Sura ya 1. Jiwe la mwanafalsafa wa Biblia

Swahili

Sura ya 1. Jiwe la mwanafalsafa wa Biblia

Utangulizi

Mifumo mingi ya Imani za kale haijawahi kuandikwa; ni mapokeo simulizi ambayoyamepitishwa kutoka kizazi. Hadithi nyingi za asili sasa zimepotea hatutazisikia tena. Bado, hata pale ambapo hadithi za asili zinapotea sehemu kubwa ya itikadi za kitamaduni zinazohusiana zinabaki. Hii ni kweli katika jamii zetu kama ilivyo kwa watu wa kale. Tuna maneno mengi ya kipekee ambayo pengine hatutajua asili ya misemo hiyo, bado tunayo. Kwanini watu hutupa chumvi iliyomwagika mabegani mwao? Tungejitahidi kupata asili katika kina cha historia. Hadithi asilia pengine ni maelfu ya miaka na imepotea milele.

Dini ya kikristo inatofautiana na hii. Ingawa kuna mapokeo mengi ya kiyahudi ya mdomo, kwa kiasi kikubwa hadithi za asili zimeandikwa kwa njia isiyoweza kufutika. Kutokana na uvumbuzi wa uandishi hasa huko Mesopotamia, tunayo Biblia, maktaba ya vitabu 66 ambavyo watu wa ndugu katika kristo wanaamini kuwa ni “Neno la Mungu lililohamasishwa”.

Kama wakristo, tunakubali mamlaka ya Biblia bila ubaguzi[1]. Lakini tutathibitishaje mamlaka ya Biblia? Baada yavitabu vingine vyote kuchunguzwa na kupatikana kutoa madai kama hayo. Nini kinachotufanya kufikiri kwamba Biblia ni bora kuliko vitabu hivyo?  Na kwanini tulikubali Biblia juu ya maneno ya mababu zetu?

Katika surah ii ya kwanza, tutajaribu kuzungumzia mada hii; na kujaribu kuthibitisha Biblia kuwa mamlaka PEKEE ambayo kwayo tunaweza kuamini.

Biblia iliongozwa na Roho na kweli

Wakati wanyama au mimea vinapoashiriana, uhakika wa ishara hiyo kimsingi ni kwa manufaa binafsi. Chukua mwigo wa Betesian[2]. Hii inahusisha, kwa mfano, kipepeo ambaye ana rangi inayozuia wanyama wanaowinda wanyama wengine kwasababu anaonekana kama spishi nyingineambayo ni sumu. Kipepeo anadanganya ili kujihifadhi. Lugha na uandishi wa vitabu vilivyotengenezwa kwa mtindo sawa na huu. Tukiangalia maandishi ya zamani Zaidi ni hesabu narisiti za kujinufaisha na uhifadhi wa kibinafsi. Babu (Aina za zamani za makuhani) na Sherman wamepata mengi kwa kuonekana kuwa njia pekee ya kuwasiliana na miungu. Kabila la walawi la Israeli halikulazimika kufanya kazi. (Kumb 18:1-2) kwa njia ya kawaida na kwa njia nyingi walipata kilicho bora Zaidi kuliko kila kitu. Ilikua vyema kwa walawi kuendeleza “hadithi za Biblia” hata kama wao wnyewe walizionahadithi hizo kuwa za uwongo “Babu” wanapata wapi mapato yao leo?

Watu wengi wanaamini (hata leo) kuwa dunia ni tambarare. Hadi nyakati za hivi karibuni Imani hiyo ilikua ngumu sana kukanusha. Ndio, kulikua na hesabu nyingi za kupendeza ambazo zinathibitisha hivyo lakini badoilikua ngumu kuthibitisha kwa mtu wa kawaida. Kasha mwanadamu akaanzisha ndege za kuruka na hatimaye akachukua vyombo vya angani. Wakati wafanyakazi swa chombo hiki walipotazama nyuma walipiga picha za dunia. Dunia haionekani tambarare kutoka anga ya juu. Bado kuna watu wenye kutilia shaka, wengine wanasema kwamba hatukuwahi kwenda mwezini na wengine wanasema picha hizo ni za uwongo. Unaweza kuamini kwamba ni wachache leo wanaofikiri kwamba dunia ni tambarare, yaani ikiwa hujakutana na mtu yeyote anayeishi kwa njia za kitamaduni ana Imani za kale za kusini mwa dunia au kukutana na mtu kutoka jumuiya dunia ya tambarare.

