Exploring the Bible - 21

Swahili

KUSULIBISHWA NA KUFUFUKA KWA YESU

 

SOMO LA 21 SOMA MATHAYO 21-28

 

Kumbukumbu zote za Injili zinatupa maelezo ya kina kuhusu juma la mwisho la maisha ya Yesu hadi kutundikwa kwake msalabani. Kila mwandishi anakazia matukio Fulani akichagua sehemu za matukio ya juma lile la mwisho. Yohana katika Injili yake toka sura ya 12 hadi ya 17 anaandika sehemu kubwa ya mazungumzo yaliyofanyika usiku wa kuamkia kusulibishwa kwa Yesu.

Tutachagua baadhi tu ya matukio yatakayojadiliwa. Inapendekezwa kuwa mtumie muda wenu kwa uangalifu mnaposoma kila moja ya maelezo ya matukio haya ya Injili (Mathayo 21-28; Marko 11-16; Luka 19-24; Yohana 12-21)

 

Siku za mwisho za uhai wa Yesu

 

SIKU

TUKIO

NUKUU

Ya 1

Maria anampaka Yesu mafuta miguu

Yesu anaingia Yerusalemu

Math. 26:6-13

Math. 21:1-11

Ya 2

Yesu anaulaani Mharadadi

Anatakasa Hekalu

Math 21:18-19

Math 21:12-14

Ya 3

Yesu anajadili Hekaluni

Anatabiri kwenye mlima wa mizeituni

Math 22:15-46

Math 24:1-31

Ya 4

Mafumbo na maonyo kwa wafuasi

Mlo wa mwisho

Mateso Getsemane na kusalitiwa

Math 24:32-25:46

Math 26:17-30

Math 26:36-56

Ya 5

Hukumu ya Yesu

Kusulibiwa na kuzikwa

Yoh 18:14-19:16

Yoh 27:31-27:61

Ya 6

Mkesha

Math 27:62-66

Ya 7

Wanawake waandaa manukato

Luka 23:56

Ya 8

 

 

Ya 9

Kufufuka

 

 

Mlima wa Mizeituni na YerusalemuuSafari za Yesu kutoka Jeriko hadi Yerusalemu

Yersualemu

Siku sita kabla ya Pasaka, siku ya kusulibiwa kwake Yesu alisafiri kutoka Jeriko hadi Bethania ambayo ilikuwa kwenye Mlima wa Mizeituni, Mashariki mwa Yerusalemu na kukaa kwa rafiki zake, Maria, Martha na Lazaro, jioni yote (Yoh 12:1-11). Nyumba yao ikawa makao yake kwa muda wa siku chache alipokwenda kilomita mbili tokaBethania hadi Yelusalemu na kurudi pale jioni (Math. 21:17). Miezi kadhaa awali Lazaro alikuwa amefariki dunia na Yesu akamfufua (Yoh. 11)

 

Yesu aingia Yerusalemu akiwa amepanda punda (Math. 21:1-9)

 

Tukio maarufu la Yesu kuingia Yerusalemu akiwa amepanda punda lilifanyika siku iliyofuata. Tukio hili lilikuwa limetabiriwa na Nabii Zakaria (Zak. 9:9) “Furahi sana ewe binti yake Sayuni paz sauti ewe binti yake Yerusalemu; tazama, mfalme wako aja kwako; yeye ni mwenye haki na mwenye wokovu; mnyenyekevu na amepanda punda na kwenye mgongo wa mwana punda.” Yesu alipoingia Yerusalemu makundi ya watu ambao walikuwa wakienda kule kwa ajili ya Pasaka walitandika mavazi yao na matawi mbele yake wakisema kwa sauti na kusema, “Hosanna (okoa sasa); mbarikiwa ni yeye ajaye katika jina la Bwana. Ubarikiwe ufalme wa Baba yetu Daudi ajaye katika jina la Bwana: Hasanna juu mbinguni.” (Marko 11:9-10) Luka aongezea kuwa walisema “Abarkiwe mfalme ajaye katika jina la Bwana” (Luka 19:38)

Umati mkubwa uliofuatana na Yesu alipokuwa anaingia jijini ulimsifu Mungu ukitumia maneno yale yale ya Zaburi 118:25-26 na hilo liliwakasirisha Makuhani Wakuu, Waandishi na Wafarisayo.

