Exploring the Bible - 17

Swahili

KURUDI KWA MATEKA WALIOKUWA BABYLONI HADI WAKATI WA YESU KRISTO

 

SOMO LA 17 SOMA EZRA 1

 

Kama tulivyokwishaona Mungu alitabiri kuwa Wayahudi wangechukuliwa mateka Babiloni kwa kipindi cha miaka 70 na baada ya hapo wangerudi Jerusalemu na Yuda. Utapata habari hizi kwa kirefu katika kumbukumbu zako “Unabii wa miaka 70 wa Yeremia,” somo la 15.

Danieli ambaye alikuwa mateka Babiloni kwa muda wote huo aligundua kuwa kipindi hiki cha miaka 70 kilichotabiriwa na Yeremiah kilikuwa kimeisha na hivyo akamtolea Mungu sala akimwomba awawezeshe Wayahudi kurudi Yerusalemu na katika nchi yao. Sala hii imeandikwa katika kitabu cha Danieli 9. Angalia kwa makini ombi lake (aya ya 1-4, 16-19).

Mungu alikuwa mwaminifu na hivyo alirahisisha masuala ya kimataifa ili utabiri wake uweze kutimizwa. Leo hii bado Mungu anaendelea kusimamia masuala ya kimataifa ili kusudi lake lililofunuliwa kwetu kuhusu kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo liweze kutimizwa bara bara kama alivyotabiri (Danieli 4:17)

 

Amri ya Sairas.

 

Sairas mfalme mkuu na kiongozi wa kijeshi wa Mede-Ajemi aliupindua ufalme wa Babiloni mwaka 538 Kabla ya Kristo (kk) muda si mrefu baada ya kutawala akatoa amri iliyoandikwa katika Ezra 1:1-4. Tunaposoma amri hii tunaona mambo ya kufurahisha.

 

Aya ya 1.

“Kwamba ili neno la Bwana kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa.” HIli linaelezea unabii wa Yeremia kuhusu miaka 70 ya utumwa (Yeremia 25:8-12; 29:10-14). “Bwana aliichochea roho ya Sairas”. Msukumo wa agizo hili ulianzishwa na Mungu mwenyewe ambaye alimfanya Sairas atomize unabii wa Isaya ulioandikwa miaka 200 kabla ya tukio hilo. Katika Isaya Sairas ametabiri kwa jina na ndivyo ilivyo kwa tangazo ambalo angetoa kuhusu ukarabati wa hekalu na Yerusalemu (Isaya 44:28; 45:1-4).

 

Aya ya 2

“Ameniagiza nimjengee nyumba Yerusalemu.” Hekalu lilikuwa limechomwa moto na Nebukadineza na kuteketea kabisa, mwaka 586 K.K katika shambulio la mwisho Yerusalemu (2 Wafalme 25:8-12). Sasa Sairas anatoa amri kuruhusu Wayahudi waliotawanyika warudi na kulijenga upya hekalu.

 

VITABU VYA EZRA, HAGGAI NA ZEKARIA

 

Wayahudi wengi waliitikia amri ya Sairas na kuanza safari ndefu ya kutoka Babiloni kwenda Yerusalemu kwa madhumuni ya kujenga upya hekalu la Yerusalemu. Kitabu cha Ezra chasema kuwa waliongozwa na Joshua na Zerubbabeli wa kuwa na msisimko mkubwa wa kujenga upya hekalu hilo, lakini walikutana na upinzani mkali kutoka kwa majirani zao.

Roho ya Mungu iliwajia wawili kati ya hao waliokuwa wanarudi; Manabii hao ni Haggai na Zekaria; tunasoma kuhusu ushawishi wao katika Ezra 5:1-2. “Halafu Zerubbabel akainuka ……… na ……… Joshua na kuanza kujenga nyumba ya Mungu ambayo iko Yerusalemu na pamoja nao walikuwepo Manabii wa Mungu wakiwasaidia”. Manabii hawa waaminifu siyo tu kwamba waliwatia moyo kupitia ujumbe wao bali pia walijihusisha katika ujenzi. Sehemu ya kitabu cha Ezra iliyobaki inatueleza juu ya ukamilishaji wa Hekalu na juhudi za Ezra kama kasisi, kuanzisha upya ibada ya kweli ya Mungu miongoni mwa watu.

 

NEHEMIA NA MALAKI

 

Hekalu lilipokamilika Wayahudi walikabili kazi ya kujenga upya za Yerusalemu. Hii ilikuwa kazi kubwa na ni Nehemia, Myahudi na Mtumishi mwaminifu wa Artaxerxes mfalme wa Ajemi aliyeomba kwa mfalme ruksa ya kurudi Yerusalemu, kusimamia kazi ya ujenzi wa kuta za jiji (Nehemia 2:1-6).

Ombi lake lilikubaliwa na alipokuwa anarudi Yerusalemu alipanga vizuri kazi hii. Habari zote za matatizo aliyokabili na jinsi hatimaye kazi ilivyokamilishwa kwa kurahisishwa na mkono wa Mungu zimefunuliwa katika kitabu cha Nehemia.

Katika kipindi kinachohusika na kitabu cha Nehemia tunaona kwamba uaminifu wa Wayahudi ulipunguka waliruhusu ibada ya Mungu kuwa utaratibu usiokuwa na maana yoyote. Mungu alimtuma malaika mjumbe wake kuwarudisha watu tena kwenye imani katika ibada zao (Malaika 1:6-8) ujumbe wake mkali lakini wenye kutii moyo japo mfupi umeandikwa katika unabii wa malaika.

