Sura ya 5. Mungu – Roho wa milele

Swahili

Sura ya 5. Mungu – Roho wa milele[1]

Utangulizi

Moja ya mambo ya kuvutia Zaidi kuhusu utamaduni ni kwamba ni sehemu ya ndani ya jinsi tunavyo uona ulimwengu. Inaweza kuonekana kama utamaduni ni kitu ambacho watu wengine tu wanacho. Ndani ya utamaduni wowote upendeleo wake wa kipekee na dhana za awali hazionekani kwa wale wanaozishiriki.

Mara kwa mara uchunguzi hufanywa ili kuuliza  watu kama wanaamini katika Mungu. Takribani watu 90% katika Afrika mashariki wanasema (ikilinganishwa na 60% katika ulaya) na karibu 40% huenda kwa ukawaida kwenye mahali pa ibada (ikilinganishwa na 10% huko Uropa). Lakini uchunguzi ukienda mbali Zaidi na kuwauliza hawa wanaojiita waumini wa mungu kile wanachoamini juu yake, utata wa ajabu sana unatokea.

Katika mtazamo wa kaskazini, mtazamo wa jumla wa Mungu unaonyesha mtazamo wa mtu binafsi. Watu wengi wana mwelekeo wa kustahimili makosa yao wenyewe na wanamfikiria Mungu kuwa yule “Napenda kumfikiria Mungu”, wanasema kama wema usio na kikomo daima kusamehe na kamwe kuhukumu mtu yeyote hata wakosaji wengine watasema “Vema, ikiwa Mungu yupo na niklifanya kile ninachofikiri  ni sawa nitapata malipo yoyote  yaliyopo”.  Dini zote sasa zinachukuliwa kuwa za kweli, hbata hivyo njia yeyote ya kumkaribia mungu ni nzuri kama zilivyo nyingine.

Kinyume chake katika ulimwengu wa kusini, mtazamo wa jumla wa ulimwengu  unaweza kuwa wa tofauti kabisa  kwasababu ya tamaduni na historia. Kwa ujumla miungu ya watu wa kale inasemwa kuwa haipendezwi na ubinadamu. Hakuna mpango au kusudi na wanadamu. Hakuna baada ya maisha. Miungu hupewa matoleo hata kuonyesha kupendezwa na wanadamu. Hawana nia ya kweli kwetu hata kidogo. Sisi ni burudani isiyo na maana.

Ukweli ni kwamba mwanadamu wa kisasa iwe kaskazini au kusini kwa kiasi kikubwa ni mpagani. Amepoteza hisia zote za mamlaka ya Mungu kwasababu amepoteza msingi wote wa Imani. akiachwa kwa mawazo yake mwenyewe anakosa usadikisho wote; amechanganyikiwa na hajali.

Msingi uko wapio?

Hakika ni dhahiri kwamba ikiwa dini inataka kuwa na nguvu na mamlaka yote kwa ajili ya wanadamu ni lazima idhihirishwe na Mungu mwenyewe. Kwa maana kuna njia moja tu, ikiwa ujumbe hautoki kwa mungu lazima utoke kwa mwanadamu. Lakini mwanaume yeyote anawezaje kujidai  kuwaambia wanaume  na wanawake wengine yaliyo ya kweli na sahihi?

Mafundisho ya dini nyingi sana za ulimwengu yanatoka kwa fikra za mwanadamu. Kuna tofauti moja mashuhuri. Dini ya Biblia. Dini ambayo kitabu hiki kinahusika nayo kwa msisitizo ni dini iliyofunuliwa  neno la Mungu kwa mwanadamu.

Ujumbe wake hautolewi kamwe kama mamlaka ya kibinadamu “Neno la Yahwe” linakuja kwa nabii na abnalitoa kama vile Agano la kale na jipyua zinavyofanana katika hili. Neno hilo linapoandikwa kwa faida ya vizazi vijavyo anasema Paulo “aliongozwa na roho wa Mungu”  “Mungu alipulizia” (Timotheo 3:16) usemi wa ajabu unaowasilisha wazo kwamba roho wa Mungu (au pumzi) ilikuwa katika maneno yaliyoandikwa.

Ndivyo asemavyo Petro maandiko “ hayakuja zamani kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu watakatifu walinena yaliyotoka kwa mungu wakiongozwa na roho mtakatifu” (2 Petro 1:21) angalia tofauti si “ kwa mapenzi ya mwanadamu” roho wa Mungu aongoze.

Sura zetu za ufunguzi zinaonyesha kwamba Biblia ni kitabu chenye mamlaka kuu. Ni neno la Mungu kwetu lakini matokeo muhimu kufuata ikiwa ni hivyo tusithubutu kulipuuza. Ni lazima tulichukulie kwa uzito.