Walakini watu walimwona Yesu kama

  • Aliyekuja kwa jina la Mungu

  • Angekuwa Mfalme

  • Angetawala katika ufalme wa Daudi

 

Japokuwa haukuwa wakati wake, walielewa kuwa Mungu alikuwa ametabiri kwamba mwana wa Daudi angeanzisha upya utawala wa Mungu hapa Duniani mjini Jerusalemu.

 

Yesu asafisha Hekalu

 

Katika mojawapo ya siku zile yesu alipoingia Yerusalemu aliingia hekaluni na kukuta wafanya biashara wakinunua na kuuza wanyama kwa ajili ya pasaka ulikuwa ni wakati mzuri kwa wachuuzi wa wanyama na ndege wa sadaka, lakini Yesu alitambua mara moja kuwa tendo hilo lilipuuza sababu ya kweli ya kukutana Yerusalemu yaani kumwabudu Mungu kwa kukumbuka kukombolewa kwao kutoka utumwani Misri. Katika mojawapo ya ghazbu zake chache Yesu “alianza kuwatupilia nje wale waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni, na kupandia meza zao wabadilisha fedha na viti vya wauza njiwa” akisema “ Haikuandikwa kuwa nyumba yangu itaitwa na mataifa yote kuwa ni nyumba ya sala? Lakini nyie mwaifanya pango la wezi.” (Marko 11:15-17; linganisha na Isaya 57:7). Nukuu ya Isaya inazungumzia wakati ujao wakati Nyumba kuu ya sla na ibada itakapojengwa Yerusalemu kwa ajili ya watu wote (Isaya 2:2-4; Zakaria 14:16-19)

 

Mambo haya unayofanya kwa mamlaka ya nani?

 

Makuhani wakuu na wazee walifadhaishwa na matendo ya Yesu. Kwa desturi zao walikuwa wameilazimisha dini na kuigeuza kuwa biashara iliyositiri mitindo yao ya maisha. Baadaye Petro alionya kuhusu mwelekeo huo. “Watatokea walimu wa uongo miongoni mwenu........ na wengi mtafuata njia zao batili na kwa sababu yao ukweli utaitwa uovu. Na kutokana na tamaa kwa maneno ya ulaghai watawafanya nyie bidhaa.” (2 Petro 2:1-3). Tabia ya Mafarisayo imerudiwa hata miongoni mwa Wakristo miaka yote hadi sasa kama Petro alivyotabiri, na viongozi wengi wa dini wameeleweka vibaya kwa vile walivyowadhulumu watu na kuwanyima ukweli (linganisha na maneno ya Yesu katika Mathayo 23:13)

Tukio hili liliongeza chuki ya viongozi wa dini dhidi ya Yesu. Waliweka rohoni mwao nia ya kula njama ili wamuue lakini juhudi zao zilishindwa hadi walipopata mwanya wa kutumia udhaifu wa Yuda Iskariote wa tamaa ya fedha kwa kuwa alikuwa mwizi (Yohana 12:6) walimpa vipande 30 vya fedha ili amsaliti Yesu naye akakubari. Taarifa za kina kuhusu siku hizi za mwisho na matukio yaliyotokea zinapatikana katika Mathayo 21-25.

 

Utabiri wa Oliveti (Luk 21; Math 24)

 

Yesu alipokuwa anatoka hekaluni kwa mara ya mwisho wafuasi wake walinadi kuhusu uzuri wa majengo hayo. Yesu aliwaambia kuwa wakati unakuja ambapo hakuna jiwe hata moja litakalobaki juu ya jiwe jingine kwa sababu hekalu litakaribiwa kabisa. Kwa mshangao walimuuilza jambo hilo litatokea lini na litafanyikaje?