 

TANGU KURUDI KWA MATEKA HADI YESU KRISTO

 

Matukio ya mwisho ya kihistoria yaliyoandikwa katika Agano la Kale yanahusukurudi kwa mateka yerusalemu, kuanzishwa upya kwa ibada hekaluni na ujenzi wa kuta za jiji. Matukio hayo yaliishia mwaka 450 k.k

Ili upate habari zote za miaka 450 tangu enzi za Nehemia na Malki adi kuzaliwa kwa Yesu Kristo tunahitaji kusoma historia ya kidunia ya wakati huo.

Danieli alitoa tabiri kadhaa ambazo haswa zinahusu kipindi chake. Tabiri hizi zinapatikana katika Danieli 8, 9 na 11. Sura ya 11 inazungumzia matukio yaliyofuatia kuangushwa Himaya ya Ajemi kulikofanywa na Wagiriki mwaka 333 K.K hadi kuibuka kwa utawala wa Roma.

Alekzanda Mkuu, baada ya kuvunja himaya ya Mede-Ajemi alifariki dunia akiwa Babiloni mnamo mwaka 323 K.K. Himaya yake, mwishowe iligawanywa katika sehemu nne na kutawaliwa na Majemedari wake wanne (angalia Danieli 7:6; 8:22; 11:4) Sehemu iliyo kaskazini mwa Israeli iliitwa Ufalme wa Seleucid ambapo ile iliyoko kusini ya Israeli katika Misri ilitawaliwa na nyumba ya Ptolemi. Falme hizi mbili zilishindania umiliki wa Israeli bila kikomo. Katika Danieli 11 zinatajwa kama “mfalme wa kaskazini” na “mfalme wa kusini” (aya ya 5-35) kwa kuwa huru ndiyo uhusiano wa kijiografia ulikuwapo na Israeli.

Hatimaye familia ya Hasmon iliunda jeshi ndani ya Israeli, la kukabiliana na hali hiyo. Walikuwa Mahsomoni na pia walijulikana kwa jina la Makabayo kutokana na vile Wagiriki walivyomwita kiongozi wao Yuda bin Mattathias. Mfalme wa Kiseleucid Antiokus IV Epifanes alikuwa amenajisi hekalu la Yerusalemu na kuwakataza Wayahudi kuabudu kulingana na sheria yao. Hili lilisababisha uasi uliolipuka katika kijiji cha Modein na kusababisha baadaye Yuda alizidi nguvu jeshi la Seleucid. Familia ya Hasmon ilikuja kudumishwa na kuwa ya Kikuhani na kutawala, mnamo mwaka 163 K.K. Familia hii iliendelea hivyo hadi mwaka 37 K.K Kuhani Mkuu na Mfalme wa Kihasmon alipouawa na Herode Mkuu aliyependelea Waroma alipopewa utawala wa Yuda na Roma.

Ufalme wa Kiseleucid wa kaskazini uliangushwa na Roma mwaka 67 K.K himaya ya Ptolemi ya Misri ilikoma wakati wa kifo cha Cleopatra mnamo mwaka 30 K.K. Yuda ilipinduliwa na Rumi na kufanywa swehemu ya Himaya ya Rumi mnamo mwaka 63 K.K

Hivyo Yesu alipozaliwa Israeli na nchi za jirani zilikuwa sehemu ya himaya ya Kirumi, Herode Mkuu akiwa Mfalme wa Yuda na Kaisari Augustus kama Mfalme Mkuu wa himaya ya Rumi.

 

MHUTASARI

 

  • Mungu alitabiri kupitia kwa Nabii yeremia kuwa Wayahudi wangebaki Babiloni kwa muda wa miaka 70 (Yer. 25:8-12)

  • Ili kutimiza unabii huu Mungu alimuinua Saras, mfalme wa Ajemi ambaye alitoa amri ya Wayahudi kurudi kwao ili wakajenge hekalu lililoharibiwa (Ezra 1:1-4)

  • Wayahudi walirudi na kujenga hekalu wakitiwa moyo na unabii wa Haggai na Zekaria na halafu kwa kuhamasishwa na Nehemia kujenga kuta za Yerusalemu.

  • Katika muda wote kuanzia mwaka 536 K.K hadi kuzaliwa kwa Yesu Wayahudi nchini walitawaliwa na Wa-mede Ajemi, halafu Wagiriki wakifuatiwa na Seleucid na Ptolemi katika falme za kaskazini na kusini mwa Israeli.

  • Baada uasi wa Makabayo na utawala wao nchi ilipinduliwa na Warumi ambao walikuwa watawala wakati Yesu anazaliwa.

 

Maswali – Somo la 17

 

  1. Wayahudi walikuwa utumwani Babiloni kwa muda gani?

  2. Ni mfalme gani wa Kiajemi aliyetoa amri ambayo ilitimiza Unabii wa Yeremia na Isaya?

  3. Isaya alitabiri nini kuhusu mfalme huyu?

  4. Ni manabii gani wawili waliohamasisha Wayahudi kujenga hekalu Yerusalemu?

  5. Ni taifa gani kubwa kiulimwengu lililokuwa linatawala wakati Yesu anazaliwa?

 

 

Swahili file
Status
Added to Internet
African text
Christadelphian Bible Mission
Translator 1
Raphael Mkeya
Literature type