Imesemwa mara nyingi kwamba Imani katika Biblia ni suala la kuamini. Aidha unaiamini au huiamini. Kwa njia nyingi ambayo ni kweli. Hata hivyo kuna ushahidi mwingi unaothibitisha kuwa Biblia si kitabu cha kawaida. Ushafidi huu unaweza kukuzwa hadi kuwa uthibitisho. Uthibitisho usioweza kuhojiwa kwani ushahidi hauna shaka. Kuthibitisha kuwa Biblia ni kweli kunaweza kuwa kama kujaribu kuthibitisha kwamba dunia si tambarare. Ikiwa watu watatilia shaka picha zilizopigwa kutoka kwa satelaiti inayozunguka dunia, bila shaka watatilia shaka Imani yako katika Biblia yako ya zamani iliyopigwa. Waweza hata kukufikisha mahali pa kuhoji Imani yako ikiwa hauko tayari kwa mashambulizi.       

Halafu hata ukithibitisha kwamba Biblia ni kweli; basi unathibitishaje kwamba ndiyo mamlaka pekee juu ya mambo haya? Mafundisho ya kaballah  (na mengineyo) yanasisitiza kwamba mwanadamu anaweza kuingia katika hali iliyobadilika ya akili na hawezi tu kuwasiliana  tumoja kwa moja na Mungu kwenye keter[3] bali kukutana naye kama watu na kujadili mambo moja kwa moja.

“kukosa uwezo wa kujiheshimu pia ni sababu kuu ya watu wengi kushikamana na Imani za mababu zao na kuziweka mbele tungetegemea watu wategemee Imani zao juu ya hoja zenye mantiki ambazo hawaziamini. Badala yake kushindwa kuacha Imani Fulani iliyopendwa kwa muda mrefu wakati ushahidi mpya unatokea, kinyume chake ni jambo la kawaida. Ni vigumu kwa mtu yeyote ambaye amejijengea sifa miongoni mwa rika lake na pengine kuwa na misingi yake. Maisha yote juu ya Imani ya kukubali kuwa na makosa na kupoteza uso na uwezo wa dhihaka” (Richard Swifte Darmstadt Ujerumani 12/2021).

Petro anaiweka kama kanuni ya msingi ambayo Biblia imehamasisha. “mkijua neon hili kwanza ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kutafsiriwa kama apendavyo mtu binafsi; maana unabii ule haukuletwa kwa mapenzi ya mwanadamu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa mungu, wakiongozwa na roho mtakatifu” (2 Petro. 1:20-21).

Lakini ni ushuhuda wa ajabu wa unabii unaoonyesha kwamba Biblia si ya kweli tu bali unabii wa kimungu unaoonyesha kwamba mungu ndiye mtungaji wake kwa maana yeye pekee ndiye angeweza kutabiri mambo yajayo kwa njia ya ajabu. Jinsi tunavyoona hapa. Hakuna kiasi cha unajimu wa kukasirisha au ugumu katika matokeo ya utabiri sahihi ambayo tunayapata katika Biblia.

  • Babeli bado iko kwenye lundo (Isaya. 13:19-21; Yer. 51:37).
  • Ninawi bado iko tupu na ulkiwa (Nahumu 2:10).
  • Misri ni miongoni mwa mataifa duni Zaidi (Eze 29:15).
  • Tairi Imezamishwa na bahari na ni mahali halisi pa kutandaza nyavu (Eze 26:15).
  • Israeli imetawanywa kati ya mataifa yote (kumb 28:64) na inakusanywa tena (Yer 30:11; Eze 37:21-22).
  • Muungano wa kaskazini wenye uadui dhidi ya Israeli umestawi (Eze 38:2-7, 15-16) kazi bora Zaidi.

Kipande bwana

Kwamba Biblia ni kazi bora ya uandishi ni kazi bora isiyo na shaka. Imefafanuliwa kama kumenya tabaka za kitunguu, wazo hili lilianza kipindi cha miaka 400 kabla ya Yesu[4], ingawa ni vigumu kubainisha nani alianzisha tamathali hii. Mara tu unapoelewa Biblia katika kiwango kimoja, inawezekana “kupepeta nyuma” kila safu ambayo inaongoza kwa uelewa  wa kina (au mwelekeo) wa maandishi. Tabaka hizi mara nyingi zinaweza kupatikana kwa undani Zaidi kuliko hata safu nne za jadi.

