Exploring the Bible - 19

Swahili

Somo la 19 Mathayo 3

 

Yohana Mbatizaji alituuwa “kuandaa njia” ya Bwana wetu Yesu Kristo (Luka 1:16-17)

Kazi yake ilikuwa imetabiriwa kinabii na manabii wa Agano la Kale (Isaya 40:1-8) na Malaki (3:1) kama inavyoonyeshwa katika Marko 1:1-5 na Mathayo 3:1-7.

 

Yohana alipoulizwa kwa nini alikuwa anabatiza alijibu kuwa yeye ndiye aliyezungumziwa katika Isaya 40:3 (linganisa na Yohana 1:22-23). Mungu alikuwa amemtuma kubatiza (Yohana 1:33)

 

Ujumbe wa Yohana ulitabiriwa na Isaya (Isaya 40)

 

Isaya alitabiri ujumbe ambao Yohana angehubiri. Yohana alizungumziwa kama “Sauti ya yule apazaye sauti Jangwani” (aya ya 3) na tunapewa ujumbe ambao “Sauti hiyo” ingetangaza katika aya ya 6-8:

 

  • Mwili wowote ni majani hunyauka na kukauka. Kwa ujumbe huu alitutangazia kuwa mtu hufa.

  • Neno la Mungu litasimama milele. Kanuni hii inaelezwa katika 1 Petro 1:23-25

 

Yohana ahubiri ubatizo (Mathayo 3:1-6)

 

Yohana alikuwa anafundisha kuwa lazima mtu akiri kuwa ni dhambi na kwa hiyo anastahili kufa (Warumi 5:12. 21; 6:23) Hata hivyo alifundisha pia kwamba wale ambao wanakiri kwamba njia za Mungu ni sahihi na wakajaribu kuishi kama Neno la Mungu linavyosema wangeishi milele (1 Yohana (2:15-17; Petro 1:22-25). Hivyo watu walipokuja kumsikia Yohana na kuelewa ujumbe wake, twaambiwa kwamba:-

  • Waliungama dhambi zao walikiri kuwa walikuwa wanatenda dhambi na kwamba njia ya Mungu ilikuwa sahihi.

  • Walijutia dhambi zao walibadilika moyoni mwao wakakubali kubadili njia zao pia. Waliacha kufanya watakavyo wakajaribu kufuata njia ya Mungu

  • Walibatizwa walikubali kuzamishwa na Yohana majini wakinadi hadharani kuwa wamebadilika. Kwa kufanya hivyo walikiri kuwa kama watenda dhambi walistahili kifo. Kwa namna nyingine walikufa katika njia zao za zamani ambazo zilikuzana na njia ya Mungu na sasa walidhamiria kumtumikia.

 

Wafarisayo waja kwa Yohana (Mat. 3:8-12)

 

Wafarisayo ndio waliokua viongozi wa dini siku hizo na wengi wao walikuwa wenye kujiona Neno “Pharisaical” limeingia katika lugha ya kiingereza likiwa na maana ya kujiona. Walipokuja kwa Yohana kuchunguza alichokuwa anafanya, Yohana alikuwa muwazi kabisa nao. Aliwaita “Kizazi cha Nyoka” ambapo alionyesha kuwa walihesabiwa kuwa miongoni “kizazi kilichotokana na joka kuu” lisemwalo katika Kitabu cha Mwanzo 3:15.

 

Kadri walivyoendelea kuvutiwa na mambo ya kuwanufaisha wao peke yao, walikuwa hawamtukuzi Mungu. Walikuwa na hoja kubwa ya kutubu dhambi zao.

 

Yesu aja kwa Yohana akabatizwe (Mathayo 3:13-17)

 

Watu walipokuja kwa Yohana kubatizwa walitakiwa wajutie dhambi zao. Ni kutokana na toba hii ndipo Yohana alipowabatiza. Walakini Yesu alipokuja kwa Yohana alikuwa na dhambi za kuungama au kujutia. Kwa sababu hiyo alijiona kama hastahili kumtaka Yesu ajishushe na kubatizwa, na alimwambia “Mimi ndiye ninayehitji kubatizwa nawe na wewe ndiye unayekuja kwangu?” Yesu alijibu, “Hivyo ndivyo unavyopasa kufanya ili kutimiza haki zote” Kwa hiyo Yohana akambatiza.

