CSSA 2-4-13 - OPPOSITION GATHERS IN THE SHADOW THE CROSS

Swahili

213. UPINZANI UNAJIKUSANYA KATIKA KIVULI CHA MSALABA

“Lakini ninyi mnasema mimi ni nani? Naye Simoni Petro n akusema wewe ndiye Kristo mwana wa Mungu aliye hai”

Watu wengi hawakuweza kumwelewa maneno Yesu aliyoyasema kuhusu mkate wa uhai, kutoka wakatu ule anasema Yohana “wengi kati ya wanafunzi wake walirudi nyuma na wala hawakutembea naye tena” (Yohana 6:60-66). Hawakushiriki imani ya Petro aliyesema “Bwana twende kwa nani? Weweuna mane ya uhai wa milele” kutokea muda huo kuendelea katika mwaka wa mwisho wa Bwana, upinzani kwake mwenyewe na mafundisho yakle uliongezeka. Ilikuwa lazima Yesu kuwaonya wanfunzi wake juu ya upinzani wa wakati huo huo kuwafundisha zawadi za milele za waanfunzi.

Mafarisayo na Masadukayo Mathayo 16:1-4)

Baada ya kuvuka bahari kwa meli (mashua) Yesu katika Magdala katika eneo la Dalmanutha hapa kundi la mMafarisayo na Masadukayo lilkuwa likimgojea. Ilikuwa siyo kawaida kuwakua pamoja wakiwa mbali hivyo kutoka Yerusalemu. Walikuwa wamejiiunga kwa lengo moja la kumpinga yesu wakimuuliza au wakimtaka atowe ishara kutoka mbinguni. Hili lingalionekana sahihi, hasa hasa kwa vile katika Kumbukumbu la Torati 13 Mungu alikuwa amesema ya kwamba viongozi wa Israeli ilibidi wawatahini manabii kwa kutaka waonyeshe ishara.

Ishara ya nabii Yona (Mathayo 16:2-4)

Lakini Mafarisayo na Masadukayo walikuwa wameona ishara nyingi za ajabu. Kwa miaka miwili Yesu alikuwa ameponya vipofu, bubu, vilema na kufanya maji kuwa mvingyo, kufufa wafu, na hivi karibuni alilisha makundi makubwa kutokana na mikate michache. Nikodemo, mmoja wa walimu, alikuwa mekubali ya kwamba hakuna yeyote angaliyeweza kutenda kazi za Yesu alizozifanya, isipokuwa Mungu awe naye (yohana 3:2)

Yesu akawatuhumu ya kuwa wanafiki, kwani waliweza kubashiri majira kutokana na rangi za anga lakini hawangeelewa ishara za nyakati zao, je ni zipi zilikuwa “ishara za nyakati” “tufani” ya kukamiwa ilikuwa inakaribia, kutokana na uongozi wao wa upofu na usio na imani. Tufani hii ya hukumu ya Mungu juu ya taifa kungepukwa pale tu wangaliziona ishara za nabii Yoha. “ishara” inapatikana katika tukio lake la kuwa siku tatu ndani ya tumbo la nyangumi kabla, kwa kweli, jhajatokewa na ufufuo kutoka kwenye kaburi la maji. Watu wa Ninawi walikuwa wametubu pia kwa mahubiri ya Yona. Sasa mtu mkuu zaidi kuliko Yona alikuwemo ndani ya Israel, ambaye mahubiri yake walikataa kuyasikia wakitafuata tu njia ya kuweza kumwangamiza na kumweka katika kilindi cha kaburi. Ingawaje wangeonekana kufanikiwa, kumuweka kwao Yesu katika kifo ungalionekana hakuna athari (madhara) kwa kule kufufuka kwake baada ya siku tatu. Lakini walikataa kusikia onyo la “dalili” hihi ya Yona.

Chachu ya MAFARISAYO NA Masadukayo (Mathayo 16:6-12)

Yesu akawaambia wale watu wanafiki na kwenda zake. Akivuka kwenda ng’ambo nyingine ya baharai ya Galilaya,hapa Yesu akwaagiza wanafunzi wake “jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Maadukayo” wanafunzi walidhani alisema hivi kw asababu walikuwa wamesahau kuleta mkate, mkate wa kawaida wenye hamila.lakini alikuwa akionya juu ya athari ya hawa watu waovu (Mathayo 16:12);. Alama ya chachu inatumika kwa sababu wakati kipimo kidogo kinawekwa ndani ya mkate kitakuwa na kitaumuka, maka mkate wote umeathirika. Basi ndiyo inaweza kuwa ishara ifaayo kwa dhambi (1Wakorintho 5:6-8) na katika onyo hili, dalili ya athari ya uharibufu wa Masadukayo na Mafarisayo. Hebu tuone jinsi Mafarisayo na Masadukayo walibyokuwa viashairia bya uharibufu.

