Spirit 00 - Introduction and foreword

Swahili

Roho

Utangulizi na dibaji

Kazi ifuatayo ni matunda ya majadiliano kwa ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu kati yangu na Ndugu zangu wawili nchini Tanzania. Mara moja ikanidhihirikia kwamba, suala la Roho Mtakatifu halifahamiki vizuri hata miongoni mwa Ndugu wenye uelewa mkubwa nchini Tanzania, na kwamba tamaduni za asili bado zina ushawishi mkubwa miongoni mwao. Kwa uhakika niligundua kwamba nilitakiwa kujihoji kwanza imani yangu binafsi na uelewa wangu na ule wa wenza wangu kabla sijaendelea mbele zaidi.

Historia ya imani na utamaduni barani Afrika ni ile ya mambo ya roho za ulimwengu, uchawi na nguvu za giza; kuamini roho za mimea, wanyama na mambo ya asili. Kuamini katika mizimu, roho na nguvu za giza kutoka kwa waganga ni mambo yaliyokuwepo kwenye tamaduni za kale za Wanubi, Wabuganda, Wabunyoro, Waswahili wa Ukanda wa Pwani, Wazulu, watu wa jamii ya Almoravidi, Almohad na Wabantu. Haya mambo yamekuwepo kwa maelfu ya miaka, na tamaduni zilizodumu kwa mamia ya miaka kabla ya uwepo wa Tanzania ya leo. Imani hizi bado zimekuwa ni sehemu ya tamaduni za Kiafrika hadi Karne ya 21, na licha ya kuyakana haya mambo wakati wa ubatizo, bado imekuwa ngumu kuachana nayo moja kwa moja. Mara kwa mara imeonekana watu wakijaribu kuendeleza hizi tamaduni za asili sambasamba na Kweli licha ya kwamba mambo hayo kutochangamana kwa namna yoyote ile.

Kwahiyo, kadri niliyosafiri sehemu mbalimbali Tanzania kwa kipindi cha miaka 30 iliyopita, moja ya maswali ya kawaida niliyokuwa naulizwa ni “Roho Mtakatifu ni nini?” Mara kwa mara nimekuwa nikijibu kwa haraka kwamba “ni nguvu za Mungu”. Hili ni jibu sahihi kabisa takribani kwa mazingira yote, lakini sio sahihi na ni jibu lisilojitosheleza kwa wengine. Nimetumia brashi pana ili kujibu swali kwa haraka kutokana na ufinyu wa muda uliopo kwangu kutokana na uhalisia. Mwanazuoni mwerevu hatimae atauliza swali la nyongeza “lakini nguvu za Mungu ni nini?” na “nguvu za Mungu zinafanya vipi kazi?” Maswali haya nimeyasikia mara kwa mara, na ni maswali magumu sana kuyajibu. Mfululizo huu wa makala ni jaribio la kusahihisha sintofahamu inayoweza kuwepo kwa msomaji juu ya mada hii ambayo aghalabu haijaeleweka, na inajaribu kutoa jibu kamilifu ili kurekebisha majibu ya haraka yaliyokuwa yakitolewa na wamisionari wangu.

Chukulia kauli ifuatayo “bwana huyu amejawa na roho”. Je, namaanisha, bwana huyu ana zawadi za roho, bwana huyu ana furaha, bwana huyu ni mwingi wa bidi, bwana huyu ameangaziwa, bwana huyu anaongozwa na roho, bwana huyu ana nguvu, au bwana huyu ni mlevi? Hakika hatutajua endapo hakuna muktadha. Wakati mwingine lugha ni kitu cha ajabu, na kuitafsiri hufanya mambo kuwa mabaya zaidi. Kwenye lugha yetu ya Kiswahili tuna herufi 24. Inapotokea maneno yote yakadhibitiwa kuwa na urefu wa herufi nne pekee, kuna uwezekano wa kuwa na maneno tofauti 330,000. Lakini pamoja na hayo, bado Kiswahili kina maneno pungufu ya 15,000, na maneno mengi zaidi yenye urefu wa zaidi ya herufi neno. Kiukweli lugha yote ingeweza kuandikwa kwa herufi tatu tu kwa kila neno! Linganisha hili na lugha kama ya Kiingereza yenye zaidi ya maneno milioni mbili. Ndo maana haishangazi kuona neno moja la Kiswahili lina maana kadhaa; huku maana halisi ikitegemeana na muktadha wa matumizi ya neno husika.

