Dibaji

Swahili

Dibaji

Katika miaka yangu 15 ya kwanza nikiwa mmishonari nilimfundisha “Ibilisi  na shetani” katika Afrika kwa njia ile ile niliyomfundisha huko ulaya, hatimaye mkitambua kwamba mimi na wamishonari wengine tunaitwa mara kwa mara  kueleza” Ibilisi na Shetani” kimsingi kwa sababu ya maelezo ya hapo awali yameshindwa kugusa vya kutosha mafundisho yaliyomo ndani ya mifumo yay a Imani ya zamani ambayo inaendelea kudumu ndani ya kusini mwa ulimwengu . Sikua ikifundisha katika muktadha. Walimu waliwageuza wale wa kusini mwa dunia  kwa kutumia ujuzi wao wa Biblia wa Imani za karne ya kwanza, lakini hii haifanyi kazi katika   kusini mwa ulimwengu. Juhudi zimefanywa kusini mwa dunia, kufundisha kwa kutumia njia zile zilezilizofanya kazi kaskazini badala ya kuelewa kwanza Imani ya zile ambazo walimu wanajaribu kufundishakusini na mazingira waliyokua wakifundisha. Haiwezekani ( na bila shaka ni kinyume cha maadili kama si ukoloni) ikiwa hujui chochote kuhusu mfumo huo wa Imani ambao unabishana nao. Lakini hivi ndivyo wengi hufanya nikiwemo mimi katika miaka hiyo kumi na tano ya kwanza.

Pia kuna dhana inayofanana miongoni mwa wale wanaotangaza ukweli wa Biblia kwamba watazamaji wa kusini mwa dunia watajua yaliyomo katika Biblia. Lakini kwa kawaida wale ewa kusini mwa ulimwengu wanatoka katika ulimwengu wa miungu  mingi na huenda hawakuwahi kusoma Biblia ikiwa kweli wanaweza kupata moja au uwezo wa kuisoma katika karne ya 19. Ulaya ya Dokta John Thomas ( na wengine) usomaji wa Biblia ulikua wa kawaida. Kila mtu alikua na Biblia yake na kila mtu aliweza kusoma katika karne ya 19 na kwa kiasi kidogo katika karne ya 20. Ulaya kila mtu alijua Biblia na alikua na maoni yake kuhusu vifungu mbalimbali vya Biblia. Hivi sivyo  ilivyo kabisa katika karne ya 21 Ulaya, lakini hii haijawahi kuwa hivyp katika ushirikina wa ulimwengu wa kusini. Bila shaka tunaweza kujifunza jinsi ya kuhubiri vyema zaidi katika kasrne ya 21 kaskazini kwa kujifunza jinsi ya kuhubiri vyema kusini. Mkitindo ya mahubiri ya Biblia ilibidi ibadilishwe katika karne ya 21 Ulaya iliendana na hadhira ya kisasa. Je, ni kwa kiasi gani tunahitaji kutathmini taratibu tunazotumia kutangaza injili barani Afrika ikiwa huwezi kuungana na wasikilizaji wako nusu ya vita tayari imepotea. Kwahiyo ni lazima wahubiri waelewe udongo ambao wanapanda mbegu ili watarajie ongezeko.

Imani nyingi za zamani zinapatana kabisa na ukristo na hata sayansi ya kisasa na fikra za kisasa zingine sio. Tunahitaji kujua tofauti. Kwa mfano: wahusika wakuu wa wazo kwamba ulimwengu wa  roho haupo watakuta wanabishana dhidi ya vipengele vya neon la mungu ambavyo wanaweza kudai kuwa watetezi wake. Wakati huo huo Imani Imani katika dhana zisizo sahihi za kimafundisho zinaweza kushikilia kwa waumini katika ukristo hadi wakati ambapo dhana hizi zinakua muhimu sana. Kushindwa kwa utaratibu mara nyingi hukutana na jamii nzima kutoelewa kile wanachodai kuamini kikatiba.

Kitabu chetu kitadhihirisha ujuzi mpya uliofichuliwa wa dini za asili za Kiafrika kulingana na kazi za watu wakubwa kama vile Kirsteen Kim na Amos Yong (miongoni mwa wengine), tutahalalisha  mifumo hii ya Imani inayokupa maarifa mapya ya kipekee ya kibiblia na hoja za majadiliano.  Kwa kutofautisha haya na mafundisho ya kitamaduni tunatumai yanaweza kukidhi hamu ya wale wanaosikiliza hotuba yetu katika ulimwengu wa kusini kupata mafundisho ya wazi juu ya mada hii muhimu ya Ibilisi huku akiwaagiza wale wa kaskazini mwa ulimwengu ambao hapo awali walikatishwa tamaa kutoka kwa ugunduzi kama huo. Ujuzi huu ulioelimika unapaswa kuwahimiza walimu katika kufundisha katika muktadha ( hii inatumika katika maeneo ya kaskazini na kusini) na hiyo italeta matokeo bora Zaidi.

Kitabu hiki pia kinajaribu kusahihisha kutokuelewana na mafundisho mengi ya uwongo yanayozunguka katika mada hii, huku tukijaribu kurekebisha mitazamo kuelekea mifumo ya Imani za kale.

Kitabu hiki basi kimeandikwa katika makundi ya msingi ya watu watatu.

. Wale wanaotaka kufundisha injili katika muktadha wa kusini mwa ulimwengu.

. wale wanaopenda kujifunza ukweli wa Biblia kutoka katika muktadha wa kusini mwa dunia.

