
Sura ya 7. Mungu- Tabia Yake
Tabia ya Mungu
Mungu huyu mmoja muumba wa mbingu na Dunia, anayestahili kuabudiwa kwa uchaji sio tu Nguvu Ya nishati. Yeye ni nafsi yenye tabia Yake mwenyewe. Ana kanuni za Maadili za Milele ambazo amewajulisha wanadamu kupitia amri na maagizo yake.
Maelezo ya kwanza ya wazi ya tabia ya Mungu yanatokea katika ufunuo wa Musa yapata mwaka wa 1400 kabla ya Yesu. Musa alikua amepokea mawasiliano mengi kutoka kwa Mungu wakati wa matukio ya Kutoka, lakini ni wazi alihisi kwamba bado hajamjua Mungu kMma utu kwahiyo anaomba ombi:
“Kama nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua…”
Mungu alipokubali ombi lake, Musa anaongeza juu yake “Nionyeshe utukufu wako” sasa musa alikuwa ameshuhudia kwa Zaidi ya tukio moja utukufu wa “kimwili” swa Mungu kwa namna ya nuru kuu na maadhimisho ya nguvu. Hapa, anataka kitu Zaidi. Mungu analijua hili.
“Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, na kulitangaza jina la Bwana mbele yako” (Kutoka 33:13-19).
Jinsi utukufu wa Yehova utakavyoonyeshwa, wotye katika jina lake na utamwezesha Musa “kumjua”. Jina hili sasa linatangazwa:
“Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa rehema, mwingi wa fadhili, na kweli, mwenye kurehemu maelfu kwa maelfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi, asiyemhesabia mwenye hatia kwa njia yeyote” (Kutoka 34: 6,7).
Hivyo inajitokeza picha kuu ya Mungu wa Biblia iliyotolewa na yeye mwenyewe. Ana tabia ya uhakika ya kimaadili ambamo rehema (polepole kwa hasira , R.V), wema na msamaha vina sehemu kubwa lakini hii daima inapatana na “ukweli” wake. Mwangwi wa maelezo haya hupatikana mara kwa mara katika vitabu vilivyofuata vya Agano la kale hasa Zaburi (ona zaburi 103 kwa mfano) na manabii.
Picha hii ya mungu inadhihirishs “Wema” wake na pia “utukufu” wake wa tabia. Ni kipengele hiki ambacho Yesu anafikiria anapomtangazia Mwanamke wa Samaria “Mungu ni Roho” (sio “Roho” ambayo inapotosha ) (Yohana 4:24). Tabia ya Mungu inaelezewa kama “Roho” inaunda tofauti kubwa na tabia ya asili ya mwili wa mwanadamu inayoonyeshwa ndani yake. tabia ya mwili wa mwanadamu inayoonyeshwa katika fikra na matamanio yake; na inaelezwa na Yohana kuwa “Roho ya mwili wa ulimwengu wa makosa”
Utakatifu wa Mungu
Inafuata kufuatia na kile ambacho tumezingatia hivi punde kwamba Mungu katika asili na tabia yake ni tofauti kabisa na mwanadamu. Anakaa katika “Nuru isiyoweza kukaribiwa” isiyoonekana kwa macho ya kibinadamu asema Paulo. Lakini “mawazo” Yake (neno ambalo daima linajumuisha makusudi yake) ni kubwa kuliko ya mwanadamu kama alivyosema.
“Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kazalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu” (Zaburi 55:9).
Kwa hiyo Mungu ni “mtakatifu” hivyo ina maana kwamba “ametengwa” na wanadamu. Mwanadamu hawezi kufanya kosa bila kujali mbele yake kana kwamba Mungu ni mtu mwingine. Kwa sababu ya dhambi zao hawawezi kumkaribia yeye hata kidogo isipokua kwa njia ambayo aliyoonyesha. Waisraeli walifundishwa katika sharia kwamba, njia katika ibada na dhabihu ingeweza tu kupitia makuhani wana wa haruni ambao Mungu aliwaweka yeye mwenyewe kuwachagua. Kusudi la sharia lilikuwa ni kukuza ndani ya watu wa Israeli kwamba akili na tabia ambayo ilikua kama yake. Aliwaamuru “iweni watakatifu kwa maana mimi ni mtakatifu” (Mambo ya walawi 11:44) na Petro anarudia hili katika kuwaandikia waamini wa kwanza katika Kristo:
“Bali kama yeye aliyewaita alivyomtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote” (1 Petro 1:15).