Chukulia matumizi ya neno “Bwana” kwenye muktadha wa Kibiblia. Inaweza kuwa na maana ya mwanaume mtaani, mkuu, mwalimu, malaika, Bwana Yesu Kristo, au Mungu Baba. Wote wanatafsiriwa kwa neno hili “bwana”. Je, inashanganza kuona wasomaji wanashindwa kuelewa? Kwenye baadhi ya Biblia watafsiri wamejaribu kupunguza tatizo hilo kwa kutumia herufi kubwa. Kwa kuangalia mfano wetu “BWANA” inaonesha ni Mungu Baba ndie anayemaanishwa au “Yehova” (YHWH) kama ambavyo ingeonekana kupitia maandishi ya mwanzoni ya Kiebrania. Wakati “Bwana” ingeonesha ni Yesu na “bwana” ingeonesha ni mwanaume kutoka mtaani. Hii inasaidia kidogo. Lakini pamoja na jitihada hizo, wengi wamepotoshwa kwa kutafsiri vibaya vifungu kutokana na neno moja kuwa na matumizi mbalimbali au kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa uchache, kwa kiasi fulani shida hii imesababisha mafundisho ya uwongo kuhusu Utatu, ambao licha ya kuaminiwa na mamilioni ya watu lakini haya sio mafundisho ya Bibilia hata kidogo. Kiukweli neno Utatu halipo sehemu yoyote kwenye Biblia ya Muungano wa Kiswahili. Tafsiri zilizopo kwenye Biblia za Kiswahili kwa kiasi kikubwa zilitokana na matoleo ya Biblia za Kiingereza. Kwa mfano, Biblia ya Umoja ilitokana na toleo la Mfalme James au Toleo la Kiingereza Lililoidhinishwa. Hali hii imefanya tatizo kuwa kubwa zaidi kuliko kama Toleo la Biblia ya Kiswahili lingetokana moja kwa moja na muswada wa awali uliokuwa kwenye lugha ya Kiebrania na Kigiriki. Tafsiri za Kiingereza zilifanywa na watu ambao wakati tafsiri zinafanyika, tayari watu hao walikuwa na upendeleo wa imani ambazo zilikuwepo wakati huo. Aidha, kwenye Kiebrania na Kigiriki kuna maneno kadhaa ambayo yote yanatafsiriwa kwa neno la Kiingereza linalomaanisha roho au mbaya zaidi bado ni mzimu.i Kurejea kwenye maneno ya asili kutatusaidia kwa kiasi kikubwa katika mazingatio yetu.

Hakuna jipya kwa mengi ya haya ninayoaandika. Kiukweli kiasi kikubwa cha maelezo haya kinatokana na kazi za watu wengine huku kukiwa na mabadiliko machache yanayotakana na mwandishi wa sasa. Najisikia fahari kutumia kazi za watu wengine. Si kwamba nataka nipate sifa kupitia juhudi zao, lakini ni kwa sababu siwezi kuboresha kile ambacho tayari wameshakiandika. Sehemu hizi zinafafanuliwa na kuonyeshwa mwishoni. Hii ndio njia yangu ya kukiri kwamba maandiko yao ni bora zaidi kuliko ambavyo ningeweza kuandika. Kwa hivyo shukrani zangu ziende kwa waandishi wakubwa kama vile Dk. John Thomas, Robert Roberts, Ron Abel, H.P. Mansfield, ambao baadhi yao nimeanzisha nao urafiki mkubwa na nimenakili maandiko yao kwa kiwango kikubwa kutoka kwa wote hao.