Yesu alianza kusimulia matukio ambayo yangetokea hadi kuvunjwa kwa Jiji (Yerusalemu) mnamo mwaka wa 70 Baada ya kristo na Jeshi la Kirumi likifuatiwa na kutawanyika kwa wayahudi katika mataifa yote (Luka 21:20-24). Hata hivyo aliendelea kuwaeleza wafuasi wake kuwa atakuja kuurejesha upya ufalme lakini japo alikuwa amewaambia mara nyingi kwamba ni lazima kwanza ateswe na kufa hawakuelewa alichokuwa anamaanisha. Hakutaka wakate tamaa bali kuhakikishiwa kuwa angerudi tena kwa hiyo aliwapa ishara za wazi ambazo zingetangulia kurudi kwake kuja kurejesha Ufalme wa Mungu (Luka 21:25-36)

Miongoni mwa ishara zilizoorodheshwa alitabiri kuvunjika kabisa kwa maadili katika jamii; maovu yatafanana na yale ya wakati wa Noa (Mathayo 24:36-39). Pia alizungumzia mvutano kati ya taifa na taifa ambao utaleta mfadhaiko na wasi wasi nyakati ambazo zitasababisha kukata tamaa kwa kuwa itaonekana kuwa hakuna njia ya kuepuka hali hiyo (Luka 21:25). Alimalizia onyo lake kwa maneno haya. ”Kwa hiyo angalieni na salini daima ili mstahiki kuepushwa na mambo yote hayo ambayo yatatokea na kusimama mbele ya mwana wa mtu” (Luka 21:36). Wote wanaopenda kukutwa wakiwa tayari wakisubiri kurudi kwa Bwana Yesu Kristo wanapaswa kusoma na kutafakari utabiri huu.

 

Mlo wa mwisho katika Chumba cha Juu (Math. 26:17-30)

 

Katika usiku uliotangulia kusulibiwa kwake, Yesu alikutana na wafuasi wake katika chumba cha juu (orofani) katika jiji la Yerusalemu. Alisema na kufanya mambo mengi ya maana safari hiyo lakini jambo moja lina umuhimu wa pekee. Hili lilikuwa kuanzisha jinsi ambayo kuanzia wakati huo na kuendelea, wafuasi wake wangemkumbuka yeye na mambo ambayo alikuwa amewafanyia. Alijua lingekuwa jambo la kufa na kupona kwao kukumbuka jinsi alivyofidhabihu kwa upendo; kwa hivyo akawapa kama ukumbusho alama za mkate na divai.

  • Mkate, Yesu ”alichukua mkate akashukuru na akaugawa, akawapa wanafunzi wake akisema, huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi (Luka 22:19) mkate ulitumika kama alama ya mwili wake, mwili ambao kila mara aliutoa kwa matakwa ya Baba yake (Waebrania 10:5-10; Wafilippi 2:8). Baada ya muda mfupi, katika bustani ya Getsemane na baada ya mahangaiko makubwa sana ya kimwili na kiakili angejiweka kwenye yale maumivu ya mwisho ya kufa kwake msalabani. ”Siyo kwa matakwa yangu bali yako yatimizwe.” ndio uliokuwa mwitikio wake kila mara. Mwili wake ulifananishwa na ule wa mwanakondoo wa Pasaka ambao ”haukuwa na doa” (1 Petro 1:18-19; 1 Wakorintho 5:7)

  • Divai, Yesu alipowapa divai wanafunzi wake alisema. Hii ni damu yangu ya agano jipya itakayomwagika kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi (Math. 26:27-28) Divai iliwakilisha damu yake. Damu yake ilifananishwa na damu ya mwanakondoo wa Pasaka iliyomwagika kwa ukombozi wa Israeli. Kwa hiyo ”damu ya Yesu yenye thamani kubwa” imemwagwa mara moja kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu wote (1 Petro 1:18-19) kupitia maisha yenye utiifu kamili yaliyoishia katika kusulibiwa kwa kutii matakwa ya Mungu amesababisha maondoleo ya dhambi kwa wote wajao kwa Mungu kupitia yeye, yawezekane.

Lile tendo rahisi la kula na kunywa vikumbushio hivi linazingatiwa na wote wale wanaopenda kutii amri za bwana (linganisha na 1 Wakorintho 11:23-29) Hili huwaunganisha katika umoja na yeye, wanapojitahidi kuelewa mfano wake wa ajabu wa maisha na gharama kubwa ambayo imelipwa kwa ajili ya uwokovu wa Mwandamu (1 Wakorintho 10:16-17). Kwa kula mkate na kunywa divai muumini, kiakili huunganisha maisha yake na maisha ya Yesu Kristo ili kwamba anaonekana kuwa anaishi ndani yake (Yoh. 6:51-57; Wagalatia 2:20)

 

Umuhimu wa Kifo cha Yesu Kristo

 

