Somo la 3: Jumuiya ya Wayahudi
Kuelekea mwishoni mwa somo letu la mwisho tuliweza kuona mfanano mkubwa kati ya sehemu ya kukutania ya Wayahudi- sinagogi- wakati wa Bwana wetu na ushirikiano wa siku hizi. Katika somo hili tunaongeza zaidi. Tutaangalia kuondoka kwa Israeli walivyo toka Misri jinsi ilivyo mfano wetu sisi wa kuuacha ulimwengu (dunia) na kwamba Pasaka ya Wayahudi ni Pasaka ile ile ambayo sisi tunaisherekea. Tutaonyesha uhalisia wa Ekklesia (Ikklesia) yetu, maisha ya Ekklesia yetu na ushirikiano wetu kuwa kweli ni mwendelezo wa Jumuiya ya Wayahudi.
Uzao wa Ibrahimu
Kwanza Ibrahimu alikaa nchi ya Wakaldayo, upande wa mashariki ng’ambo ya mto Frati, alipokuwa na umri wa miaka 75 aliondoka aliwaacha jamaa zake na kwenda mpaka nchi ya Kanaani (Yoshua 24:3; Nehemia 9:7; Matendo ya Mitume 6:4).Abramu aliondoka kwa sababu Mungu alimwagiza kufanya hivyo (Matendo ya Matendo7:2-3; Mwanzo 12:1). Amri ya Mungu ilikuja kwa sababu kusudi la Mungu liweze kufanyika kumhusu Abramu na dunia nzima (Isaya 55:2-5, Isaya 43:21, Isaya 41:8). Kusudi lile lilikuwa kumfanya Ibrahimu kuwa taifa kubwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu na mwisho awe baraka kwa jamaa zote za dunia (Mwanzo 12:2-3; Hesabu 14: 14; Isaya 45:23).
Mungu alimjulisha mwana wa Ibrahimu, Isaka na kwa mwana wa Isaka, Yakobo kuhusu kusudi hili; na mwaka wa Isaka, Yakobo (Mwanzo 26:4; Mwanzo 28:14; Zaburi 105:9; Waebrania 11: 8-9).Mungu aliweka msingi wa kazi yake na Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kufanya agano nao na kuwapatia nchi ya Kanaani;ambamo walikuwa ni wageni,katika urithi wao wa milele (Mwanzo13:14; 15:18; Zaburi 105: 10-11; Mwanzo 26: 2-4; Mwanzo 28:13-14).
Ibrahimu, Isaka na Yakobo hawakupokea ahadi yao ya kumiliki nchi ya Kanaani kama walivyoahidiwa; walikuwa ni wageni katika nchi ya ahadi maishani mwao na mpaka wakafariki (wote watatu walizikwa Hebroni) pasipo kuipokea ahadi (Waebrania 11:3-13, Waebrania 11: 39-40; Matendo ya Mitume 7:5 Waebrania 11: 8-9). Hata hivyo, ni kweli kuwa Mungu atatimiza ahadi yake kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kuwapatia nchi ya Kanaani ambamo walikaa kama wageni katika siku za maisha yao. Atawafufua Ibrahimu, Isaka na Yakobo kutoka kwa wafu na kuwapatia kumiliki nchi, wakati ufalme wa Mungu utakapokuwa umeanzishwa huko, nayo itafanyika nchi ya mbinguni (Mika7:20; Marko 12: 26; Luka 13:28; Mathayo 8:11; Waebrania 11: 16).
ambao ni watu wa mataifa (tusiokuwa Wayahudi) tumefanywa washirika wa ahadi hizi hizi kwa njia ya ubatizo. Tumekubaliwa na Mungu kuwa wana na binti na kwa hiyo kuwa warithi pamoja na Wayahudi (Wagalatia 3:26-29; Wagalatia 4:6; Warumi 11:11-31)
Kristadelfia ndio wazao walioahidiwa kwa Ibrahimu. Na kama sisi ni uzao wa Ibrahimu, basi kwa ufafanuzi sisi ni Wayahudi (Kiebrania: יְהוּדִים ambalo Wayahudi hulitamka: Yehudim) au watu wa Israeli.
