214. KUGEUKA SURA KWA YESU
“Huyu ni mwanangu mpendwa ninayependezwa naye, msikilizeni yeye”
Pale Kaisaria Filipo, Yesu aliwafundisha wanfunzi wake ya kwamba ingawa ilkuwa ya kwamba alikuwa ndiye Kristo mwana wa Mungu aliye hai, hata hivyo iliwapasa waelewe ya kwmaba angeliteseka kabala ya kupokea utukufu wa ufalme. Yesu akachukuwa fursa hii kuahidi wachache kati ya wanafunzi muonjo w aufalme huo.
Mmoja wao, Petro aliandika baadaye ya kwamba walikuwa “amashahidi wa uso kwa uso wa utukufu wake”. Tukio lile lilikuwa ni “kugeuka sura” kwa Yesu Mathayo 16:28; 17:13; Marko 9:1-3; Luka 9:28-36.
Mlima wa kugeuka sura
Wakati Yesu aliposema na wanafunzi wake kuhusu uanafunzi, aliwaambia, “wapo baadhi yao wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona mwana wa Adamu akija katika ufalme wake” au kama Marko asemavyo “hadi wawe wameuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu”(Mathayo 16:28; Marko 9:1). Juma moja baadaye Yesu aliwachukua wanfunzi watatu aliwaowapend asana Petro Yakobo na Yohana hadi kileleni mwa mlima mrefu (pengine moja ya vilele vifupi kidogo vya mlima Hermon)
Huko (Hapa) Yesu aligeuka sura (ikimaanisha kubadilika umbile) mbele yao, aliposali kwa baba yake mwonekano wake ulibadilika, sura yake ikang’aa “kama jua” kwa nuru ya ki-Mungu, na nguo zake zikawa nyeupe kama theluji (Mathayo 17:2; Marko 9:3; Luka 17:1-3)
Musa na ELiya (Mathayo 17:1-3)
Petro, Yakobo na Yohana walikuwa wamelala usingizi, kwa uchovu wa kupanda mlima na kipindi cha kusali kwa makini (au juhudi) pamoja na Yesu. Sasa waliamshwa na hali ya utukufu kuwazunguka. Wakamwona Bwana wao akizungumza na hawa watu wakuu, Musa na ELiaya ambao waliwakilisha sheria na manabii ambao alikuja kuwatimiliza. Wakti wakiogelia kifo cha Yesu wanafunzi watakuwa walishangaa kuhusu kifo cha Bwana wao kwani lilikuwa suala la wadhifa wa Masihi ambalo hawakulielewa na ambalo Petro alikuwa amelipinga kwa kutisemea hivi karibuni.
Wakiwa katika kuangalia kwa mshangao Eliya na Musa wakaanza kuondoka. Petro asijue jinsi ya kujibu lakini mwenye kushangazwa na tukio hili la kushitua na akitaka Musa na Eliaya wabaki, akatoa sauti kuu bla kufikiri “Bwana ni vyema kwetu kuwa hapa hapa, nasi tujenge hema tatu”(Luka 9:33). Huko jangwani kulikuwa na hema moja ambamo utukufu wa Mungu ulikaa lakini Petro alitaka hema tatu, ili utukufu huu ubakie pamoja na hawa watu watatu.
Huyu ndiye mwanangu mpendwa (Mathayo 17:4-5)
Wingu lenye mwanga (nuru) kali liliwazingira hivi kwamba wanafunzi walianguka kifudifudi kw ahofu. Kutokea ndnai ya wingu sauti kutoka mbinguni ilisema “huyu ni mwanangu mpendwa ninayependezwa naye msikieni yeye”
Ombi la ghafla na bila fikira la Petro lilijibiwa. Yesu halkuwa sawa na Musa na Eliya. Ngazi yake ilikuw akuuu mno kuwazidi ngazi yao, ailkuwa ni mwana wa Mungu aliye hai. Hawana budi kumsikiliza na kumwamini yeye, alisema baba kwani alitimiza sheria na manabii.
