Revelation Chapter Two

Swahili

_____________________

 

UFUNUO MLANGO WA PILI - MAELEZO YA MANENO YA MSTARI KWA MSTARI

Revelation Chapter Two - Verse by Verse

_____________________

UFUNUO MLANGO WA PILI.

NYARAKA ZA KRISTO KWA MA-EKLEZIA.

Ujumbe huu ni wa kuvutia mno zaidi kuliko ilivyodhaniwa kuwa mara ya kwanza. Nafasi zinazoshughulikia ni za kuleta fikra sana moyoni, Kwanza zinakuja kwa kuonyesha mambo ambayo yalikuja tokea karibuni kati ya mataifa ya dunia. Kabla Kristo hajaendelea kuweka wazi mambo haya, anatoa hotuba yeye mwenyewe kwa ndugu zake, kwa kupitia mmoja wao aliyehamishiwa kifungoni kwenye kile kisiwa cha Patmo. Hakuna kinachoweza kuwa na maana zaidi kwa nafasi ya marafiki wa Kristo kushughulika na kusimulia mwenyewe na madhumuni ambayo yeye ni kitovu, Tunaletewa kwa nguvu nyingi sana hapa ukweli uliotangazwa na Paulo, "Maana mambo yote ni kwa ajili yenu" - (2 Wakorintho 4:15).

Utendaji halisi wa mataifa kila mahali - biashara zao, mapinduzi yao ya kisiasa, mageuzi yao katika jamii - ni mambo yote mengi ya mwanzo ya kuifanya dunia kuhama na kufika kwenye serikali ya Yesu na miongoni mwa wale wanadamu anaowastahi kwa kukubali kwake na kuchagua kuwa ndugu katika siku ya kufika katika utukufu wake. Wakati ule ule watapatikana miongoni mwa masikini na wenye kuonewa kama wale wa kwanza. Ni wale wanaouamini ushuhuda wa Mungu, na ambao daima hutii amri zake, au kama mfano wa maelezo ya ufunuo "wale wanaoshika amri za Mungu, na wana ushuhuda wa Yesu Kristo."

WARAKA KWA EKLEZIA LA EPESO - MLANGO WA PILI MISTARI 1-7.

MSTARI WA KWANZA.

"Yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu"

Somo la huu mstari ni lenye nguvu kwa mtazamo wa tafsiri ya kuwa "vinara vya taa saba ni ma-eklezia saba". Kristo anatembea ndani katikati ya vinara hivi maana yake ni kwamba mambo yote kati ya ndugu zake yapo wazi katika fahamu zake na machoni pake kama yalivyo kwa kila eklezia kwa wale wanaounda eklezia hilo. Maana yake ni zaidi ya hivi. Inamaanisha kwamba sio tu anao uweza wa kuona, bali pia nguvu za kuongoza, na kumgeuza kila mmoja kwa namna apendavyo.

MSTARI WA PILI.

"Nayajua matendo yako"

Ukweli huu unafuata kutoka kwenye masimulizi ya Kristo kuhusu vinara saba. Hi ukweli wenye faraja kwa kila mtu anayejitahidi kuenenda inavyokubalika mbele za Mungu, na labda kukosekana kuweka mpaka kwa watu, Inaweza kuonekana kwa upande wetu kwamba mambo yetu hayajulikani na hayasikiki. Muda unakwenda na hakuna kinachokuja, nasi twaweza kuwa "wachovu na kuzimia mioyoni mwetu".

Labda walikuwepo watu wengine pale Efeso ambao walijiona namna hii. Walikuwa na miaka arobaini au hamsini katika eklezia kabla ya kupokea onyesho hili la nia ya Bwana kuhusu wao. Bwana anaonya na hivyo kusema, kuandika habari kunaeadelea kutoka siku hata siku. Atakapokuja atatujulisha aonavyo, na kutupa matokeo kwa namna ya uhakika kabisa.

"Huwezi kuchukuliana na watu wabaya"

Hili ni jibu lililo bora kwa wale wanaotulaumu kwa kutokuwa na huruma kwa habari ya uadui uliopo kati yetu kwa kile kinachopingana na mapenzi yaliyofunuliwa ya Kristo, na kwa kuwa kutumia kipimo chetu katika kuupima ukweli kwa waalimu wa leo juu ya uongozi au ufuasi wa mitume. Ikiwa mwenendo huu wa Waefeso kwa mambo haya ulipata sifa ya Kristo, nasi mwenendo wetu uwe hivyo ikiwa tunataka haki idumishwe. Na kama tukijipatia sifa ya Kristo haidhuru ikiwa ulimwengu wote unatuhukumu.

"Mitume wa uongo"

Inaonekana kwamba walikuwepo watu wengine pale Korintho waliojiinua jua ya Paulo wao wenyewe, wakimuhabiri "Yesu mwingine", na kufundisha injili nyingine, kuliko ukweli. Paulo anawaita watu hawa "manabii wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo" (2 Kor. 11:13). Hata katika kipindi cha Paulo walikuwepo mitume wa uongo pale Efeso; hii ndiyo sababu Paulo alimtaka Timotheo "abaki Efeso ... ili awakataze watu wengine wasifundishe elimu nyingine", wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili; wapenda kuwa waalimu wa sheria; ingawa hawayafahamu wayasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti" (1 Timotheo 1:3,6-7). Sifa ya Kristo inaonyesha kwamba eklezia la Efeso kwa uaminifu walilipokea onyo, nao walikataa mafundisho ya wale waliodai kuwa ni "mitume nao sio".

MSTARI WA NNE.

"Umeuacha upendo wako wa kwanza"

Yatupasa kufahamu katika mwangaza wa ufafanuzi wa Maandiko kuhusu upendo, na sio kufuatana na wazo la siku hizi linalouwekea mpaka upendo wa kuvutwa ili kupenda. Inamaana ya zaidi kuliko shauku. "Na huu ndiyo upendo, kwamba tuenende kufuatana na amri zake" (2 Yohana 1:6). Vile vile Yesu anasema, "Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, huyo ndiye anipendaye." (Yohana 14:21). Kwa sababu hiyo, kurudi kwenye upendo wa kwanza ni kurudi kwenye matendo ya kwanza. Hii ndiyo tafsiri anayoitoa Yesu kuhusu huo upendo katika ujumbe, "tubuni na mfanye matendo yale ya kwanza". Kristo anataka uendeleo - kwa saburi katika kuendelea kutenda mema (Warumi 2:7).

MSTARI WA TANO.

"Nitakiondoa kinara chako"

Ikiwa kinara cha taa ni eklezia, basi hii ni sawa aa kusema kwamba atalivunja eklezia ikiwa ndugu hawakuwa wasikivu kwa bidii kwenye matakwa yake. Hili ni onyesho lingine la uongozi wa Kristo kwa busara; maana ni kwa njia gani angekiondoa kinara cha taa? Sio kwa kuwajia wazi bali kwa tendo la kuvunjika linalotokana na hali ya mambo isiyofaa ikirekebishwa ua yeye.

