Exploring the Bible - 10

Swahili

IBRAHIMU – BABA WA MATAIFA MENGI

SOMO LA 10 MWANZO 16-19

 

Ibrahim apata mwana Ishmael (Mw. 16)

Mungu alikuwa amemwambia Ibrahim kuwa “yule atakayetoka katika utumbo wako wewe mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako” (mwanzo 15:4). Ibrahim aliamini neno hili bila shaka yoyote kama tulivyoisha ona na imani hii ndiyo kwayo alihesabiwa haki (mwanzo 15:6) lakini Sarai alikuwa tasa na alitambua kuwa kibinadamu ilikuwa haiwezekani tena kwake kupata mtoto. Na bado Mungu alikuwa ameahidi kumpa nchi mzao wa Ibrahim.

Huzuni na masikitiko ya kuwa tasa mwishowe yalisababisha atafute ufumbuzi wa tatizo hili. Aliamua kumpa Ibrahim Hagar mjakazi wake Mmisri ili amzalie mwana. Hili aliona kuwa lingemkwaza na pia lingempatia Ibrahim mrithi “wa utumbo wake”. Hata hivyo badala ya kuleta furaha kwa Sarai lilimletea huzuni na uchungu kwa sababu Hagar aliposhika mamba alianza kumdharau Sarai (aya ya 5-6). Sarai alimtendea hagar kwa ukali ikabidi Hagar akimbilie porini (aya ya 6).

Hagar alipokuwa katika hali ya mahangaiko malaika wa Mungu alimtokea na kumwambia arudi kwa Sarai na kumnyenyekea (aya ya 9). Malaika alimliwaza kwa kumfunulia kuwa Mungu angezidisha sana uzao wake (aya ya 10) angepata motto ambaye angeitwa Ishmael maana yake “Mungu atasikia” kwa sababu malaika alisema “Mungu amesikia taabu yako” (aya ya 11). Kwa kutii agizo la malaika Hagar alirudi kwa Ibrahim na Sarai na baada ya muda si mrefu alimzaa motto wa kiume ambaye Ibrahim alimwita Ishmael (aya ya 15).

Mungu alimuahidi Ibrahim kuwa angembariki Ishmail na kumfanya awe taifa kubwa (17:20) lakini pia kwamba mzao alioahidiwa ungekuwa umetokana na Ibrahim na Sarai (17:21) Ishmael alikuja kuwa baba wa Waarabu. Wanawake kumi na wawili ambao walikuwa wakuu wa makabila kumi na mawili ya Waarabu (Isaiah 60:6-7) wametajwa katika mwanzo 25:12-16. Hatimaye Waarabu watabarikiwa pia katika utawala wa Kristu katika Ufalme wa Mungu.

 

Jina lako litakuwa Ibrahimu (badala ya Abram) mwanzo 17:1-8

Miaka mingine 13 ilipita, Ibrahim akatimiza miaka 99 Bwana alipomtokea tena. Safari hii Mungu alirudia tena lile agano alilokuwa amefanya naye awali (mwanzo 15:18) akizungumzia mambo ya mbele zaidi, Mungu alimwambia “Nitakuzidisha sana na hivyo utakuwa baba wa mataifa mengi.” (aya ya 4) kwa sababu utimilifu wa agano hili ungejumuisha umati mkubwa Mungu alisema; wala jina lako halitakuwa Abram ila jina lako litakuwa Abraham kwa kuwa nimekufanya uwe baba wa mataifa mengi (aya ya 5). Jina Abram lina maana ya baba mrefu au wa juu ambapo Abraham lina maana ya baba wa mataifa mengi.Mabadiliko ya jina lake yalikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na ahadi pamoja na agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahim. Tuliona hili likielezwa katika sehemu zifuatazo ndani ya Agano Jipya:

Wagalatia 3:7-8

 

 

 

 

Mjuwe kwa hiyo kwamba wale ambao wana imani ni wana wa Ibrahim”

Yeyote yule (Myahudi au mtu wa mataifa) ambaye imani yake ni sawa nay a Ibrahim anaonwa na Mungu kama mmojawapo katika familia ya Ibrahim. Famila ya Ibrahim misingi yake ni imani na siyo nasaba ya kimwili kwa sababu ni familia ya kiroho.

