Exploring the Bible - 22

Swahili

 

MITUME WAFUNDISHA INJILI BAADA YA KUPAA MBINGUNI KWA YESU KRISTO

 

SOMO LA 22 Soma Matendo 1 na 2

 

Marko aandika amri ya mwisho ya Yesu kwa wafuasi wake kabla hajapaa mbinguni:”Na akawaambia, Nendeni ulimwenguni kote na mfundishe Injili kwa kila kiumbe. Yule atakayeamini na kubatizwa ataokolewa. Lakini yule asiyeamini atalaaniwa” (Marko 16:15-16)

Ujumbe huu ni rahisi kuuelewa lakini ni wenye nguvu katika upeo na umuhimu.

“Enendeni ulimwenguni kote” Injili - habari njema ya wokovu sasa ingefundishwa duniani kote, maelezo ya kina kuhusu Mitume walivyofanya yameandikwa katika Matendo ya Mitume (Matendo 1:8)

Fundisha Injili. Wafuasi wa Yesu walitakiwa wafundishe ujumbe ule ule ambao Yesu alikuwa akifundisha- habari njema ya ufalme wa Mungu. Kwa kuwa sasa yesu alikuwa amefufuka waliongezea sehemu hiyo muhimu-wokovu kupitia jina la Yesu Kristo (Matendo 4:12, 8:12, Marko 1-14). “Yule atakayeamini” Hapa ndipo penye sharti la kwanza la wokovu. Imani na kushawishika kwamba Injili ndiyo njia pekee ya uovu. Imani hiyo ndiyo motisha katika maisha ya yeyote yule anayetaka kumpendeza Mungu (Warumi 10:17, Waebrania 11:1-2,6) ”na akabatizwa”. Ubatizo ni njia iliyoteuliwa na Mungu ili mtu adhihirishe kuwa anakiri kuwa ni mtenda dhambi anayestahili kifo na anataka kutubu na kumtii Mungu. Kwa kupitia ubatizo dhambi za zamani zinafuatwa na maisha mapya yanaanza kwa kufuata nyayo za Yesu Kristo (Matendo 2:38, Warumi 6:3-8) “Wataokolewa” Watu wote hutenda dhambi na mshahara wa dhambi ni mauti, lakini Mungu kwa neema yake ametoa njia ya wokovu. Kupitia kwa Bwana wetu Yesu Kristo Mungu hutupa msamaha wa dhambi na kwa hiyo wokovu kutoka katika matokeo ya dhambi na mauti (Warumi 5:12, 6:23)

 

KUPAA MBINGUNI KWA YESU

Yesu alikaa na wafuasi wake kwa muda wa siku arobaini baada ya kufufuliwa kwake. Katika muda huo aliongea nao hasa kuhusu “Ufalme wa Mungu”(Matendo 1:3). Baada ya hapo alipopaa mbinguni mbele kabisa ya macho yao malaika wakisema maneno haya ya faraja kwa wafuasi wenye mshangao: “Nyie watu wa Galilaya, kwa nini mnasimama mkikodolea macho mbingu? Yesu huyu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu mbinguni atarudi wafuasi wake walijizatiti kufanya kazi aliyowapa kufundisha Injili ya ufalme.

 

Matendo ya Mitume

Matendo inaweka kumbukumbu ya jinsi Injili ilivyoenea kutoka Yerusalemu kama mionzi ya jua katika Dola nzima ya Warumi. Ufunuo wa Matendo unapatikana katika sura 1:8 ambao unaweka kumbukumbu ya agizo la Yesu kwa Wafuasi wake kumi na mmoja. “Mtakuwa mashahidi wangu Yerusalemu na Yudea yote na Samaria na katika sehemu zote za dunia” Katika kitabu chote cha Matendo kuna ushahidi wa kuenea kwa injili kwa utaratibu, ikiwa na ujumbe wa wokovu.

