Sura ya 4. Biblia- Neno la uzima wa milele

Swahili

Sura  ya 4. Biblia- Neno la uzima wa milele[1]

Wakosoaji wamechanganyikiwa

Bila shaka siku zote kumekuwa na wale ambao wamependelea kukataa badala ya kukubali Biblia kuwa neno la Mungu. Nyoka katika Eden kwa mafanikio alidhoofisha Imani ya wazazi wetu wa kwanza katika neno lililonenwa la mungu kwa swali ambalo limesikika kwenye midomo ya wachambuzi wengi wa Biblia wenye uadui tangu “ndiyo amesema Mungu…?” (Mwanzo 31). Mfalme mwovu Yehoyakim ambaye alilikataa neno la Mungu lililoandikwa na kutafuta bila mafanikio kuliangamiza (Yeremia 36) amekuwa na wenzake miongoni mwa wasioamini karibu kila zama. Hata hivyo Biblia imeokoka huku wachambuzi wayo wakiipita.

Na Biblia imeokoka si tu katika maana ya kuhifadhiwa katika kitu cha kimwili pia imedumisha uadilifu wake wa ajabu kama kitabu cha kiada cha imani inayookoa. Kila kizazi kipya cha wakosoaji kimeibua au mara nyingi Zaidi kutumika tena madai ya ugumu au hitilafu za Biblia. Bado matatizo yote kama haya yana uwezo wa kupata suluhisho la busara kabisa ambalo hujipendekeza kwa wanaume na wanawake wa nia njema. Mara nyingi zaidi katika nyakati za hivi majuzi uvumbuzi wa akiolojia umeonyesha ukosoaji mwingi wa Biblia kuwa sio sahihi “Musa”, tuliambiwa kwa ujasiri  “hataweza kjuandika Pentateuch kwa sababu aliishi kwa ustadi wa kuandika Belshaza, Sargon na Wahiti wote walisemekana kuwa watu wa Biblia wa kubuniwa”; na sensa ya kaisari Agusto wakati wa kuzaliwa kwa Yesu iliyotajwa na Luka ilikataliwa kuwa si sahihi. Bado katika mifano hii yote kama ilivyo katika mingine mingi, Biblia imethibitishwa na utafiti zaidi wa kitaalam.

Jambo la kusikitisha ni kwamba ukosoaji mwingi wa Biblia unaenda sambamba na kutokuwa tayari kujibu matakwa ya ujumbe wake na mara  nyingi hutegemea nadharia zilizotungwa ambazo zenyewe hazina uthibitisho au zisizoweza kuthibitishwa. Ujinga huo wa kupenda ni msiba wa kibinafsi kwa wale wanaohusika na vile vile kwa wale wanaoshikiliwa nao. Bila shaka Biblia inaweza kustahimili uchunguzi wenye kuvutia Zaidi lakini kama ilivyosemwa kwa kufaa hapo awali “haitoi hazina zake kwa wachambuzi wake”.

“Sauti ya mungu kwa kila mtu”

Akizungumzia Biblia iliyokamilika Mwalimu Mkristo wa Karne ya tatu Origen alikuwa na haya ya kusema “Hata wakati wa sasa maneno ya utimilifu katika maandiko matakatifu yanakuambia, wale walio na macho ya kuona siri za mbinguni na kutunza kusikia sauti ya Mungu”. Hilo linaonyesha kanunin ya Biblia nyenyewe ya kushughulikia jambo linalotegemea hali ambayo Yesu aliweka. “Yeye aliye na masikio ya kusikia na asikie” (Luka 8:8, imenukuliwa katika ufunuo 2:7 na mahali pengine). Mtume Paulo aliwaambia waathene kwamba Mungu  “sasa anawaamuru watu wotye wa kila mahali watubu” (Matendo 17:30) lakini amri hiyo inasikika katika siku zetu kwa njia ya uchapishaji na si tena manabii na mitume wanaongozwa na roho. Biblia ni neno la Mungu lililochapwa kwa njia za miujiza na maongozi na Mungu anahitaji watu wasikilize sauti yake katika kurasa zake, lakini yeye  hawalazimishi kufanya hivyo. “Nitamwangalia mtu huyu” asema Bwana “mtu aliye mnyonge mwenye roho iliyopondeka atetemekaye asikiapo neno langu” (Isaya 66:2)

Katika enzi hii ambapo Biblia iliyochapwa inapatikana katika wingi wa lugha ndicho chanzo cha pekee cha ufunuo  kuhusu akili na mapenzi ya Mungu usomaji wa maombi wa kila siku wa neno lake ndio njia pekee  ambayo wanadamu wanaweza kusikia sauti yake. Thawabu nyingi zinazotokana na hadhira kama hiyo ya kawaida na Mungu zinzhitaji uzoefu ili kuaminiwa. Lakini kuna mifano ya kutosha katika maandiko kufanya hivyo kuwa na thamani ya kujaribu sisi wenyewe. (Ona Yoshua 18 na Zaburi 1 :3-3)