Tunakumbuka kuwa Yohana Mbatizaji alipomwona yesu karibu na Yordani alisema. Tazama Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya dunia (Yoh.1:29) Yohana alikuwa anarudia maneno ya Nabii Isaya ambaye ghafla alitabiri kazi ya Yesu ya ukombozi katika Isaya 53. Katika utabiri huo wa kustaajabisha watu wanazungumziwa kama kondoo waliopotea kila mmoja wao akiwa amegeukia upande wake (aya ya 6). Lugha hii inaeleza vizuri iliyoje! Kwa sababu wote wameacha njia ya Mungu na kutenda dhambi (Warumi 3:19-23)

Na bado kuna mtu mmoja ambaye ni tofauti na wengine, mtu ambaye alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu mwenye huzuni na majonzi (aya ya 3). Mtu huyu anaitwa mwanakondoo ambaye juu yake umerundikwa udhalimu wetu wote (aya ya 6-7), Petro ananukuu aya huyo huyo anapokiri deni kubwa la shukrani ambalo tunamnuwia Yesu Kristo Mwana wa Mungu (1 Petro 2:22-25)

Katika enzi za mitume msafiri mmoja Muethiopia alikuwa anatatanika kuhusu maneno haya na kujiuliza, ”Nabii anamzungumzia nani katika maneno haya? Anazungumzia mwenyewe au mtu mwingine?” (Matendo 8:34). Filipo aliyetumwa na Mungu alimuelewesha na kuanzia kwenye andiko hilo hilo na kumhubiria kuhusu Yesu.” Isaya kwa wazi kabisa anamrejelea Yesu, Bwana na kazi yake ya kumkomboa mwanadamu katika mauti na dhambi.

Isaya anamsema huyu ambaye ”angebeba dhambi za wengi” (aya ya 12) akuifanya ”uhai wake sadaka au tolea la dhambi” (aya ya 10) na tena akimimina roho yake hadi kifo” (aya ya 12). Kwa hiyo Yesu Kristo, kutokana na kujitolea uhai wake katika kumtii Mungu kikamilifu hadi kifo cha kujidhabihu, msalabani aliwapa binadamu wote njia ya msamaha wa dhambi na hivyo kumpatanisha mwanadamu na Mungu.

Hili lilikuwaje hivyo?

  • Yesu ambaye pia alikuwa na asili ya kufa na kutenda dhambi kama wanadamu wengine wote alishinda kishawishi cha kuenda dhambi kwa kitendo chanya cha kutimiza matakwa ya Mungu mara zote. Mtunga Zaburi alitabiri hili akisema ”Nina furahia kutenda utakavyo, Ewe Mungu wangu: ndiyo sheria yako imo moyoni mwangu.” (Zaburi 40:7-8; Waebrania 10:7). Japo alijaribiwa katika mambo yote kama sisi, hakutenda dhambi kamwe (Waebrania 4:15)

  • Ilikuwa ni kupitia katika kifo chake ndipo alipolaani na kuharibu kabisa hadharani ile tabia ya kutenda dhambi ambayo sote tumerithi kutoka kwa Adamu: ”Kwa kiasi kile ambacho watoto wana mwili na damu yeye pia alitwaa sehemu ya vitu hivyo; ili kupitia kifo aweze kumharibu yule aliyekuwa na uwezo wa mauti yaani shetani” (Waebrania 2:14)

  • Katika kifo chake ”alisulubisha mwili pamoja na mapenzi na tamaa” (Wagalatia 5:24) Japo alisulubiwa, ni yeye ndiye aliyepata ushindi! Dhambi haikumshinda, kwa sababu kila mara alitekeleza mapenzi ya Mungu. ”Siyo kwa mapenzi yangu, ila yako yafanyike” lilikuwa ndilo itikio lake hata katika majaribu yake makubwa kabisa (Luka 22:42)

  • Paulo anaeleza mafanikio yaliyopatikana kutokana na kifo cha Kristo alipoufanya mwili wake kuwa sadaka kaajili ya dhambi na kumimina roho yake katika kifo,( Isaya 53:10-12) ”kwa maneno haya kwa maana kile sheria ilishindwa kufanya, kwa sababu ilikuwa dhaifu kutokana na mwili, mungu aqkimtuma mwanaume aliye fanana na mwili wenye dhambi na kwa ajili ya dhambi alilaani dhambi katika mwili (warumi 8:3) Ni yeye peke yake ambaye anaweza kutuokoa kwa sababu tuko kama sisi lakini si mtenda dhambi.

