Exploring the Bible - 09

Swahili

IBRAHIMU AHESABIWA HAKI KWA IMANI

 

SOMO LA 9 MWANZO 14-15

 

Tumeona kuwa ile ahadi ambayo mungu alimpa Ibrahimu (mw.14-17) ilikuwa na tumaini lenye utukufu,si kwake tu bali kwa wale wote wanaochangia tumaini hilo naye kwa njia ya ubatizo katika Yesu Kristo.(Wagalatia 3:16,26-29)

Baada ya kupokea ahadi hii Ibrahimu alihamia Hebron kusini Mwa nchi ya Kanaani

Ibrahimu amwokoa Loti kifungoni(Mw.14:1-160)

Matukio ya sura hii yanaendelea kwenye makutano ya kupendeza kati ya Ibrahimu na Melkizedeki.Muungano wa tawala za kaskazini ulikuwa umeiweka Sodoma na miji mingine ya kusini ya mbali chini ya mamlaka yake.Baada ya miaka Kumi na tatu kupita Sodoma na hiyo miji mingine ilihasi,na wafalme wa tawala za Kaskazini wakiongozwa na Kedorlaomer walishuka kasi kuzima hayo maasi.

Vita iliyofuata ilifanyika”katika bonde la Siddim ambalo ni Bahari ya chumvi” (aya ya 3).Eneo hili lilikuwa lenye rutuba sanaenzi hizo(Mwanzo13:10) lakini tunaambiwa kuwa liliitwa”Bahari ya chumvi”kwa sababu ya msiba mkubwa uliotokea pale baadaye wakati Sodoma ilipoteketezwa(Mwanzo19:24-25).Wafalme wa kaskazini walishinda vita na wakatwaa mateka,Loti mpwa wa Ibrahimu akiwa mmojawapo wa mateka hao;naye wakati huu alikuwa akiishi Sodoma(aya ya 12)

Mtu mmoja aliyefanikiwa kutoroka,Mwebrania alikuja akamwambia Ibrahimu yaliyompata Loti(aya ya 13).Hii ilikuwa ndiyo mara ya kwanza ya neon Mwebrania kuonekana katika Biblia,lina maana ya “mtu ambaye tika upande mmoja kwenda upande mwingine”.Ni cheo alichopewa Ibrahimu kwa sababu alivuka mto Efrati baada ya kuwaacha ndugu zake na nchi yake, kwa kutii amri ya mungu(Mwanzo12:1-3).Ibrahimu akiwa na watumishi wake wachache alifuatilia na kupitia jeshi la tawala za kaskazini na kuwapindua usiku,(aya ya 15).Aliporudi,akiwa na Loti na watu wote na mali zao alilakiwa na wafalme wawili.

Mfalme wa Sodoma alitoka kwenda kumlaki Ibrahimu”katika bonde la Shaveh ambalo ni bonde la mfalme”(aya ya 17).Sasa tunajua kuwa wanaume wa Sodoma walikuwa waovu kupindukia(Mwanzo13:13) na hapa mfalme wa mji uliojulikana kwa uasherati alikuja kumlaki Ibrahimu ambaye alikuwa mchamungu.

Ibrahimu akutana na Melkizedeki,mfalme Kuhani(Mwanzo14:17-24)

Katika sehemu ile ile Melkizedeki mfalme wa Salem,naye alitoka kumlaki Ibrahimu,mfalme huyu alikuwa tofauti kabisa na mfalme wa Sodoma na yale yote aliyopendezwa nayo.Melkizedeki alikuwa mfalme lakini pia alikuwa kuhani wa mungu(aya ya 18).Ibrahimu alimshukuru Melkizedeki aliyekuja kumlaki akiwa na mkate na divai akimsifu mungu kwa kumnusuru Ibrahimu na adui zake.Kama kuhani mkuu angemtetea Ibrahimu wakati wa kumwabudu mungu

Mwandishi wa barua kwa Waebrania anatoa mafunzo mazuri kuhusu Yesu Kristu kutokana na tukio hili.Tunaona kwamba huyu mfalme/kuhani Melkizedeki anatuonyesha mapema madaraka ya Yesu Kristu kama mfalme na kuhani mkuu wa mungu.Katika Waebrania 5-7 anazungumzia jambo hili kama ifuatavyo:-

1.Mungu aliwahi kututabiria kuwa mtu alikuwa aja ambaye angekuwa”kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki”Zaburi 110:4.Mwandishi anaonyesha kuwa utabiri huu ulikuwa unumzungumzia Bwana watu Yesu Kristu(Waebrania 5:5-6;6:20;7:17,21)