 

Maandiko, kwa kubashiri kuwa Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani”

Baraka ya kuhesabiwa haki kama Ibrahim alivyohesabiwa haki (mwanzo 15:6 angalia somo la 9) inatolewa kwa watu wote ambao wanaonyesha imani ile ile kama Ibrahim kwa Mungu. Watu wa mataifa na Wayahudi wanaweza kushiriki katika baraka hii kwa kigezo kile kile (Wagalatia 3:27-29)

 

Alimhubiria Ibrahim kabla ya Injili akisema katika wewe mataifa yote yatabarikiwa”

Sentensi hii inajumuisha nukuu iliyomo katika kitabu cha mwanzo 12:3. Neno “Injili” lina maana ya “habari njema” Ni habari njema kwa watu wote, Wayahudi na wa mataifa sawia. Yesu Kristo ameifanya baraka hiyo ipatikane kwa watu wote. Ndiyo maana “mataifa yote” wanaweza kushiriki tumaini la uadilifu kwa njia ya imani na kupata suluhu na Mungu kwa njia ya ubatizo katika Yesu Kristo. Kumbuka kwamba hili linatufanya tuwe warithi wa ahadi zilizotolewa kwa Ibrahim na uzao wake (Wagalatia 3:16, 27-29)

 

Warumi 4:16-17

Katika sura hii ambayo tuliiweka maanani wakati tunasoma mwanzo 15:6 tunakuta mwanzo 17:15 iliyonukuliwa na Paulo.

“Kwa hiyo ni kwa imani ili iweze kuwa kwa njia ya rehema; hadi mwisho ahadi ingeweza kuwa ya uhakika kwa uzao wote; siyo kwa wale washikao sheria (Wayahudi) tu bali pia kwa wale wenye imani kama ya Ibrahim (Myahudi na mtu wa mataifa) ambaye ni baba yetu sote (Myahudi na mtu wa mataifa).

Ahadi aliyopewa Ibrahim haikuwa kwa Wayahudi peke yao bali ilkuwa kwa watu wote kwa kanuni ya imani. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahim ilifanywa miaka 430 kabla Israel haijapewa sheria kupitia kwa Musa (Wagalatia 3:17-18) sheria ambayo iliwahusu Wayahudi peke yao haikufuta ile ahadi kwa sababu ilfikia mwisho wake wakati Yesu alipokufa lakini ahadi bado haijatimizwa na ni lazima itimizwa “(Kama ilivyoandikwa nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi)”.

Kwa kunukuu mwanzo 17:5 Paulo anasisitiza tu jinsi ahadi inavyowahusu watu wote. Kwa badiliko hili la jina kutoka Abram hadi Abraham hakuna Myahudi anayeweza kudai kuwa yeye ni wa uzao wa Abraham. Badiliko la jina linaonyesha wazi watu wa mataifa yote wanaweza kushirikishwa katika baraka ya ahadi iliyomo ndani ya Injili.

 

Warumi 9:6-9

Hapa Paulo anaonyesha pia kwamba kuwa mzao wa Ibrahimu pele yake hakumfanyi mtu apendeke mbele ya Mungu.

Kwa kuwa Israeli siyo wote ambao ni wa Israeli”

 

Kwa kuwa mtu wa ukoo wa Ibrahim peke yake hakutoshi kuwa mzao wa Ibrahimu. Mtu hana budi kuwa na uhusiano tofauti na Ibrahim siyo tu ule wa kimwili.

Utakaoitwa uzao wako utatokana na Isaka.

Ibrahim alikuwa na watoto kadhaa wa kiume pamoja na Ishmael na wale walioorodheshwa katika mwanzo 25:1-6. Hata hivyo Mungu alipomuahidi Ibrahim alisema wazi “Utakaoitwa uzao wako utatokana na Isaka” (mwanzo 21:12) Mungu alikuwa amechagua.

Hawa si watoto wa Mungu; bali watoto wa ahadi wanahesabiwa katika uzao”

Ili tuitwe “watoto wa Mungu” ni lazima tuwe tunahusiana na ahadi ya Mungu. Tunajifananisha na ahadi kwa njia ya imani inayodhihirishwa na ubatizo katika Kristo (Wagalatia 3:26-29)

Tutakapoelewa sababu ya badiliko la jina la Abram kuwa Abraham tutaweza kuona jinsi ahadi itakavyoshirikisha “mataifa mengi”

Tunaporudi kwenye mwanzo 17:7-8 tunaona kwamba Mungu anatuhakikishia kwamba Agano lake ni “Agano la milele”. Mungu wa milele anapotangaza kuwa agano lake ni la milele, tunaweza kuwa na uhakika kuwa litatimizwa.