  • Kristo alikuwa nayo ile hali ya kufa kama walivyo wajukuu wote wa Adamu , walakini japo aliuawa na watu waovu haikuwa sahihi kwamba angeendelea kuwa mtu. ”Mshahara wa dhambi ni mauti ( warumi 6:23) na hapa alikuwapo mtu na hivyo hakuwa amelipwa mshahara huu. Ufufuo wa myu huyu kwa sababu hiyo ulikuwa hauepukiki ” Mungu amemnyanyua baada ya kuruhusu maumivu ya kifo yamtese kwa kuwa alikuwa haiwezekani kuwa aendelee kushikiliwa nayo’’ (matendo 2:2; wafilipi 2:8-9) Mungu ambaye ni mwenye haki ; kwa furaha alimnyanyua mwanawe mpendwa baada ya siku tatu tu kaburini kama alivyokuwa ametabiri (zaburi 16:10 ulionukuliwa katika matendo 2:270 kwa hiyo akawa mtu wa ukombozi wa milele kwa wote wanaomtu” waebrania 5:9)

 

UBATIZO ( MFANO WA KUSULUBISHWA KWA KRISTO (WARUMI 6:3-6)

 

Sasa tunaweza kuelewa vizuri zaidi umuhimu wa ubatizo, ambao kwao tumesulubishwa na Mungu. Katika ubatizo tunafanana na kile ambacho Bwana wetu Yesu Kristo alipata katika kifo chake, ushindi wa hali ya juu dhidi ya nguvu ya dhambi (Waebrania 2:14). Paulo anafananisha kifo cha Yesu na ubatizo wetu akisema ” mzee wetu amesulubiwa naye ili mwili wa dhambi uharibiwe ili tangu sasa tusitumikie dhambi (Warumi 6:6)

”Mzee wetu” ni sisi tulivyokuwa kabla hatujasulubishwa na Mungu. Katika ubatizo ”mzee wetu” hufa. Tunaukataa ”mwili wa dhambi” tabia zetu za awali ambazo hazimtukuzi Mungu. Tunakiri kuwa Mungu ni mwenye haki tunapolaani dhambi. Lakini kuna lile jambo lingine katika ubatizo. Vile Yesu alivyofufuka katika mauti asife tena ndivyo na sisi tunavyoibuka katika maji kama ”mtu mpya” (au nafsi) katika Kristo (Waefeso 4:20-24). Dhambi zetu za zamani zimesamehewa na tunaanza namna mpya ya maisha kufuata mfano wa yesu Kristo Bwana wetu (Warumi 6:16-18; 1Petro 2:21-25)

Kuna sehemu kadhaa za maandiko ambazo zinasaidia kutuonyesha mambo haya – Warumi 6, Wakolosai 3:1-15, na Waefeso 4:17-32. Tafakari baadhi ya masomo mengine ambayo Paulo anayapata kutokana na kufanikisha kusulibiwa kwa Yesu na ubatizo.

 

  • Paulo alijiona kama mtu aliyekufa, na maisha anayoishi yalionyesha maisha ya Yesu ndani yake (Wagalatia 2:20)

  • Wale ambao kupitia ubatizo ni waYesu wamesulubu mwili pamoja na vitu viwapendezavyo na tamaa zao (Wagalatia 5:24)

  • Kwa kujifananisha na kifo cha Kristo dunia ”ilisulubiwa” kwake na yeye kwa namna ya maisha ya kidunia. Maisha katika Kristo yalikuwa kila kitu (Wagalatia 6:14)

 

Kusulibiwa lilikuwa jaribu lenye kuuleta maumivu makali sana. Kusahau tabia zetu za awali, kuyapa mgongo maisha yetu ya zamani kunaweza kwa uhakika kuleta maumivu na kugumu. Lakini tunapojitolea kumtumikia Mungu na kutimiza mapenzi yake furaha itokanayo na utumishi huo inatupa nguvu za kutuhamasisha kuendelea kwa neema ya Mungu. Kuhusu Yesu inasemekana kuwa ”kutokana na furaha iliyokuwa mbele yake alivumilia mateso ya msalaba, akidharau aibu na sasa ameketi kuume kwa kiti cha Enzi cha Mungu.” (Waebrania 12:2)