MSTARI WA SITA.

"Wanikolai”

Neno "Wanikolai" linatokana na muungano wa maneno mawili ya Kiyunani (Kigriki): "Niko" - kushinda, kufaulu na "Laitos" - watu. Kwa hiyo jina linamaanisha wale "wanaowashinda watu". Daktari Thomas anathibitisha ya kuwa Wanikolai ni wakoseshaji wa watu walioingiza elimu ya watu wa mataifa ndani ya ma-eklezia. Maarifa wanayoyaita yao yalitolewa kwa Plato, nao wakaingiza ile imani ya asili ya kutokufa nafsi (roho). Mafundisho ya ufufuo yalikuwa ni kuzuia mambo yaliyofundishwa kama haya, lakini hawa wakoseshaji watu walikuwa pande zote kwa kufundisha kwamba huo ufufuo tayari ulikuwa umeisha pita. Paulo anataja kabisa jambo hili moja kwa moja kuhusu hali hii kwa kijana Timotheo - "Na neno lao litaenea kama donda ndugu, na miongoni mwao wamo Himenayo na Fileto; waliikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha" (2 Timotheo 2:17-18).

ASILI YA MTU.

 

  1. Mtu ni kiumbe aliyetokana na mavumbi naye anakuwa hai kwa nguvu za uzima wa Mungu (roho na pumzi ya Mungu). akiwa shirika moja na viumbe hai vingine. Mwa. 2:7; Ayubu 33:4-6; 27:3; 10:9; Zaburi 104:29.30.

  2. Nguvu za uzima wa Mungu zikiondolewa, mtu, kama wanyama anarudi mavumbini. Ayubu 34:14,15; Muhubiri 3:18-21; 12:7.

  3. Hivyo, uhai unaomilikiwa kwa sasa sio wa milele, bali ni kama mvuke unaopita mara. Yakobo 4:14; Ayubu 14:1,2; Zaburi 39.

  4. Hali ya mauti

    1. Mtu hawi na fahamu, hajui lolote kana kwamba hakuwahi kuishi Muhubiri 9:5,6.10; Zaburi 6:4-5; 146:3,4; Isaya 38:18,19.

    2. Mwili wake huoza. Zaburi 49:9,14; 30:9; 88:10-12; Yohana 11:39.

  5. Mungu amewahukumu watu wote kifo kwa kuwa wametwaa asili ya Adamu, na kutembea katika njia zake za dhambi. Mwa. 3:17-19; Warumi 5:12-21; 6:23; 1 Wakorintho 15:22,55,56.

  6. Mtu hana uzima wa milele. Ikiwa mtu atasemwa kuwa anao uzima wa milele basi vipingamizi vinajitokeza:

    1. Watu wasingeangamia kama wanyama. Zaburi 49:14,19-20.

    2. Uzima wa milele usingekuwa kipawa kwa wenye haki. Warumi 2:6-8.

    3. Uzima wa milele usingekuwa ni kipawa cha Mungu. Warumi 6:23

    4. Wala kutokufa sasa kumefichwa na Kristo katika Mungu. Kol. 3:3.

    5. Kutoharibika kusingesemwa kumeletwa na Yesu kwa kuufunua uzima kwa ile injili. 2 Timotheo 1:10.

    6. Kutokufa kusingetegemea juu ya kumwamini Yesu Kristo. Yoh. 6:40; 11:25; 3:16.36.

    7. Ufufuo usingehitajika 1 Wakorintho 15:16-18.

    8. Paulo asingesubiri kwa hamu "ukombozi wa mwili" Warumi 8:23.

MSTARI WA SABA.

"Yeye aliye na sikio"

Maneno haya yamerudiwa mara saba, yanatupa tufahamu kwamba kile kilichosemwa kwa eklezia maalum katika waraka wao hakijawekewa mpaka kwa eklezia mahusasi lililo ambiwa, bali kinahusu ma-eklezia yote ambayo hali yao kiroho kwa hatua fulani ya ukengeufu ilionyeshwa kwa kupitia moja maalum. Ahadi zilizofanywa kwa wote ni ahadi kwa waaminio wote wa kweli wa nyakati zote na vizazi vyote.

"Mti wa uzima"

Maelezo ya kitabu cha Mwanzo yanatujulisha kwamba mti huu unafunua siri ya uzima wa milele. Ulikatazwa kwa Adamu na wazao wake; lakini utapatikana kwa Adamu wa pili (Kristo Yesu) na ndugu zake. Anasema Daktari Thomas "Kula mti wa uzima ni kuwa jani lisilo nyauka, mmiliki wa uzima na utukufu, heshima na kutokufa kwa ufalme ambao Mungu wa mbinguni atausimamisha wakati ujao" Ona 1 Wakorintho 15.

"Paradiso"

Hili neno halipatikani katika Biblia ya UV. Ni neno la Uajemi lenye maana 'bustani' Nchi Takatifu, urithi maalum wa watakatifu, itakuwa hivyo: kama nabii Ezekieli alivyoandika, nao watasema, "Nchi hii iliyokuwa ukiwa, imekuwa kama Bustani ya Adeni, nayo miji iliyokuwa mahame, na magofu, sasa ina maboma, ina kaliwa na watu" (36:35).

WARAKA KWA EKLEZIA LILILO SMIRNA MLAKGO WA PILI:8-11.

MSTARI WA TISA

"Lakini u tajiri"

Maisha ya wamiliki wa ufalme wa Mungu vema wanaweza kusemwa ni matajiri. Mambo yote ni yao. Kama Paulo anavyosema (1 Kor. 3:21). Sio swali la ni lini watamiliki. Kwa kitambo kidogo, kama Paulo, yawapasa kuteseka na "kupoteza vitu vyote”.

“Matukano (makufuru)"

Neno "kutukana" linamaanisha "kuvunja sifa, kunena vibaya, lugha mbovu". Kutukana ni kuumiza jina zuri la mtu, kumnenea mabaya au kumchukiza. Kutukana kwa kusema sisi ni Wayahudi, wakati sivyo, ni kuvunja sifa na madhara kwa jina la Kristo. Maana waongo kuthibitisha kuwa ni wa Kristo, ni kudhuru sifa ya Kristo pamoja na wale wanaoliamini jina hilo, na kupinga maendeleo ya kweli. Hivi, watu wanaposema ni Wakristo, lakini hawana cha kuwapita wa-Yuda au. Wanikolai, aa wale wanaokwenda kanisani mara tatu yote katika maisha yao, ni watukanaji; maana kama katika ulinganishaji wa uovu wa ujinga wao unatoka ndani ya mioyo ya wote, "kweli kama ilivyo kwa Yesu" inaanguka, na kinakuwa ni kitu cha dhihaka na kudharauliwa na hao ("EUREKA", Vol. 1).

"Hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi".

Wapo Wayahudi wa "kiroho" vile vile Wayahudi wa asili. Paulo aliwajulisha Wayahudi walioishi Rumi kwamba "kwa ajili ya mnyororo yaani kwa ajili ya tumaini la Israeli nimefungwa na mnyororo huu" (Matendo 28:20) na kuwaambia kwa maneno mengine kwamba wale wanaoitii Injili, wanashika tumaini la Wayahudi. Wale wanaolikabali tumaini la Wayahudi Maandiko yanawaita "Wayahudi". "Maana hawi myahudi kwa nje; Wala aliye wa tohara, inayofanyika kwenye mwili: bali yeye ni Myahudi kwa utu wa ndani; na tohara ni ya yulealiye fanyiwa tohara ya utu wa ndani; na tohara ni ya moyoni, katika roho, na sio wa andiko; na sifa haitokani na watu, bali kwa Mungu" anasema Paulo (Warumi 2:28-29).

SHETANI

  1. "SHETANI" ni neno la Kiebrania ambalo hasa linamaanisha "adui", mpinzani. Neno dogo "Shetani" linatokea mara 55 katika Biblia ya Kiingereza - mara 19 katika Agano la Kale na mara 36 katika Agano Jipya. Katika Agano la Kale neno "adui" kwa usahihi limetafsiriwa mara 16. Kutofautiana huku na upendeleo wa upande mmoja umeficha ukweli nao watu wengi wamedanganyika. Katika kitabu cha Ayubu neno hili "SHETANI" linaonekana namna hiyo mara 14. Hivyo ndani ya Agano la Kale ukijumuisha kitabu cha "Ayubu", ni mara 5 tu linatokea katika neno "SHETANI" na mara 16 limetafsiriwa katika maneno mengine.

  2. NEKO DOGO "SHETANI" LINATUMIKA KATIKA MAANA MBAYA NA MAANA NZURI.

    1. MAAIU MBAYA - Mapenzi ya Mungu yanapopingwa.

      1. Kwa mambo yaliyo moyoni - mawazo mabaya ya watu Lk. 22; 3; Matendo 5:3.

      2. Mtu mmoja mmoja - mpinzani Math. 16:23; Ayubu, 1:6; 1 Wafalme 11:14;23.25.

      3. Kwa ujumla - kwa kisiasa na kidini, vyama na ulimwengu kwa wote. 1Wathesalonike 2:18; Ufunuo 2:13; 20:2,7; Zekaria 3:1-2.

    2. MAANA NZURI - inatumika kwa upande wa Mungu, malaika wa Bwana, na watu wema wanapokuwa wapinzani wa maovu. 1 Mambo ya Nyakati 21:1; Hesabu 22:22,32; 1 Samueli 29:4.

Neno "Sinagogi" maana yake "mkusanyiko" na "Shetani" - "adui". Watu hawa ambao kwa uongo walijiita wenyewe Wayahudi wa kiroho wote kwa pamoja Yesu amewaita ni "mkusanyiko wa adui" kwa upande wa waamini wa kweli - "Hata sasa wapo wapinga Kristo wengi, ndiyo laana tunajua kuwa ni siku za mwisho, haya ndiyo maneno aliyosema Yohana kwa kuwataja watu wengine waliounda ushirika ulioipinga ile kweli. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu: Maana kama wangalikuwa wa kwetu wangekaa na sisi, lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu" (1 Yohana 2:18-19).

MSTARI WA KUMI.

"Huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani"

IBILISI

1). MVUTO MKTJU.

Injili ni jambo la kwanza ambalo linapaswa lifahamike, kama ujumbe halisi wa Kristo ulioweza kusikika ulikuwa ni kwa ajili ya kutuokoa kutoka kwenye hatari yake

(1 Yohana 3:8; Waebrania 2:14).

2). MUHUTASARI V/A MAMBO YOTE.

  1. Ibilisi sio mtu mkubwa sana anayemjaribu mtu ili kufanya uasi juu ya Mungu, bali ni kuonekana wazi kwa dhambi kwa watu mmoja mmoja na kwa jamii ya watu.

  2. "Malaika aliyetupwa" ni wazo lililodumu la Upagani ambapo miungu ya mema na mabaya walionyeshwa kwa picha wakigombania roho za watu.

  3. Wazo hili halipati MSAADA WOWTE WA KWELI KATIKA MAANDIKO, ingawa inaweza kusomwa kwa mawazo yaliyotangulizwa mbele. Kwa hivi mahali ambapo maneno "Ibilisi na Shetani" yanatokea basi hufikiriwa kwa makosa juu ya kiumbe asiye wa kawaida kwa kusadiki ya kuwa maneno yenyewe yanapotokea huwa na maana hiyo, lakini hakuna pahali popote palipofundishwa namna hii katika Biblia.

3). MAMBO MAKUU YA KWANZA AMBAYO YANAONDOA FIKRA.

  1. Ikiwa pengine Ibilisi ameaminika kuwa hafi: jambo hili haliwezi kuwa hivyo kwa sababu yeye ni mwenye dhambi na kwa hivi yampasa afe! (1 Yohana 3:8; Rum.6:23) pia ni "Mungu peke yake asiyepatikana na mauti" (1 Timotheo 6:16).

  2. Kama Ibilisi anaaminika kwamba anakufa: Ni kwa jinsi gani kiumbe mfu, amiliki nguvu za magonjwa, mauti na ulaghai, awe amepata ruhusa toka kwa Mwenyezi Mungu na kuwa adui kwake katika shughuli zake na watu? Kila sheria ya haki ya Mungu ivunjwe.

  3. Ikiwa Ibilisi anadumu daima ... Kwa sababu gani hakuna ufafanuzi uliowazi unaomuhusu yeye katika Maandiko? (ukweli usio na idadi unaodumu katika hoja ya Mungu).

  4. Katika taarifa ya Agano la Kale Mungu aliposhughulika na taifalla Israeli hakuna chochote kinachotoa kibali kwa wazo la Ibilisi mwenyewe. Kwa sababu hiyo, ni maneno ya kubuniwa. Kwa kweli neno "ibilisi" linatokea mara 4 katika Agano la Kale Biblia ya Kiingereza ya AV. lakini katika Biblia ya Kiswahili kuna maneno tofauti nayo ni 'majini, mashetani na pepo’ na katika hoja ya kila maneno yake yanaonyesha kwa uwazi kuwa na sanamu ambazo zimetajwa. Maneno yanapatikana kwa Walawi 17:7; 2 Nyakati 11:15; Kumbukumbu la Torati 32:17; Zaburi 106:35-37.

  5. Mungu anawashika watu wanaopasishwa kwa njia zao. Haki yake ipo wapi ikiwa watu hawana hatia ya udanganyifu wa ibilisi mwenyewe? Lakini dhambi asili yake ni kutoka ndani ya moyo wa mtu, na ni haki kwa mtu kupasiwa kwa njia zake (Yakobo 1:13-15; Yeremia 17:9; Marko 7:20-23).