2.Anaonyesha kuwa jina Melkizedeki ni muhimu sana.Limeundwa kwa maneno mawili ya Kiebrania ambayp ni Melchi maana yake”Mfalme wa Zedek maana yake “uadilifu”.Kwa hiyo Melkizedeki ni cheo-“Mfalme wa uadilifu”(Waebrania 7:1-2)

3.Pia anaonyesha kuwa neno”Salem”ambalo maana yake ni “amani”ni muhimu vilevile.Tukiweka hivi vyeo viwili pamoja tunaona kuwa mtu huyu hakuwa tu “Mfalme wa amani”(Waebrania 7:1-2).Anatuonyesha mapema utawala wa Yesu Kristu ambao utasifika kwa uadilifu na amani(Zaburi 72:7)

4.Bwana wetu Yesu Kristu yuko kuumeni kwa mungu mbinguni kama kuhani mkuu akiwatetea wale wanaomkaribia mungu kupitia kwake(Waebrania 7:3;10:21-22)

5.Ukuhani huu wa Kristu ambao ni mfano wa Melkizedeki ni mkuu zaidi kuliko ule uliokuwa umetolewa kwa Israel chini ya sheria ya Musa(Waebrania 7:7-10).Ukuhani wa mfano wa Warumi ulifikia mwisho.Ukuhani wa Yesu Kristu hautakuwa na mwisho kwa sababu Yesu ni wa milele

Kutokana na tukio hili katika maisha ya Ibrahimu tunaona kwamba Kuhani mkuu zaidi alitabiria kupitia kwa huyu Kuhani mkuu zaidi,Yesu Kristu,wale ambao wanajenga imani kama ya Ibrahimu na kubatizwa,kwao njia ya kwenda kwa mungu mbinguni iko wazi.

 

Ibrahimu anakataa kupokea mali ya Mfalme wa Sodoma

Ibrahimu alipokuwa amemaliza ibada yake na Melkizedeki,Mfalme wa Sodoma alijitokeza akiwa na wazo hili:”Nipe hao watu wewe uchukue mali”(aya ya 21).Jibu la Ibrahimu lilikuwa rahisi na linaonyesha imani yake thabiti kwa mungu:”Ninainua mkono wangu katika kiapo kwa mungu aliye juu,mmiliki wa mbingu na dunia,kwamba wala uzi wala kamba ya kiatu sitachukua,usuje ukasema”Ni mimi uliyemtajirisha Ibrahimu”(aya ya 22-23)

Ibrahimu hakutaka kuingiza nyumbani mwake kitu chochote kilichotokea kwa mojawapo ya jamii zisizomjua Mungu. Hivyo ndivyo alivyochukia mwenendo wa aina hiyo, kwamba aliapa kabisa kutochukua zawadi yoyote kutoka kwa mtu huyu. Mungu wake alikuwa amempa ushindi na aliridhika na kumwamini yeye. Kwa kuwa Mungu alikuwa “mmiliki wa mbingu na dunia” kama Ibrahimu alivyokiri basi Mfalme wa Sodoma asingeweza kumpa chochote ambacho hakikuwa mali ya Mungu.

Ingawa Loti alisikia na kushuhudia mjadala wote huu alirudi nyumbani kwake Sodoma. Alipaswa kutambua kwamba kwamba kubaki na Ibrahimu kungempa yeye na familia yake usalama na amani na kuwaweka katika mwenendo wa Ki-Mungu.

 

Ibrahimu anaahidiwa mzao (Mw. 15: 1-6)

Kufuatia tukio hili, ambalo linadhihirisha imani aliyokuwa nayo Ibrahimu katika uangalizi na ulinzi wa kupindukia wa mwenyezi Mungu, Mungu alimtokea tena akisema: “Usiogope, Ibrahimu: mimi ni ngao yako, na zawadi yako kubwa kabisa” (aya ya 1)

Ibrahimu alikuwa ameshamtangazia mfalme wa Sodoma tegemeo lake kamilifu kwa Mungu, na sasa Mungu alijitokeza na kuthibitisha kuwa angemlinda (kuwa “ngao” yake) na kumpa ridhiki (kuwa “zawadi yake kubwa).

Hata hivyo Ibrahimu alikuwa na swali lililomtatanisha sana. Mungu alikuwa amemuahidi yeye na mzao wake nchi ya Kanaani, lakini hadi wakati huo hakuwa na mtoto. Kwa hiyo akasema: Angalia, mimi hujanipa mtoto (aya ya 3)

Mungu alimjibu kwa kusisitiza ahadi yake ya kumpa mtoto wa kiume “huyo atakayetoka katika tumbo lakeo mwenyewe atakuwa mrithi wako” (aya ya 4). Akamtoa Ibrahimu nje chini ya anga lenye nyota na kumwambia atazame juu na kuhesabu nyota. “Ndivyo hivyo uzao wako utakavyokuwa,” Mungu akasema (aya ya 5). Siyo tu kwamba alimuahidi mtoto bali kwamba wazao wake watakuwa wengi kama nyota.