Yesu alikuwa tayari, amesema mengi kwa mwanamke wa samaria:
“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabudo halisi swatamwabudu Baba katika Roho na kweli. Kwa maana baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwaduo yeye imewapasa kumwabudunkatika roho na Kweli” (Yohana 4:23,24).
Utakatifu ambao Mungu anauhitaji kutoka kwa waamini wa kweli sio roho ya kujinyima iliyoonyeshwa wakati uliopita na wahanga; wala si kudai kumwabudu Mungu na “kupitia kila jambo”, nab ado kudhihirisha roho ya akili ambayo inadaiwa zaidi na ubinafsi wa kibinadamu wa tamaa na kiburi kuliko inavyofanya kwa Roho wa Mungu. Mungu hakuvumilia tabia hiyo katika Israeli. Wala Yesu hatakuwepo hukumuni. Kuna wengine atawaambia “siwajui kamwe ondokeni kwangu” (Mathayo 7:23).
Mungu kama Baba
“Baba yetu uliye mbinguni” mstari huu wa kwanza kutoka kwa “sala ya Bwana” uliwahi kuwa mojawapo ya zile zinazojulikana sana katika Agano Jipya . Leo hii hairudiwi mara kwa mara. Lakini hata katika kilele cha matumizi yake ni ya kuogopa kwamba neno “Baba” lilitumiwa kwa maana ya kawaida bila kufikiri sana juu ya maana yake.
Katika nuyakati za Agano la kale, Mungu alikua tayari, amejidhihirisha kama “Baba”. “Israeli ni mwanaangu mzaliwa wangu wa kwanza” (Kutoka 4:22) lilikua ni tangazo lake kwa Farao huko Misri. Kwa karne nyingi za uzoefu wao, waaminifu walithamini uhusiano huo.
“Kama vile Baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahururmia wamchao; anakumbuka yakuwa sisi tu mavumbi” (Zaburi 103:13-14).
Katika Agano jipya uthihirisho mkuu wa Mungu kama baba yupo katika utu wa m, wanawe mpendwa. Yesu mara kwa mara anamrejelea mungu kama “Baba yangu” na anapozungumza na wanafunzi kuwa “Baba yenu wa Mbingu”. Neema ya Mungu isiyo na kikomo iliyopendwa sana na watunga zaburi na manabii ilionyeshwa kwa kumtoa mwanawe kama upatanisho wa Dhambi. Na hivyo, waaminifu wanapewa uhusiano mpya na mungu ambamo wao sio tu “warithi pamoja na Kristo” bali “wana na binti za Mungu”. Yohana anashangaa:
“Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo” (1Yohana 3:1 R.V).
Lakini katika siku hizi za mazoea ya kawaida ni rahisi kuingia katika tabia ya kumfikiria Mungu na kwa hakika hata kumwita “mmoja wetu”. Yesu aliweka vipaumbele vyake wazi kila wakati hasa katika sala zake . “Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi” (Mathayo 11:25) anatuonya kwamba ingawa mungu ni Baba yetu kweli anabaki kuwa “Bwana swa mbingu na nchi” na anapaswa kuabudiwa kama Mungu. Mara mbili katika maombi yake kwa ajili ya kusulubishwa kwake, anaongea na Mungu moja kwa moja “Baba mtakatifu… O Baba mwenye haki” (Yohana 17:11,25). Hakuna kuzoeana hapa lakini utambuzi wa kina wa “mwingine” huu kutoka kwa mwanadamu.
Vile vile mtume Paulo akinukuu kutoka katika sharia na kuutumia usemi huo kwa waumini wa Korintho anawahimiza “kutoka nje” na “kujitegemea” na ibada ya sanamu na mazoea katika jamii ya Wagiriki. Mujngu anawaahidi “nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakua wanangu wa Kiume na Wakike”; lakini Paulo hakusita kukamilisha manukuu “asema Bwana mwenye nguvu zote” na kuendelea kuwahimiza wasomaji wake wajitakase “na unajisi wote wa mwili na roho huku wakikamilisha utakatifu katika kumwongoza Mungu”, hiyo ni katika ibada ya uchaji (2 Wakorintho 6:17,7:1).