  6. Kuona mapenzi ya Mungu yakifanyika mbinguni uasi ni kitu kisichoweza kuonekana (Mathayo 6:10).

4). IBILISI AHAELEWEKA.

Ibilisi ni neno la kimaandiko lenye maelezo kana kwamba ni mtu la matakwa ya mwili yaliyo ya dhambi (tamaa ya uasi wa mtu), kwa kufuata mtindo wa mfano, unaozungumzia Hekima kama "mwanamke" (Mithali 8); Utajiri kama "mali" (Mathayo: 6:24); Dhambi kama "mfalme" (Warumi 5:21) na "bwana" (Warumi 6:16; Israeli Kama, "bikra" (Yeremia 31:4). "Dhambi" imeitwa kana kwamba ni mtu kwa vipindi vyake tofauti tofauti vya kudhihirika katika historia, katika matukio ya siku hizi, na katika unabii.

  1. FIKRA ZILIZO MOYONI: Tamaa za watu yaani zilizo mioyoni mwao (Yak. 4:7; Yohana 13:2; Waefeso 4:27; Waebrania 2:14).

  2. NDANI YA WATU MMOJA MMOJA: Ameitwa hivyo katika mfano wa maneno, kwa kuwa tamaa hukaa ndani yao na kuwashinda (Yohana 6:70).

  3. KATIKA JUMLA: Kwa watu wanaokaa kwa jamii, kisiasa na kidini kwa desturi za watu kwa sababu ya kawa katika "fikra za mwilini" zikitawaliwa na au kwa kifupi zinatawala mipango yao aa mafundisho (Ufunuo 2:10; 20:2; 1 Petro 5:8 Efeso 6:11-12).

  4. KWA NINI DHAMBI IMEITWA KANA KWAMBA NI MTU. Ni mtindo wa pekee wa Biblia katika kutumia vielelezo vya mfano mahali palipotajwa jambo lililohusishwa mno kwa maelezo yenye mambo mengi. Kupambwa huku na mfano ni mambo yasiyo ya kushikwa bali ni ya kuwazika yanayofunikwa na udhahiri na kuzidi kubidiishwa kwa maneno na maelezo yaliyofafanuliwa wazi yasiyowezekana kwa elimu ya maneno kuwa halisi na ukweli. Wakati ni ya maana zaidi yapo wazi kutumika vibaya - kama ilivyo katika suala hili. Neno limetafsiriwa lakini limepewa maana ngeni kwa matumizi ya mitume.

  5. WAEBRANIA 2:14: FUNGUO YA MAANA YA NENO "IBILISI". VICHEKESHO VINNE VYA MTAZAMO WA WANAOJIITA WANA IMANI SAHIHI.

  • Kwa ajili gani kushiriki "mwili na damu" ili kumharibu ibilisi wa wenye imani sahihi?

  • Ibilisi anayewaziwa na hao watu aweza kuharibiwa na Yesu kwa kujitiisha hata mauti?

  • Basi ibilisi angekuwa amekufa, lakini imesemekana yu mtenda kazi zaidi!

  • Mungu humtembelea mtu kwa mauti kwa sababu ya dhambi, na sio sababu ya ibilisi, Mwanzo 2:16,17; 3:17-19; Kumbukumbu la Torati 32:39.

Ni kwamba Ibilisi katika Waebrania 2:14 ni "dhambi” ambayo inaweza kuthibitishwa kwa njia mbili.

  1. KIFO CHA KRISTO KILBSHARIBU IBILISI

Lakini Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu (1 Kor. 15:3). Kwa hivi "ibilisi' ni "dhambi zetu" pia ml. Isaya 53:5; Ebr. 9:28; 1 Pet. 1:18-19; 1Yoh. 3:5; Tito 2:13-14; Rumi 8:3.

  1. YEYE ALIYE NA "NGUVU ZA MAUTI" YAANI "IBILISI"

Hivyo dhambi ndiyo inayosababisha kifo; "dhambi huleta mauti" (Yak. 1:14,15). Kwa sababu hii "ibilisi" ni dhambi. ml. pia wa kusoma Rumi 5:12,21, 6:28; 5:56,21.

  1. NYOKA: "IBILISI": "BABA WA UOHGO."

  2. Aliumbwa "mzuri sana" naye alikuwa ni mnyama mwerevu (Mwa. 1:31; 3:1). Hakuwekwa chini ya Sheria ya Mungu na hakuwa na uwezo wa kuabudu na kuwa na tabia njema (2:16-17).

  3. Ni kwamba hakuwa "chombo" kilicho mikononi mwa "ibilisi" ni dhahiri kutokana na ukweli kwamba naye alifika kwenye hukumu (Mwanzo 3:14).

  4. Hi kwamba hakuwa "ibilisi" katika umbile la kutambaa kwa uwazi kutoka kwenye ukweli kwamba alikwenda kwa tumbo "KATIKA SIKU ZAKE ZA MAISHA"! (mst.14) Je! Ibilisi wa watu walio na imani sahihi anafanya hivi (kutembea kwa tumbo)?

  5. Alikuwa ni wa kawaida kwa sababu ya uwezo wake wa kusema, kama mengine yanavyodokeza (Hesabu 22:28; 2 Petro 2:16).

  6. Nyoka aliwekwa katika Adeni ili kuipima imani. Jaribu hupima ndani ya sheria za Mungu. Kupimwa mwenendo mzima wa mtu kwa njia ya majaribu ni mwongozo uliowekwa na Mungu, (Mwanzo 22:1; 1 Petro 1:7; Waebrania 11:1-12).

  7. Kwa kuwa nyoka alisema uongo wa kwanza na kumhadaa Eva, amekuwa ni baba wa uongo au "Ibilisi" (mchongeaji, au msingiziaji). (Mwa. 3:4-5; Yoh. 8:44).

  8. Wote wasiotii Kweli na kuiharibu, kama nyoka alivyofanya, ni watoto wake wa kiroho.

1 Yohana 3:8,10,12; Matendo 13:10; Math. 13:38. Kwa sababu hizo hizo wameitwa "nyoka, wazao wa nyoka" (Mathayo 3:7; 12:34).

  1. IBILISI SIYE MALAIKA ALIYETUPWA. (Isaya 14:12-14; Ezekieli 28:2,12-14; Luka 10:18-19; Ufunuo 12:7-8; 2 Petro 2:4; Yuda 6,7. Sehemu 2 za mwisho hapa zinataja tukio moja.