Taarifa hii ifuatayo ni mojawapo ya zile taarifa nzuri sana katika Biblia. Inaeleza kigezo ambacho Mungu atatumia katika kusamehe dhambi. Sasa tutazame kwa uangalifu kile kinachosemwa.

Aya ya 6

“alimwamini Bwana” Ingawa Ibrahimu hakujua itatokeaje lakini, hakuwa na shaka kwamba Mungu angetimiza ahadi yake. Katika hali ya kibinadamu ilikuwa haiwezekani kwa Ibrahimu na Sarah kupata watoto (Mwanzo 11:30; pia Warumi 4:16-22) na bado Ibrahimu aliamini maneno ya Mungu.

“aliamini” Tunapaswa kuelewa kuwa maneno “imani” na “kuamini” yana maana moja katika Biblia. Mfano wa hili unaonekana katika Warumi 3:22 – “Uadilifu wa Mungu kupitia imani katika Yesu Kristu, kwa ajili ya wote wanaoamini.” Hapa maneno “imani” na “amini” yanatokana na neno lile lile la Kigiriki katika manohishi ya awali na yanatumiwa, moja badala la lingine na Wafasili. Itatusaidia kuelewa kama tutakumbuka hilo kadiri tunavyoendelea na somo hili.

“Naye (Mungu) akamhesabia (Ibrahimu) kuwa uadilifu.” Mungu alihesabu imani ya Ibrahimu kuwa uadilifu. Imani ya Ibrahimu ilimtukuza Mungu na kwa hiyo Mungu akamhesabu kama mwadilifu. Mtume Paulo akitambua umuhimu wa hilo anatenga sura nzima katika barua yake kwa Warumi kueleza umuhimu wake (Warumi 4).

Na hapa inafaa tujue pia kuwa “haki” na adili ni maneno yatokanayo na neno moja kiGiriki. Kwa hiyo “kuhesabia haki” ni sawa na “kumfanya mtu, mwenye uadilifu.

 

Baraka ya uadilifu (Warumi 4:1-8)

Nini maana ya kutangazwa na Mungu kuwa Wadilifu?

Maana yake ni kwamba Mungu ametusamehe dhambi zetu. Katika Warumi 3: 10, Paulo anaonyesha “hakuna mtu mwenye haki hata mmoja” kwa kuwa wote wametenda dhambi na kukosa utukufu wa Mungu, (aya ya 23). Hata hivyo, Mungu, kwa huruma yake yu radhi kumwona mtu mwenye imani kuwa mwenye haki na kusamehe dhambi zake. Tukisoma Warumi 4:1-8) tutaliona hilo likiwa limewekwa wazi kabisa.

Wayahudi waliishi chini ya sheria ya Musa na wakajaribu kuitumia sheria hiyo kikamilifu. Hata hivyo walijiingiza katika mambo madogo madogo mno kwamba mara nyingi wakashindwa kuona yale ambayo Mungu alikuwa anawafundisha. Na kwa kweli, hawakuwa wakizingatia haja ya kumtii Mungu bali kuonekana kama waadilifu. Paulo anasema walikuwa wanajaribu “kuanzisha aina yao ya uadilifu.”

Lakini jitihada zao hazikuzaa matunda, kwa kuwa walishindwa kutimiza sheria kwa sababu kila mara ilikuwa inamulika upungufu wao na dhambi. Ilionyesha ukweli kwamba hawakuweza kutimiza. Kwa hiyo Paulo akaandika: Hakuna mtu atakayehesabiwa haki kwa njia ya matendo yanayozingatia sheria mbele ya Mungu kwa maana ujuzi sahihi juu ya dhambi ni kwa njia ya sheria (Warumi 3:20). Kwa hiyo, kwa sababu ya dhambi mtu hakuwa na matumaini ya kuhesabiwa haki mbele ya Mungu wake kwa kutii sheria.

Paulo anaendelea kuonyesha kuwa Mungu katika utukufu wake huwa anamuhukumu mtu kwa kigezo tofauti. Anamhukumu kwa imani yake. Mungu atamhesabia mtu “haki” kwa kigezo cha “imani” kwa sababu imani ya mtu inamtukuza. Anachukua maelezo haya kutoka Mwanzo 15:16 na kuyanukuu katika Warumi 4:3. “Ibrahimu alimwamini Mungu na imani hiyo ikahesabika kama haki.” Ibrahimu alihesabiwa haki, kwa hisani ya Mungu kwa sababu ya imani yake.