Pia kuna muundo kwa mfano “chiasmus” na “acrostics” iliyopachikwa kwa uangalifu  ambapo haungetarajia kuwa na miundo kama hiyo.

Inapatikana hata kwa kompyuta ya kisasa kwamba kuna ujumbe uliowekwa katika maandishi ya asili ya kiebrania na kigiriki (Drosnin, 2003).

Kuna ukamilifu kabisa na mamlaka ambayo yanaweza kuhisiwa katika kila neon na kila fungu la maneno tunayosoma katika Biblia. Ni sawa na yale yanayosemwa na maofisa walioagizwa kumkamata Bwana Yesu kwenye siku kuu “hakuna mtu aliyesema kamwe kama mtu huyu” (Yohana 7:46). Wale maofisa hawakumtii mkuu wao wa jeshi kwasababu waliguswa sana na maneno amnbayo Yesu alisema. Hakukuwa na kukana mamlaka yake. Hii ndiyo hisia hasa tunayopata tunaposoma Biblia. Ni jambo tukufu zuri na lenye neema.

Bilashaka Biblia ni kazi bora. Bila shaka kuna vitabu vingine huko nje ambavyo ni bora lakini kati ya mamilioni ya vitabu ambavyo vimeandikwa kwa karne nyingi Biblia inajitokeza  kwa ubishi juu ya vyote.

Kitabu cha ajabu Zaidi ulimwenguni

Wasomi wengi wa Biblia wanaamini kitabu cha Mwanzo kilikua kitabu cha kwanza cha Biblia kilichoandikwa; ingawa kuna ushahidi Fulani kswamba kitabu cha Ayubu kinaweza kuwa kimekuja mapema kidogo. Hii ilitokea karibu miaka 1400 hadi 1450 kabla ya Kristo. Kuweka hii katika muktadha huu ni katika zama za kati za maandishi ya shaba; karibu enzi ya mwandiko wa kiebrania wa paleo wakati alfabeti zilipokuwa changa wakati watu wengi wa ulimwengu walikua  bado wanaandika katika maandishi ya kjutumia picha ikiwa walikua na uwezo wa kuandika kabisa.

Taratibu za mapema Zaidi tunazojua ni za kipindi cha mapema cha nasaba ya misri Mesopotamia na Sumerian (mfumo wa kuandika huko Mesopotamia ya kale 2013) ambayo iliibuka bila ya kila mmoja kutoka takribani 3500 kabla ya Kristo. Kwahiyo rekodi za kihistoria zilikuwepo kwa karibia miaka 2000 kabla ya biblia kuandikwa. Biblia si kitabu cha kale Zaidi cha historia kinachopatikana lakini mwanahistoria yeyote mzuri atakuambia ndicho kitabu chenye kutegemeka Zaidi.

Mwalimu wangu wa historia alinifundisha kuwa sababu ya sisi kusoma historia ni ili tusifanye makosa ya siku za nyuma. Ilikua ni miaka tu ndipo baadaye nilipogundua kwamba pengine alikua anamnukuu vibaya mwanafalsafa wa kihispania George Santayana ambaye anaripotiwa kusema “wale wasioweza kukumbuka yaliyopita wanahukumiwa kuyarudia”. Hakika hii ndiyo sababu mojawapo kubwa inayotufanya tusome Biblia. Hakuna kitabu kinachoweza kulinganishwa na Biblia inapohusu kujifunza kutoka kwa wakati uliopita ili kutufundisha jinsi ya kuishi Leona wakati ujao.

Kati ya vitabu kumi vya zamani vilivyosalia ambavyo tunavyo ni Biblia na viwili ni vitabu[5] vya Tenzi vya Biblia na kimoja ni kitabu cha maombi cha kiyahudi “vitabu vya kukunjwa vya Bahari ya chumvi” ni vya miaka ya 300 kabla ya Kristo.

Kwa sasa kuna Lugha 7,117 zinazojulikana. Muungano wa vyama vya Biblia uliripoti kwamba “Biblia ikiwa nzima au sehenu imetafsiriwa katika lugha Zaidi ya 3,324” (mambo muhimu katika Biblia kupatikana. U.B.S).

Biblia ndio msingi wa dini tatu kuu za ulimwengu, Ukristo, Uyahudi, na Uislamu. Mamilioni  ya watu wamefikia kuamini katika Biblia kama chanzo cha mamlaka na mwongozo katika maisha yao. Ndugu katika Kristo ni miongoni mwa watu ambao wameamini na kuiamini Biblia. Ingawa ni kweli kwamba kwa sababu tu wengine wanaamini jambo Fulani haimainishi mimi lazima hata hivyo ikiwa wengine wanaamini haimainishi inafaa kuwekeza wakati na nguvu ili kuona m ambno haya ni ya kweli hasa ikiwa tunaweza kupata manufaa makubwa kutoka chanzo hiki.