 

Ufundishaji wa Injili Yerusalemu

(Matendo 2-7)

Ufundishaji ulianza siku ya pentecoste tafrija ya kiyahudi iliyofanyika siku 50 baada ya pasaka- kwa wakati huo siku 50 baada ya kusulubiwa kwa yesu kristo na siku chache baada ya kupaa kwake mbinguni. Wayahudi kutoka sehemu zote za ulimwengu wa kirumi walikusanyika yerusalemu kwa ajili ya tafrija hii kama tunavyoona katika Matendo 2;5-11. Ilikuwa katika pindi hili mtume walipopewa roho mtakatifu ambaye aliwawezesha kuzungumza lugha mbalimbali za watu wote waliohudhuria katika tafrija hiyo. Hii bila shaka ilikuwa kazi ya Mungu, na ilikuwa nafasi nzuri iliyoje kutangaza injili kwa wayahudi ambao walikuwa wameshuhudia muda mfupi uliotangulia, kusulubiwa kwa yesu wa Nazareti. Fundisho muhimu katika ujumbe wa wafuasi wa Yesu lilikuwa kwamba huyu, kwa kweli ndiye alikuwa Masia waliyeahidiwa na maandiko, kuwa angekuja. Uhakika amefufuliwa, na kwa wakati huo alikuwa ameketi upande wa mkono kulia wa Mwenyezi Mungu mbinguni (matendo 2:22-36) Petro ambaye alikuwa msemaji mkuu alitumia maneno ya manabii kwa wingi kuthibitisha neno lake. Wengi wa watu waliokuwepo walikubali ukweli wa maneno ya Petro. Wakistushwa kutokana na kosa kubwa walilokuwa wamefanya, waliuliza “Jamani, ndugu zetu, tufanye nini?” Jibu la Petro lilikuwa wazi ;Tubuni na mbatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi (matendo 2:37-38)

 

Twapaswa kuelewa kishindo cha jambo lililokuwa linatokea. Walikuwepo watu wapatao 3000 ambao “Kwa furaha walipokea neno lake na wakabatizwa” (matendo 2:41). Siku moja Injili ilifundishwa Yerusalemu na wengi waliamini. Hivyo ndivyo kuenea kwa Injili katika ulimwengu wa kirumi kulivyoangaza, kwa sababu watu ambao walikuwa wametoka sehemu za mbali walirudi makwao baada ya sikukuu wakiwa wamebeba imani mpya katika Yesu kristo

 

Baada ya tukio hili Petro na Yakobo walimponya mtu mmoja mlemavu ambaye alifahamika vema hekaluni ,(Matendo 3) Tokeo la muujiza huu lilikuwa la papo kwa papo na wengi zaidi waliamini, safari hii watu kama 5000 (Matendo 4: 4) .Idadi ilizidi kuongezeka kutokana na mafundusho yao pamoja na miujiza waliyokuwa wakifanya ili kwamba ‘waamini waliongezeka zaidi kwa Bwana makundi kwa makundi, wanawake kwa wanaume ‘ kwa (Matendo 5:14-16)

 

Hata hivyo mafanikio ya kuenea kwa Injili hayakukosa matatizo. Makuhani wakuu na watawala waliendelea kuwa wapinzani na kuwatesa waamini. Matokeo yake waamini walitawanyika wakiwa wamebeba Injili (Matendo 8: 1)

 

Injili yafundishwa Samaria (Mat 8:1-12)

 

Katika sura hii tunapata habari za Filipo akienda Samaria ,eneo ambalo liko kaskazini mwa Yerusalemu akifundisha mambo yahusuyo ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo (aya ya 12).Matokeo yake yalikuwa kwamba waliosikia waliamini “na wakabatizwa wanaume kwa wanawake”(aya ya 12).

 

Toashi Mhabeshi abatizwa(Mat 8:26-40)

 

Hapa twasoma kuhusu Mhabeshi toashi aliyekuwa anarudi nyumbani kutoka Yerusalemu. Alipokuwa anasafiri alikuwa anasoma kwa makini sana sehemu iliyohusu manabii lakini alipata shida kutambua ni yupi aliyekuwa akizungumziwa.