Katika sala ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake alimwita Mungu kama “Baba yetu uliye Mbinguni” (Mathayo 6:9). Hakika Mungu ni Baba kwa waaminifu akionyesha utunzaji na hangaiko yote baba angehisi kwa watoto wake. Lakini wale “wana na Mabinti” huku wakithamini reheme zake kwao, hawapaswi kamwe kujibakiza kusahau ibada ya uchaji ambayo ni haki yake. Mtazamo huu wenye msawaziko unatishwa vikali katika nyakati zetu za uhuru wa kujieleza na haki za binadamu. Biblia pekee ndiyo hutuwezesha kudumisha usawaziko huo.
Upendo wa Mungu
Leo maoni yaliyoenea zaidi ni kwamba “Mungu ni upendo”. Je, mtume Yohana hasemi hivyo katika waraka wake (1 Yohana 4:1 6) na katika injili yake? “Mungu aliupenda ulimwengu na hata akamtoa mwanawe pekee” ili wanaume na wanawake waishi na wasife (Yohana 3: 16). Mungu ni fadhili zote ilisemwa, na hatamhukumu au kumkataa mtu Yeyote. Mtokeo ya mwanzo haya ni mtazamo wa kihisia wa Mungu unaoundwa kutokana na tamaa za kibinadamu. C.S. Lewis aliwahi kueleza haya kama mtazamo wa mungu kama “Babu mwenye fadhili” anayehangaika tu kuwaweka watoto wake furaha kwa kutimiza kila matakwa yao.
Lakini huu ni upotovu mkubwa sana wa upendo wa Mungu unaofunuliwa katika Biblia. Hakuna Baba wa kibinadamu anayetamani kwa dhati ustawi wa watoto wake, anayeamini kwamba matokeo haya yanaweza kupatikana kwa kutimiza kila matakwa yao. Sasa Mungu ndiye Baba mkuu aliyewaumba wanadamu ili waweze kuakisi tabia yake mwenyewe ya ukweli, rehema na utakatifu. Kwahiyo “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake mwenyewe” (Mwanzo 1:27) na akawapa wanaume na wanawake uwezo wa ajabu wa kufikiri, kuelewa dhamiri na wote wsatakataliwa kwa kiwango sawa na wanyama ili weweze kuwatumia, kuwalea na kukuza tabia zinazofaa kwa hatima ya milele aliyowatakia.
Mtazamo huu kwa wanadamu wenye makosa unaonyesha kwamba yeye “hapendi kwamba yeyote apotee balli kwamba wote wafikie toba” (2 Petro 3:9), “ambaye anataka watu wote waokolewe na kupata ujuzi wa kweli” (1 Timotheo 2:4), inaonyeshwa katika kushughulika kwake na taifa la Israeli linalofafanuliwa katika maandiko kuwa “mwana” wake na pia “mke” wake. Kuelewa mahusiano haya ya kibinadamu na kujua kwamba kimsingi mafanikio yao yanatokana na kutegemeana na kutokuwa na ubinafsi, husaidia kueleza sifa za subira na huruma ambazo mungu huonyesha kwa watoto wake binafsi.
Yesu alipokuwa akiwaeleza wafuasi wake jinsi Mungu anavyopendezwa kamwe na hali njema ya watoto wake, alisimulia hadithi ya mwana mpotevu. Uchungu wa Baba wakati mwana wake anapodai fungu lake na haki zake hulingana na uchungu wa Mungu mwenyewe, wanaume na wanawake wanapata kuanza bila kujali njia zake na utunzaji wake wenye upendo. Katika mfano huo kukesha daima kwa Baba ambaye anangojea wenye dhambi, wanaotubu ambao wanaweza kufunikwa na mavazi ya dhambi yanayotolewa kupitia dhabihu ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Wala maelezo haya ya mungu hayapatikani tu katika Agano Jipya au katika Mafundisho ya Bwana. Mambo yaliyompata nabii Hosea akiwa na mke asiye mwaminifu hayakuwa ya tofauti na jinsi Mungu alivyotendwa na taifa la Israeli lililopotoka. Kama vile Hosea alivyomrudisha mke wake vivyo hivyo Mungu siku zote alinyoosha mikono yake ili kuwapokea Israeli tena. Kwa kifanya hivyo, hata hivyo hakuonyesha kibali chechote cha yale ambayo watu wake walikua wamefanya: matukio waliyovumilia kwa sababu ya ukosefu wao wa imani yalikusudiwa kuwafundisha kuhusu aina ya maisha ambayo watoto wake wanapaswa kuishi.