Alikuwa ndiye “neno lililofanyika mwili” na “mwana wa peke wa baba aliyejaa neema na kweli…. Kwani sheria ilitolewa na Musa, lakini neema na kweli zilikuja Yesu Kristo” Yohana 1:14,17
Mateso kabala ya utukufu (Mathyo 17:7-9)
Wakati huo mkono uliwagusa na sauti ijulikanayo ikasema”amkeni msiogope” wakitazama kote kote wakaona ya kwmaba wingu lilishaondoka na walikuwa peke yao na Yesu.
Wakaiwa katika kteremka kutoka mlimani aliwaagiza kutomwambia yeyote (au hata mmoja) juu ya waliloliona, hadi atakapofufuka kutoka kwa wafu. Maneno hayangaliweza kuelezea matukio waliyokuwa wameyashuhudia, nayo yangeleta upinzani tu, au kuamsha tamaa potofu kumfanya mfalme juu ya Israeli katika wakati ule. Kabla ya ule muonekano wa utukufu ule. Kabla ya ule muonekano wa utukufu ungetimia katika ufalme, mateso ya Yesu na kifo vilikuwa mbele yake. Wanafunzi hawakuweza kuelewa maana ya ufufo kwa sababu wakati ule waliamini kuwa ufalme ungeanzishwa upesi. Walakini, Yesu alieleza ya kuwa Yohana Mbatiza alikuwa ameuawa na hivyo mwana wa Adamu inampasa ateswe mikononi wa watu. Msalaba ungekuja kabala ya taji. Hata hivyo, maono ya utukufu wa daima ulikuwa mbele yake katika enzi ijayo inpasa ilimwimarisha Yesu wakati alipoendela katika njia ya kuendea msalaba.
Athari juu ya wanafunzi
Wale wanafunzi watatu hawangeweza kusahau maono yale ma huenda walitafakari juu yake mara nyingi wakati wa miaka migumu ya m,bele wakati walipokabili mateso kwa ajili ya Kristo. Katika 2Pero sura ya 1 mtume anarejea tukio aliandika “kwani hatukufuata kw aujanja ujanja hadithi za uwongo, tulipowajulisha ninyi nguvu na ujilio wa Bwana yetu Yesu Kristo, lakini tulikuwa mashahidi wa utukufu wake”. Kwani alipokea kutoka kwa baba heshima na utukufu, wakati ilipokuja sauti kama ile kwake kutoka kwenye utukufu wa ajabu “huyu ni mwanangu mpendwa amabye napendezwa naye”. Na sauti hii iliyotoka mbinguni tuliisikia tulipokuwa naye katika mlima mtakatifu (Mst 16-18)
Huu ulikuwa uthibitisho /uhakikisho wake Petro kwa makanisa (Eklesia) mpaya ya kwmaba maneno yake aaylikuw ayamevuna nay a kweli, yakithibitisha au yakiimarisha yale ya “watu watakatifu wa kale” kama vile Musa na Eliya (mst 21). Aiweza kwa kujiamini kuhakiki, katika. Mst 19 “tunalo pia neno la uhakika la unabii” la kweli (hakika) kwa sabau walikuwa wameona ufunuo binafsi wa utukufu wa Kristo kutoka kwa baba.
Nisaidie kutokuamini kwangu(Mathayo 17:14-21)
Kutokana na utukufu wa “vitu vya kimbingu” Yesu na wanafunzi wale watatu walirudi na kuwapata wale wanafunzi waliobaki tisa walibishana na baadhi ya waandishi wa Kiyahudi, na wakiwa wamezungukwa na watu wengi. Wengi a watu, alipomwona Yesu walikimbia na kumsalimia, wakiwa na hakika ya kwmaba angetatua tatizo.
