya pamoja na wa- mataifa ingawaaje kwanza ingalihubiriwa kw amataifa kumi na wawili wa Israeli.

Tunaweza na shukurani mno ya kwamba ujumbe wa njili ambao Yesu na wanafunzi wake waliusambaza umetufikia hata sisi tukiwa wachache kati ya kundi kuu pana ambao, tokea nyakati zao, wamelishwa mkate wa uzima. Kwa vile tunaweza kujazwa na kuridhishwa bna mlo huo, hatuna haja tena kuona njaa na kiu kwa ajili ya matunzo ya kiroho, huu ndio mkate wa uzima, unaozidi mahitaji yetu (Ona Isaya 55:1-2; Kumbukumbu la Torati 8:3)

Watu wanatamani kumfanya mfalme(Yohana 6:14-15)

Wattu wengi zaidi hawakufahamu maana ya miujiza huu, lakini wakiwa na shukrani kwa chakula na kushangazwa na nguvu za uumbaji walizoziona, waliamini ya kwamba Yesu alikuwa ndiye Masihi, nabii kama Musa ambaye angalikuja duniani (Kumbukumbu la Torati 18:14). Hakika kama vile Musa alivyowaongoza watu kutoka Misri, hivyo hivyo walifikiri Yesu angewakomboa kutoka kwa Warumi waliamua kumchukua kwa nguvu na kumfanya mflame. Akilifahamu hili Yesu upesi aliwaondoa wanafunzi kwa m,eli kwenda Kaperinaumu na kuondoka kutokana na kundi yaliyokuwa yanamng’ang’ania akaenda zake mlimani tena, kupata nguvu kutokana na tafakari na sala kwa baba yake. Sasa haukuwa muda wake wa kuwa mflame mbeya yake kulikuwako msalaba (kusulubiwa) ambako watu, hata na wanfunzi hawakuelewa.

Kutuliza tufani(Marko 6:45-52)

Wanafunzi wali[pokuwa wanapiga makasia kwenye giza la usiku, tufani ilitokea ziwani, ile meli ndogo ilirushwa na mawimbi na haikluweza kushindana na upepo. Hawakuwa na nguvu dhidi ya ile tufani kali. Ndipo katika giza la usikuakaonekana mtu akitembea juu ya bahari na kuwafanya wali kwa kelel za woga. Lakini sauti inayofahamika iliwatuliza “tulieni msiogope” aliposikia ya kuwa alikuw ani BWANA WAKE Petro mwenye ujasiri akaomba kama angeweza kutembea kuelekea kwak juu ya bahari. Alianza vyema lindi macho yake ayakondoka kumwelekea Yesu, kwenda kwanye bahari iliyochafuaka kumzunguka. Imani yake ikayumba alipoanza kuzama Yesu akamdaka na wote wawili wakaingia melieni, wakati ule ule upepo ukanyamaza na kabla ya hawajajua, meli ikafika ukingoni “kwa hakika”, wakasema “wewe ni mwana wa Mungu” Marko anaongeza “kwani hawakufikiri ule muujiza wa mikate kwa kuwa mioyo yao ilikuwa migumu” Petro na wanfunzi wengine hawakuwa wametambua ya kwamba mwana wa Mungu siyo tu angaliweza kuoneza mkate, bali hata upepo na bahari vingemtii. Ni nguvu ya ajabu iliyoje! Inatupasa kuwa na imani katika nguvu yake, kwnai atakaporudi atamaliza vita yetu katika tufani ya maisha, ikiwa pamoja na kuituliza bahari iliyochafuka ya migongano ya kimataifa kwa kuanzisha utawala (enzi) yake ya haki na amani.

Mkate wa kweli kutoka mbinguni(Yohana 6:22-71)

Wakiwa wamerudi Kaperinaumu tena watu wakakusanyika kwa Bwana. Akawaambi ya kuwa walimkusanyikia (walinijia) tu kwa sababu walikuwa wamejazw amatumbo yao kwa chakula. Aliposema ya kwamba wasikifanyie kazi chakula kinchoharibika bali kwa ajili ya chakula kile ktakachodumu hadi uzima wa mileel, ambacho alikuwa tayari kuwapa.