Fillipo alitumwa na Mungu kumuelewesha mtu huyu maana halisi ya maandishi ambayo mtu huyo alikuwa anatafakari. Ilikuwa sehemu ile ilivyokuwa Inazungumzia kujidhabihu kwa Masia.Kwa hiyo Filipo alieleza mambo kuhusu Yesu Kristo ambapo baada ya hapo toashi aliomba abatizwe.Filipo alisema, kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa (aya ya 36-39), toashi akasema , “Ninaamini kuwa Yesu Kristo ni mwana wa Mungu” , na kwa hiyo Filipo akambatiza. Ujumbe ukawa njiani kuelekea Uhabeshi (Ethiopia).

 

 

 

Paulo Ageuzwa (Mat.9)

Katika sura hii tunapata habari ya kushangaza, ya kugeuzwa kwa Sauli (ambaye baada ye aliitwa Paulo katika Matendo 13:9).Alikuwa anapinga kwa uchungu mkubwa mafundisho kuhusu Yesu wa Nazareti na alikuwa akiwatesa wale walioamini. Katika tendo la kuwawinda wafuasi wa Yesu aligeuzwa alipokuwa akienda Damascus,Yesu Kristo mwenyewe akimtokea alipokuwa akisafiri. Akiwa amepigwa bumbuazi kwa ono hili Sauli akabadilika kabisa na kwa kuwa sasa alikuwa anaamini akabatizwa (aya ya 18) kazi ambayo Mungu alikuwa amemwekea imefupishwa katika maneno ya Kristo .”Ni chombo kiteule kwangu kubeba neno langu mbele ya watu wa kimataifa na wafalme na watoto wa Israeli” (aya ya 15) sura za Matendo zinazofuata zinahusu kazi nzuri ya kushangaza iliyofanywa na Mtume Paulo,ya kueneza Injili katika Dola nzima ya Rumi (Mat 13-28)

 

Korineli, mlinzi wa kirumi aamini Injili (Mat 10)

 

Mtume Petro aliagizwa kupeleka ujumbe wa Injili kwa Korineli, askari wa kirumi aliyekuwa Kaisaria. Kijadi lilikuwa kosa la kisheria kwa Wayahudi kuongozana na watu wamataifa (aya ya 28), kwa kuwa waliaamini kuwa kwa kufanya hivyo walinajisika. Katika tukio hilo mtazamo huo usio kuwa na ukweli uliwekwa kwa pembeni na Bwana,na Petro mwenyewe ndiye aliyekuwa wa kwanza kutambua kuwa “Mungu haheshimu nafsi’’ ila anatoa wokovu kwa watu wote kwa misingi ya usawa. Kwa hiyo Petro alitumwa kumpelekea Injili mtu huyu wa mataifa pamoja na nyumba yake yote. Matokeo yake, Korineli na nyumba yake nzima waliamini na kubatizwa (aya ya 7-48)

 

“Aaminiye na kubatizwa’’

 

Mbali na kwamba tumeona kuwa Injili ilienea taratibu, katika sura ambazo tumeshatafakari, pia tunaona kuwa mitume waliwabatiza watu walioamini. Ni wazi kwamba walikuwa wakifuata kwa usahihi kabisa maagizo waliyopewa na Yesu alipowaamuru waende ulimwenguni kote na kufundisha Injili. Ni wale tu walioamini na kubatizwa ndiyo wangeweza kuokolewa.(Marko 16:15.

 

Kumpa mtu jina la kikristo ni ubatizo ?

 

Katika matukio yote yaliyomo katika “Matendo’’ tumeona kuwa imani kilikuwa kitu cha lazima kwa wokovu. Baada ya kufundisha Injili kwa uangalifu, motisha wa mtu kutaka abatizwe ulikuwa ni kukiri kuwa yale waliyofundishwa yalikuwa kweli. Katika kila ubatizo, ni wale waliokuwa na umri wa kutosha kuelewa walichofundishwa. Ndio waliobatizwa.

 

Kumpa mtu jina la kikristo je? Kuwapa watoto wachanga majina ni jambo lisilofundishwa katika Biblia. Ni mojawapo ya mafundisho yasiyo kuwa kweli ambalo limekubalika katika makanisa ya kikristo lakini linapingana na fundisho la Biblia. Kuwapa watu majina ya Kikristo kulianza kama mtindo katika makanisa ya kikristo mwaka 1000 hivi,baada ya Kristo.