Wakati muda wote nadumisha mada ya "Roho" itakumbukwa kuwa nimeingiza maandishi yenye muktadha wa ushawishi. Hii naamini husaidia kuinua maandishi yetu juu ya zoezi la kitaaluma na huleta mada kwenye uhalisia. Pale “tunaposimama mbele ya kiti cha hukumu ya Mungu” (Warumi 14:10) tutahukumiwa kwa Neno (Yohana 12:47-49, Warumi 2:12). Hatuwezi kuokolewa kwa kazi zetu (Waefeso 2:5,8) lakini tunaweza kuokolewa kwa kumpokea Mungu ndani yetu (Warumi 14:12). Kuelewa roho ni nini, na kuwa na Neno la Roho lililokaa ndani yetu, itakuwa ni nguzo muhimu katika kuyasikia maneno hayo “umefanya vizuri mtumishi mwema na mwaminifu” (Mathayo 25:21)

Mungu - Mkuu

Kama tulivyosema, Roho Mtakatifu ni nguvu ya Mungu. (Luka 1:35). Kwa maana hiyo, ambacho Roho Mtakatifu huwa anafanya ndicho ambacho Mungu anafanya. Kwa mfano, “Msaidizi, ambae ndie Roho Mtakatifu… atakufundisha mambo yote” (Yohana 14:26) ina maana kwamba, “Mungu atakufundisha mambo yote kupitia nguvu zake za Kimungu.” Hali kadhalika, ingawaje kimsingi Maandiko hayawezi “kusema” chochote, imeandikwa: “Maandiko Matakatifu yanasema hivi kwa Farao”(Warumi 9:17). Mungu alisema hivi, na mwandishi Wake mwanadamu, akiongozwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, aliirekodi kwa uaminifu. Katika nukuu hii kuna kuunganishwa kwa kile ambacho “Mungu anasema” na kile ambacho “Maandiko yanasema.” Hali kadhalika, inasemekana Roho Mtakatifu “anasema”, “kushuhudia”, na kuwa “msaidizi” wakati kiuhalisia ni Mungu ndie anasema, anashuhudia na kuwa msaidizi, kwa nguvu zake- Roho Mtakatifu.

Yohana 14:26iii

Lakini huyo Msaidizi, ambae ni Roho Mtakatifu… atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Yohana 15:26

Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi.”

Yohana 16:13,14
Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.”
Matendo 5:3
Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu, kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?”
Matendo 5:9
“…Mbona mmekula njama kumjaribu Roho wa Bwana?”
Matendo 5:32
Nasi ni mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.”
Matendo 8:16
(Kwa maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa amemshukia yeyote miongoni mwao: walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.)
Matendo 10:19
Wakati huo Petro alikuwa akifikiria juu ya yale maono, Roho Mtakatifu akamwambia, Kuna watu watatu wanakufuta.”
Matendo 13:2
Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”
Matendo 15:28
Kwa maana Roho Mtakatifu ameona vyema, na sisi tume kubaliana tusiwatwike mzigo mkubwa zaidi ya mambo haya ya muhimu”
Matendo 16:6
Sasa baada ya kuwa wamesafiri kupitia Firigia na mkoa wa Galatia, kwa sababu Roho Mtakatifu aliwazuia wasihubiri neno sehemu za Asia.”
1 Wakorintho 12:11
Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.”
Waebrania 3:7
Kwa hiyo (kama asemavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake,”
Kwa msingi wa vifungu hivyo hapo juu, waumini wa Utatu wanadai kwamba Roho Mtakatifu yupo sawa na Mungu Baba na Mungu Mwana na pia ni Mtu shirika kwenye uzima wa milele.
  1. Roho Mtakatifu anaweza kuoneshwa kuwa ni nguvu kwa kulinganisha vifungu vifuatavyo kwa umakini:

    1. Mwanzo. 1:1, 2 - " Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia... Na Roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji." Lakini marejeo mengine kuhusu uumbaji yanatoa sifa ya kazi hiyo kwa nguvu za Mungu. Fikiria vifungu vifuatavyo:

      1. " Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio katika nchi, kwa uweza wangu mkuu..." (Yeremia. 27:5).

      2. " Ameiumba dunia kwa uweza wake..." (Yeremia. 51:15 cp. 10:12).