Wakaomba awaonyeshe ishara ili wamwamini, ingawaje alikuwa amewalisha makundi kwa muujiza. Jinsi walivyokuwa vipofu kimakusudi! Wakasema Musa alikuwa amewapa Israeli  mkate kutoka mbinguni.

Yesu akawaeleza ya kuwa yeye alikuwa ndiye mkate wa kweli uliopelekwa kutoka mbinguni, akitimiliza “aina” ya mana ambayo baba zao walipata jangwani, mana ina maanisha “ni nini?”na hapa Kaperinaumu watu hawakuweza kuamini ya kwamba Yesu huyu alikuwa kipawa cha mUngu kama mana angalao walikuwa wamena miujiza yake.

Bwana alisema ndiye aliyekuwa mkate wa kweli, wala siyo “wa mfano” wangekula mwili wake na damu yake yaani kuweka maishani mwao mawazoyake, maneno na matendo hawangekufa kama wale wa jangwani ila hatimaye wangeishi milele.

Kati ya wengi walioshuhudia miujiza yake wachache sana walielewa ujumbe wake na ukuu, nguvu zilizo za Mungu muumbaji zilikuwa zimedhihirishwa mara mbili. Lakini Petro aliharakisha kusema “wew unayo maneni ya uzima wa milele nasi tunaamini na tunauhakika kuwe wewe ni Kristo mwana wa Mungu aishieye”(Yohana 6:69)

Somo kwa ajili yetu

Kwa vile Yesu aliwapa mkate yale n akunyamazisha dhoruba hivyoanayo nguvu yaukombozi, hii inatolewa kwa wale wote ambao katika ubatizo wanamkubali yeye kuwa ni mkate utokao mbinguni, anayeweza  kutoa uhai wake kwa ulimwengu. Inatupasa tujibidishe kudhuhirisha maishani mwetu akili ya Kristo katika mawazo yetu yote, m,aneno na matendo. Tukiamini ya kwmaba anaweza kutupatia pia mahitaji yetu ya kila siku na kunyyamazisha dhoruba (tufani) za maisha. Ni budi tumwamini amabye MUngu amemtuma. Lakini hili linahitaji mawazo ya uangalifu juu ya maneno yake na lengo (jukumu) lake ndipo tutathamini ya kuw ayeye pekee ndiye mwanzo wa manenno ya uhai (uzima) wa milele.

Maktaba ya rejea

“The eight sign of John” (J.Ullman)  pages 45-58

“A life of Jesus” (M.Purkis) pages 189 -197

“Nazarethi Revisited” (R.Roberts) pages 279-292

“Story of the Bible” (H.P. Mansfield) vol 9 pages 107 -130

“The gospel of John” (J.Garter) chapter 6

“The gospel of theson of God” (R.G.Sargent) pages 91-99

Maswali ya fungu

  1. Yesu aliitikiaje azimio la kumfanya awe mfalme na kwa nini aliitikia kwa njia ile?
  2. Kabla Yesu hajalisha wale 5000 alichukuw amkate, akashukuru na kuumega. Hili linakukumbusha wewe juu ya nini?
  3. Ni atahri gani ilitokea kwa Petro Yesu alipotembea juu ya maji wakati wa tufani katika bahari na juu ya wanafunzi wele wengine ndani ya mashua?

Maswali ya insha

  1. Kulisha wale 5000 kuna maana gani kiroho?
  2. Eleza hadithi ya Yesu akituliz atufani wakati wa usiku baada ya kulisha wale 5000?
  3. Fafanua jinsi Yesu alivyo mkate kutoka mbinguni?

 

 

 

 

 

 

 

 

Swahili Title
212. KULISHA MKUSANYIKO
English files
African text
CSSA
Translator 1
Jonathan Nkombe
Translator 2
Carl Hinton
Literature type
Sub type
Sub sub type