Kuondoka Misri
Karibu miaka 500 baada ya kifo chake Ibrahimu, wana wa Israeli walijikuta chini ya kongwa la ukatili wa wasimamizi wa Wamisri.
Israeli, wakiwa wamekombolewa kutoka Misri na kupewa ahadi ya urithi, ilikuwa mfano wa waamini “waliokombolewa --- kutoka nguvu za giza”, na kusitahimilishwa “kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru”. (Wakolosai 1:12, 13). Lakini, huu mfano unakwenda mbali zaidi, ili kuweka msisitizo wa tendo hili la ukombozi wao wa kutoka utumwani mpaka kuwa huru, Israeli walipaswa kushiriki kula dhabihu (kafara) ya ushirika wa pamoja, sikukuu ya Pasaka ambayo ilifanyika “ilikumbukwa” kila mwaka (Kutoka 12:14) kwa ajili ya kukombolewa kwao. Na ndivyo inavyo kumbukwa mpaka sasa, waamini wanaungana katika ushirika wa “sherehe” ya ukumbusho (Yuda mstari 12) ya mkate na divai; ambazo ni ishara zinazonena ni dhabihu iliyo kuu zaidi, “Kristo ambaye ndiye Pasaka wetu”, ambaye “aliyetolewa dhabihu kwa ajili yetu”.
walifundishwa kanuni za kiroho kupitia sikukuu(karamu) ya Musa inayoendelezwa katika ukumbusho wetu – basi, Paulo anatusihi,“ tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli” (1Wakorintho. 5:8).
Kitabu cha Kutoka, ni mwanzo wa ukumbusho, mara moja kabla wana wa Israeli kutoka katika nchi ya dhambi na utumwa ilianzishwa Pasaka. Lakini kabla ya kuelezea jambo lolote kuhusu sikukuu (karama) yenyewe, kuishika Pasaka lilihusiana na mwanzo mpya. “BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu”.(Kutoka 12:2). Tendo hili ni muhimu sana, - hata kalenda ilibadilishwa, ili iwe sambasamba na ibada, kwa ajili ya kuzingatia sana ule mwanzo mpya.
Kwa maana Israeli, ni mzaliwa wa kwanza wa (Yahwe) BWANA (Kutoka 4:22), yalitakiwa yawe maisha mapya wakiwa watu waliotengwa kwa haki yao ya kipekee “taifa toka kati ya taifa” (Kumbukumbu la Torati – 4:34). Walipewa hadhi ya taifa jipya na utaratibu mpya wa kuabudu ambao ungewafundisha kanuni za Ukombozi ambazo baadaye zilionekana katika mzao wa ahadi wa Ibrahimu (Wagalatia 3:24).
Na vivyo hivyo, waamini siku hizi, wanapobatizwa katika Bwana Yesu Kristo wana anza huu mwanzo mpya – wa kuenenda katika “upya wa uzima”, (Warumi 6:4) kwa kuwa wanaenenda kwa roho wakitoka katika uovu, wakipokea hadhi ya kuwa ndugu wa Bwana Yesu Kristo. Hakika, kanuni hiyo hiyo imeonyeshwa na Bwana mwenyewe – “naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu,” (Wakolosai 1:18), na watu wote wanaoamini na kuzingatia kanuni ya dhabihu yake, wanatamani kutumia viwakilishi vyake kwa kula mwili wake na kunywa damu yake (Yohana 6:53-58), wanafanyika “viumbe wapya” ambao sasa wanaumbwa ndani yake.
Vilinywewa vikombe vinne kwenye Pasaka
Pasaka ndani ya chumba cha ghorofa, ilikuwa ni sikukuu ya Pasaka ile ile ambayo Wayahudi waliagizwa kuitunza. Katika karamu ya Pasaka ya Wayahudi kulikuwapo vikombe vine.
Kila kikombe kilinywewa kwa maana maalumu katika karamu. Vikombe vine vilinywewa kwa kufuata hatua kama ifuatavyo:-
Kikombe cha kwanza kilikuwa ni kwa ajili ya (קידוש) Kiddush (matamshi kwa Kiebrania), kikombe cha pili ni kwa ajili ya (מגיד) 'Maggid' (matamshi kwa Kiebrania), kikombe cha tatu ni kwa ajili ya (ברכת המזון) Birkat Hamazon (matamshi kwa Kiebrania) na kikombe cha nne ni kwa ajili ya (הלל) Hallel (matamshi kwa Kiebrania).
