Exploring the Bible - 20

Swahili

MAISHA NA KAZI YA BWANA WETU YESU KRISTO.

 

Somo la 20 Injili ya Marko

 

Maandishi yafuatayo ni mhutasari wa maisha na kazi ya Bwana wetu Yesu Kristo. Utume wa Yesu ulichukua kipindi cha takribani miaka mitatu na nusu, na unaelezwa kwa kifupi kama ifuatavyo:-

 

Diagram

 

Ili kupata onesho lote la maisha yaye ni lazima kusoma kumbukumbu za Injili za Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Katika muhtasari wa hapo juu Mathayo imetumika ili kuweka vema mtiririko wa matukio yaliyotokea. Injili ya Yohana hasa ni somo la vichwa vya habari, ikijikita zaidi kwenye matukio muhimu kuliko kwenye hatua zote za maisha yake.

 

Baadhi ya mambo muhimu ya maisha ya Yesu yafuata:

 

Kubatizwa kwa Yesu

 

Hatuna kumbukumbu kamili za maisha ya Yesu katika kipindi cha tangu kuzaliwa hadi kubatizwa kwake, akiwa na umri wa miaka 30. Kubatizwa kwake kunatufikishakwenye kazi ya Yohana (angalia Somo la 19, Mathayo 3)

 

Kujaribiwa kwa Yesu:

 

Baada ya kubatizwa Yesu aliongozwa na “Roho” hadi jangwani (Math 4:1) Elewa kwamba siyo “Shetani” aliyemwongoza hadi jangwani ila “Roho”

 

Habari ya Shetani na Ibirisi itazungumzwa kikamilifu katika somo la 24 ambapo maneno Shetani na Ibilisi yanaelezwa. Walakini yafuatayo yatatusaidia kuewlesa tukio lililo mbele yetu.

 

Neno shetani maana yake ni “Mpinzani” Linaweza kutumika kwa maana ya watu wanaopinga njia ya Mungu. Yesu alilitumia kwa maana hii kuhusu Petro alipomwambia “Kaa nyuma yangu, we shetanii, wewe ni chukizo kwangu, kwa sababu hufuati mambo ya Ki-Mungu bali unafuata mambo ya kibinadamu (Mathayo 16:23)

 

Neno hilo pia laweza kutumika kuhusiana na fikra ambazo zinakinga au ni kinyume na nja ya Mungu na linatumika kwa maana hii na Petro wakati Anania na Sapphira walipoamua kuiba fedha kwa ajili yao wenyewe. Hapa tunasoma kuwa Petro alimwambia Anania, “Kwa nini shetani amejaa ndani ya moyo wako hata ukaongopa kwa Roho mtakatifu” ambayo anaeleza katika aya ifuatayo “Kwa nini umetunga jambo hili katika moyo wako? (Matendo 5:3-4).

 

Kwa hiyo tunaona kwamba neno shetani latumika kwa nafsi moja au kwa kundi la watu ambao wananena maneno ambayo yanakingana na njia ya Mungu au kuhusiana na mawazo ya mioyo yetu yaliyojaa udanganyifu ambayo yanaweza kutotoa katika nja yake.

 

Kutokana na jinsi kujaribiwa kwa Yesu kulikoelezwa katika Mathayo, Marko na Luka hatuwezi kufikia ushahidi kamili kuhusu sura ya Shetani. Walakini twaweza kuwa na uhakika wa jinsi isivyo. Dhana ya kawaida ya malaika mwovu asiyekufa na mwenye uwezo usiokuwa na kukinga matakwa ya Mungu haiungwi mkono na Biblia. Tulichokwishajifunza kuhusu Mungu alivyo na tabia yake kinatufanya tusifikirie kwamba kumbe kama hicho kinaweza kuwepo au kuvumiliwa na Mungu (tazama Isaya 45:5,7)

 

Shetani aliyekuja kwa Yesu angeweza kuwa mtu halisi au kikundi cha watu waliomtafuta Yesu jangwani baada ya ubatizo wake. Walikuwa wamesikia habari ya sauti iliyotoka Mbinguni na walikuwa wanataka kupinga wazo la kuwa yeye alikuwa Mwana wa Mungu, wakitaka ishara. Suala hili liliendelea kuwa tata katika utume wake wote. Kuhani Mkuu mwenyewe alipokuwa anasikiliza mashitaka dhidi ya Yesu alidai kwa kiapo kuwa Yesu “Ukiri kuwa wewe ni Mwana wa Mungu” (Math. 26:63) Kwa kweli tangu wakati wa kubatizwa kwake hadi kufa kwake wengi katika Israel walimpinga Yesu. Walikuwa wapinzani au mashetani. Watu hawa hawakukubali kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu (Math. 26:63-66) Hasa kabisa viongozi wa dini walionyesha kuwa walikuwa “shetani” (Zaburi 109:6; Luka 22:3-5) au “Wana wa Ibirisi” (Yohana 8:43-44) siyo tu kwa kumpinga Mwana wa Mungu bali kwa kumuua hatimaye.