Ufunuo wa Mungu mwenyewe

Kwahiyo kenye Biblia twende je. Ina nini cha kutuambia kuhusu Mungu?

Habari hizi si haba, ni nyingi. Inaanzia katika ukurasa wa kwanza wa Biblia na inadumishwa hadi mwisho, yaani kupitia Torati zaburi na manabii wa agano la kale na kupitia injili na nyaraka za agano jipya. Lakini picha hii ya Mungu si ngumu au kuchanganyikiwa maana kunatokea mtu mmoja wa pekee na tabia yake yenye uamuzi inayohusika sana na wanadamu na mustakabadhi wa ulimwengu. Hawezi kuachwa kwenye kingo za mahangaiko ya kibinadamu wala kusukumswa “mahali Fulani” katika mbingu za mbali ili kupuuzwa kwa urahisi.  Ikiwa wanaume na wanawake watafanya hivyo, matokeo kwao wenyewe yatakua mabaya.

Maelezo ya kawaida katika Biblia kuhusu asali ya Mungu ni “milele”. Fikiria mifano hii:

“kabla haijazaliwa milima wala hujaiumba dunia tangu milele hata milele wewe ndiwe Mungu (Zaburi 90:2).

Je hujui, hujasikia kwamba Mungu wa milele, Yahwe muumba miisho ya dunia hachoki? akili zake hazitafutikani” (Isaya 40:28).

“Yahwe ndiye mungu wa kweli; yeye ndiye mungu aliye hai, mfalme wa milele” (Yeremia 10:10).

Hapa kuna ubora wa kuwepo nje ya uzoefu wetu. Hakika mwenyezi mungu anajionyesha hivyo kupitia Nabii wake:

“Wamisri ni wanadamu na si Mungu, na farasi zao ni nyama na si Roho (Isaya 31:3).

Hapa kuna tofauti ya wazi kati ya “wanadamu / mwili” na “Mungu /  roho”. Asili ya Mungu ni “Roho” kwahiyo inaunda tofauti kabisa na asili ya mswanadamu ambnayo ina mipaka katika akili dhaifu ya tabia na kuungamia katika kifo.

Lakini hiyo inamaainisha nini? Je, tunafikiria nini tunapozingatia kuwa roho wengine watafikiria juu ya mzuka au mzimu, lakini hiyo sio maana ya neno hili hata kidogo. Tunapofikiria roho basi tunapaswa kufikiria chanzo cha nishati au ushawishi (ona sawa na mwandishi  Roho mtakatifu mwenye nguvu, Young).

Kewahiyo Mungu wa Biblia si kitu kama mwanadamu hata kidogo, yeye ni roho au nishati.

Kama katika maumbile ndivyo katika ukombozi wa mwanadamu. Mungu aliumba jua kwanza kutawala siku. Alifanya jua kwa uwezo wake, yani aliumba kutokana na uwezo wake yaani alifanya kutoka kwa sehemu ya nishati yake mwenyewe zake au kiini chake kama tunavyoweza kusema. Jua si ewazo la uchawi... Hakuna kitu. Ni theolojia maarufu ambayo imefundisha kwamba Mungu aliumba vitu vyote kutoka kwa utupu, Aliviumba kutoka kwake mwenyewe nay eye hana kikomo. Vitu vyote ni ufupiosho wa kutumia neno wazi la nguvu yake ya milele isiyoonekana iliyoundwa na kuongozwa na hekima yake”. (Robert Roberts)

Wazo hili linapokelewa Zaidi na wale wa kusini mwa ulimwengu  kuliko swale wa kaskazini mwa ulimwengu. Tamaduni za kaskazini mwa ulimwengu hufikiria miungu yao kama wanadamu; ilihali miungu ya kusini mwa ulimwengu mara nyingi huhusishwa na nishati asilia  kama vile umeme wa upepo au nishati ya mwaloni.

Mungu ni wa milele

Maelezo ya swazi Zaidi katika Agano jipya yanatoka kwa mtume Paulo:

“Ufafanuzi ulio wazi Zaidi katika agano jipya ni kutoka kwa mtume Paulo sasa kwa mfalme wa milele asiyeharibika asiyeonekana Mungu pekee iwe heshima na utukufu milele na milele Amina” (1 Timotheo 1:17 R.V.).