Na vikombe vinne huwakilisha maana nne ya tendo la ukombozi ambao Mungu aliahidi.
“Nitawatoa ninyi...”
“Nitawaokoa...”
“Nitawakomboa...”
“Nitawatwaeni ...”
Kutoka 6:6-7.
Kama tukisoma Maandiko kwa makini, kunywa kila kikombe inaweza kutambuliwa tukio hili lililoandikwa katika chumba, pale ghorofani.
Pasaka kwa kweli ilikuwa ni chakula cha ushirika, inaonekana wazi kuwa kutokana na sheria (utaratibu wa kwanza uliofanyika: “Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja; na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu,...”(Kutoka 12:3-4).
Kwa hiyo kulikuwa na (utaratibu) sheria ya Mungu jinsi ya kushirikiana ili kula mwanakondoo. Kila nyumba walipaswa kuwa na mwanakondoo mmoja tu –siyo zaidi ya huyo. Mwanakondoo mmoja wa Pasaka alitosheleza mahitaji yao, hata kama ni watu wa familia ni wengi katika nyumba hiyo.
Vivyo hivyo, ndivyo iliyo hata kwetu siku hizi, sisi ni Nyumba ya Mungu (1Timotheo. 3:15), Ekklesia imepatiwa Mwanakondoo Mkubwa zaidi wa Pasaka ili wamle katika ushirika; Bwana Yesu- dhabihu moja tu, anayetosheleza mahitaji yetu yote. Lakini ikiwa, idadi ya watu ndani nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi washirikiane na familia ya nyumba moja tu aliye karibu na nyumba yake na wa mle mwana-kondoo yule mmoja pamoja katika ushirika na katika tumaini la ukombozi.
Pia vilevile, ukweli halisi, kwa kuwa familia ya Wayahudi haikutoshereza kusudi la Mungu maana wao ndiyo waliofikiwa na Mwana-kondoo wa Mungu. Walikuwepo watu wachache mno waliokubali mwaliko wa kula “chakula kikubwa cha jioni” walichopewa (Luka 14:16-20).
Hata hivyo, bado ilikuwepo “nafasi zaidi” (mstari 22), na ndipo watu mataifa (watu ambao siyo Wayahudi) walialikwa kuingia ndani, na kula pamoja nao pia (mstari 21-24). Ndivyo ilivyo, kwamba nyumba zote mbili, yaani Wayahudi na Watu wa mataifa wanaletwa wote pamoja katika Kristo, ili wote wawili waweze kushiriki faida ya dhabihu yake katika ushirika mmoja na tumaini moja.
Tumaini la Israeli
wa Masiya (Masihi), wakiwa wameshapokea siku 40 za mafunzo kuhusu kuja kwa ufalme, walimwuliza, wakisema, “Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” (Matendo ya Mitume 1:6). Ingawaje hawakujua majira yake, lakini, walifahamu kwamba ufalme ujao utakuwa muhimu sana kwa ajili ya kurudishwa kwa ufalme wa Israeli. Mtume Paulo alipelekwa akiwa amefungwa kwa mnyororo “kwa ajili ya tumaini la Israeli”. (Matendo ya Mitume 28:20).
Yesu mwenyewe alifundisha kuwa “wokovu watoka kwa Wayahudi”. (Yohana. 4:22).
Ekklesia (Ikklesia) ya Mungu, imepatikana kutokana na maagano ya ahadi alizopewa Ibrahimu, na Daudi, zinazofafanuliwa katika Wagalatia kwa “Israeli wa Mungu” (Wagalatia 6:16). Wakiwa ndiyo mzao wa Ibrahim kwa imani, ni wayahudi kweli kweli, wametahiriwa katika govi la mioyo yao: “Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu” (Warumi. 2:28-29).
Hivyo basi, Injili ni “habari njema”, kuhusu ufalme wa Mungu utakaorejeshwa kwa Israeli, Ufalme ambao utaongezeka na kuwa wa dunia yote, hatimaye utaondoa falme nyingine zote duniani.