 

Kwa nini Yohana alikubali kumbatiza Yesu? Ni kwa sababu Yesu alitambua kuwa aliamini kuwa “miili yote ni kama majani” Kwa maana kwamba watu wote wana muda mfupi wa utukufu wa kupita, kama ua la porini linalonyauka na kufa. “Mwili haunufaiki na chochote” Yesu baadaye alisema (Yohana 6:63) Asili ya binadamu kila mara inapenda kulalia upande wa kunifaisha nafsi yake na kila wazo au tama ambayo haimtukuzi Mungu ni kitendo cha dhambi. Fikra na mwelekeo wa kutenda dhambi hazina budi kusagwa – “Kuuliwa” Hili linatekelezwa kwa njia ya mfano katika ubatizo. Lakini ubatizo hauna thamani yoyote mpaka tutkaporuhusu neno la Mungu kubadilisha fikra zetu na kufanya tama zetu zote zikubaliane na matakwa yake. Imani katika neno hai la Mungu itatuimarisha katika kutii amri zake na kutuongoza kwenda kwenye uzima wa milele. uba na kufanya tama zetu zote zikubaliane na matakwa yake. Imani katika neno hai la Mungu itatuimarisha katika kutii amri zake na kutuongoza kwenda kwenye uzima wa milele. Ubatizo ulikuwa ushahidi bayana wa jambo hili.

 

Yesu ambaye alikuwa na hali sawa na wanadamu wote pamoja na mapungufu yote ya asili, ya dhambi na ufedhuli alikuwa akipambana kila siku ili kushinda majaribu (Waebrania 4:15; 2:18) Yesu anaitwa “Neno lililofanywa Mwili” kwa sababu alikuwa ni jumuisho la yote yale ambayo Mungu alikuwa ameandika katika Neno lake.

 

Maneno na matendo yake yalikubaliana kabisa na yale ya Baba yake (Yohana 1:14). Kila mara alitekeleza matakwa ya Baba yake, akishikaa Neno lake, maishani mwake na kwa hilo aliweza kusinda welekeo wa asili ambao kila Mwanadamu anao. Kile ambacyo Yesu alioesha katika ubatizo wake kilikuwa kielelezo cha yale ambayo angetimiza katika maisha yake na hatimaye Baba yake, akishikaa Neno lake, maishani mwake na kwa hilo aliweza kusinda welekeo wa asili ambao kila Mwanadamu anao. Kile ambacyo Yesu alioesha katika ubatizo wake kilikuwa kielelezo cha yale ambayo angetimiza katika maisha yake na hatimaye katika kusulibiwa kwake. Kilikuwa ni dhambi kwa utiifu mkamilifu kwa Mungu hadi kufa (Warumi 8:3; 1Petro 1:21-25)

Ilikuwa ni baada ya Yesu kuungama hadharani na kubatizwa na alipokiri kuwa njia za Mwenyezi Mungu zilikuwa sahihi ndipo Mungu aliposema: “Huyu ni Mwanangu nimpendaye, nipendezwaye naye”

Yohana afungwa na kuuliwa:

 

Si muda mrefu baada ya ubatizo wa Yesu Yohana alitupwa gerezani na Herode kwa sababu alilaani kitendo cha Herode cha kumchukua Herodias, mke wa Philipo nduguye. Herodias alipopata fursa ya kulazimisha Yohana auawe aliitumia na Yohana akauliwa, takribani mwaka mmoja kabla ya kusulubiwa kwa Yesu (Marko 6:17-29)

MUHTASARI

  • Kazi ya Yohana, kama mtangulzi wa Yesu ilitabiriwa katika maneno ya Isaya 40:3-8. Ujumbe wake ulielezwa kwa kifupi katika maneno yafuatayo

    • “Mwili wote ni majani” hunyauka na kufa.

    • „Neno la Mungu litakuwepo milele“

  • Yesu aliwataka wale walioamini wakabatizwe

  • Ubatizo ulikuwa tangazo la hadhara lililotolewa na wale walioungama na kutubu dhambi zao kuwa njia za Mungu ni sahihi (Mathayo 3:6)

  • Katika ubatizo wake, Yesu alishikilia kanuni kwamba „Mwili wote unastahili kufa na kwamba watu wanapaswa kutupilia mbali njia hiyo na kutembea katika njia ya Mungu kama Neno lake lifundishavyo (Mathayo 3:15)

  • Kwa sababu ya Tangazo lake hadharani kwamba angetoa maisha yake kumtumikia Mungu, Mungu alimkiri Yesukama Mwanaye Mpendwa (Mathayo 3:17)

 

Somo la 19 Maswali:

 

  1. Isaya alitabiri mafundisho ya Yohana Mbatizaji kwa maneno haya: “Mwili wote ni majani” na Neno la Mungu litakuwepo milele” Vifungu hivi vya maneno vina maana gani?

 

  1. Watu walipoamini mafundisho ya Yohana ni hatua zipi tatu walizochukua kuonyesha kuwa walikuwa tayari kumtii Mungu?

 

  1. Ni nukuu gani katika Biblia ambayo Yohana alikuwa anarejea alipowaita Mafarisayo “Kizazi cha Nyoka”?

 

  1. Kwa nini Yesu alibatizwa na Yohana?

 

  1. Mungu alikirije kufurahishwa kwake na utii wa Yesu hadi kukubali kubatizwa?

 

Swahili Title
Somo la 19
Swahili file
Status
Added to Internet
African text
Christadelphian Bible Mission
Translator 1
Raphael Mkeya
Literature type