Inastaajabisha kwamba katika maelezo haya maneno mawili ya wazi Zaidi kuhusu asili ya Mungu yanaonyeshwa mkuwa hasi. Yeye “hawezi kuharibika” (haharibiki) na “hafi”. Mungu ana “asili”  kinyume cha moja kwa moja cha “mwili wa mwanadamu” kwahiyo yeye ni wa milele kihalisi wa nyakati. (R.V.  Pembezoni). Ni jambo la maana kwamba Paulo anatumia neno hili mara tatu katika mstari mmoja “kwa mfalme wa milele uwe utukufu milele na milele” (hata milele na milele) asili ya milele ya Mungu. Ni lazima awe amevutiwa sana na wazo la hali ya milele ya Mungu.

Ukuu wa Mungu

Ukuu kamili wa Mungu na utukufu ambao unapaswa kuonyeshwa kwake na wanadamu duni ni mada ya kudumu katika maandiko matakatifu ilionyeshwa na Daudi mfalme wa Israeli.

“Bwana ni mkuu na muweza na utukufu na kushinda na enzi kwamaana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako. Ufalme ni wako bwana nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote” (1 Mambo ya nyakati 29:10,11).

Ukuu… nguvu… utukufu… ushindi, vyote mbinguni na duniani. ufalme ulioinuliwa kichwa juu ya vyote. Tunafanya vyema kusoma maneno haya polepole ili kufahamu maana ya kina ya Daudi ya ukuu wa Mungu. Ilishirikiswa na mtume Paulo kama tulivyoona.

Usadikisho huu wa ukuuu wa Mungu unashirikiwa na waumini wote wa nyakati za agano la kale. Sasa hatupaswi kulipuuza Agano la kale kwa maana ndani yake zinafunuliwa misingi ya tabia  za  Mungu kweli za msingi juu ambazo zimethibitishwa na kupanuliwa katika Agano jipya. Zaidi ya hayo ni Israheli waliopewa ufunuo mkuu wa ukuu wa Mungu juu ya miungu yote ya wanadamu katika matukio ya kusisimua ya kutoka kwao Misri. Waisraeli waliona matokeo ya mapigo juu ya Wamisri na kujionea ukombozi wao wenyewe wakati wa kuvuka bahari nyekundu. Musa aliiweka kwa kushangaza sana miaka 40 baadaye.

“Kwa maana jiulizeni sasa katika siku zilizopita, kwamab limewekwa jambo kama hili kubwa?... je, kuna watu walisikia sauti ys Mungu ikinena kutoka kati ya moto kama mlivyosikia na kushi, au je, Mungu alijaribu kwenda kujitawalia taifa kutoka kati ya taifa linguine (R.V Pembezoni) kwa majaribu kewa ishara na maajabu? Kulingana na hayo yote  Bwana Mungu wenu alivyowatendea huko misri mbele ya macho yenu” (Kumbukumbu la torati 4:32-34).

Juu ya onyesho hili la wazi la uwezo wake na wokovu kwa niaba yao Mungu aliweka ombi lake kwa niaba ya utumishi wao kwake.

“Mmeona jinsi nilivyowatenda wamisri na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mabawa za tai na kuwaleta kwangu. Basi ikiwa mtaitii sauti yangu  kweli kweli  na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakuwa tunu kwangu (maalum) katika mataifa yote” (Kutoka 19:4,5).

Ona hasa hapa kwamba ombi la Mungu la kumwamini mwenyewe halikuegemezwa kabisa juu ya ubora wake wa kimaadili (ambao angetoa ushahidi mwingi baadaye) bali juu ya thibitisho wa ukuu wake juu ya mfumo mkuu wa kipagani duniani wakati huo (Misri). Hii inatiwa nguvu wakati Mungu anafunua kupitia Musa kwa sharia yake  kwa Israeli kwa kifungu cha kwanza kabisa huanza.

“Mimi ni Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba hya utumwa” (Kutoka 20:2).

Kasha zifuate amri kumi kiini cha sharia ya mungu wako.

Mamlaka huja kwanza, fundisho la maadili linafuata. Haiwezekani kuachana na agizo hili, kwa kushangaza Yesu anachukua msimamo huo huo. Maneno aliyozungumza alisema hayakuwa yake mwenyewe bali ya baba yake katika Sala kwa Mungu, anamwita “Baba Bwana wa mbinguni na dunia” (Mathayo 11:25).  Ingawa Mungu alikua Baba kwa wote waliomtafuta yeye alibaki kuwa “Bwana wa mbingu na Dunia”. Kwa kusikitisha lazima kusemwe kwamba mambo haya ya kutangulizwa yamepuuzwa sana katika siku zetu hata na watu wengi ambao wangejiona kuwa wafuasi wa Yesu Kristo.

Upekee wa Mungu

Kutokana na kisomo chake cha kazi zote kuu za Mungu, kwa niaba ya watu wake Musa alitoa hitimisho lifuatalo.