Na njia ya kukua kwa ufalme huu imefafanuliwa katika Daniel 2 inavutia na kutia shauku.
Na jiwe liloipiga sanamu miguu yake, limefafanuliwa kuwa “lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono” (Daniel 2:45). Nalo jiwe lenyewe likakua, na kuwa “mlima mkubwa, ukaijaza dunia yote” (Dan 2:35). Hivyo ni kusema, kuwa jiwe lilifanyika chapa halisi ya kule lilikotokea. Na tendo hili, kwa vyovyote vile, ni kiini na kanuni ya kiroho tunayoita “kujidhihirisha kwa Mungu”.
Ujumbe unaofana kuhusu kusudi la BWANA kwa dunia ni “dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana” (Habakuki 2:14; Zaburi 72:19). Katika unabii wa Danieli 2; lile Jiwe linafanyika chapa au nakala halisi wa kule lilikotokea. Kwa hiyo, ukiweka vitu hivi vyote pamoja, basi, tunaona kwamba Mwana wa Mungu atauanzisha ufalme wa ulimwengu wa wayahudi ambao hatimaye utahakikisha kwamba unaona ulimwengu ukiwa umejaa watu wale wanaoonesha tabia zake za uadilifu, yaani utukufu wake.
Mwanakondoo wa Pasaka.
Familia ya wana Israel walitakiwa kula mwanakondoo, yaani ni kusema kuwa, iliwapasa wao wenyewe wachukue,na watafune, ili watiwe nguvu, na kuimarishwa na viini lishe vilivyomo. Na hili lenyewe liliwafundisha jinsi walivyohitaji kubadilishwa na kanuni za kiroho ambazo Pasaka ilizifundisha ndani ya utu wao, ili ziweze kuwaimarisha wampatie Mungu wao.
Na tukizungumzia jambo lingine, Bwana Yesu alisema:-
“Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli,na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake”. (Yohana 6:55-56).
Kwa hiyo, ni kusema kwamba “kula” na “kuinywa” ni ishara zenye maana sana. Kula mwili na kuinywa damu ya Mwana wa Adamu, ni kula na kunywa virutubisho muhimu vya kiroho kutoka kwake. Ni kula na kuvinywa virutubisho muhimu vinavyopendeza vya “Neno lililofanyika mwili” kwa kutafakari kwa kina, ujumbe wa Neno linalomhusu yeye.
Hata hivyo, kushiriki kumla mwana-kondoo wa Pasaka, kwa Mwisraeli mwaminifu, ilikuwa ni kutafakari maana ya kiroho zilizofundishwa na mafunzo yaliyotokana na sheria walizopewa. Na haikuwa kuitazamia tu dhabihu kamilifu ya Bwana Yesu, bali pia iliwafundisha kanuni ambazo zingesababisha kuwaongezea waamini (waumini) maisha ya kiroho maishani mwao.
Maandalizi
wa Pasaka, alitakiwa asiye na ila (kasoro), aliye mkamilifu kimwili. “Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja…” (Kutoka 12:5). Lakini, wakati huo huo maana yake halisi ni kuwa ilielekeza wakati ujao wa dhabihu kamilifu kabisa ya Bwana Yesu (Linganisha 1Petro 1:19), katika kuitafakari kanuni hii wana wa Israeli walikuwa wakifundishwa jinsi wao wenyewe wanavyotakiwa wasimame mbele ya Mungu.
kweli kuwa “mwili” wa jamii ya waamini unapaswa uwe “ pasipo ila”, wao wenyewe kwa ajili ya Bwana Yesu “aliyejitoa mwenyewe kwa yake, ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno, apate kujiletea Ekklesia(Ikklesia) tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa ili apate kujiletea Ekklesia(Ikklesia) tukufu, lisilo na ila wa kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”
5:25-27).