 

Hata kuzamisha majini siyo ubatizo wa kweli isipokuwa kama kumetangulia na imani katika sehemu kuu mbili za Injili kama ilivyo ainishwa katika (Matendo 8: 12) na kuungama dhambi. Ni muhimu kabisa kwamba mtu anayapenda kubatizwa aelewe kuwa anaingia katika uhusiano mpya na Mungu.

 

 

 

Ubatizo –uzamishaji kamili majini.

 

Kama tulivyofuatilia mafundisho ya ubatizo hadi Matendo ya Mitume, tumeona kwamba waliobatizwa “walikwenda chini majini’’ na kuibuka “kutoka majini’’(Matendo 8:38-39).Hii ndiyo sababu Yohana alibatiza “katika mto wa Yordani”(Mathayo3:6) na mahala panapoitwa Aenou “kwa sababu palikuwana maji mengi’’(Yohana 3:23) twasoma kuhusu Yesu “akiibuka kutoka majini’’ baada ya kubatizwa (Marko 1:10).

 

Ubatizo ni uzamishaji kamili majini,kwa sababu, kama tulivyo kwishaona unaashilia mazishi.Ni Injili ambayo Mungu amechagua ya sisi kujifananisha kwanza na kifo halafu ufufuo wa Yesu Kristo. Kwa hiyo Paulo anaandika : “Tumezikwa pamoja naye (Kristo) kwa ubatizo katika mauti.” Katika tendo la kubatizwa tunadhihirisha kwa Mungu kuwa “mzee wetu” (msemo unaoonyesha maisha yetu ya zamani) ameuawa na kuibuka tena majini,kutembea tukiwa wapya katika Kristu (Warumi 6:3-6)

 

Muhtasari

  • Baada ya kufufuka Yesu aliwaamuru wafuasi wake waende ulimwenguni kote na kufundisha Injili……atakayeamini na kubatizwa ataokolewa” (Marko 16:15-)Ni kwakutii agizo hili wafuasi wake walipo kwenda katika dola nzima ya kirumi wakieneza Injili na kubatiza walioamini

 

  • Yesu alipo paa mbinguni malaika waliwahakikishia wafuasi wa Yesu kuwa atarudi kwa uhakika kabisa (Mat 1:9-11).

  • Matendo ya mitume inatusimulia kuenea kwa Injili katika ulimwengu mzima wa kirumi.Inatueleza kwa kuendelea kuwa wale walioamini walibatizwa .

  • Baada ya hotuba ya Petro siku ya pentecoste katika mji wa yerusalemu watu 3000 walibatizwa (Mat.2:37-38,41).

  • Mhabeshi Mhasiwa alibatizwa (Mat 8:26-48).

  • Kama tokeo la mafundisho ya Filipo, Samaria wengi walibatizwa (Mat 8:12).

  • Paulo alibatizwa baada ya kugeuzwa (Mat 9:18), huunganishwa na (Mat 22:12-16).

  • Korneli na nyumba yake nzima walibatizwa (Mat 10:47-48).

  • Ubatizo ni uzamishaji kamili majini (Mat 38-39).

  • Kumpa mtu jina la kikristo sio kubatiza na hakuna msingi wa kiBiblia. Kulifanyika kwanza katika kanisa la Kristo takribani miaka 1000,baada ya kifo cha Yesu kristo

 

 

SOMO LA 22- MASWALI.

 

1. Yesu aliwapa amri gani wafuasi wake kabla hajapaa mbinguni?

2. Bila imani na ubatizo mtu anaweza kukolewa?

3. Malaika waliwaambia nini wafuasi wa Yesu alipopaa mbinguni?

4. Siku ya Pentecoste, watu walipouliza wafanye nini Petro aliwajibuje?

5. Wale waliopokea neno lake kwa furaha walifanya nini?

6. Filipo alihubiri nini Samalia?

7. Watu waliomwamini Filipo walifanya nini?

8. Ubatizo ni nini?

9. Kumpa mtu jina la kikristo ni fundisho la Biblia?

10. Ni jambo gani la lazima ili kuzamishwa majini kuwe ubatizo wa kweli?

 

 

Swahili file
African text
Christadelphian Bible Mission
Literature type