Basi ijue leo ukaweke moyoni mwako ya kuwa Bwana ndiye Mungu Mbinguni juu,  na juu ya nchi  chini hakuna mwingine” (Kumbukumbu la Torati 4: 39).

Hii ilikuwa ni uthibitisho muhimu katika ulimwengu wa miungu ya Kipagani. Iliendelea kuwa muhimu katika karne zote za kutomjali kwa kudumu kwa Waisraeli kwa Mungu ambaye alikuwa amewakomboa.  Katika mawaidha yake ya mara kwa mara kupitia kwa manabii kwamba ni yeye aliyewakomboa kutoka katika ukandamizaji wa Misri anatangaza kuwa yeye ndiye Mungu peke yake.

Mimi ni Bwana wala, wala hapana mwingine; hakuna Mungu ila mimi” (Isaya 45:5).

Katika Agano Jipya mtume Paulo anatambua kuwepo kwa ibada nyingi na miungu ya kipagani; lakini kwa wanaomwamini Kristo, sanamu hizi si kitu.

“Twajua yakua sanamu si kitu katika ulimwengu na yakuwa hakuna Mungu mwingine ila mmoja kwa maana ijapokuwa wapo waitwao  miungu… lakini kwetu sisi kuna Mungu mmoja, Baba ambaye vitu vyote vimetoka kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo” (1 Wakorintho 8:4-6).

Na katika kuwaandikia Waefeso, Paulo anasema:

“Kuna mwili mmoja, roho moja, tumaini moja Bwana Imani moja, ubatizo mmoja Mungu mmoja na Baba wa wote” (4:4-6).

Hili ni tangazo lenye sauti kubwa la umoja wa vipengele mbalimbali vya Imani ya Kristo vyote vinavyomtegemea “Mungu mmoja”.

Mitazamo ya kisasa

Yote tuliyoyazingatia hadi hapo juu ya ukuu na utukufu wa Mungu mmoja muumba wa mbingu na Ardhi, yanadokeza kwamba anapaswa kupokea ibada ya uchaji kutoka kwa wanadamu dhaifu na hivyo anafanaya kutoa kwa waaminifu kupitia kurasa za Biblia.

Lakini tuseme nini kuhusu mitazamo kwa Mungu hata miongoni mwa watu wengi wanaodai kuwa waumini?

Maoni ya kidini katika kaskazini mwa ulimwengu yamebadilika sana kupitia ongezeko la wafuasi wa madhehebu menginene. Sasa inashikiliwa na wengi kwamba Dini zote  zinatoa njia yao wenyewe kewa Mungu n azote ni “Halali” kwa usawa. Watu wanakataa madai makuu ya Ukristo kuwa njia pekee ya “wokovu” iliyoonyeshwa hivi na mtume Paulo.

Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote (ila Yesu Kristo) kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbigu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (Matendo 4:12).

Kwa wale wa kusini mwa ulimwengu huu ni wa kustaajabisha. Sanamu za mababu zao katika vizazi vyote hivyo “si kitu”. Hakuna maana katika kuwaabudu. Huwezi kuhuzuria mikusnyiko ya kikabila na kwa Yahwe. Yahwe hatakubali huo mkusanyiko “si kitu” na  kuna “wokovu katika [hakuna] mwingine”, wengi wataona kuwa hii ni ngumu sana kukaribisha.

Haishangazi kwamba kwa mwanadamu wa kisasa, Mungu kama inavyoonyeshwa katika Biblia amepungua kutoka katikati ya usikivu na ameachwa kwenye ukingo. Kutokujali na kuzoeana nyakati Fulani hata katika mazoezi ya kidini hunyesha kwamba Mungu hapewi heshima inayostahili kwa jina lsake. Hata maneno yenye umuhimu mtakatifu kama vile “Haleluya” (ambayo ina maana ya “msifuni Yahwe”) yamevurugwa karibu kupata kibali cha waigizaji wa vicheshi wasio waaminifu.

Kwa hili lazima iongezwe roho ya Ubinadamu nay a kimaada ambayo huinua akili  ya mwanadamu na kuwa na mawazo kidogo juu ya uwepo wa Mungu au kwa Ibada yake. Hata tafakari hizi fupi juu ya hali ya maoni ya kisasa zinaonyesha pengo lililopo kati ya mitazamo ya leo kwa Mungu na ile iliyodhihirishwa na Yesu na Mitume.

 

 

[1] Sura hii inategemea kabisa kijitabu cha Ndugu katika Kristo kiitwacho Kumjua Mungu: Nini Biblia Inafunua na Fred Pearce chenye mabadiliko machache na nyongeza ndogo.

Swahili Title
Sura ya 5. Mungu – Roho wa milele
Translator 1
Emanuel
Literature type