kwamba tufikiriwe kuwa “hatuna ila” kwa njia ya matendo yetu wenyewe; bali hasa hasa kwa njia ya imani yetu katika Yesu Kristo, Bwana wetu, dhambi zetu ziwe zimeoshwa, kwa imani na msamaha wa dhambi, na ndipo sasa tunapoonekana kuwa hatuna dhambi mbele ya Mungu. Na hili ndiyo sababu, tunajitahidi kuichuchumilia tuweze kuipata, kwa kushinda tama ya mwili na kusafisha njia zetu (Zaburi 119:9) kwa kutii Neno la Mungu, kwa kuwa tukisha takaswa na atusimamishe “bila mawaa” (Yuda 24), mbele ya kiti cha utukufu wake.
unafundisha kuhusu Pasaka ulielezea majuto na simanzi sana. “Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.” (Kutoka 12:6). Chini ya sheria ya matoleo, tendo la mleta matoleo kumchinja yule mnyama aliyemleta, ilikuwa njia ya utambulisho wa kufa pamoja na yule mnyama (linganisha Walawi 1:4,5). Kwa njia hiyo, mleta matoleo alijitambua kuwa sawa sawa na ile dhabihu aliyoleta, mtoaji alikuwa akitamka kwamba yeye mwenyewe anastahili kifo, lakini akitambua kuwa angeweza mwishowe kupata tumaini la wokovu, katika Dhabihu kamilifu iliyotolewa na BWANA, ya kumtoa Mwanaye, yaani Mwana-kondoo wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa, katika maana ya Pasaka, “Kusanyiko lote la Mkutano”, (yawezekana kila mzaliwa wa kwanza wa nyumba?) iliwapasa wachinje mnyama ili kujifananisha na kifo chake – na kwa hiyo kuwa na tumaini litakaloletwa na ukombozi.
Lakini jambo la kushangaza lilikuwa katika Pasaka ya kweli hasa, yaani Bwana Yesu Kristo, ambapo mkutano wote waliokusanyika walitaka Mwokozi wao asulubishwe – walimwua Mwana wa Mungu Mwenyezi, na “mkamtaka mwuaji” aachiliwe kwa ajili yenu (Matendo ya Mitume 3:14,15). Hata hivyo ni sawa sawa na mfano ule ue kwa mafundisho yake dhahiri – tunapaswa tujifananishe na sawa na kifo chake Mwanakondoo halisi ili tushiriki faida za Dhabihu yake. Alikufa kwa ajili yetu, ili sisi tupate ukombozi na msamaha wa dhambi.
Utaratibunaofuata kuhusu Pasaka (uliakisi) kuleta ufahamu wa majuto na simanzi sana. “Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.” (Kutoka 12:6). Chini ya sheria ya matoleo, kumchinja yule mnyama aliyemtoa, ilikuwa njia ya kijulisho pamoja na kifo cha yule mnyama (linganisha Walawi 1:4,5). Hivyo kwa kujitambulisha na kafara, Yule mtoaji alikuwa akitamka kwamba yeye mwenyewe anastahili kifo, na hapo hapo akitambua kuwa angeweza kupata tumaini la wokovu, hatimayae katika dhabihu kamilifu iliyotolewa na Bwana.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwamba katika suala la Pasaka, “Kusanyiko lote la Mkutano”, (yawezekana mzaliwa wa kwanza wa kila nyumba?) ilikuwa wachinje mnyama ili kujifananisha na kifo chake – na kwa hivyo kuwa na tumaini la ukombozi uliowekwa.
Lakini jambo zito lilikuwa katika Pasaka yenyewe ya kweli hasa, yaani Bwana Yesu Kristo, ambapo ilikuwa jumuia ya wote waliokusanyika waliotaka mwokozi wao atolewe dhabihu (kafara) – wakimuua mwana wa Mungu aliye juu sana, na “kumtaka muuaji” aachiliwe (Matendo ya Mitume 3:14,15). Hata hivyo mafundisho ya mfano ni wazi – inapasa tutambulishwe na kifo chake Mwanakondoo halisi ili tushiriki faida za dhabihu yake. Alikufa kwa ajili yetu, ili tupate ukombozi na msamaha.
Tendohili lilisisitiza zaidi katika matendo yaliyofanyika kwa njia ya damu. “Nao watatoa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla” (Kutoka. 12:7).