Tunalielewa neno "Ibilisi" likiwa na maana "mchongeaji". Katika suala hili hasa la ibilisi kwenye hoja inatajwa mamlaka ya jamii ya Rumi, kwa kuwa iliwatesa hao Wakristo wa kwanza. Katika uongo iliwachongea Wakristo kwa kuwaita hawamwamini Mungu, kwa sababu waliichukia miungu yote ya Kipagani ya Rumi. Petro akiandika kuhusu mamlaka ya nguvu za Rumi. "Mkeshe na kuwa na busara; kwa maana adui yenu ibilisi, kama simba aungurumaye, anatembea, akimtafuta nani wa kummeza: Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani".

"Nanyi mtakuwa na dhiki (taabu) kwa siku kumi"

Hiki kilikuwa ni kipindi cha mateso makali yaliyowapata Wakristo wakati wa miaka ya B.K 110 - 120 yakiongozwa na Mtawala wa dola aliyeitwa Trojani. Alijaribu kukomesha jamii ya Wakristo iliyokuwa na watu walioongezeka, naye aliwaamrisha maafisa wake watiishwe pamoja na ukatili sana. Barua ya mtawala Trojani iliyotoka kwa liwali mmoja wa majimbo inaonyesha jinsi Wakristo walivyoenea: "Kuenea kwa mambo ya imani sio tu imesambaa katikati ya miji, bali hata vijijini na katika nchi. Sio kwamba nadhani haiwezekani kuchunguza na kusahihisha mambo hayo. Mafanikio ya jitihada yangu hapa inazuia hasara ya mawazo ya kukosa matumaini: Maana hekalu lipo katika hali ya ukiwa kabisa, limeanzwa kuendewa, na sherehe za Mungu, ambazo zamani zilikuwa za vipindi, zinahudhuriwa upya; na dhabihu za matoleo zinauzwa kila pahali ambazo ziliweza kuwa haba kupata mnunuzi. Ni napomaliza, hapo wengi walioweza kuadilishwa, walikuwa na tumaini la adhabu, la kwenye toba, karibu kabisa kumeimarishwa." Jibu la Trojani linaonyesha kwamba ni nia yake kufutilia mbali Ukristo: "Ikiwa wakiletwa mbele zako na kuzuiwa huku, ya kwamba yeyote akiukana Ukristo, na kushuhudia unyoofu wake kwa kuomba miungu miungu yetu, ingawa hivyo akitiliwa mashaka anaweza kuwa yaliyopita, atapata msamaha kwa wakati ujao, kwa majuto yake".

Wazo la kuichukua siku moja kama maana ya mwaka mmoja sio wazo geni. Tunaliona linatokea katikati ya unabii mwingi wa Biblia yote.

Waraka huu kwa wa-Smirna ni wa sehemu ya kwanza katika Ufunuo mahali ambapo "siku" zinasimama badala ya miaka. Ufunuo ni kitabu cha mifano ya alama fulani, ambayo mifano mikubwa inaonyeshwa kwa midogo. Vitu vyake vinavyogeuzwa, na shughuli zake na muda wake unaotangulia miaka elfu, yote ni mifano midogo ikionyeshwa kwa uhakika wa - mambo makubwa yanaelezewa kwa madogo. Huu ni mwongozo wa unabii, iwapo ukweli umesemwa jinsi ulivyo au kwa alama za mifano - daima maneno tu yanashindwa kulinganishwa na yaliyo halisi, ambayo ni "furaha isiyoelezeka yenye kujaa utukufu;" mambo ambayo hayawezi kusemwa. Kwa sababu ya utendaji kazi wa Roho kwa mwongozo huu ni kwamba mengi sana yamefunuliwa katika kidogo sana. Ni mtazamo uliongezwa nguvu, wa mambo yaliyo ndani ya Mwenyezi, ambayo, kama kwa ukubwa yangefunuliwa: "Nadhani, anasema Yohana, "hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuwa na vitabu ambavyo vingeandikwa."

Kufupishwa kwa habari iwe muhutasari, basi, ni jambo lililo kubwa la ufunuo wa Mungu; bali kwa alama za mifano, ni maalum. Habari ya kwanza ya siku kuwa jambo la mwaka ni katika Mwanzo 47:9, mahali ambapo Yakobo anasema, "siku za kusafiri kwangu ni miaka 130; na katika mstari wa 28 "siku za miaka ya maisha yake ni miaka 147." Hapa tuna 47, siku 450 za kusafiri kwake zimeonyeshwa kwa miaka 130. Sasa, ikiwa siku elfu nyingi zimefupishwa na kuwa miaka michache, juu ya jambo lili hili miaka mingi inaweza kubinywa na kuwa siku chache. Kwa hivi, "siku za miaka zilikuwa miaka 147," au, Yakobo aliishi siku 147, siku moja kuwa mwaka wa siku, au siku 52, 691.

MSTARI WA KUMI NA MOJA.

"Mauti ya pili"

Hii ni mauti ya hao watakao kataliwa kwenye kiti cha hukumu cha Kristo.

MAFUNDISHO YA BIBLIA YA WANAOPASIWA NA HUKUMU.

  1. KUPAHAMU - NDIYO MSIKGI WA KUPASIWA.

Kufahamu ukweli, iwe umeaminiwa au kuukataa, kuna mfanya mtu awe na wajibu. Kwa njia moja kama hii "wazazi wa kidunia" huwajibisha watoto wao kwa ajili ya mwenendo wao mara wakiwa wamefundishwa vya kutosha. Yoh.3:19; Lk. 12:47-48; 19:22, 23; Yakobo 4:17; Rumi 5:13.

  1. KUPASIWA NA HUKUMU NDIKO KUNAPAMBANUA YUPI ATAFUFULIWA TOKA WAFU.

Kwa hivi ni wale wanaopasiwa na hukumu ndiyo watafika kwenye kiti cha Hukumu. Wale wasiopasiwa na hiyo wanakufa na kusahauliwa kama hawakuwahi kuishi kamwe. Hawatafufuliwa. Isaya 26:14; Waefeso 2:1.12; 4:18; Zaburi 49:20; Yeremia 51:39,57; Obadia 16; Zaburi 37:10,20,34; Saburi 104:35.

  1. KUPASIWA NA HUKUMU KUMEELEZWA.

Kupasiwa kunategemea juu ya akili uwezo wake mtu na katika hali ya mambo.

      4. UWEZO WA AKILI KUWA NA UFAHAMU:

Watoto wadogo na wenye wazimu hawana uwezo wa kufahamu injili na kwa sababu hiyo hawawajibiki kwa matendo yao.

      5. HALI YA MAMBO ILIVYO:

Wengine wanaweza kuwa na uwezo wa kuelewa injili lakini wanakuwa hawajaisikia basi hao hawata hukumiwa na Kristo. Kwa kuwa hawajaisikia injili ya wokovu hawategemewi kujibu mwenendo wao.

      6. ISRAELI - KITAIFA WANA PASIWA.

Israeli wameadhibiwa vikali mno kwa ajili ya dhambi yake kuliko mataifa mengine. Hii imetokana na uhusiano wake mahususi na Mungu. Wakiwa ni watu wa Mungu Israel walifundishwa katika Sheria Zake na kusudi lake. Kuelimishwa zaidi kumeleta kupasiwa zaidi. Amosi 3:2; Kumbukumbu la Torati 28:15.