 

Ukwweli unabaki, hata hivyo, kwamba Yesu alilazimika kupambana na jaribu rohoni mwake na kuazimia kujibu jaribu kwa kutumia maneno ya Mungu. Mtume Yakobo asema kuwa “Kila mwanaume hujaribiwa anapovuliwa na tama zake mwenyewe (au tama ya asili) na kushawishika (Yakobo 1:14) na Yesu alikuwa mwanaume. Alikuwa na asili ile ile kama sisi ili aweze kushinda nguvu ya dhambi (Waebrania 2:14) Mara tu alipokuwa ameshushiwa Roho Mtakatifu bila kipimo hapo Yesu alipaswa kupambana na jaribu jingine la kuitumia vibaya. Wakati huo alikuwa na nguvu ambazo zingetumika kutuliza njaa au kufanya tendo la kushangaza kama matendo yanayofanywe leo na wale wanaopenda watu wawaone na kusikiliza ujumbe wao au kudhibiti Falme z wat papo kwa papo badala ya kukubali njia ya Msalaba. Majaribu yote haya yalimvuta atende vitendo vya ubinafsi ambavyo ilibidi avipinge.

 

Kama tulivyokwishaona Yesu alikuwa na asili ya ubinadamu kama binadamu wote. Kwa sababu hiyo aliweza kuhusishwa na udhaifu, majaribu na hisia ambazo sisi wote tunazo (Waebrania 2:14-18; 4:15; 5:8) Walakini somo chanya tunalopata kutokana na majaribu yake ni kutenda dhambi kwa kuligeukia neno la Mungu. Kila jibu lilitanguliwa na Neno la Mungu lililokuwa limemkaa barabara moyoni mwake ndilo lililompa ufunguo wa kushinda kila wazo. Kwa hiyo mfuasi wa Yesu angemsema Yesu kuwa “alijaribiwa kwa namna zote hata hivyo hakutenda dhambi” (Waebrania 4:15) Kwa kurejea kwenye Neno la Mungu mara kwa mara alizingatia mafundisho mahsusi ya Yohana Mbatizaji kama yalivyoandikwa katika Isaya 40:6-8.

Tunapata fundisho hili muhimu kutokana na majaribu ya Yesu. Ushindi wake dhidi ya majaribu ulipatikana akilini mwake. Hilo nai kweli hata kwetu sisi vita dhidi ya majaribu inapiganwa na ama tunashindwa au tunashinda, katika akili zetu. Tunapaswa kujitahidi kulifanya kila wazo litii matakwa ya Mungu (2 Wakorintho 10:5)

 

Kuhubiri kwa Yesu kwanza:

 

Kuhubiri wazi wazi hadharani kwa Yesu kulianza hasa baada ya kufungwa kwa Yohana Mbatizaji gerezani (Mathayo 4:12) Hili lilitokea miezi mingi baada ya Ubatizo wake Yesu.

Kauli Mbiu kuu ya fundisho lake umefupishwa katika mafundisho yake ya mlimani (Mt. 5:8) Tunaposoma sura hizi tunaona maajabu ya funzo lake anapoona maajabu ya funzo lak4 anaowaonyesha wafuasi wake jinsi ya kuishi maisha ya ki-Mungu. Mungu ndiye kielelezo na Yesu mwenyewe ndio mfano. Ni katika fundisho hili ndipo Yesu anapoonyesha sura ya Mungu kama “Baba kwa wafuasi wake (linganisha Mat. 5:43-48; 5:8-9; 6:31-33; 7:7-11)

 

Katika fundisho hili, pia Yesu anawapa “Sala ya Bwana” kama kielelezo cha kuwafundisha wafuasi wake jinsi ya kuomba (Mat. 6:9-13)

 

