CSSA 1-1-02 - CREATION

Swahili

2. UUMBAJI

Mungu akaona kila alichokifanya na tazama ni chema sana”

 


Shabaha

Kuonyesha kwamba Mungu aliumba vitu vyote ili dunia ijawe na Utukufu wake.

Muhtasari

Biblia inaanza na kitabu cha Mwanzo. “Mwanzo” maana yake ni Uumbaji, mstari wa kwanza katika Biblia unasema “Hapo mwanzo Mungu aliumba mbigu na nchi”. Hatuna uhakika kabisa ni wakati gani Mungu alipoumba mbingu na nchi, tunalolifahamu ni kwamba Mungu ambaye ni wa milele aliumba nchi miaka mingi sana iliyopita. Mwanzo 1:2 husema kuwa “nayo nchi ilikuwa  ukiwa tena utupu ”. Hatuambiwi ni kwa nini lakini tunaambiwa katika Mwanzo Sura 1,kwamba Mungu alikusudia kutenda jambo duniani. Alikusudia kuiwekea utaratibu kusudi ikaliwe na watu ili  wampatie  sifa na utukufu yeye. Alifanya hivi miaka 4000 KK (Hii yapata kama miaka 6000 iliyopita ) Kutoka 1 hadi 2:7, 18, 25.

KUSUDI LA UUMBAJI

Sura ya kwanza ya Kitabu cha Mwanzo inatuambia  Mungu alipoumba vitu vyote na kuviweka duniani.Alikuwa na lengo tayari katika fikra zake.Tangu mwanzo lilikuwa kusudi la Mungu kwamba uumbaji wake wote ni lazima umpatie utukufu Yeye. “Hakika yake kama niishivyo mimi na dunia yote itakavyojawa na utukufu wa BWANA”. (Hesabu 14:21). Kwa kuijaza dunia na “Utukufu wake”, Mungu ana maana kuwa kila kitu kilichoumbwa kinapaswa kumwabudu na kumtii Yeye. Haitakuwepo dhambi tena, na hayatakuwepo magonjwa au kifo. Maana dunia itakuwa imejawa na watu ambao Mungu amewapatia uzima wa milele. Tunasoma hili katika badiliko lililo kuu katika ufunuo 21: 3-4.

SIKU SITA ZA KUFANYA KAZI: Mwanzo 1 hadi 2:3,7,18-25.

Dunia haikuwa nzuri kabisa, wakati huo Mungu alipokuwa amekusudia kuiweka katika mpangilio. Ilikuwa giza na utupu. Haikuwa na uhai au nuru ama uzuri wa aina yoyote. Ndipo Mungu alipoamua kuibadilisha dunia na kuifanya iwe  mahali panapofaa  watu kuishi . Akawaamuru malaika zake wafanye kazi hiyo. Katika Zaburi 103:20 tunasoma kuwa malaika zake ni  hodari:Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, “mtendao Neno lake, Mkiisikiliza sauti ya Neno lake”. Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye aliamuru, ikasimama Zaburi 33:9 

Ilikuwa ni kazi kubwa sana. Lakini kwa kuwa Mungu ndiye mwenye nguvu zote, kazi ya uumbaji ilifanyika kwa muda wa siku sita.

Kila siku “ikawa ni jioni na  ikawa asubuhi” zaidi ya  muda wa masaa ishirini na nne. “Kwa muda wa siku sita BWANA akaifanya mbingu na nchi, bahari, na vyote vilivyomo ndani yake” (Kutoka 20:11) Kwa kila siku uumbaji ulifanyika kwa siku sita, jambo moja jema na la mhimu lililoongezwa duniani, mpaka hapo dunia ilipo kuwa tayari kwa mtu kuishi, ambaye Mungu alimkusudia kumuumba mwisho wa viumbe vyote. Ndipo Mungu  “akapumzika” siku ya saba. Na tuangalie ni nini kilichofanyika katika juma hilo la uumbaji.