Kwahiyo inatokea kanuni kuu kwamba sio tamaa za kibinafsi za wanaume na wanawake amabzo zina nafasi ya kwanza katika kusudi la Mungu kwa ajili yao, bali ni wema wao wa mwisho. Mtazamo wa Mungu umejaa rehema wema na msamaha kwa watoto wake, kama Agano Jipya linavyotangaza kwa wingi: lakini yote yamo ndani ya mfumo wa ustawi wao wa mwisho katika kusudi lake.
Dhahabu ya Mungu
Lakini vipi ikiwa wanaume na wanawake wanampa kisogo yeye, wakikataa mamlaka yake na kupuuza amri zake na kuendelea kufanya mapenzi yao wenyewe? Jambo moja lipo wazi kwa vile mwenyezi Mungu ni mola mlezi wa mbingu na Ardhi; na muumba wa wanadamu, Hawezi kupuuza maasi yao kwakuwa ni kuachia mamlaka yake katika ulimwengu ule aliouumba, ni lazima ajaribu kurekebisha hali hiyo ili kuwafanya watu wabadili njia zao. Hili analifanya kwa kwa kuleta mashinikizo ya kubeba juu yao. Mojawapo ya mifano iliyo wazi zaidi ni kisa cha Israeli chini ya Waamuzi baada ya kifo cha Yoshua.
“Wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, nao wakamsahau Bwana Mungu wao wakawatumikia Mabaali na Maashtorethi, kwahiyo hasira za Bwana zilikuwa juu ya Israeli, akawauza na kuwaita mkononi mwa Kushani – Rishathaim mfalme wa masopotamia; wana wa Israeli wakamtumikia muda wa miaka minne, na wana wa Israeli walipomlilia Bwana akawainulia mwokozi aliyewaokoa” (Waamuzi 3:7-9).
Somo liko wazi. Israeli kumwacha Mungu wao ambaye alikuwa amewakomboa Misri, kuliamsha Hasira Yake. Analeta shinikizo la kubeba juu yao kwa maana ya uvamizi wa kigeni na utumwa. Baada ya muda shinikizo lina matokeo yake – Israeli walitubu. Toba tao ilikuwa hya kweli kwani Mungu alikuwa mwepesi kujibu na kuleta ukombozi.
Mchoro huu unarudiwa mara nyingi katika historia ya Israeli.
Takribani miaka 700 Kabla ya Kristo washauri wanaharibu ufalme wa kaskazini uliojengwa juu ya Samaria; na hatimaye Wababiloni wakapindua ufalme wa kusini wa Yuda yapata mwaka wa 600 Kabla ya Kristo. Kwanini mungu aliruhusu uvamizi huu? Kwa sababu licha ya Jitihada zake za kuwatuma manabii wake ili kuwasihi watu na kuwaonya “waliwadhihaki wajumbe wa Mungu na kuyadharau maneno yake”. Rekodi inaisha kwa maneno haya muhimu “mpaka hasira ya Bwana ilipoinuka juu ya watu wake hata kusiwe na Dawa” (2 Mambo ya nyakati 36:16).
Wakati licha ya maombi yete, watu hawatatubu, Mungu anakomesha hali. Hiki ndicho alichofanya kwenye Gharika wakati dunia ilikuwa “imeharibika… imejaa jeuri kila mwenye mwili alikuwa ameiharibu njia yake juu ya dunia” (Mwanzo 6:11,12). Kizazi hicho cha wanadamu hakingetubu; hawakuweza kurekebishwa. Suluhisho pekee lilikuwa kuwaondoa ili kusudi la Mungu liendendelee katika waaminifu waliobaki.
Kabla hatujafika kwenye Agano jipya, maneno mawili nyalioyotumiwa katika kale, mahitaji ya kuzingatiwa. Katika vifungu vichache Mungu anatangazwa kuwa “Mungu mwenye wivu”. Neno hili huwaudhi wasomaji wa kisasa kwakuwa limechukuliwa katika maana yake maarufu na kudokeza unyonge Fulani wa kibinadamu. Lakini huku ni kutoelewa maana yake ya kimaandiko. Hapo kila mara hutumiwa na mungu katika maonyo kwa Israeli dhidi ya kumwacha na kugeukia sanamu.