“Kugeuza Roho”

Mungu ameliweka neno lake duniani ili lizae matunda kwa utukufu wa jina lake (Isaya 55:10-11), nah ii inafanikiwa kwa wanaume na wanawake kujifunza mawazo na njia zake na kuitikia. Kwahiyo malengo ya Biblia ni kwanza kuwajulisha na kuwarekebisha wanadamu. Hichi ndicho anachomainisha mtunga zaburi anaposema;

“sharia ya Bwana ni kamilifu huiburudisha nafsi ushuhuda wa bwana ni hakika humpa mjinga hekima” (Zaburi 19:7)

Uongofu kutoka kwa njia za asili za Dhambi za wanadamu hadi njia za haki za kiroho za Mungu, ni hatua ya kwanza muhimu katika njia ya wokovu kama Yesu mwenyewe alivyosema.

“Msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo hamtaingia katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 18:3).

Kazi yote ya neno la Mungu ni kurudisha mioyo ya wanadamu kwa  Mungu. mchakato huo unapoanza mtu anaweza kusemwa katika maneno ya mtume Petro kuwa “kuzaliwa kwa mara ya pili si nkwea mbegu iharibikayo bali kwa ile isiyoharibika, kwa neno la mungu lenye uzima, lidumulo hata milele (1 Petro 1:23).

Neno lenye nguvu

Itakuwa kosa kudhani kwamba neno la Mungu kwa namna Fulani limepoteza uwezo wake wa ukoimbozi kwa kupunguzwa kwa uchapishaji na kwamba ni muhimu kwa roho mtakatifu kufunua maana yake moja kwa moja kwetu kabla ya kuelewa Biblia. Kama vile mwandishi mwingine alivyosema vizuri  “Biblia kimsingi ina mantiki lakini kwa sababu ya uandishi wake wa kimungu  ina silika yenye nguvu isiyo na kitabu na sehemu nyingine zote zina faida”. Mtazamo huu unathibitishwa na taarifa muhimu ya Paulo kwa Timotheo kwamba “maandiko matakatifu yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu” (Timotheo 3:15). kwa maana maneno “wanaweza” yanaweza kutafsiriwa kama “kuwa na nguvu”.

Biblia humfunulia msomaji anayeuliza  “ujuzi wa Mungu” na ukweli uliomo ndani yake wakati mwingine huitwa “nguvu za Mungu” au “roho” kwasababu ilikuja kwa njia ya roho mtakatifu na yenyewe inaweza kuhuisha kile kilichokua kimekufa (ona Yohana 6:63; Waefeso 6:17; 2 Petro 1:3; Yohana 5:7 R.V). Ingawa sasa tunatakiwa kusimama katika huduma ya kibinafsi ya moja kwa moja ya mitume kama Paulo, bado tunasifiwa na wazee wa Efeso kama walivyosifiwa. “kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaweza kutujenga na kutupa (sisi) urithi miongoni mwao wote waliotakaswa” (Matendo 7:38). “Maneno yenye uhai” ya Mungu (Matendo 7:38) si herufi iliyokufa neno la Mungu  “bado ina nguvu zake za kale”.

Hisia ya kusudi.

Nguvu ya Biblia ipo katika asili yake ya kimungu na inayoonyeshwa katika athari zake mbalimbali katika maisha ya wanaume na wanawake.

Tofauti kati ya wazo hili la uwezo wa Biblia na uchawi lazima isisitizwe. Matumizi  ya uchawi nji uthibiti wa mtu binafsi ambao ni kinyume na matakwa ya mtu Binafsi . Lakini nguvu ya biblia ni uthibiti wa mtu binafsi anayetaka kudhibitiwa. Kuna tofauti ya hili lakini muhimu sana.

Jambo kuu kati ya athari hizo ni uwezo wa Biblia wa kuleta maana ya kusudi maishani yenyewe. Ujumbe wa injili ulio katika Biblia kimsingi unahusika na mipango ya Mungu ya wakati ujao kwa injili ya dunia na wa injili ya wanadamu. Biblia ni rekodi ya utendaji wa Mungu unaoendelea unaokaziwa katika kazi ya mwanawe Yesu na kuongoza hatimaye kwenye ukombozi wa mwanadamu. Ujuzi na usadikisho wa “ahadi kuu na za thamani” zinazotolewa kwetu katika neno la Mungu  hutia kusudi katika kuwako kwa mwanadamu kwa njia isiyokuwa na kusudi. Kumekuwa na watu wengi chini ya enzi ambao wamejionea maishani mwao mwelekeo wa mtunga zaburi alipoandika.

Neno lako ni taa ya kiguu yangu na mwanga wa njia yangu” (Zaburi 119:115).