Mafarisayo waliamini kwa dhati sheria katika kila kipengele angalao walikuwa vipofu hasa kuhusu “mambo mazito zaidi ya sheria, hukumu, rehema na imani” (mathayo 23:23). Hawakuweza kuona kwamba Yesu alikuwa ndiye utimilizo wa sheria nayo sheria ilikuw ani mwalimu tu akiwafundisha kumpokea (kumkubali) Kristo (Wagalatia 3:24).

Masadukayo kw aupande mwingine waliamini tu vitabu vya kwanza vitano vya Biblia vilivyoandikwa na Musa, hivyo kuacha manabii wote wale waliosema juu ya Yesu. Hawakuamani katika ufunuo, ambo ulikuja kwa kipengele cha msingi katika imani kwa Yesu kuwa ndiye Kristo (1 Wakorintho 15:13-14; Mathayo 16:21). Masadukayo pia walithamini sana nguvu ya fedha, walitumia sehemu kubwa ya muda wao katika kujilimbikizia na kutafuata mali.

Athari zote hizi zilienea katika taifa lote kama chachu, hadi wachache sana walitafuata kwlei katika Yesu. Kwa hiyo alikuwa akiwaonya wanafunzi kutokuathiriwa na watu hawa ambao waliungana katika upinzani wenye ari dhidi yake,

Kukiri kwa Pertro (mathayo 16”13-17)

Pale bethasaida Yesu alipomponya mtu kipofu n akisha kwenda kaskazini viungani mwa Kaisaria Filoppi, mbali kutoka mahali ambapo pangalikuwa na watu wengi. Njiani baada ya kuomba (kusali) kwa baba yake, akawauliza mitume wake, akisema “watu wanasema mimi ni nani?” wanafunzi wakatoa maelezo ya mawazo yaliyokuwa yakitamkwa katika makundi Yohana Mbatizaji, Eliya Yeremia au mmojawapo wa manabii. Lakini angalia kwamba hata mmoja sasa alikuwa kisema ya kuwa Yesu alikuwa ndiye Masihi wa Israeli, ila mwingne kati ya manabii. “Lakini ninyi mnanita kuwa ni nani?” aliuliza, Jibu la Petro lilikuwa la uhakika “wewe ni Kristo mwana wa Mungu aliye hai” Oh jinsi lilivyokuwa la maana tamko hili .

Petro hakuwa ameambiwa hili na mtu yeyote lakini Mungu alikuwa memwonyesha hili kupitia uhusiano wake na Yesu siku ka siku, katika ubatizo wake, miujiza yake, maneno yake, yenye Uungu vyote hivi vilibeba ushaidi wa kwamba baba alikuw amemtuma (Yohana 5:36). Yesu basi, hakuwa nabii wa kawaida wala hakuwa Yohana mbatizaji Yesu alikuw ani “Mpakwa” (Zaburi 2), yule ambaye Mungu angalimfanya mfalme katika kiti cha enzi cha Daudi (2 Samweli 7), uzao wa Abrahamu kupitia kwake amabye mataifa yote yangebarikiwa (Mwanzo 22:17-18) na “mzao wa mwanamk” ndiye mshindi . jinsi basi, yaliyokuwa na maana maneno ya Petro!

Yesu alikuwa mwana wa Mungu, jinsi ilivyokuwa ya maana kwa ajili ya wanfunzi kufahamu hili na kuendelea lkuamini hili katikia siku ngumu zijazo.

Funguo za ufalme (Mathayo 16:18-19)

Kufuatia kukiri huku kwa Petro Yesu akamwambia “wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitajenga kanisa langu” Petro angetumika katika kuhubiri injili na uanzilishi wa kanisa la nguvu ungalijengwa juu ya kweli ya tamko la Petro. Kweli ile ya Umasihi wa Yesu haingeathrika hata kwa kifo cha walimu wake. Petro aliahidiwa “funguo za ufalme” kufungua mlango wa ufalme. Katika matendo Petro alitumia funguo hizi katika kuhubiri kwa Wayahudi katika siku ya Pentekoste (mathayo 2: 14-41), na tena katika kufungua “mlango wa imani” kwa wa mataifa katika Matendo ya Mitume 10.