Siku ya kwanza (mistari 3-5) Kwanza Mungu akasema “Na iwe nuru”.  Mungu alisema na Malaika wakafanya kama alivyoamuru). Dunia ilikuwa imefunikwa kabisa na giza, lakini sasa Mungu akatenganisha nuru (ambayo aliita “mchana”) na giza, (ambalo aliliita “Usiku”).

Siku ya Pili (mistari ya 6-8) Inaeleza kuwa Mungu aliumba mbingu kati ya maji ya juu na yale ya chini, inazungumzia kuhusu anga, hewa tunayovuta. Hii ilikuwa ni mhimu kabla ya miamba, au wanyama au mtu kuweza kuishi duniani. Hivyo Mungu aliumba hilo baadaye.

Siku ya Tatu (mistari ya 9-13) Siku hii Mungu alitenganisha maji kati ya nchi kavu ,Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu alipofanya hivi , aliiwekea mipaka bahari ili kwamba bahari isiipite hiyo. 

Kisha Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake,ikawa hivyo. Na hii ndiyo sababu tunapopanda mbegu za mahindi tunapata mahindi. Mbegu za machungwa hazibadiliki kuwa za mti wa limao au mahindi kuwa ngano.
Tunapaswa kutulia na kufikiria jinsi Mungu alivyopangilia vizuri kazi zake zote za uumbaji ulivyokuwa  kwa kuwa “kwa hekima yake ameviumba vitu vyote” (Zaburi 104:24).

Siku ya Nne (mistari ya 14-19) Jua, Mwezi na Nyota pia ziliwekwa mahali pake sahihi katika anga kuleta mwanga wakati wa mchana na usiku. Nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka. Kwa hiyo tuna majira manne kwa mwaka, na masaa ishirini na nne kwa siku, Jua huchomoza na kuzama kila siku bila kushindwa na limeendelea kufanya hivyo tangu siku hii ya nne ya Uumbaji, siku na miaka hakuna wakati majira yalipokuwa marefu au mafupi.

Siku ya Tano (mistari ya 20-23) Siku hii Mungu aliumba viumbe vyote viishivyo baharini , na aina ya ndege wote warukao angani.

Siku ya Sita (mistari ya 24-31) Hatimaye, siku ya sita , Mungu aliviumba viumbe vyote viishivyo nchi kavu , wanyama wa kufugwa,kila kitambaacho na aina zote za wanyama mwitu. Kisha kabla ya siku ya sita kuisha  alimwumba Mtu. “Na BWANA, Mungu akafanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai” (Mwanzo 2:7).

Mungu akamweka  huyu mtu, Adamu, katika bustani nzuri sana ambayo aliipanda katika Edeni. Akawaleta wanyama wote kwa Adamu naye akawaita majina yao. Lakini Mungu akaona si vyema Adamu awe peke yake. Alihitaji awe na msaidizi wa kufanana naye, ambaye angemsaidia kumsifu Mungu. Kwa hiyo Mungu akamuumba “msaidizi (anayemfaa) wa kumsaidia Adamu”. Mungu akamletea Adamu usingizi , akasinzia , na akachukua ubavu  mmoja wa Adamu. Akamuumba mwanamke kutokana na huo ubavu) “Mwanamke” maana yake “aliyetwaliwa kutoka kwa mwanaume”).Kisha Mungu akampeleka huyu Mwanamke , Hawa, Kwa Adamu kuwa mkewe (Mwanzo 2:18-24).Yote hayo Mungu aliyafanya siku ya sita.

Siku ya Saba (Mwanzo 2:1-3) Siku ya saba “Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya, Mungu akapumzika siku ya saba” (mstari 2) Neno “kupumzika” halina maana kuwa Mungu alikuwa amechoka akahitaji kupumzika,maana yeye ni mwenye nguvu zote na kamwe haja acha kufanya kazi.(Zaburi 12:4,Yohana 5:17). Alipumzika kwa sababu alikuwa amemaliza kazi kubwa aliyokuwa ameazimia kuifanya. Mungu “aliacha kazi ya uumbaji”. Kwa muda wa siku sita aliumba nchi na akaweka mtu na viumbe vyote katika nchi.