Kwa kawaida, kumwaga damu ni ushuhuda wa kweli wa kifo – yule mnyama alikufa ili kutoa kiasi cha damu. Ni ishara au alama inayowakilisha, kwa hiyo,damu hunena kuhusu kifo cha Pasaka ya kweli, ambayo waamini wanaikumbuka katika “sikukuu”ya kila juma. Ili waweze kuingia ndani ya nyumba ya wokovu, wana wa Israeli iliwapasa kupitia katika damu – iliyokuwa juu, na kwenye miimo yote miwili, nao ilibidi wawe humo mpaka asubuhi (Kutoka. 12:22).
Kwa hiyo, katika mfano huu , ni kwamba walilazimika kupitia katika kifo cha dhabihu kwenda uzimani – ndani ya kimbilio alilotoa Bwana. Hata hivyo ni katika suala la mwamini. “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima” (Warumi 6:3-4).
Jinsi itupasavyo kuenenda katika “Nyumba ya Mungu, iliyo Ekklesia (Ikklesia) ya Mungu aliye hai” (1Timotheo. 3:15), huanzia katika kupitia kwetu kwenye kifo chake Kristo, aliye Pasaka yetu, na kupitia ndani ya kaburi la maji ya ubatizo.
Na tunapoibuka na kutoka ndani ya maji yale, tuenende katika upya wa uzima, tunaanza maisha mapya – tuna kuwa na kitambulisho kipya, hata kusema kwetu, na sasa sisi ni sehemu ya familia ya Kristo, na warithi sawa sawa na ahadi. Katika ubatizo, tunaingia ndani ya damu ya Kristo, na kuingia katika Nyumba ya Wokovu, tukingojea ukombozi, wakati tutakapoitwa asubuhi, wakati wa kuchomoza kwa Jua la Haki.
Tukitafakari zaidi na hasa sehemu za nyama zilizoliwa, kwa mara nyingine tena, tunapata mambo ya muhimu ya kutufundisha. Chakula chenyewe ilibidi kitayarishwe kwa njia maalum – ilitakiwa kuokwa motoni: “Watakula nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena pamoja na mboga zenye uchungu. Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama zake za ndani”. (Kutoka 12:8-9).
Zingatia hili; mnyama asipikwe – bali aokwe motoni.
Katika Biblia, moto huwakilisha ishara ya mitihani katika imani au kipindi cha mtihani.
Kwa hiyo, katika kuzungumzia imani ya mwamini, Petro alisema “Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto ...” (1Petro 1:7). Tena, alifundisha na kusihi kuwa: “ Wapenzi msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho lakini kama mnavyoshiriki mateso ya Kristo , furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe kuu” (1Petro 4:12, 13).
Basi, moto, unazungumzia jaribu (mtihani) hasa hasa majaribu (mitihani) inayowajia wenye haki, ambao kwa uzoefu wa kupatwa na mambo wao nao wanayahiriki mateso yake Kristo. Kwa hiyo, mwanakondoo wa Pasaka, alifundisha kuwa dhabihu au matoleo husafishwa katika moto – yaani, ikizungukwa na mateso na dhiki ambayo yalimpata Bwana wetu: “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata” (Waebrania 5:7-8)
Na katika kushiriki mambo haya kila mwana wa Israeli mwenye mwenye kuzingatia alifundishwa kanuni ya utaratibu ili aweze kushiriki faida za Pasaka kubwa zaidi, na pia angehitaji kushiriki kupitia dhiki ya moto wa mateso ya Kristo – hatuwezi kupitia dhabihu bila pia kushiriki kuokwa motoni.
kwenye sikukuu
Tena, katika kuhusiana na hili ni kwamba usingekuwepo utamu wa mwanakondoo bila kula pia mboga zenye uchungu (Kutoka 12:8). Hapa, neno la Kiebrania linalotafsiriwa kuwa “mboga zenye uchungu” linatumika mara moja tu kwenye muktadha huu, yaani, katika Maombolezo ya Yeremia, akizungumzia juu ya uchungu wa nguvu ambao uliompata Yeremia wakati wa maangamizi ya Yerusalemu na mambo aliyoyavumilia (Maombolezo 3:15). Kwa hiyo, “mboga zenye uchungu” ina maanisha mateso na dhiki waliyoyapitia wale waliotaka kubaki waaminifu nyakati za dhiki- watu kama Yeremia, ambao waliovumilia moto wa mateso, ambao hata hivyo walitoka ndani ya moto kama dhahabu safi ; wenye kutakaswa vyema zaidi kwa ajili ya kutumiwa na Bwana.