      3. "Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake..." (Zaburi. 33:6). Kifungu cha miwsho kinaeleweka ikiwa Roho Mtakatifu ni nguvu, yaani ndie mwenye uweza lakini lugha iliyotumika sio sahihi endapo, kwa kweli, Roho Mtakatifu ni Mtu mwenye uweza wa hali ya juu, mwenye nguvu nyingi, na mjuzi anayeishi ndani ya Mungu.

    2. Waebrania 6:4, 5 – “Kwa maana haiwezekani tena kuwarejesha katika toba watu ambao waliwahi kuongoka, na wameonja zawadi ya mbinguni, na wakashiriki Roho Mtakatifu, Na wameonja uzuri wa neno la Mungu na nguvu za nyakati zijazo…” Roho Mtakatifu anahusishwa na “nguvu ya nyakati zijazo”

    3. Luka 1:35 - "...Roho Mtakatifu atakushukia na nguvu za Mungu Mkuu zitakufunika kama kivuli.” Muundo sambamba unaonesha kwamba, “Roho Mtakatifu” ni sawa na “nguvu za Mungu Mkuu”

    4. IsaYA 11:2 - "Na roho ya BWANA atakaa juu yake..." Hii imefasiriwa kwenye Agano Jipya kuwa “"Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu. (Matendo 10:38).

  2. Ilikuwa ni nguvu ya Mungu Mkuu ambayo ndiyo “ilimfanyia kivuli” Maria (Luka 1:35). Lakini endapo Roho Mtakatifu angekuwa ni Mtu ndani ya Mungu Mkuu, basi, Roho Mtakatifu na sio Baba, ndie baba halisi wa Yesu.

  3. Yesu alipuliza juu ya wanafunzi wake, na wakampokea Roho Mtakatifu. (Yohana 20:22). Lugha hii inaeleweka ikiwa nguvu ilifikishwa, lakini sio sahihi ikiwa Roho Mtakatifu alikuwa ni Mtu wa Mungu.

  4. Hali kadhalika, Roho Mtakatifu alisambazwa kwa kuweka mikono ya watu. (Matendo 8:17-19). Huu ulikuwa ni usambazaji wa Mungu Nafsi ndani ya Mungu Mkuu?

  5. Roho Mtakatifu alitolewa “bila kipimo” kwa Yesu. (Yohana 3:34). “Bila kipimo” ni maelezo sahihi kuhusu nguvu za Roho Mtakatifu, lakini sio aina ya lugha inayohusiana na mtu. (Linganisha na Matendo 10:44 “Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wanasikiliza neno.” Na pia Matendo 2:17 “Nitawaminia Roho wangu”

  6. Mungu alimtuma Roho Mtakatifu akampake Yesu mafuta (Mathayo 3:16, Luka 4:16). Je, inaaminika kwamba “Mungu Baba” alimtuma “Mungu Roho Mtakatifu” kwenda kumpaka mafuta, yaani kumtakasa “Mungu Mwana” kwa “Mungu Roho Mtakatifu?”

  7. Katika ufunguiaji wa nyaraka 17 na ombi la neema na amani, ni katika moja tu ndimo Roho Mtakatifu ametajwa, na kisha kama njia ya utakaso. (1 Petro 1:2), na sio chanzo cha neema. Kwanini ombi kwa Mungu na Yesu, na sio kwa Roho Mtakatifu, ikiwa Roho Mtakatifu alikuwa ni Mtu ndani ya Mungu? Hali kadhalika, katika matukio 11 ya kutoa shukrani au baraka ambayo hufuatia maombi kwenye nyaraka, hakuna hata moja iliyotaja juu ya Roho Mtakatifu.

  8. Agizo la Kimungu limewekwa kupitia 1 Wakorintho 11:13. “Lakini ninataka mjue kwamba kichwa cha kila mwanamume ni Kristo; na kichwa cha mwanamke ni mwanamume; na kichwa cha Kristo ni Mungu.” Kama Roho Mtakatifu ni mtu, ni kwanini basi hajatajwa?