“Msifuate miungu mingine ya miungu ya mataifa yanayowazunguka; kwakuwa Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu, isije kuwa hasira (yake) juu yako akakuangamiza” (Musa kwa Waisraeli Kumbukumbu la Torati 6:14-15 R.V)
Sasa ni muhimu kwamba neno lile lile la mzizi wa kati mwingine hutafsiriwa “bidii” Mungu mwenyee anatuambia kile ambacho ni bidii kwa ajili yake:
“Mimi ni Yahwe; ndilo jina langu na utukufu wangu, sitawapa mwingine na wala sitawapa sanamu sifa zangu” (Isaya 42:8).
Bwana Mungu swa Mbingu nan chi amezimia kwamba ibada impasayo haitatolewa badala yake kwa vitu vya uumbaji wa mwanadamu au mawazo tu. Hii “ndiyo” wivu wake inafungamana na ghadhabu yake kwani hatimaye atawahukumu wale wanaodharau ibada yaye.
Neno la pili ni “ kiasi cha Yahwe”. Matumizi ya kisasa yanapendekeza roho ya kulipiza kisasi, tabia ya asili ya mwanadamu lakini isiyostahiliwa na Mungu. Tena ni muhimu kuelewa neno hilo katika maana yake ya kibiblia “kisasi cha Yahwe” kitatumiwa kwenye hukumu yake kwa wenye dhambi. Lakini sifa hiyo hiyo inatumika kuhusiana na wokovu wa waaminifu. Isaya aeleza vizuri jambo hili la mwisho.
“Itieni nguvu Mikono iliyo dhaifu, waambieni walio na moyo wa hofu, iweni hodari, tazameni Mungu wenu atakuja na kisasi na malipo ya Mungu (R.V) atakuja na kuwaokoa” (Isaya 35:3,4).
Kisasi cha mungu siku zote ni kisasi cha haki ni hukumu inayostahiki kwasababu ya dhambi inayodumu, uthibitisho wea utakatifu na ukweli wa mungu mbele ya ugumu wa kibinadamu na kiburi.
Agano jipya na Hukumu
Kama vile hukumu ya Mungu ilivyolijia taifa la Israeli kwa ajili ya uasi na dhambi zao zenye kuendelea, ndivyo itakavyoujia ulimwengu wetu kwa ajili ya kutomcha Mungu na usherati. Katika kifungu cha kushangaza Yesu analinganisha “siku ambayo mwana wa Adamu atafunuliwa” (yaani atyakaporudi duniani) na hukumu za Gharika za Sodoma na Gomora.
“Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu ndivyo itakuwa katika siku za Mwana wa Adamu” (Luka 17:26-30).
Ni mada thabiti ya Agano jipya kwamba kutakuwa na siku ya hukumu kwa ulimwengu. Paulo anawahakikishia waaminifu katika Thesolanike kwamba Mungu atahukumu “katika ufunuo wa Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake katika mwali wa moto akiwalipiza kisasi wale wasiomjua Mungu na wale wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu” (2 Wathesolanike 1:6-10 - kifungu kizima kisomeke).
Haya ni maelezo ya moja kwa moja ya hukumu ambayo yanawashtua wanafikra wengi wa kisasa. Lakini Paulo anatumia lugha yha sharia na Manabii “kisasi” ni kwamba malipo ya haki ni kwamba malipo ya haki ambayo yamezungumzwa; wale “wasiomjua Mungu” sio wajinga kama vile wale “wasiomkiri” na “kutotii” ni kukataa na kutotii. Chechote tunachoweza kuhisi hakuna shaka juu ya yjumbe wa Paulo.
Lakini Agano jipya pia linatangaza kwamba wakati Kristo atakaporudi kutakuwa na hukumu ya mtu binafsi kwa wale ambao wameijua injili. Tofauti itafanywa kati ya “waadilifu” wale ambao wametafuta kuwa waaminifu na “waovu” wasio waaminifu kama Paulo atangazavyo:
“Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za mungu” (Warumi 14:10-12).
Hukumu basi ni sehemu ya ufunuo wa kusudi la Mungu, azimio lake la kutovumilia dhambi ya kudumu ambayo nyakati nyingine huitwa katika maandiko “Ghadhabu ya Mungu”.