Rudi nyuma yangu shetani (Mathayo 16:21-23)

Walipokuwa wakiendelea njia baada ya kukiri kwa Petro yesu akajaribu tena kuwaonya wanafunzi wake kuhsu ujilio wa kifo chake, bila shaka wakiwa na dalili /ishara ya Yona akilini, Yesu aliwaonyesha ya kwamba ibngalimpasa afe, lakini kwamba angalifufuka tena siku ya tatu. Petro, aliyekuwa amekiri Kristo mara hiyo. Alimpinga Bwana wake, kw ahilo akiwa “kikwazo” au kipingamizi na adui kam neno “shetani” linavyomanisha akisema “hili halitaweza kutokea kwako Yesu akageuka na kwa karipia kali aksema “wewe hufikiri vitu vya Mungu,bali vile vilivyo vya watu”

Mihimili (taratibu) za uanafunzi (mathayo 16:24-27)

Yesu alimwonyesha Petro na mitume wengine ya kwamba mtu yeyote atakaye kuwa mwanfunzi wake inampasa

  1. Ajikane mwenywe
  2. Achukuwe msalaba wake,
  3. Amfuate

Yeyote anayejaribu kwa nguvu kuokoa uhuia wake ataupoteza, alakini wanaoyaacha maaraka ya dunia kwa ajili ya Kristo, watapata uzima wa milele. Je pana thamani halisi gani nay a kudumu katika utajiri na raha za dunia hii? Kwani wakati wa kuja kwa Kristo vitu liwe vyote vitapotea, na wote walioviacha watuzawadia vile vile kama Kristo alivyotoa uhai wake na kuzawadiwa na uziam wa milele. Tutatenda vyema kutafuata usalama katika Kristo, kuliko kluweka imani yetu katikavitu vya dunia hii.

Yesu aliwaonya wanfunzi wake kutokumwambia yeyote kwamba alikuwa ndiye Kristo. Kukiri hivyo kungeliweza tu kuleta upinzani zaidi, kwani hata wanafunzi hawakuelewa kikamilifu. Kifo chake kule Yerusalemu mbele yake na ufufo wake ungetamka kwa watu wote ya kuwa alikuwa ndiye kwlei mpakwa wa Mungu “Kristo mwana wa Mungu aliye hai”

Somo kwa ajili yetu

Yesu anakuja na hukumu kwa wale waliokataa kuona ishara za nyakati. Ishara tunazoweza kuona duniani juu ya kuondolewa kunakokuja kwa jamii hiii isyo na Mungu ziko wazi kama zile ishara ambazo Mafarisayo na Masadukayo waliziona lakini wakazidharau inapasa tuamini pia, ushahidi kutokana na mafunzo yetu ya kwamba Yesu kweli ndiye Kristo , mwana wa Mungu. Na tujibidishe kufanyika sehemu ya kusanyiko (Eklesia) lake lililojengwa juu ya kweli ya kukiri  kwa Petro. Kupitia funguo za ufalme injili imehubiriwa kwa wapagani na hivyo hivyo kwetu, hivi kwamba tuna tumaini la uzima wa milele. Kama vile Yesu alivyokufa na kufufuka tena ndivyo tutakuwa naye katika ufalme wake utakaokuja iwapo tupo tayari kuishi kama “wanafunzi” wake hivi sasa.

Maabara ya rejea

“A life of Jesus”(M.Purkis) pages 206-214.

“Nazarethi Revisited”(R.Roberts) chapters 36-37

“The story of the Bible”(H.P.Mansfield) vol 9 pages 149-166

Maswali ya fungu

  1. Ni nini ilikuwa ishara ya nabii Yona?
  2. Ni nini ilikuwa chachu ya Mafarisayo na Masdukayo?
  3. Nini kilicho muhimu hivyo kuhusu tamko la Petro ya kwamba Yesu ndiye Kristo mwana wa Mungu aliye hai?
  4. Ni mihimili gani 3 ya uanafunzi na zinakusikaje sasa?

Maswali ya insha

  1. Petro alimtamkia Yesu “wewe ndiye Kristo, mwana wa MUngu aliye hai” eleza
    1. Mazingira ya itikio (tamko) hila na
    2. Umuhimu wa tamko

 

Swahili Title
213. UPINZANI UNAJIKUSANYA KATIKA KIVULI CHA MSALABA
English files
African text
CSSA
Translator 1
Emanuel
Literature type
Sub type
Sub sub type