      7. KUONEKANA KRISTO KULIONGEZA KIWANGO CHA KUWAJIBIKA.

Tangu Yesu Kristo alipodhihirika, Mungu anawaona watu wanapasiwa zaidi mno. Hii ni kwa sababu utukufu wa Mungu kwa mwangaza zaidi uling’aa toka kwake kuliko ilivyokuwa hapo kwanza kwa mtu yeyote mwingine. Utukufu wa Mungu ulidhihirika katika nguvu ya maneno yake, uzima, miujiza, na hatimaye kwa ufufuo wake (Yohana 15:22-24; 9:39-41; Matendo 17:30-31; Waebrania 2:1-3; 10:28-29).

      8. MUNGU PEKEE NDIYE ANAWEZA KUHUKUMU WANAOPASIWA.

Maana ni Yeye tu anayejua uwezo na hali ya mambo ilivyo kwa kila mtu. Math. 25:15; Yohana 12:47-50.

      9. HAKI YA MUNGU DAIMA IMEDUMISHWA KATIKA KUPAMBANUA MAISHA YA MTU.

Nguvu na hekima ya Mungu imedhihirika kwa watu wote, ndani na kwa maajabu ya viumbe. Hivyo wana lawama kwa kushindwa kuitafuta hekima na wokovu wa Muumba. Kwa sababu hii Mungu hubakia ni mwenye haki kwa kutokuwafufua. Baba zao waliowatangulia (kwa mfano kama katika Mwanzo 11:1-9) "walipomjua Mungu hawakumtukuza kuwa ndiye Mungu", bali "walipotea katika uzushi wao". Kwa ajili ya hayo Mungu "aliwaacha katika tamaa zao za mioyo". Wazao wao bado wanauona utukufu ulio katika uumbaji na kuushiriki wema wake (nyakati za mazao, mvua, n.k, ona Matendo 14:16-17; Mathayo 5:45). Bado wanachagua mambo ya ubatili na ibada ya sanamu. Kwa hiyo hawana "udhuru" na kuangamia kwao ni kwa baki. Rumi 1:19-22.

     10. HAWA 'WASIOPASIWA NA HUKUMU’ IDADI KUBWA ZAIDI KULINGANA NA WATU.

Nadharia ya watu wengi wakati mwingine wanasema "Watakwenda kuzimu" na kisha wakati mwingine "ni kwamba watakwenda mbinguni". Tendo la kwanza la ukatili wa haki. La pili linaharibu kila jambo la Mungu. Watapotea mautini kama hawakuwahi kuwepo.

     11. WATU HUWA KATIKA MAKUNDI 2 KWA KUHUSIKA NA HUKUMU. WANAO HUSIKA

Ambao watafika mbele ya Kiti cha Hukumu cha Kristo wawe ni wenye haki au wasio haki.

      12. WASIO `HUSIKA

Ni ambao hawatafika mbele zake kujibu.

Wakati huo wale watakao kataliwa kwenye Hukumu hii inabidi wafe tena yaani - ni kupata mauti ya pili.

WARAKA KWA PERGAMO.

MLANGO WA PILI :12-17.

MSTARI WA KUMI NA MBILI.

"Huo upanga mkali, wenye makali kuwili"

Mmiliki upanga wenye makali kuwili anataka sharti kuangalia chombo hicho kama ni tendo linalotangulia lenye kuonya vita, Upanga unasimama kama mfano wa uweza wa Kristo wa kutekeleza amri zake atakavyo. Yeye mwenyewe anawahutubia ndugu waliokaa makao makuu ya Shetani mahali ambako maadui wa ile kweli walikuwa na nguvu. Nyoka hakuwa ndiye chanzo moja kwa moja cha dhambi iliyoingia ulimwenguni, hivyo basi amekuwa ni kielelezo kinachofaa cha dhambi yenyewe, Wale ambao maisha yao yanaongozwa na au kutawaliwa na dhambi wamekuwa ni uzao wa nyoka. Watoto wa nyoka ni namna ya msemo wa Biblia uhusuo wale wanaopinga au walio kinyume na njia ya Mungu. Yesu aliwasema Mafarisayo waovu kuwa "Enyi nyoka, wana wa nyoka" Mathayo 22:33, na mara nyingine aliwataja huku kitabu cha Mwanzo 3:15 kikiwa kichwani mwake (Yohana 8:44). Hivi "nyoka", ambaye ataharibiwa na "uzao wa mwanamke" ni dhambi iliyo kama mtu ambayo inaonekana katika wanadamu, na ndani ya wale inamoonekana hivi ni "uzao" wa nyoka. Inafaa hapa kutamka kwamba katika Biblia dhambi ya kitabu cha Mwanzo 3 ni upinzani kwa Mungu imeitwa kama ni mtu kwa namna nyingine. Kuita kitu kama ni mtu mara nyingi kumetumika kwa mfano wa namna ya kusema ambapo wazo lililo kwa muhutasari linaelezwa kwa picha kama vile ni mtu. Mifano imejaa tele katika vitabu vyote na pasipo shida inaeleweka:

"Tumaini linanyauka kukimbia, na Rehema inapumua kwa majonzi ikiaga"

(Byroni, Bibi arusi wa Abydos).

"Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu; hutoa sauti yake katika viwanja" (Mithali 1:20).

Uchunguzi wa karibu wa matumizi ya Maandiko kwa maneno ‘Ibilisi’ NA ‘Shetani’ yataonyesha kuwa nayo pia yameitwa kana kwamba ni mtu kwa dhambi, kuliko kutaja mtu mwovu aliyejuu ya watu.

Angalia maelezo mafupi juu ya SHETANI.

MSTARI WA KUMI NA TATU.

"Ukaapo ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani"

Kwa kawaida miongoni mwao waliojiita Wakristo, wengine walishika "mafundisho ya Balaamu" na ya "Wanikolai". Haya yakasababisha ugonvi wa siku zote, hivyo basi Eklezia likagawanyika, wengine wakimfuata Antipa, na waliobaki wakifuata wapotoshaji au wakoseshaji. Walio upande wa Antipa walikuwa wachache, ndiyo waliokuwa mashahidi "waaminifu waliouawa" katika Kristo, wakachinjwa kwa chuki na ulimi wa adui. Hapo kweli palikuwa Pergamo, ndipo penye kiti cha Shetani, au makao makuu ya ukengeufu.