FUNDISHO KWETU

Kuna mambo mawili tunayotakiwa kujifunza kutenda – :kumsifu Mungu na kumshukuru yeye kwa wema wake. Mfalme Daudi alisema: Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu yajua sana”. (Zaburi 139:14).
Kwa hiyo kila tutazamapo juu mbinguni au tunapoona wadudu wadogo sana; wameumbwa kwa ajabu mno, au tunapovuta harufu nzuri sana ya maua ama tunapotazama mawimbi yanavyovuma yakiishia ufukweni, na tumshukuru Mungu, Muumbaji Mkuu wa vitu hivi vyote. Tunawezaje kumshukuru kwa ajili ya uumbaji wa vitu vyote kwa ajili yetu? — kwa kuliamini Neno lake na kutii amri zake, “Ee BWANA, jinsi yalivyo matendo yako! “Kwa hekima umevifanya vyote pia”(Zaburi 104:24).

MAELEZO YA NYONGEZA

Ni watu wachache sana siku hizi wanaoamini kwamba Mungu ndiye aliyeumba vitu vyote . Watoto wetu katika shule na vyuo vikuu hawafundishwi Uumbaji wa Mungu badala yake wanafundishwa nadharia ya mabadiliko ya maumbile ya vitu (hasa ni wazo lililopendekezwa) linalokubaliwa na wanasayansi wengi kueleza jinsi Mwanadamu alivyokuja kutofautiana na wanyama wengine. wanasema kuwa maisha katika dunia yanabadilika badilika (yaani yalikua au yalibadilika) yalitokea zaidi ya mamilioni ya miaka iliyopita . Wanasema kuwa maisha yalitokea kwa nasibu;hayakutokana na mpango maalumu wa Mungu. 


Watu wengi wanapenda kumwamini Mungu na kumtii. Hata hivyo nadharia hiyo haiwezi kuthibitishwa. Biblia ni ya kweli  na ni rahisi kuithibitisha kuwa ni ya kweli . (Soma somo la 1, Maelezo ya nyongeza ). Bwana Yesu Kristo yeye mwenyewe aliamini na akafundisha kwamba Mungu pekee ni Mwumbaji mwenye hekima wa vitu vyote (Soma Marko 10:6).Mitume pia walifundisha kwamba “Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na  vitu vyote vilivyomo” (Matendo ya Mitume 17:24-26,pia linganisha na 1Petro 4:19).

MASWALI

Majibu Marefu

1.Ni nani aliyeumba ulimwengu na vitu vyote vilivyomo? 
2.Ni nani aliyemsaidia Mungu wakati alipoweka dunia katika utaratibu maalumu? 
3.Majina ya mtu wa kwanza na mwanamke  wa kwanza ambao Mungu aliowaumba? 
4.Neno “mwanamke” maana yake nini? 
5.Mtu wa kwanza na Mwanamke waliishi wapi? 
6.Mungu aliumba vitu vyote kwa muda wa siku ngapi? 
7.Mungu “akapumzika”. Hii ina maana gani? 

Majibu ya Kina

Hapo mwanzo Mungu aliumba vitu vyote
1.Eleza Mungu aliumba  nini:- 
a.    Siku ya kwanza na 
b.    Siku ya nne. 
2. Ni jinsi gani Mungu alivyomwumba mtu wa kwanza? 
3. Ni jinsi gani Mungu alivyomwumba Mwanamke? 

Majibu ya Nyongeza

Hapo mwanzo Mungu aliweka utaratibu wa kuumba vitu vyote duniani
4.Eleza yote unayofahamu kuhusu siku sita za uumbaji
 
 

A black and white drawing of a person lying down under a tree

Description automatically generated

Swahili Title
002 UUMBAJI
English files
Swahili file
Sub type
Sub sub type