 

Tohara-Ishara ya agano (mwanzo 17:9-14)

Mungu, kwa kutaka kuweka kumbukumbu ya kudumu kwa uzao wa Ibrahim kwamba agano hili lilifanywa na Ibrahim alianzisha alama au ishara ya kuwakumbusha juu ya hili agano tukufu na la tumaini. Tohara ndiyo ingekuwa “alama ya agano kati yangu na wewe” (aya ya 11) “kila motto wa kiume katika kizazi chako , yule aliyezaliwa nyumbani mwako au aliyenunuliwa kwa fedha ya mgeni yeyote” alitakiwa atahiriwe (aya ya 12). Tohara ilikuwa ishara ya agano kwa kizazi halisi cha Ibrahim pamoja na wageni waliojiunga na familia yake. Ilikuwa ukumbusho bayana kwamba ahadi ya Mungu isingetimizwa na nguvu yoyote ya kimwili ya mtu ila kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

 

Tohara ishara ya ubatizo.

Paulo aonyesha kuwa tohara ililenga kwenye ubatizo katika Yesu Kristo (Wakolosai 2:11-13). Tunakumbuka kuwa kupitia ubatizo katika Kristo mtu anakuwa mrithi wa ahadi aliyopewa Ibrahim (Wagalatia 3:27-29) ubatizo sasa ni badala ya tohara. Kama tulivyokwishaonyesha tohara ilikuwa ukumbusho kwamba tama za mtu za kimwili lazima ziachwe. Katika ubatizo pia tunadhihirisha kuwa tunaweka pembeni mambo yanayohusiana na mwili (Wakolosai 2:11-13; Wagalatia 5:16-25)

 

JINA LA SARAI LABADILISHWA KUWA SARAH (mwanzo 17:15-16)

Siyo jina la Abram tu lililobadilishwa kuwa Abraham ili kuzingatia wazo la ile ahadi kuu ambayo Mungu alikuwa amempa bali hata Sarai jina lake lilibadilishwa na kuwa Sarah ambalo maana yake ni “binti mfalme” na hivyo kupandisha hadhi yake, kwa kuwa alikuwa awe mama wa mataifa mengi ambayo Ibrahim alikuwa awe baba yao.

 

Malaika wamtembelea Ibrahim na Sarah (mwanzo 18)

Sura hii inasimulia ziara ya wajumbe watatu wa Mungu. Angalia, japo wanaume watatu (aya ya 2) walimtembelea Ibrahim, ni muda mfupi tu baadaye ilipodhihirika kuwa walikuwa malaika (mwanzo 19:1, pia 18:17). Tunaweza kuhisi hali ya furaha iliyotawala nyumbani kwao jinsi Ibrahim na Sarah walivyokuwa wanawakirimu wageni wao. Kuna somo hapa kwa wale wote ambao wangependa kufuata mfano wao (Waeb. 13:2)

Malaika hawa wanarudia mbele ya Ibrahim ujumbe kwamba yeye na Sarah wangepata mtoto wa kiume. “Sarah alicheka rohoni mwake akijisemea baada ya kuzeeka kiasi hiki, nitapata raha kweli na Bwana wangu akiwa mzee pia” (aya ya 12). Kwake ilionekana haiwezekani, na kibinadamu kweli haiwezekani (aya ya 11)

Petro akirejea kwenye kisa hiki anatuonyesha kuwa Sarah alimwita Ibrahim “Bwana wake” na kutaka tujue kwamba “mabinti halisi” wa sarah nao pia watawatambua waume zao waaminifu, kama bwana zao, wakijiweka chini yao (1 Petro 3:5-7). Fundisho hili lilitoka kwa Mungu linadhihakiwa na jamii siku hizi. Hii inachangiwa na ukweli kwamba ubwana ambao waume wanatakiwa kuuonyesha haueleweki. Siyo uonevu wa wanaume bali ni uangalizi na ulinzi wa kiupendo na huduma kwa mke kwa mfano uliodhihirishwa na Bwana yesu Kristo kwa wafuasi wake (Marko 10:42-45; Yohana 13:13-15; Waefeso 5:22-29).

Ingawa Sarah kwa wakati huo alikuwa na shaka malaika alimjibu akasema “kuna jambo lolote gumu mno kwa Bwana?” (aya ya 14). Muda ulipofika kulingana na neno la Mungu mwana alizaliwa kwa Abraham na Sarah, ambaye Abraham alimwita Isaka (mwanzo 21:1-7). Paulo anafasiri kwamba “kwa njia ya imani Sarah alipokea nguvu ya kushika mamba na akazaa mototo wakati umri wa kuzaa ulipokuwa umepita (Waebrania 11:11-12).