Katika enzi ya kutoheshimika na uyakinifu ambapo kutoheshimu mapokeo ya kale kumekaribia kuwa  mtindo, biblia bado imeweza kuhifadhi kitu chenye sifa ya kipekee lakini imetiwa madoa na damu ya madoa. Katika ulimwengu wa kusini biblia itafichwa na inaweza hata kutemewa mate.

Biblia imetumiwa vibaya na wakoloni Desmond Tatu aliwahi kusemawamisionari walipokuja Afrika walikua na Biblia na sisi tulikua nan chi. Walisema, Tuoombe’ tulifunga macho. Tulipofungua tulikua na Biblia na walikua na ardhi”. Tutu aeleza jinsi waafrika weusi wengi wanavyohisi kuhusu Biblia. walowezi wa kikoloni wa kizungu waliotumia Biblia kuwanyonya waafrika weusi kuwa Biblia kimsingi ni propaganda za wazungu.

Hisia hii ni maarufu katika sehemu kubwa ya Afrika. Nchini Tanzania mara kwa mara tunakutana na watu wenye kutilia shaka ambao wanauliza mioyonio mwao au kwa sauti kubwa “kwanini niiamini Biblia ya  kikoloni? Nikiwa na mawazo kama haya tutasema nini? Je, kuna ukweli wowote kwenye nukuu ya Tutu? Ndivyo wakoloni wengi weupe walitumia Biblia kuwanyonya waafrika weusi. Lakini kwanini tuifute Biblia kwa sababu hyao? Kwakweli nitabisha… kwamba maovu ya ukoloni kwa uhakika ukweli wa Biblia… hebu tuweke jambo moja sawa kwamba Biblia haikuundwa na wazungu” (Je, Tunaweza kuamini ‘ Biblia ya kikoloni//Jeremiah Von Kuhn2022).

Ukoloni umefanya mengi kuchafua Biblia, lakini unasimama kichwa na mabega juu ya yote makuu Zaidi katika Fasihi ya ulimwengu na una madai makubwa juu ya tahadhari na heshima yetu. Wacha tuipe nafasi inayostahili.

Biashara kubwa

Kununua na kuuza Biblia ni biashara kubwa. Kitabu cha kumbukumbu kinakadiria idadi hiyo kuwa Zaidi ya nakala bilioni 7 zilizochapishwa na kuiweka Biblia kama kitabu kinachouzwa Zaidi wakati wote. Ikizingatiwa kuwa kuna watu bilioni 7 tu kwenye sayari hiyo, hiyo ina maana kuna kutosha kwa kila mwanadamu aliye hai kuwa na nakala ya Biblia mikononi mwake (ingawa baadhi ya watu wenye pupa kama mimi wanaweza kuwa na nakala Zaidi ya mia moja). Makundi mawili hasa yamejitahidi kufanya. Hili lilitokee akina Gideon na jumuiya ya Biblia. Jambo linguine la kushangaza ni kwamba katika nchi za magharibi  nyingi ya Biblia hizo ni za kumbukumbu.

Ukweli mwingine wa kustaajabisha ni kwamba katika nchi za magharibi nyingi ya Biblia hizo hubaki kwenye rafu za vitabu zikiwa zimetiwa muhuri kwenye kanga zao za asili na kupata vumbi. Hili kwa akili ya mtu yeyote katika ukanda wakusini mwa dunia ni jambo la kuchukiza. Vitabu ni vya thamani havipaswi kuachwa vioze kwa mtindo huu. Kitu chochote chenye thamani lazima kitumike ni mali. Kwasababu hii, Biblia katika nchi nyingi za kiafrika itatumika kama kitengo cha fedha. Kuuza na kununua Biblia ni karibu kama ununuzi wa dhahabu kwenye soko la bidhaa. Biblia haijasomwa lakini inatumika kama sarafu.

Kwasababu Biblia zinatumiwa kwa njia hii kuna kusita sita katika ulimwengu wa kusini hata kuchukua Biblia kutoka kwenye sanduku lake lilillofungwa sembuse kufungua kurasa ya biblia na kuisoma. Kufanya hivyo kutapunguza thamani ya hisa zao.