Katika mafundisho yake, yesu anaweka wazi umuhimu wa kiroho na wa kina, wa sheria ya Musa. Hapingi sheria hiyo kama baadhi ya watu wanavyodhani, bali anatenga kanuni zilizomo katika kila agizo au katazo, sheria ilisema “Usiue” (Kutoka 20:13) lakini Yesu anatuonyesha kuwa hasira peke yake ni kosa. Kama tunawapenda jirani yetu hatutaweza kumkasirikia (Mathayo 5:21-22) Hali kadhalika sheria ilikuwa imesema “Usizini” (Kutoka 20:14) lakini Yesu anaonyesha kuwa kile kitendo cha kufikiria wazo la kuzini peke yake hakikubaliki mbeye ya Mungu kwa kuwa kinapingana na sheria (Mathayo 5:27-28). Anaeleza kwa kifupi undani wa sheria na manabii kwa maneno haya: “Chochote unachotaka watu wengine wakutendee na wewe watendee” Mathayo 7:12)

 

Injili ambayo Yesu alihubiri (Marko 1:14-15)

 

Kauli Mbiu kuu ya Ujumbe wa Yesu inaitwa “Injili” Neno hili lina maana ya “Habari Njema” au “Habari za Furaha” Kuna vipengele viwili vikuu katika ujumbe wa Injili kama viivyofupishwa katika Matendo 8:12.

 

  1. Ufalme wa Mungu Yesu alizungumzia Ufalme ambao Mungu alikuwa ameahidi (Luka 8:1 linganisha na Daniel 2:44; Ufunuo 14:15) Aliwaambia wafuasi wake kuuomba kwa sababu ungeleta utawala wake wenye haki na amani (Mathayo 6:10) Pia aliainisha sifa muhimu za Ufalme huu katika mifano yake iliyo mingi (Luka 19:11-27; Mathayo 25:31-34)

  2. Uokovu kutoka kwenye dhambi na mauti kupitia katika Jina la Yesu. Hiki ni kipengele cha pili cha Injili na chenye umuhimu ulio sawa na cha kwanza. Kinamuathiri mtu mwenyewe kwa kuwa kinahusiana na jinsi tunavyoweza kuokolewa kwa njia ya Yesu Kristo.

Kuwa na imani katika vipengele hivi viwili vya Injili inaelekea kwenye tendo la kwanza la utii ambalo ni Ubatizo (Marko 16:15-16; Warumi 5:21; 6:23)

Wanafunzi na Mitume:

Neno Mwanafunzi linatokana na neno la Kigiriki likiwa na maana ya “Mtu anayejifinya kutoka kwa Mwalimu” Yesu alikuwa na wanafunzi wengi, sisi pia twaweza kuwa wanafunzi wake leo kwa kusoma kwa uangalifu, hadithi ya maisha yake na kuishika na kujitahidi kuishi mafundisho yake na kuyafanya mfano wetu.

Neno Mtume” lina maana ya “mtu aliyetumwa” akiwa na ujumbe. Yesu alichagua kutoka miongoni mwa wanafunzi wake, wanaume 12 ambao aliwaita Mitume kwa kuwa aliwatuma wakafanye kazi mahsusi ya kuhubiri Injili. Majina yao na jinsi walivyochaguliwa yameandikwa katika Luka 6:13-16 na Mathayo 10:1-7.

Neno la Kigiriki “Apastello” lilitumika wakati Yesu alipotuma wale kumi na wawili (Mathayo 10:5)

Ufalme wa Mungu na Ufalme wa Mbingu”

Katika maandiko ya Biblia maneno haya mawili yote yanapatikana. Walakini kwa kulinganisha kumbukumbu tunaona kuwa matamko yote mawili yanahusu Ufalme utakaosimikwa hapa duniani Yesu atakaporudi.

Kwa mfano linganisha Mathayo 8:11 na Luka 13:28-29. Katika Luka 13:28 tunasoma kuwa Abraham, Isaka na Yakobo watakuwa katika Ufalme wa Mbingu, na katika Mathayo, katika “Ufalme wa Mbingu”. Ni Ufalme ule ule unaozungumziwa katika sala ya Bwana. Yesu aliposali “Ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama Mbinguni (Mathayo 6:10) Ufalme utakaosimikwa hapa duniani ni Ufalme wa kimbingu kwa sababu ni Ufalme wa Mungu. Wakati wanyenyekevu watakaporithi dunia (Mathayo 5:5) Watafanya hivyo wakiwa na watu kama Abraham, Isaka na Yakobo (Mwanzo 13:14-17 angalia maelezo juu ya ahadi kwa Abraham Somo la 8). Yesu Kristo atarudi karibuni kuja kusimika Ufalme huu (Ufunuo 11:15; Daniel 2:44) na kutawala akiwa Yerusalem kama Mfalme (Math. 5:35, Jeremia 3:17)

Miujiza ya uponyaji aliofanya Yesu.