Kwa hiyo wale wafuatao namna yake ya kuishi wanaweza kuhamasishwa kila siku kuyaona maisha yao kama maandalizi kwa ajili ya wakati ule ambapo watakuwa kitu kimoja naye pamoja na Baba yake katika kiti chake cha enzi (Ufunuo 3:21)

 

Kufufuka kwa Yesu (Mathayo 28 & Luka 24)

 

Ujumbe mzima wa Injili (habari njema) unategemea ufufuo. Ufufuo wa Yesu Kristo umeandikwa katika Injili zote nne. Ukweli wa jambo hili ulipodhihirika kwa mitume na wafuasi wa Yesu majonzi na kukata tamaa viliondoka na kuwaacha wakiwa na furaha kuu. Ufufuo wake ukawa uthibitisho kuwa yote yale Mungu aliyoahidi yatatekelezwa. Kwa kweli mtume Paulo, kwa ujasiri kabisa asema ”Kristo asingefufuka mafundisho yetu yangekuwa kazi bure na imani yenu pia ingekuwa kazi bure.” (1 Wakorinto 15:14). Katika sura hii anathibitisha ukweli wa kihistoria kuwa Yesu alifufuka kwa kuwataja wale ambao walimwona akiwa hai baada ya kufufuka (1 Wakorinto 15:4-8)

Maajabu ya ufufuko wa Yesu ni ukweli usiopingika na pia msingi ambao imani yetu katika Mungu aliye hai imejengeka vilivyo kutokana na kufufuka kwa Kristo njia ya kuelekea kwenye ushindi dhidi ya dhambi na mauti imefunguliwa kwa wote wajao kwa Mungu kupitia imani katika yeye. ” Kwa maana kwa kuwa kutokana na mtu kifo kilikuja kupitia kwa mtu pia ufufuo wa wafu ulikuja. Kwa kuwa kutokana na Adamu wote hufa, hivyo hivyo kutokana na Kristo wote watafanywa wazima. Lakini kila mtu kwa utaratibu wake: Kristo, matunda ya kwanza; baadaye wale wote walio wa Kristo atakapokuja.” (Wakorinto 15:21-23)

Kristo atakaporudi kazi yake ya kwanza itakuwa kuwafufua wote waijuayo injili na kwa hiyo ambao ambao wanawajibika. Hii ni pamoja na wale ambao katika uhai wao waliamini Injili wakabatizwa katika Kristo. Kwa kuwa walikufa wakitumaini kufufuliwa, japo ni wafu kabisa, wanaitwa waliolala katika Yesu (1 Wathesalonike 4:14). Wakati wa hukumu (Yohanza 5:27-29; 2 Wakorinto 5:10) wale watakaoonekana mbele ya Yesu mwamuzi mwenye haki, kustahili kuishi watapewa uhai usiokufa. Paulo aeleza hili katika 1 Wakorinto 15, akisema ”Tazama, nakuonyesheni fumbo; hatutalala wote ila tutabadilishwa katika muda mfupi, kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho: kwa kuwa parapanda italia na wafu watafufuliwa katika hali adilifu na tutabadilishwa. Maana hali hii ya ufisadi itavalishwa uadilifu na hii hali ya kufa itavaa hali ya kutokufa” (aya ya 51-53).

Kwa hiyo kufufuka kwa Yesu Kristo ndio msingi wa ”matumaini” yaliyomo katika Injili. Hali hii ”ya kufa” yenye asili ya umauti itabadilishwa na kuwa hali ya ”kutokufa” ili tuweze kushiriki katika Ufalme wa milele na Kristo.

 

Kazi ya Kristo Mbinguni kwa sasa Kuhani Mkuu wa Nyumba ya Mungu.

 

Tunajua kuwa Yesu Kristo amekwenda Mbinguni (Matendo 1:9-11) na kwamba sasa hivi ameketi kuumeni kwa Mungu akingoja wakati Mungu atakapomtuma tena hapa duniani (Zaburi 110:1; Marko 16:19; Matendo 3:19-21). Kuna marejeo mengi yanayoeleza kuwa yuko katika upande wa kulia wa Mungu sasa hivi (Matendo 2:33-34; Warumi 8:34; Wakolosai 3:1-2; Waebrania 1:3; 10:12; 12:2; 1 Petro 3:22).

