Mei 29

Swahili

Mei 29

Katika Yoshua kuna maelezo mengi ya kufaa tafakari ya leo, tuna mpaka na miji/vituo vya biashara vya Yuda. Baadhi ya majina ya miji hiyo ni magumu kutamka, baadhi tuliwahi kuyasikia tuliposoma mahali pengine katika Biblia, lakini mambo hayo yote yanathibitisha kwamba Mungu anapendezwa na maeneo ambayo watu wake waliishi na alipendezwa na mpaka wa kila kabila. Ukijumlisha, ninadhani inafika miji 120 ukiondoa vijiji, hii ni kwa Yuda tu! Kwa hiyo, Mungu anapendezwa kwa undani na maisha yetu. Subira ya Kalebu ilithawabishwa anapopata urithi wake, kwa hiyo ni lazima sisi pia tuwe na subira na kungojea wakati wa Mungu! Maelezo katika Isaya yanaweza kutatanisha pia, lakini hizi ni picha za kushangaza za kile kinachotokea, katika kesi hii ya taifa, ambayo tunamtegemea Mungu. Israeli waliitegemea Misri badala ya kumtegemea Mungu, na Mungu anaonyesha kupitia Isaya kwamba Misri itafedheheshwa na kuwa dhaifu. Kimsingi, Mungu anatuasa tumtegemee yeye tu, kila kitu ni cha muda tu, tunaweza kufikiria kuwa ni wazo zuri kwa wakati huo, lakini ni ubatili mtupu. Jambo la kusikitisha ni kwamba, Waisraeli walimwacha Mungu, hawakumsikiliza ili wasirudi Misri. Mataifa yote yanayozunguka Israeli yalipaswa kuwa dhaifu, hii ni kanuni thabiti katika maisha yetu ya Kikristo, kila kitu ambacho si cha Mungu ni dhaifu, ni cha muda tu. Tuna mfano mzuri wa jinsi ya kumweka Mungu mbele na juu ya haki zetu za kibinadamu katika Filemoni. Onesmo anaonekana kuwa alikuwa mtumwa wa Filemoni na alikimbia. Lakini, baadaye akawa Mkristo na ndugu wa Filemoni. Sasa, chini ya sheria ya nchi, Filemoni angeweza kumfanya Onesmo aadhibiwe, lakini Paulo alikuwa akimkumbusha kwamba alipaswa kuitikia akiwa Mkristo. Sasa alikuwa na madaraka tofautitofauti. Kwa hiyo, sote tunapaswa kutambua kwamba Mungu anapendezwa na undani wa maisha yetu. Tunapaswa kumtegemea Mungu kila wakati na si kumfananisha na kitu kingine chochote. Pia, tuna jukumu kama Wakristo katika maisha yetu ya kila siku kuwafikiria wengine na kutambua kwamba tumepewa uzima. Kanisa hukutana katika Nyumba ya Filemoni, hivyo hatuhitaji kila mara kuwa na kumbi za kuabudu! Mungu awabariki sana.

Swahili Title
Mei 29
Swahili file
Literature type
Month