Miujiza hii ya uponyaji wa magonjwa na hata kufufua wafu ilikuwa na mafundisho ya aina mbili ambayo ni:

  1. Ishara kuwa Mungu alikuwa akifanya kazi kupitia kwake. Miujiza ya ajabu aliyofanya ilitoa ushahidi kwamba Mungu nduye aliyemtuma na kuwa yeye ndiye Masihi (yaani, “Kristo) ambaye alitabiriwa na manabii – Neno la Kiebrabnia Messiah na neno la Kigiriki Christ yana maana ya “Mpakwa mafuta”. Yesu alikuwa amepakwa mafuta wakati wa kubatizwa na Roho Mtakatifu ili aweze kufanya miujiza hii anapofundisha Injili (Isaya 61:1; linganisha na Mathayo 11:4-6; Luka 4:16-21 pia Isaya 42:1-3, 7 linganish na Mathayo 12:17-21) Kazi hizi zilikuwa ishara kwamba alitumwa na Mungu (Yohana 5:36; 10:25; Matendo 2:22)

  2. Ishara kwamba dhambi na mauti vinaweza kuondolewa kupitia kwake. Ugonjwa, maradhi na mauti vilimfikia mwanadamu kwa sababu ya dhambi ya Adam na Eva. Watu wote hatimaye hufa na kurudi mavumbini. Somo la Miujiza ya Yesu linaelezwa kwa kifupi na kwa kupendeza katika Mathayo 8:16-17 Fungu ambalo menukuliwa kutoka Isaya 53:4. Yesu alikuwa na huruma kwa wale waliokuwa na maumivu kwa kuwa yeye pia “alipaswa na hisia za udhaifu wetu “(Waebrania 4:15). Kuponya kwake magonjwa na mauti kwa nguvu ya Mungu ilikuwa ishara ya kwamba alitumwa kumkomboa mwanadamu kutoka kwenye chanzo cha tatizo lake ambacho ni dhambi. Zingatia uponyaji wa mtu aliyekuwa amepooza (Mathayo 9:1-8, Zaburi 103:3)

Kwa sababu ya maisha safi ya Yesu na utiifu mkamilifu kwa Mungu hadi kufa (1 Petro 2:22-24;Wafilippi 2:8), Mungu alimrudishia uhai wake awe Mkombozi wa watu wote (2 Timoteo 1:9-10; Warumi 5:10) Kupitia kwake sisi pia tuna tumaini la ufufuko kutka kaburini na tunaweza kuopolewa kutoka kwenye mauti na ufisadi (1 Wakorintho 15:20-23, 50-58) Miujiza ya uponyaji ilitufundisha somo hilo zuri ajabu.

Mafumbo ya Yesu

Mara nying Yesu alizungumza kwa mafumbo. Kwa nini alifanya hivyo? Sababu imetolewa katika maelezo yake ya Fumbo la Mpanzi (Mathayo 13:10-16). Fumbo ni hadithi mara nyingi ya mambo ya kila siku lakini ikiwa na maana ya kina kuhusu mambo ya Kiroho ambayo inabidi ichotwe kutoka katika maelezo yasiyo magumu. Yesu alizungumza kwa mafumbo ili kutenga wanafunzi wa kweli na wale waliomfuata kwa sababu ya miujiza aliyokuwa akifanya. Manabii walitabiri kuwa Yesu angeumia njia hii ya kufundishia (Isaya 6:9-10) linganisha na Mathayo 13:10-17; Zab. 78:2 linganisha na Mathayo 13:34-35)

Fumbo la Mpanzi (Mathyo 13:1-23)

Hadithi ni rahisi na inaeleweka lakini funzo la kiroho ni muhimu sana. Mbegu iliyopandwa ni “Neno la Mungu” (aya ya 19) watu wamo katika makundi manne:-

  1. Ardhi ngumu kando ya njia

  2. Ardhi yenye miamba (mawe)

  3. Ardhi yenye miba

  4. Ardhi nzuri yenye rutuba

Aina hizi nne za ardhi zinawakilisha aina nne za matokeo ya wasikilizaji wa Injili. Fundisho la fumbo hili ni lenye nguvu na ncha kali. Ni ukweli ulioje kwamba kama miiba na mbigili zinavyosonga mbegu inayokuwa ndivyo utajiri na wasiwasi wa maisha vinavyoweza kusonga mvuto wa neno la Mungu ambao mtu anaweza kuwa nao. Ni ardhi nzuri tu ndiyo yenye matokeo mazuri yenye kuzaa matunda. Tunahitaji kukabiri kwa makini usomaji wa neno la Mungu (Mbegu, katika fumbo la Mpanzi) na kuliruhusu likuwe katika udongo bora wa akili zetu ili maisha yetu yaboreshwe na tuzae matunda kwa utukufu wa Mungu.