"Nawe walishika sana jina langu"

Jina Yesu ni (Yahshuah) - Kiebrania limeundwa kwa jina la Yahu na Shuah, likiwa na maana "Nitakuwa wokovu” Jina lake Yahu (Yahweh) ni binafsi - ni jina limewekwa la Mungu, lililotangazwa hapo kwanza kwenye kijiti kilichokuwa kinaungua kuwa kumbukumbu kwa Waisraeli wote wa kweli. Jina hili linatangaza nia ya Mungu, kujifunua kwa uwazi mwenyewe katika kizazi cha wenye haki juu ya kizazi hiki Kristo ndiye mkuu. Katika Maandiko jina la mtu linaeleza nia na sifa ya tabia yake. Kushika sana jina lake maana yake ni kulidhihirisha. Tunashika sana jina lake wakati shabaha yake inatawala maisha yetu, na tabia ya sifa yetu inarudisha nuru ya mfano wake. Ikiwa tukiwa wana wa Mungu kweli na ndugu zake Kristo, basi, inatubidi tujenge katika maisha yetu tabia njema ya Mungu ambayo imeelezewa kwa uzuri wa kuvutia katika maisha ya Yesu.

"Antipas, shahidi wangu mwaminifu aliyeuawa"

Ameitwa shahidi "wangu mwaminifu". Jina linaonyesha ni yeye yule, au wao ambao walilishika sana jina nao hawakulikana wala imani ya Yesu Kristo, iwe ai Pergamo au mahali popote katikati ya mateso. Jina ni la mfano hasa wa wakati ule, nalo linamaana "kuwa kinyume chote". Hapa limeingizwa kama kutaja katika Ufunuo wale ambao walikuwa waaminifu, kwa kuwa kinyume na wote waliojifanya kawa Wakristo.

MSTARI WA KUMI NA NNE.

"Unao huko"

Walikuwepo wazushi katika eklezia la Pergamo ambao kuwapo kusinge ruhusiwa. Kwa kuwa waliruhusiwa kubakia, eklezia halikuwa na amani, isipokuwa tatizo likishughulikiwa, lilikuwepo tatizo lenye hatari kubwa ambalo nuru ya kweli ingelisababishia kuizamisha jumla. Hilo lilikuwa ni onyo la Kristo kwa wazee wa Pergamo.

"Wale ambao wanashika mafundisho ya Balaamu"

Petro anaifafanua tabia ya sifa ya wale kwa kusema "wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wakiiacha njia iliyonyoka, wakiiacha njia ya Balaamu mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu (2 Petro 2:15). Kwa hivi Wabalaamu walikuwa ni watu wa kuleta nia mbaya, ambao sio tu waliitumia kweli kwa lengo la kupata, bali walifuatisha njia au waliiga zisizo za Maandiko kwa ajili ya kupata pesa ambazo pengine hazikupatikana.

"Atie ukwazo mbele ya Waisraeli"

Balaamu hakuweza kurudisha nyuma shauri zuri la Mungu katika uhusiano kwa Israeli bali, kwa ajili ya kupata faida fulani, alivumbua njia ya kuleta laana juu yao. Aliwashawishi watoke kwenye utakatifu wao (kujitenga) kwa kuwavutia wawachukue wanawake warembo wa Moabu waliowasababisha waabudu sanamu. Ili kuonyesha "utayari wao kusikia mashauri", walijichanganya na waabudu sanamu, na kuwa chanzo cha kujikwa toka kwenye kweli.

“Kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu …. na kuzini"

Tunaweza "kutoa sadaka kwa sanamu" kama tunaruhusu kitu chochote kusimama kati yetu na Kristo; kiroho tunaweza kuzini kwa kuchagua elimu na matendo yaliyomo kipindi hiki tunacho ishi. Paulo alijitahidi kulilinda eklezia la kwanza toka kwenye uzinzi wa kiroho, akitaka kulileta eklezia "kwa Kristo bikira safi" (2 Kor. 11:2).

"Kula mana iliyofichwa"

Katika Yohana mlango wa sita, Wayahudi walipousema muujiza wa mana Jangwani, Yesu alionyesha ya kuwa ilikuwa ni kivuli chake mwenyewe ambaye alikuwa ni "mkate wa kweli" ulioshuka kutoka mbinguni. Aliwahutubia kwamba: "Msipokula mwili wake Mwana wa Adamu, na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu". Tunafanya hivi tunaposoma na tunapofahamu moyoni Neno lake la Kweli; lakini sisi, kama Waisraeli jangwani, yatupasa kushiriki mkate kila siku kwa ajili ya kuwa chakula. Waisraeli walikuta kwamba mana yoyote iliyobaki hata asubuhi siku iliyofuata ilioza, hivyo walilazimika kuikusanya kila siku. Pia ni jambo la kufurahisha kujua kwamba mana iliyokusanywa kwenye siku ya sita na watu ilidumu hata Sabato, hakuna aliyehitajika kuikusanya kwenye siku ya Sabato. Ndivyo ilivyo na kwetu: Neno ambalo tunalikusanya sasa litatuchukua katika kutokufa hadi kwenye saba elfu ya miaka kwa kipindi cha Adamu (utawala wa miaka elfu moja wa ufalme wa Mungu) - Paulo anaitaja hii anapoandika, "Kwa hiyo, imesalia raha ya watu wa Mungu" (Waebrania 4:9). Haruni aliamriwa aitunze omeri ya chungu cha mana kwa kutunza ndani ya Sanduku la Agano la Ushuhuda. Ilisalia humo kwa muujiza ilitunzwa kwa karne nyingi, ukiwa ni mfano wa kutokuoza au kwa lugha nzuri kutoharibika. Kwa utimilifu wa "kuhesabika kuwa mfano", kutokufa (yaani kuweka mana) kwa sasa kumefichwa ndani ya Yesu (Sanduku la Agano), atakaye itoa mana, au uzima wa milele kwa wale washindao, atakaporudi.

"Nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya"

Hii ni alama ya ahadi ya kukubalika na urafiki katika hukumu. Msingi wake upo juu ya desturi za Mashariki pande mbili kwa korti na jamii. Desturi ya mahakama ni kutoa kortini jiwe jeupe kwa mtu aliyehukumiwa kwa ishara ya kumwachilia na kumwona hana hatia. Ilikuwa ni desturi ya jamii kwa mwenyeji kugawa jiwe jeupe katika nusu mbili, na kisha kuchora jina la mgeni juu ya nusu hizi mbili, kushika moja yaani kubakia na nusu moja, na nusu ingine kumpatia mgeni ikiwa kama cheti cha ruhusa ya upendeleo ujao na urafiki. Kutokana na desturi hii ya zamani umetokea msemo wa kwamba mtu "amezuiwa asichakuliwe kwa kumpigia kura". Paulo anatumia lugha kama hii anaposema, "na walipouawa nalitoa idhini yanga au walipouawa, nalitoa jiwe langu la mviringo juu yao" (Matendo 26:10).

"Jina jipya limeandikwa katika jiwe"

Hili "jina jipya" ni la kutawala/au kwa kasisi jina, kuitwa (kama mfalme, mkuu, liwali, kuhani) na katika ufalme wa Mungu atapewa kila mtakatifu "ashindaye”. Katika mlango wa 11:13 tunasoma kuangamia kwa hesabu ya "majina ya watu". Wakati ule, kiutawala na makasisi majina yao yaliondolewa nchini Ufaransa.