Tatizo lilielezwa na mtu mmoja katika kundi. Alikuwa amemleta kwa wanafunzi mwanye, mwenye kifafa, amabye hakuweza kusema (alikuwa bubu) na amabye aliteseka na mishtuko iliyomfanya kuangukia motoni na majini. Wanafunzi hawakuza kumponya na hivyo kuchekwa na waandishi. Jinsi ilivyokuwa tofauti kati ya ishara tukufu kule juu kwenye mlima wa kugeuka sura na aibu ya kushindwa mbugani chini. Kana kwamba akiwa na shauku kwa ajili ya muda ambapo ufalme ungalikuja na mateso na madhaifu ya kiutu hayatakuwepo tena, akazungumza nao wote waandishi wenye dhihaka, wanafunzi waliobika na baba mwenye shauku “oh kizazi kisicho na imani, ni kw amuda gani zaidi nitabaki kuwa nanyi? Ni kwa muda gani wa ziada nitawavumilia? “mleteni kwangu”(mst 19)
Wakati yule mvulana akiletwa kwa Yesu mshituko ulimkaba kwa maumivu makuu, akaanguka chini, akitoa povu mdomoni, “ukiweza kufanya lolote, utuhurumie” akaomba baba yake. Akitambua udhaifu wa iamni yake, lakini yule baba akapaza sauti, “Bwana ninaamini” na kwa ari “nisadie kutoamini kwangu”
Kwa kukuri huku Yesu mara moja akasema na yule mvulana ili kumtibu na inagwa baadhi yao watazamamaji mwanzoni walidhani amekufa, aliamka mwenye kutibiwa (mzima) kukiri huyo kabisa, na wote waliohudhuria “walishangazwa kwa nguvu kuu za Mungu” (Luka 9:43)
Fundisho kwetu
Hatuna budi kuhamasishwa na habari ya kugeuka sura vile vile kama “shangwe” iliyowekewa mbele ya Bwana Yesu Kristo ilivyomsaidia kuvumilia mapaka mwisho” (Waebrania 12:2). Tujaribu kuonyesha maishani mwetu ile imani isiyolisikia ya mwana wa Mungu, ambaye Mungu alipendezwa naye. Inatupasa kukuza imani ya nguvu ingawaje tunaishi katika nyakati zenye utovu wa imani, kwani “bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu” (Waebrani 11:6), “lakini vitu vyote vinawezakana kwake yeye aaminiye” (marko 9;23). Kwa hakikisho hili tunaweza kuona siku z ambele kwa tumaini, na siyo kukata tamaa na kukanyaga mbele kwa kujiamini katika njia ya ufalme.
Tunatazama mbele hadi wakati ambapo ufalme wa Mungu utakapokuja kwa nguvu kugeuza jamii tunamoishi ambapo yule aliyeponya wagonjwa atatuponya yetu ya kufa au kutokudumu. Katika siku hiyo utukufu wa Mungu utaonekana ulimwenguni pote na ndani yao wote ambao katika siku hii wnamwamini yeye na mwanawe mtukufu.
Maktaba ya rejea
“A life of Jesus” (M.Purkis) book 5, chapter 8
“Nazarethi Revisited” (R. Roberts) chapter 37
“The story of the Bibli” (H.P. Mansfield) vol 9, pages 166-172
Maswali ya paragrafu
- Kwa nini Petro alitaka kujenga hema tatu mhali pa mageuko y sura na alijibiwa vipi?
- Ni kwa jinsi gani kugeuka sura kulimuimarisha Yesu?
- Kwa nini wanafunzi hawakuweza kumponya yule kifaa wakati wa kugeuja sura?
Maswali ya insha
- Fafanua matukio yaliyotokea wakati Yesu alipogeuka sura
- Eliya na Musa walikuw ana Yesu juu yam lima wa mageuko. Kw avipi ilibainka ya kwamba Yesu alikuw amkuu kuliko wote watatu
- Kugeuka sura kulikuwa na kusudi gani na ni somo gani hili?