Mtu wa Ukoo wa Kifalme aenda nchi ya Mbli (Luka 19:11-27)

Kwa mara nyingine hadithi ni rahisi ukiiangalia ki-juu juu, lakini funzo ni muhimu sana. Yesu alisimulia fumbo hili kwa sababu wanafunzi walitegemea Ufalme uwekwe wakati ule ule. Hawakuelewa kuwa ni lazima kwanza Yesu asulibiwe na kufufuliwa na kwenda kwa Baba yake Mbinguni kwa muda mrefu kabla hajarudi kusimika Ufalme duniani. Fumbo hili lilitolewa ili wanafunzi wake waweze kuelewa hivyo. Funzo kwetu katika fumbo hilo ni kuwa Yesu Kristo Bwana atarudi karibuni hapa duniani lakini kabla hajarudi tunahitaji kutoka jasho katika utumishi wake kama watumishi waaminifu. Tukifuata mfano huu basi, sisi pia tutapokea ridhaa yake. Sasa wewe mtumishi mwema kwa sababu umekuwa mwaminifu katika madogo, unapewa mamlaka juu ya miji kumi (aya ya 17).

Tunaposoma mafumbo ya Yesu tunahitaji kutafuta mafunzo ya Kiroho na kuwa makini kwa yale yanayofundishwa ili tuweze kuhesabiwa miongoni mwa wanafunzi wake wa kweli.

Wanafunzi na Mitume:

Neno mwanafunzi linatokana na neno la Kigiriki likiwa na maana ya “Mtu anayejifunza kutoka kwa Mwalimu” Yesu alikuwa na wanafunzi wengi. Sisi pia twaweza kuwa wanafunzi wake leo kwa kusoma kwa uangalifu hadithi ya maisha yake na kuishika na kujitahidi kuishi mafundisho yake na kuyafanya mfano wetu.

 

 

 

 

 

MUHTASARI

  • Utumishi wa Yesu hadharani ulichukuwa muda wa miaka mitatu na nusu tangu kubatizwa kwake na Yohana Mbatizaji hadi kusulibiwa kwake.

  • Kujaribiwa kwa yesu kulionyesha kuwa alijaribiwa kama wanaume wengine wote kukiwa na tofauti hii muhimu kwamba hakutenda dhambi (Waebrania 4:15; 1 Petro 2:22) Alishinda kila kishawishi kwa kusema “Imeandikwa” (Mathayo 4:4, 7, 10) akituonyesha kwa mfano wake kuwa njia ya kushinda kishawishi tunapojaribiwa ni kufuata mafundisho ya Neno la Mungu.

  • Ujumbe ambao Yesu alitufundisha unaitwa “Injili” Neno linalomaanisha “Habari Njema” au “Habari za Furaha” Hii habari Njema inajumuisha vipengele viwili vikuu kama ilivyoandikwa katika Matendo 8:12

  1. Mambo yahusuyo Ufalme wa Mungu utakaoanzishwa Yesu arudipo duniani

  2. Mambo yahusuyo Jina la Yesu Kirsto ambayo yanaonyesha kuwa Mungu ametujalia ukombozi katika mauti na msamaha wa dhambi kwa njia ya Jina la Yesu Kristo.

  1. Miujiza ambayo Yesu alifanya ilikuwa ishara kwamba alitumwa na Mungu (Yohana 5:36; 10:25)

  2. Mafumbo ambayo Yesu alitumia katika mafundisho yake yalikusudiwa kuwafanya watu wafikirie kwa undani ujumbe wake na kutumia mafunzo hayo katika maisha yao (Mathayo 13:10-17) Mafumbo yaliyo mengi yalihusu Ufalme ujao wa Mungu kwa mfano wa Mtu wa Ukoo wa Kifalme kwenda nchi ya mbali (Luka 19:11-27)

 

MASWALI:

  1. Yesu aliwezaje kuhusianishwa na majaribu na hisia ambazo sisi sote tunazo?

  2. Neno Injili lina maana gani?

  3. Ni vipi vipengele viwili vikuu vya Injili?

  4. Neno Mwanafunzi lina maana gani?

  5. Yesu alipakwa nini na kwa nini?

  6. Tunajifunza nini kutokana na uwezo wa Yesu wa kuponya magonjwa na kufufua wafu?

  7. Tunajifunza nini kutokana na fumbo la Mwana wa Kiflme kwenda nchi ya mbali?

 

Swahili Title
MAISHA NA KAZI YA BWANA WETU YESU KRISTO.
Swahili file
Status
Added to Internet
African text
Christadelphian Bible Mission
Translator 1
Raphael Mkeya
Literature type