"Asilolijua mtu, ila yeye aliyelipokea"

"Huu ni msemo wa kitabu cha Ufunuo, ambao haudokezi ya kwamba jina kwa maneno au kutamkwa haliwezi kujulikana. Jina alilonalo Mwaminifu na wa Kweli limesemwa kuwa halijulikani na mtu bali yeye mwenyewe; bado, katika mstari wa mbele baadaye, jina hilo limesemwa ya kuwa "ni mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana", (Ufunuo 19:12,16), Maana yake ni kwamba hakuna mtu alijuaye kwa kulichunguza jina bali yeye ambaye ana jina. Ikiwa mtu hawi mfalme wa wafalme, hawezi kulijua jina au heshima yake. Halimfai. Hivyo kwa heshima ya JINA JIPYA la jiwe jeupe la mviringo; ni kwa ajili ya mtu kulijua, naye hanabudi kuwa chini ya hukumu, Ndipo JINA JIPYA litaeleza ya kuwa yeye ni nani, na atalijua kwa kujaribia. Yeye na jina ai yule yule (kitu kimoja)." ("Eureka", Vol. 1).

WARAKA KWA THIATIRA

MLANGO WA PILI:18-29.

MSTARI WA KUMI NA NANE

"Macho yake kama mwali wa moto”

Hasira.

"Miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana"

Tayari kukanyaga katika hukumu.

MSTARI WA KUMI NA TISA

"Matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza"

Kristo analisifu eklezia kwa maendeleo 3 ya mwanzo katika upendo, utumishi, imani, uvumilivu, na matendo. Yalikuwa mazuri sana, lakini lilikuwepo jambo lingine ambalo lilihitaji kusahihishwa.

MSTARI WA ISHIRINI.

"Yule mwanamke Yezebeli"

Yezebeli, mke wa mfalme Ahabu, alijitoa kawa mwabudu wa Baali, na kwa kiwango cha hali ya juu hakuivumilia imani nyingine. Akafanya vita isiyotulizika juu ya manabii wa MUNGU, akapanga njama ya kumua Eliya, Nabothi aliuliwa, lakini mwishowe aliangamizwa na kisasi cha Mungu. Yeye ni mfano wa aina ya watu katika Thiatira waliodai kufundisha ("nabii mke"), lakini kama Yezebeli, alikuwa adui mkubwa wa mwisho kwa wale wanaishika kweli.

"Kuwafundisha watumishi wangu ili wazini"

Tabia ya mwelekeo wa mafundisho yao ilikuwa ni kuwavuta ndugu ili kujiunga na kushiriki imani ya Upagani wa wengi uliowazunguka, kwa kupinga mafundisho ya Kristo ya kwamba ndugu zake "sio wa ulimwengu huu" (Yohana 15:18-19); na kwamba urafiki na dunia hauwezekaniki kama urafiki na Mungu ukitaka kudumishwa. Ushirikiano wa nuru na giza kwa kawaida umesemwa kuwa ni uzinzi.

MSTARI WA ISHIRINI NA NNE.

"Na wote wasio na mafundisho hayo"

Hii inatuonyesha hali ya kweli ya Yezebeli ilivyo, na uzinzi ulivyokuwa uadilifu na mafundisho.

"Fumbo za Shetani"

Hapa, fungu la maneno "fumbo" limenukuliwa toka kinywani mwa Shetani (Wabalaamu na Wayezebeli). Inaonyesha kwamba walikuwa na majivuno sana kwa kadiri ya mapato yao. Walinena yaliyo ya mtazamo wao kama "fumbo", ambazo bila shaka, zilikuwa na maana kwamba mawazo yao yalikuzwa na kwenda chini sana kwa kulinganishwa na fumbo la kwanza la injili na mshirika mjinga wa kwenye kusanyiko alikuwa anaridhika. Hali ya kweli ya suala limefafanuliwa na Paulo anaposema kwamba "wao wenyewe wakisema ni wenye busara wakawa wajinga". Fikra zao yalikuwa ni mawazo tupu yasiyo ya kawaida; lugha yao ya kujifanya yalikuwa ni maneno ya kupayapaya kwa ujinga wa namna ya ubaya zaidi wa Mwanzo 3: ujinga unaofikiri wenyewe umearifiwa: akili chache inayofikiri yenyewe imekwenda chini sana. Elimu ya kweli imo ndani ya Biblia: fumbo la kweli ni katika Mwanzo 3 kwa mambo mengi.

MSTARI WA ISHIRINI NA NANE

"Nami nitampa nyota ile ya asubuhi"

"Yeye ashindaye …. atakuwa na utukufu wa kuwa na haki ya kufanya "Mwili Mmoja" , litakapo chaguliwa wakati wa kufunuliwa Wana wa Mungu (Rum.8:19-24). Wakati huo atakuwa nyota inayohusika na miaka elfu ya Ma pambazuko - Nyota ya Asubuhi; maana "wale walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; nao wawageuzao wengi ili kutenda haki, kama nyota katika kipindi (miaka elfu) na kuendelea" (Dan.12:4); aa kama Yesu alivyosema, "Ndipo wenye haki watang'aa kama jua katika ufalme wa Baba yao." (Mathayo 13:43). Waliokombolewa wakati huo, wote pamoja, watakuwa Wingu la Nyota ya Asubuhi, "wakiwa sawa na malaika", ambao walikuwa ni nyota za asubuhi walioimba pamoja, na wana wa Mwenyezi walipopiga kelele kwa furaha" wakati jiwe la msingi la pembeni lilipowekwa na wa milele (Ayubu 37:8)” ("Eureka")

Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia kaitka somo hili muhimu.

Lina itwa Kuishi katika Ukweli. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki.

 

CBM Publishing

32 Blenheim Road, Far Cotton

Northampton, England. NN4 8NW

ISBN 1 902059 16 -6

Registered Charity Number: 248979 / 1020558

Company Number: 2796412

Telephone +44 (0) 1604 765068

 

Muumba: Carl Hinton

Kufasiri: Simon Uswegi

Tena:

 

1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo

1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4

1 902059 02 - 6 Ukimwi

1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi

1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8

1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11

1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15

1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19

1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23

1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27

1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31

1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36

1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40

1 902059 13 - 1 Ufunuo Mlango wa Kwanza

1 902059 14 - X Ni kweli Yesu Kristo alishuka kutoka mbinguni?

1 902059 15 – 8 Nyimbo za ndugu wa Kristo

1 902059 16 – 6 Ufunuo Mlango wa Pili

 

Swahili Title
Ufunuo Mlango wa Pili - Maelezo Ya Manen
English files
Swahili file
Status
Printed
African text
Carl Hinton
Translator 1
Simon Uswegi
Literature type