Kuna mboga zenye uchungu zaidi kuweza kuzionja wakati fulani kuliko wakati mwingine, lakini hata hivyo tuhakikishiwe kuwa kuwa zipo, maana hatuwezi kushiriki Pasaka bila kuwepo hizo, ni kama vile ambavyo hatuwezi kuingia katika Ufalme wa Mungu bila kupitia “dhiki nyingi” (Matendo ya Mitume14:22). Hekima ya kweli ni kutambua hali halisi iliyopo, na kuamini kwamba BWANA anayeweka mboga zenye uchungu mbele yetu atatuokoa na kututoa tukiwa kwenye sifa na utukufu.
Pia kitu kingine kilichojumuishwa kwenye chakula cha Pasaka ulikuwa ni mkate usiotiwa chachu (hamila) (Kutoka.12:8).Huu mkate usiotiwa chachu ulimaanisha nini? Ikiwa dhabihu hatimaye inawakilisha Kristo – ni kitu gani tena kilichojumuishwa na Dhabihu yake? Je, siyo kuwepo kwa mwamini? Huu ndiyo ushuhuda wenye uvuvio wa Paulo. “Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo; basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na kweli” (1Kor. 5:7, 8).
Hivyo basi, mkate usiotiwa chachu unawazungumzia waamini wenyewe, jinsi wanavyotakiwa kuwa “donge” jipya lisilotiwa chachu, na katika nyumba zao wakiwa wamekwisha tupilia mbali “chachu ya uovu na ubaya”. Tunaitunza karamu, yaani, chakula cha shirika pasipo kuwa na chachu ya uovu na ubaya kwa ajili ya mambo yaliyotendeka kwa ajili yetu kwa kumtoa “Kristo aliye Pasaka yetu”. Na kwa hiyo, tunaitunza karamu “kwa unyofu wa moyo na kwa kweli”, tunakitupilia mbali chochote kila kinachochukiza, ili donge zima liwe safi, kama na Kristo Bwana wetu alivyo safi.
Jambo la kupendeza, katika neno hili “kwa unyofu wa moyo na kwa kweli” neno hili tena limetumika kwenye tukio moja tu katika Maandiko – limetumika katika muktadha huu wa kuzungumzia kuondoka kwa Israeli kutoka Misri. Katika Yoshua 24, tunapata maneno ya mwisho ya Yoshua kwa Israeli kabla ya kifo chake, ombi lake la mwisho – “Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kwa kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie yeye BWANA.” (Yoshua. 24:14). Walipokuwa wanaondoka Misri, kama tulivyoona, iliwapasa Israeli kuanza na mwanzo mpya, wa kutupilia mbali mambo ya mwili (tamaa ya mwili) ili wa mwabudu Mkombozi Mkuu wao.
Na katika kushiriki mkate usiotiwa chachu wakati wa Pasaka yao, walikuwa wamefundishwa kanuni hii, jinsi wakati ule walivyotakiwa kutupilia mbali miungu waliyokuwa wakiiabudu huko Misri. Lakini bado hawakufanya hivyo; ndipo Yoshua alipotoa wosia wake wa mwisho ili waitupilie mbali kabla hajafa.
Na hii ilikuwa ni kanuni ndani ya mafundisho ya Mitume kwa Ekklesia (Ikklesia) ya Kristo; katika kutunza karama (sherehe) inatupasa kuondoa kati yetu kila kilicho cha kidunia, na njia zake za kuabudu vinyago, ili tuweze kushiriki kula Dhabihu hii “kwa unyofu wa moyo na kwa kweli”.
Wala msisaze kitu chake chochote hata asubuhi
wa mwisho unatufafanulia sana jinsi tunavyopaswa kukaribia vitu vya ibada gizani kwa kuwa sisi ni wageni na wapitaji katika nchi. Israeli waliagizwa, “Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana, msiache kibakie chochote hadi asubuhi mtakichoma kwa moto tena mtakula hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mkononi mwenu; nanyi mtakula kwa haraka ni Pasaka ya BWANA” (Kutoka 12:11).