 

Kuteketezwa kwa sodoma (mwanzo 19)

Baada ya kufikisha ujumbe wa kufurahisha kwa Abraham na Sarah, wawili kati ya wale wajumbe watatu, waliendelea na safari yao kuelekea sodoma (aya ya 22; 19:1). Mmoja alibaki nyuma ili amuonyeshe Abraham kuhusu hukumu ya Mungu iliyokuwa inakuja juu ya Sodoma na Gomorrah. Abraham alifadhaika kuhusu Loti na familia yake na kuomba kwamba Mungu awanusuru wale ambao ni waadilifu “Je utaangamiza wenye haki na wasiyokuwa na haki?” (aya ya 23). Malaika alikubali kwamba kama kuna wenye haki kumi katika mji basi hatauteketeza (aya ya 23-33).

Wale malaika wawili walipofika Sodoma Loti aliwashawishi kukaa na kupumzika nyumbani kwake. Tunaposoma habari za mambo yaliyokuwa yanatendeka usiku tunagundua uovu mkubwa kabisa wa mji ule (aya ya 4-11) na kuelewa kwa nini hukumu ya Mungu ilikuwa inataka kumwagwa juu ya wakazi wake. Malaika walimwonya Loti aondoe familia yake katika mji ule mara moja. Loti aliwabembeleza watu wa familia yake lakini hawakusikiliza (aya ya 12-14).

Asubuhi ilipofika malaika waliwasihi Loti, mke wake na mabinti wake wawili waukimbie mji bila kugeuka nyuma, “halafu Bwana akashusha moto juu ya Sodoma na Gomorrah kutoka kwake mbinguni” (aya ya 24). Mke wa Loti aligeuka kwa kuwa moyo wake ulikuwa bado unawakumbuka watu wa mji ule mwovu. Na hivyo naye akanaswa katika msiba wao na kuwa mnara wa chumvi, (aya ya 26) uharibifu wa miji hiyo ulikuwa mkamilifu. Inaaminka uharibifu wa maumbile ya ardhi ulisababisha kuwepo bonde kubwa ambalo sasa ni bahari iliyokufa na mazingira yake yasiyokuwa na rutuba, na kwamba Sodoma na Gomorrah iko chini ya bahari hiyo upande wa kusini wa bahari.

 

 

 

Mafundisho yatokanayo na kuteketezwa kwa Sodoma.

Mafundisho yatokanayo na kuteketzwa kwa kile kizazi kibovu yamegusiwa mahali pengi katika Biblia.

  • Yesu Kristo alisema kuwa utovu wa maadili uliotapakaa kila mahali kama ule wa Sodoma ungekuwa mojawapo ya ishara zinazoonyesha kuwa kurudi kwake kumekaribia (Luka 17:28-32). Ni kwa usahihi namna gain haya maneno yanatimizwa mbele yetu siku hizi, serikali nyingi zikihalalisha upotofu namna hii. Alituasa tukumbuke mke wa Loti na kutoruhusu mioyo yetu kunaswa katika mambo ya dunia hii ovu.

  • Mtume Petro alitumia mfano wa hukumu ya Mungu juu ya Sodoma kama uthibitisho kwamba uovu kama huo hauwezi kupita bila wahusika kuadhibiwa(2 Petro 2:6-9; Yuda 7)

  • Nabii Ezekieli katika kuwakemea watu wake alifananisha hali ya uovu iliyokuwa imejengeka katika Israel na tabia chafu ya Sodoma. Anaorodhesha dhambi za Sodoma (Ezekiel 16:49-50)

 

Maswali – Somo la 10

  • Mtoto wa kiume aliyezaliwa kwa Abraham na Hagar aliiywa nani?

  • Kwa nini Mungu alibadilisha jina la Abram na kumwita Abraham?

  • Injili ilihubiriwa kwa Abraham kwa maneno haya “katika wewe mataifa yote yatabarikiwa (Wagalatia 3:8) Tunajifunza nini kutokana na hili?

  • Tunawezaje kuwa miongoni mwa uzao wa Abraham.

  • Tohara ilikuwa ishara ya Agano ambalo Mungu alifanya na Abraham. Tohara ililenga jambo gain kwa waumini leo hii?

  • Uovu wa Sodoma ulileta uharibifu kwenye mji huo, Yesu alifundisha nini kutokana na tukio hili?

 

 

 

 

Swahili Title
IBRAHIMU
Swahili file
Status
Added to Internet
African text
Christadelphian Bible Mission
Translator 1
Raphael Mkeya
Literature type