Halafu Paulo anaeleza faida ya kustaajabisha inayotokana na kuhesabiwa haki – baraka ya msamaha wa dhambi. Ananukuu mfano wa Daudi, ambaye aliandika kuhusu hili katika Zaburi 32: 1-2: “Daudi anaeleza kubarikiwa kwa mtu ambaye Mungu anamhesabia haki bila kuangalia matendo yake akisema, Wamebarikiwa wale ambao udhalimu wao umesamehewa na wale ambao dhambi zao zimefunikwa. Amebarikiwa mtu yule ambaye Mungu hatamhesabia dhambi “Warumi 4:6-8). Mungu katika huruma yake kuu alikuwa radhi kumsamehe Daudi kwa kuwa Daudi alikuwa mtu mwenye imani dhahiri aliyeungama na kutubu dhambi zake.

Kwa hiyo, hapa tumepata kigezo cha msamaha wa dhambi kikiwa kimeelezwa wazi kabisa. Ni kwa njia ya imani ndipo mtu anapohesabiwa haki (Warumi 5:1) Tukihesabiwa haki au kutangazwa kuwa waadilifu maana yake ni kwamba kwa hisani yake amesamehe dhambi zetu. Na hii ina maana kwamba tumepata upendeleo kwa Mungu. Sisi ambao ni watenda dhambi, kwa njia hii tumesuluhishwa na Mungu.

Paulo anamalizia sehemu hii kwa maneno haya yenye faraja: “Hata hivyo haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba alihesabiwa haki bali pia kwa ajili yetu ambao itahesabiwa kwa sababu tunamwamini yeye ambaye alimfufua Yesu kutoka katika wafu; aliyetolewa kwa sababu ya makosa yetu na kufufuliwa kwa ajili kututangaza sisi kama waadilifu.” (Warumi 4:23-25)

 

Ibrahimu apokea agano kuhusu nchi (Mwanzo 15: 7-21)

Baada ya kupata jibu la swali lake kuhusu mzao wake (15:13), Ibrahimu aliuliza swali kuhusu ahadi ya nchi. “Nitajuaje kuwa nitarithi nchi?” (aya ya 8) Mungu aliitikia kwa kufanya agano na Ibrahimu. Katika enzi za Biblia agano lilifanywa kwa kumkata mnyama vipande vipande na watu wawili wanaohusika na agano walikuwa wakitembea kati ya kipande na kipande (angalia pia Jeremia 34: 18-19) Ibrahimu kwa kumtii Mungu alichukuwa wanyama aliotaka Mungu na kuwakata sehemu sehemu na kuvipanga kama ilivyotakiwa. Siku nzima alishindwa akichunga visichukuliwe na ndege na jioni ilipofika alilala usingizi mzito ikiwa ishara ya kifo.

Halafu Mungu akamwambia Ibrahimu vipengele vya agano. Baada ya kifo chake uzao wake ungekwenda Misri na kuteswa huko na kufanywa watumwa. Lakini baada ya miaka 400 watarudi katika nchi walioahidiwa na Mungu, (aya ya 13-14). Mungu alikuwa anamwonyesha, pamoja na mambo mengine, kuwa agano lisingetekelezwa katika uhai wake.

Mungu alithibitisha ahadi yake kwa agano hili. Kuwepo kwake kulikoashiriwa na taa ya moto, ambayo ilipita kati ya vipande vya wanyama waliokatwakatwa kuonyesha kwamba Mungu mwenyewe alikuwa tayari kutimiza agano na ahadi. “Siku ile ile Mungu alifanya agano na Ibrahimu akisema ‘nitaupatia uzao wako nchi hii’ (aya ya 18). Hapo Mungu akamfahamisha mipaka ya nchi aliyoahidiwa ambayo ilikuwa “kutoka kwenye mto wa Misri hadi mto mkubwa, mto Efrati.

 

Katika sura hii tumeona kanuni mbili muhimu

  • Ibrahimu alihesabiwa haki kwa njia ya imani.

  • Mungu, kwa njia ya agano, alithibitisha Ahadi ya nchi aliyomuahidi Ibrahimu na uzao wake.

 

MASWALI – SOMO LA 9

  1. Melkizedeki alikuwa nani?

  2. Ni nani sasa Kuhani wa Midle kwa mfano wa Melkizedeki?

  3. imani ya Ibrahimu ilihesabiwa nini? (Mw. 15:6).

  4. Ni nini baraka ya kuhesabiwa haki na Mungu?

  5. Ni kitu gani tunachotakiwa kuonyesha mbele ya Mungu ili tuhesabiwe haki au tupewe sifa ya uadilifu?

  6. Mungu aliahidi kumpa nini Ibrahimu wakati huu?

 

 

 

Swahili Title
IBRAHIMU AHESABIWA HAKI KWA IMANI
Swahili file
Status
Added to Internet
African text
Christadelphian Bible Mission
Translator 1
Raphael Mkeya
Literature type