  9. Yesu alitoa maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu, (Matendo 1:1,2). Je, hii ilikuwa ni moja iliyo sawa akiiagiza nyingine iliyo sawa?

  10. Ingawaje imeelezwa kwamba Roho Mtakatifu (yaani, "Msaidizi") angefanya makao yake ndani ya wanafunzi, (Yohana 14: 16,17), hii si lazima imaanishe utu wa Roho Mtakatifu, kwa kuwa wote wawili, yaani Baba na Mwana (katika muktadha huo) pia ilikuwa wafanye makao yao kwa wanafunzi. (Yohana 14:23). Ni wazi basi, Mungu na Mwanae wangebaki kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Kama Yesu alivyosema, "Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi.." (Yohana 15: 26).

  11. Roho Mtakatifu alitokea kama "njiwa", (Mathayo 3:16), kama "ndimi za moto", (Matendo 2:3), na iliambatana na sauti ya upepo wenye nguvu unaovuma, (Matendo 2:2). Ikiwa Roho Mtakatifu alikuwa Mtu, kwa nini Watheofania wapo tofauti sana na wale wa Baba? (Kutoka 33: 18-23; 34: 5-7).

  12. Kwa nini Roho Mtakatifu haonyeshwi akiwa ameketi kwenye kiti cha enzi cha Mungu? (Angalia Ufunuo. 7:10 - "Wokovu unatoka kwa Mungu wetu, anayeketi kwenye kiti cha ufalme,na kwa Mwanakondoo." Pia Matendo 7:55, 56) Kwanini Roho Mtakatifu hatajwi?

  13. Utu wa Roho Mtakatifu wakati mwingine hutolewa kutoka kwa Luka 12:10 - "Na kila mtu anayesema neno baya kumhusu Mwana wa binadamu atasamehewa, lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa " Lakini kifungu hiki kinathibitisha mengi. Watu wa Utatu kutoka Orthodox wanadai kuwa Roho Mtakatifu ni sawa na Baba na Mwana, lakini tafsiri yao ya kifungu hiki inamfanya Roho Mtakatifu kuwa juu ya Baba na Mwana, na kwa kuwa ni kosa kubwa kutenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu, kuliko ama dhidi ya Baba au Mwana.

Imani ya Waathanasia inasomeka kama ifuatavyo: "...Lakini Mungu wa Baba, wa Mwana, na wa Roho Mtakatifu, wote ni moja: Utukufu wao ni sawa, Ufalme wao ni wa milele... Lakini Watu wote watatu wapo milele kwa pamoja: na wapo sawa. " Imechapishwa tena katika Percy White, The Doctrine of The Trinity: Analytically Examined and Refuted, (London: "The Dawn" Book Supply, 1937), Uk. 49, 50.

  1. Neno "roho" (nafsi) katika maandishi ya Kigiriki ni isiyo na jinsia, na kwa hivyo, yenyewe ikisimama peke yake, haimaanishi utu. Jambo hili linaweza kuonyeshwa katika maandishi ya Matendo 8:16: ". "Ambao wakashuka kwenda huko, wakasali kwa ajili yao ili wapate Roho Mtakatifu; kwa maana bado haikuwa imekuja juu ya yeyote kati yao, bali walikuwa wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu." Tafsiri ya haraka kwa kiwakilishi husika ni "roho" ambayo haina jinsia, na kwa hivyo ni kiwakilishi kisicho na jinsia. Tafsiri zingine nyingi zinawakilisha "kutokuwa na jinsia" badala ya kiwakilishi kubeba jinsia ya kiume. Tazama kwa mfano: N.W.T., Diaglott, Rotherham's, The Emphasised Bible.

Hivyo basi, kwa mujibu wa Bibilia, Roho Mtakatifu sio sehemu ya Mungu. Kwa hakika, neno Utatu halipatikani popote katika maandiko. Wazo zima la Utatu sio la Kimaandiko na imani ya Wathanasia iligundulika kuwa ni potofu.

i Word studies on the Holy Spirit – E.W. Bullinger ISBN 978-0-8254-2246-1

Swahili Title
Utangulizi na dibaji
English files
Swahili file
Literature type
Sub type