Kazi yake kuu mbinguni ya ”Kuhani Mkuu katika nyumba ya Mungu” (Waebrania 10:21). Nafasi hii ya sasa ya Bwana pia ilitabiriwa katika Zaburi 110:4. Kazi anayofanya sasa ina umuhimu mkubwa kwa wote wanaotaka kumtumikia Mungu kwa kukubalika. Tumeona katika mafunzo yaliyopita kuwa kupitia ubatizo dhambi zetu zilizopita zimesamehewa. Hata hivyo baada ya ubatizo, japo tunajaribu kwa bidii zaidi kumpendeza Mungu bado sisi wote tunashindwa, kutokana na dhambi. Hapo ndipotunapoelewa maajabu ya Kuhani wetu Mkuu Mbinguni ambaye kupitita kwake tunaweza kuwasilianana Baba kwa njia ya sala na kuomba msamaha, msaada na mwongozo katika maisha (Waebrania 4:16). Yeye ndiye ”mtetezi pekee kati ya Mungu na Mwanadamu” (1 Timoteo 2:5).

Kuna marejeo mengi yanayozungumzia kazi hii ya Bwana Kristo na kutuonyesha jinsi anavyofaa kutimiza kazi hiyo kwa niaba yetu. ”Aliguswa na hisia za udhaifu wetu” na katika hali zote alijaribuwa kama sisi sote tunavyojaribiwa lakini hakutenda dhambi ( Waebrania 4:17-16 ). ”Yeye ni kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu ambaye kwa sababu amevumilia majaribu yuko tayari kusaidia wenye shida” ( Waebrania 2:17-18 ). Isitoshe njia ya kumfikia Mungu inapatikana siku zote kupitia kwake kwa kuwa huishi siku zote kama kiungo kati ya wale wajao kwa jina lake na Mungu ( Waebrania 7:24-25 ). Ni mtetezi wetu kwa Mungu ( 1 Yohana 2:1-2).

 

Wale ambao wamekuwa wana wa ” Nyumba ya Mungu” kutokana na imani na ubatizo katika Kristo wana upendeleo huu mtukufu wa kumwomba Mungu kupitia yeye wakitaka msamaha wa dhambi. Walakini Mungu huwa anaweka kumbukumbu za sala za wale wote ambao kwa kweli wanapenda kumfahamu na wako tayari kujifunza na kujifunza njia zake. Mungu hatatuwekea pingamizi kama tunayo nia hiyo. Kama Yesu mwenyewe alivyosema,”huu ni uzima wa milele, ili waweze fahamu wewe, Mungu pekee wa kweli naYesu Kristu uliyetuma” ( Yohana 17-3). Tunao mfano wa Korneli aliyemwomba Mungu, (Matendo 10:1-2) na Mungu akasikia sala yake na akamwonyesha ukweli katika Kristo Yesu; na alipoamini ukweli huo akabatizwa (Matendo 10:47-48).

 

Sala – Sehemu muhimu katika maisha ya Muumini

 

Yesu alisema kuwa, ”watu wanapaswa kusali kila mara na siyo kuzimia” (Luka 18:1) akionyesha umuhimu wa sala kama chanzo cha raha na nguvu katika maisha ya wafuasi wake. Yeye mwenyewe ametupa mfano kuhusu hili kwa maana mara nyingi twasoma habari za kusali kwake kwa Mungu. Pia alitupa mfano wa jinsi ya kusali katika Mathayo 6:9-13 na Luka 11:1-4. Zaburi ni sala zilizoandikwa ambazo zaweza kuwa chanzo cha msaada wa kutuongoza katika maombi yetu kwa Mungu.

Mtume Paulo aliandika: ”usiwe na wasiwasi kuhusu chochote bali kwa kusali, kusujudu na kutoa shukrani kwa kila kitu maombi yenu yatafahamika kwa Mungu. Na amani ya Mungu ishindayo akili yote itaweka mioyo na akili zenu kupitia Kristo Yesu (Wafilipi 4:6-7) moja ya mambo ya mwisho ambayo Yesu aliwahimiza wafuasi wake kufanya ni kukesha na kusali kila mara (Luka 21:36)

Ni upendeleo ulioje walionao wale waliowa nyumba ya Mungu katika Yesu Kristo upendeleo wa kuweza kumfikia Mungu kupitia kwake katika sala na msamaha wa dhambi.