Mbinu chache ambazo tumeona zinafaa katika kuhimiza usomaji wa Biblia ni:

  • kutoa biblia bure (inayoathiri ugavi na mahitaji)
  • toa Biblia nje ya kisanduku chake
  • andika kwenye mali ya Biblia n.k.
  • onyesha sehemu Fulani kwa kalamu ya kuangazia
  • hata kama kurasa chache zisizo za muhimu

Kitu cha thamani Zaidi ambacho ulimwengun huu hutoa”

Iwe tunaishi Kaskazini mwa Ulimwengu au Kusini mwa Ulimwengu tutakuwa tumesikia juu ya utafutaji wa muda mrefu wa Jiwe la Wanafalsafa dawa ya maisha ambayo mwanadamu ametafuta ili kufufuliwa na kufanikishwa kwa kutokufa (uzima wa milele). Albertus Magnus inasemekana aligundua jiwe hilo katika karne ya 14 wengine hata wanasema yupo hai leo. Vipi ningekuambia kua nimepata kichocheo cha uzima? Ninacho mikononi mwangu kichocheo cha uzima wa milele. Usicheke kwakua ni kweli, na jambo la kushangaza ni kwamba kichocheo hiki ambacho wanadamu wametafuta kwa maisha yote kimekaa mbele  ya macho yetu wakati wote. Ndiyo, dawa ya maisha alipewa Adamu katika bustani ya Edeni na mabilioni wana nakala ya mapishi hayo hata leo. Biblia ni hiyo mapishi. Inaweza kugeuza hiyo mapishi kuwa dhahabu. Inatoa kichocheo cha uzima wa milele “kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama hya mungu ni uzima wa milele katika Kristo bwana wetu” (Warumi 6:23).

Bwana wetu Yesu Kristo anatoa mfano “ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mwenye kutafuta lulu nzuri; na alipopata lulu moja ya thamani kubwa akaenda, akauza alivyo navyo na kuinunua” (Mathayo 13:45-46).

Kuitia Biblia moyo wangu wa jiwe unageuzwa kuwa dhahabu ya Imani ndani yake nina tumaini la uzima wa milele. Katika enzi ya ufalme. Hili ni jiwe la mwanafalsaafa; kichocheo ambacho kitanipa kutokufa.

Ikiwa ungekutana na mzee wa ajabu ambaye anajiita Albertus Magnus, basi labda ungesimama kwa muda kusikiliza alichosema. Labda inafaa kusikiliza Biblia Ili kuona kama unaweza kupata hiyo mapishi. Bwana wetu Yesu Kristo aliweka hivi “Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa” (Marko 16:16). Inaonekana Kama kichocheo rahisi cha kutosha. Unapochunguza maneno haya sio rahisi kufuata lakini angalau tunayo mapishi.

Katika ulimwengu wa kaskazini wengi hudai kuwa wakristo wanaishi katika nchi zinazojuklikana kuwa za kikristo, ilhali wachache wamepata kichocheo cha uzima wa milele. Biblia inatumika kuapa katika mahakama ya sharia. Nakala ya Biblia inatolewa Kwa mfalme au malkia wakati wa kutawazwa kwao. Lakini nini kuwa mkristo wa kweli? Kuhudhuria kwenye sherehe za kikristo. Harusi au mazishi au Zaidi. Nujkuu hapo juu inaonyesha kwamba ili kuwa mkristo kweli unahitaji kujitoa kikamilifu maisha yako kwa njia za biblia na kwa kristo, na unaweza kufanya hivyo ikiwautasoma na kujifunza kitabu hiki cha ajabu kila siku.

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                       

[1] Ingawa ni lazima ikubalike kwamba, baadhi ya madhehebu  ya ukristo sasa yanakataa sehemu kuu za Biblia.

[2] Imepewa jina la Henry Walter Bates ambaye alikua mwanasayansi wa asili wa Karne ya 19.

[3] Hii  inafafanuliwa kama ufahamu wa hali ya juu au taji. sefirah

[4] Wahenga wa kiyahudi walieleweka kama viwango vine vya ufahamu na utafsiri wa maandiko P’shat, Remez, D’ rash na Sod ikilinganishwa na kumenya kkitunguu.

 

[5] Hoja kuhusu Vitabu vya zamani Zaidi 10 zipo.  Hii inaweza kupuuzwa kwa Hadithi.

 

Swahili Title
Sura ya 1. Jiwe la mwanafalsafa wa Biblia
Literature type