Na wale ambao kupitia ufahamu wao wa neno hilo wanakuja kufuata kielelezo cha “Neno aliyefanyika mwili” lengo na kusudi la kuwako  huwa kama lake lilivyo kuwa kufanya mapenzi ya Mungu kama ilivyoandikwa “katika gombo la kitabu” (Waebrania 10:7).

Chanzo cha Faraja

“Yote yaliyoandikwa zamani yaliandikwa ili kutufundisha sisi kwa  faraja ya maandiko ili tupate tumaini”.

Ndivyo alivyoandika mtume Paulo katika Warumi 15:4. Katika ulimwengu huu wenye matatizo kama haya, maneno ya Paulo yana maana ifaayo  hata Zaidi kuliko m, tume angejua. Biblia haitufungui sisi tu kama ilivyofanaya kwa karne nyingi kwa vizazi vya wasomaji wake  baadhi ya mafumbo yanayosumbua ya maisha na kifo, pia huleta ile bidhaa ya lazima sana wakati wa dhiki. Amani hiyo ambayo Yesu aliwaahidi wanafunzi wake yaweza kuwa yetu kikamili kupitia kurasa za neno la Mungu (Yohana 14:27). Hakuna tatizo la kibinafsi lisilo na ufumbuzi wake katika neno la “Mungu wa faraja yote” (2 Korintho 1:3); na zaidin ya magumu na mahangaiko yote ya maisha binafsi.  Wakati wowote tunapokuwa na shida katika maisha haya siku zote  kutakuwa na suluhu kwa tatizo hilo linalopatikana katika neno la Mungu. Mawazo yanayotegemea Biblia yanaweza kutumiwa kutatua tatizo lolote katika enzi yoyote ya historia ya mwanadamu na katika muktadha wowote.

Biblia inaweka uhakikisho wa ile dawa ya hakika kabisa kwa magonjwa yote makubwa zaidi ya ulimwengu; ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo (Matendo 1:11; 3:20-21). Tunaposoma juu ya ahadi hiyo kuu katika Biblia na kusakidishwa juu ya utimizo wayo unaokaribia tunaweza “kufarijiana kwa maneno hayo” (Wathesalonike 4:18).

“Maneno ya uzima wa milele”

Bswana Yesu akaristo alikuwa akitoa ushauri mzuri siku zote alipowaambia watu wa nyakati zake  “yachunguze maandiko” (Yohana 5:39). Himizo hilo halikupotea kwa Petro na wanafunzi wengine  wachache kwakuwa walitambua kwamba hapakuwa na chanzo kingine cha maarifa ya kuokoa mbali na maneno yaliyotoka kwa Mungu. “Bwana” alisema Petro kama msemaji wa wale kumi na wawili  tutaenda kwa nani “wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki na tunajua yakuwa wewe ndiwe Kristo mwana wa Mujngu aliye hai” (Yohana 6:68). Ungamo la Petro la imani katika Yesu liliunganishwa bila kutenganshwa  na kukubali ujumbe waje kama neno la Mungu, ingawa yeye na wanafunzi wa kwanza hawakuelewa kikamili kila kitu ambacho Yesu alisema.

Leo kama siku zote inawezekana kama wanafunzi wasio na kina zaidi wa Yesu. Katika Yohana 6:67 “Kwenda” kutoka kwa Mungu kwa kupuuza au kukataa  uzima wa milele ambao umo katika Biblia neno la Mungu katika kuchpishwa. Kuelekea mwisho wa maombi yake marefu  kwa ajili ya wanafunzi wake katika chumba cha juu kilichoandikwa  katika Yohana 17, Bwana Yesu aliwaombea hasa wale ambao baadaye wangemuamini kupitia maneno ya wanafunzi wake (V 20). Biblia ni jibu la mungu kwa maombi hayo, je, utafungua masikio yako kwa maneno ya wokovu wa kitabu cha Mungu au utakuwa muujiza wa Biblia?

“Je, Ninyi pia mtaondoka”

Msingi

Biblia inapoaminika na kueleweka kuwa ndiyo mamlaka pekee  ambayo kwayo tunaweza kuweka ufahamu wetu juu ya ibilisi na shetani basi tunakuwa na nafasi ya kuanzia ambayo kwayo tunaweza kuweka msingi wa mafundisho yetu; lakini si mpaka Biblia  kujiamini kusadiki na kukubali ukweli huu. Hakuna msingi Zaidi unaoweza kupatikana katika mjadala wa jambo hilo, Imani lazima ije kwanza. Imani ndiyo kanuni ya kwanza ya injili.

 

 

[1] Sura hii inategemea kabisa kijitabu cha Ndugu katika Kristo kiitwacho Muujiza wa Biblia Neno la Mungu Lililochapishwa na Reg Carr chenye mabadiliko machache na nyongeza ndogo.

Swahili Title
Sura ya 4. Biblia- Neno la uzima wa milele
Translator 1
Emanuel
Literature type