Ingawa watu walikuwa wamepokea ahadi ya muda wa kuokoka kwao, lakini wao hawakufahamu wakati watakapoongozwa ili kuondoka kwenda kwenye Ufalme wao. Kwa hiyo, walitakiwa kula karamu hiyo wakiwa tayari kwa kuondoka mara moja, wakiwa wamevaa viatu vyao, na hali viuno vyao vimefungwa, wakiwa wamejiandaa kuondoka mara moja. Na ndivyo ilivyo hata kwetu sisi. Tupo chini ya amri ya mitume ya “kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani (Waefeso.6:15),na kujifunga “Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo” (1Petro 1:13).
Tunangoja wakati wa kutokea kwa Bwana, ili atuongoze kuondoka ulimwengu huu wa giza na hata tuweze kuyafikia mapambazuko ya mbingu mpya ya Haki na Amani. Lakini hatufahau saa ya ukombozi wetu, “hakuna ajuaye siku wala saa”. Ndiyo maana tunapaswa kuwa tayari kila wakati, tukiendelea kudumu katika roho tukiwa tayari kuondoka wakati wowote, ili kuwa naye Bwana.
Lakini kama ilivyokuwa kwa Israeli, wakati wa kushiriki kanuni za ukombozi ni sasa. Hakuna faida kuacha chochote mpaka asubuhi, kwa kuwa tutakuwa tumechelewa mpaka wakati huo. Siku inapopambazuka, na “Jua la Haki”(Malaki 4:2) litawazukia lenye kuiangazia dunia likiwa na maarifa ya Utukufu wa Mungu, na muda wa kujiandaa utakuwa umekwisha; na vitu vyote vitakuwa vimeletwa nuruni; ili vihukumiwe mbele ya kiti cha hukumu.
Basi, kwa sababu hiyo tuwe na juhudi ya kuzingatia kanuni za Pasaka, ili tuonekane watakatifu, na bila mawaa mbele ya kiti cha utukufu, baada ya kuvumilia mateso, na bado tukiwa tumehuishwa na kanuni za dhabihu ya Bwana. Na katika siku ile, tunaomba, kwamba tuonekane tukimngojea kwa uaminifu Bwana wetu, ili kwamba kama ilivyokuwa kwa Israeli wa zamani, tuongozwe na tuwekwe huru na kutolewa katika giza na utumwa wa dhambi, hata tuingie “katika uhuru wa utukufu wa wana wa Mungu” ( Warumi 8:21).
Sasa, kama kweli tumefanyika Wayahudi na tunaitana ndugu wakiwa ni wanamume au wakiwa wanawake tunajitambulisha kwa kwa tabia na mwenendo upi? Kwa kuwa tumevua kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani (Waefeso. 4:22; Wakolosai. 3:9). Hatuwezi tena kujiita Watanzania, Waingereza, Wakongomani, kwa sababu sisi ni Wayahudi. Hatuwezi tena kujiita Wanyakyusa au Waha au kujiita kwa kabila lingine lolote lile; kwa kuwa tu Wayahudi.
Tumetupilia mbali mila na desturi zetu za wale ambao wanaoitwa watu wa ukoo au kabila letu, sasa watu hao siyo wa familia moja na sisi tena. Kwa maana, sasa tunayo familia mpya, ambao tunapaswa kuwatii na kuwajibika kwao. (Mathayo 10:37; 12:49; Marko 3:34).
Kwa watu wengi neno hili ni gumu sana kwao (Mathayo. 19:29, Marko. 10:29), na kabila lako la zamani haliwezi kupokea badiliko lako la imani kwa urahisi. Lakini hili ndilo fundisho lake Bwana Yesu Kristo.
Fundisho hili linazidi kuwa gumu zaidi wakati wale wanaokuwa ndugu zetu wanaume na wanawake baadhi yao ni wale waliotoka katika makabila tuliyokuwa tukipigana nao vita katika makabila yetu ya zamani kizazi na kizazi.