. Na wale walio na shauku rahisi  katika utamaduni wa kale na mifumo ya Imani.

Kwakweli kuna vikundi vikubwa ambavyo vitapata maandishi yangu ya kupendeza.

Hatguwezi tu kufuta milenia ya utamaduni kama takataka za kishenzi bila kujua kile tunachoandika. Imani za kale zimekatwa sana katika akili ya mamilioni ya watu. Kwa uytafiti tunaweza kuelewa orodha na kugawanywa mafundisho ya kale. Baada ya kugawanywa tunaweza kuamua ni kwa kadri gani watu wa kale walielewa kweli. Kasha tunaweza kujenga hoja zenye nguvu ambazo zitapinga ukweli, hoja ambazo zitadumu kwa muda mrefu.hili litatoa utimamu wa kudumu Zaidi kwenye Imani zinazoamini Biblia.

Kwahiyo tunaanza mjadala wetu wa Ibilisi na Shetani, si kwa ufafanuzi wa  wa Biblia wa maneno ambayo Biblia hutumia kwa Ibilisi na Shetani ( vyanzo vingine hufanya vizuri Zaidi kuliko mimi) lakini kwa muhtasari wa kwanza wa kusini mwa ulimwengu ambamo ibilisi na shetani wanadaiwa kuwepo, basi tutaendelea kuweka hili dhidi ya msingi wa uelewaji wa biblia  katika ulimwengu war oho tukichukua uangalifu maalum ili kubaini makosa katika Imani za ulimwenguni.

Kirsteen king na Amos yong katika “ mazungumzo ya kiutamaduni na kidini juu ya ulimwengu uliojaa roho”(Palgrave Macmillan) wanakusanya maandishi ya kitaaluma kutoka kwa wataalamu wengi juu ya mada mbalimbali za pneumatolojia  kusoma asili” si kwa ajili ya watu wenye mioyo dhaifu” lakini kwa muhstasari. Vifungu hivi vinatoa ushahidi ili kufikia mahitimisho kadhaa bila uchache kwamba:-

  1. Mbinu za kimapokeo za kushughulikia mada ya ibilisi na shetani hazikabiliani na chanzo cha masuala ya kimafundisho katika muktadha wa kusini mwa ulimwengu.
  2. Wale wanaogeukia ukristo katika muktadha wa kusini mwa ulimwengu wana  uwezekano wa kubeba maweazo mengi ya kitamaduni ya ushirikina katika Imani zao za kikristo, kwa kubadilisha  tu misamiati na kwa ufanisi kutobadili Imani zao hata kidogo
  3. Waalimu wa injili wanahitaji kuelewa mawazo  ya kimapokeo ili kuhakikisha kwamba mafundisho yao yanapatana na malengo ya kujifunza kukubali mafundisho kupachikwa vya kutosha na mabadiliko ya mtindo wa maisha yanayoakisi mabadiliko ya Imani.
  4. Kwamba kwa uchaguzi wa bahati mbaya katika mwongozo wa maneno au shughuli, ufahamu usio sahihi unaweza kuimarishwa kwa wale tunaojaribu kuwaangazia.,

Kwa mahitimisho hayo, akili inaweza kuonekana  kuwa isiyo ya kawaida, kwamba tunaweza kujaribu kufundisha kwa kutumia hoja za kimapokeo. Lakini hoja za kimapokeo za kile ambacho Biblia inasema kuhusu Ibilisi na Shetani bado zinasimama na kufuata mantiki  kutoka katika mafundisho ya muktadha. Biblia haijabadilika; Mungu hajabadilika;Ukweli haubadiliki; ni muktadha tu na watazamaji ambao wamebadilika. Wala tusibadili mafundisho ya msingi ili yaendane na hadhira, hiyo itakua ni upotoshaji tu wa injili.  Ili kuhakikisha idadi kubwa Zaidi , kitabu chetu kitashughulikia muktadha , na hakirudii mafundisho ya kimapokeokama vile  “maandiko matakatifu” ( Ron Abel) yanafafanua vya kutosha.

Katika muktadha wa kiafrika mhubiri atalazimika kufanya Zaidi ya kuwasilisha tu hoja za kimapokeo ambazo kimsingi zilijengwa kwa ajili ya hadhira ya wazungu. Kwa hivyo kuna maelezo kuhusu jinsi fafanuzi zetu za kitamaduni zinaweza kuakisi katika muktadha wa kiafrika. Kitabu chetu kitashughulikia mtazamo wa ulimwengu kwa misingi ya uwazi. Kuhubiri “ ibilisi na shetani” katika muktadha wa kiafrika . Tungependekeza kuanza na hilo na sio nyendo za jadi ambayo kwa kawaida yanakuja baadaye kwa kusoma neon Takatifu la Mungu.

Maelezo

Mengi yaliyomo mkatika kitabu chetu yametumia maandishi ya wengine katika matukio mengi ambayo marekebisho machache yamefanywa kwa njia ya kuongezea. Kimsingi hii inatokana na ukweli kwamba, maandishi haya hayapatikani kwa urahisi katika lugha ya Kiswahili. Lakini  bila ambavyo hii itakuwa katika kiasi kidogo cha kushawishi, shukrani zetu ziwaendee waandishi hao kwa ruhusa yao ya fadhili kuruhusu utafsiri huu. Maelezo ya waandishi hawa na hati asili yatapatikana  katika sehemu zenye mafundisho mbalimbali.

 

Swahili Title
Dibaji
English files
Swahili file
Literature type