 

MHUTASARI

 

  • Wiki ya mwisho katika utume wa Yesu inachukua kipindi cha tangu alipowasili Bethania, siku sita kabla ya kifo chake hadi kusulibiwa kwake (Mathyo 21:20-36)

  • Unabii wa kwenye mlima wa mizeituni ulitabiri kuteketezwa kwa Yerusalemu na Warumi, mwaka 70 Baada ya Kristo (BK) pamoja na kutawanyika kwa Wayahudi na pia ishara zitakazotangulia kurudi kwa Yesu Kristo hapa duniani kuja kuanzisha Ufalme wa Mungu (Luka 21:20-36)

  • Kutokana na maelezo kuhusu mlo wa mwisho ghorofani (Mathayo 26:17-30) tumepewa kwa kina maelezo kuanzishwa na Yesu kwa mkate na divai kama ukumbusho wa mwili wake na damu yake vilivyotolewa katika kumtii Baba yake (Mathayo 26:26-29) kutokana na kujidhabihu kwake ametupa msingi wa msamaha wa dhambi kwa wote waaminio na kubatizwa.

  • Paulo awakumbusha waumini juu ya ubora na umuhimu wa kumkumbuka Yesu Kristo Bwana kwa njia hii wanapokusanyika katika Ibada (1 Wakorinto 11:23-29).

  • Kusulubiwa kwa Yesu lilikuwa ndilo tendo kuu la mwisho lenye utiifu uliokamilika na wa hiari kwa Mungu ambao kutokana nao alipata ufufuo kwenye uzima wa milele (Wafilipi 2:8-9; Matendo 2:24; Warumi 5:17-18,21; 6:9-10

  • Kufufuka kwa Yesu kulifungua njia ya kuelekea kwenye uzima wa milele kwa wale wote waaminio na kubatizwa katika yeye (1 Wakorinto 15:21-23; Warumi 5:21; 6:9, 23)

  • Sasa hivi Yesu yuko mbinguni upande wa kulia wa Mungu (Zaburi 110:1), ambapo anatenda kama Kuhani Mkuu juu ya ”nyumba ya Mungu” (Waebrania 10:21). Katika wadhifa huu anawatetea ”waliomo ndani yake” akiombea kwa niaba yao kwa Mungu (Waebrania 7:24-25). Kwa hiyo sisi tunamfikia Mungu kupitia kwake (Warumi 8:34; 1 Yohana 2:1-2)

  • Maombi kwa Mungu kwa jina la Yesu Kristo ni sehemu ya lazima katika maisha ya mfuasi – upendeleo mkuu kwa wale waliomo ”ndani ya Yesu” (Wafilipi 4:6-7; Luka 21:36; Mathayo 6:9-13).

 

Somo la 21 – Maswali

 

  1. Katika Unabii wa kwenye mlima wa mizeituni Yesu aliwaambia wafuasi wake kuwa ni lazima wafanye nini ili wawe tayari kumpokea atakaporudi duniani?

  2. Kule ghorofani Yesu aliwaambia wafuasi wake wafanye nini mara kwa mara katika kumkumbuka yeye?

  3. Mkate unawakilisha nini?

  4. Yesu aliwapa divai wafuasi wake alisema nini?

  5. Orodhesha baadhi ya mambo tunayojifunza kutokana na kifo cha Yesu Kristo?

  6. Ni kwa jinsi gani ubatizo unafananishwa na kifo cha Yesu Kristo?

  7. Kwa nini ufufuo wa Yesu ndilo tumaini kuu la Injili? (Angalia ! Wakorinto 15:21-23)

  8. Ni kazi gani afanyayo Yesu Mbinguni kwa niaba ya waumini sasa hivi?

  9. Ni upendeleo gani walionao wana wa nyumba ya Mungu kupitia kwa Yesu Kristo?

 

 

 

 

 

 

 

Swahili Title
KUSULIBISHWA NA KUFUFUKA KWA YESU
Swahili file
Status
Added to Internet
African text
Christadelphian Bible Mission
Translator 1
Raphael Mkeya
Literature type