CSSA 1-1-03 - DISOBEDIENCE IN THE GARDEN OF EDEN

Swahili

3. KUKOSA UTIIFU KATIBU BUSTANI YA EDENI

“Bwana Mungu akapanda bustani upande wa Mashariki wa Edeni”

 

Shabaha

Ni kuonyesha nini kilitokea baada ya Adamu na Hawa kutomtii Mungu.

 

Muhtasari

Mungu alikuwa ametayarisha bustani nzuri kwa ajili ya kuishi mwanamume na mwanamke ili waishi ndani yake. Iliitwa busani ya Edeni.Iikiwa na maana ya “furahia”. Ilikuwa na miti mingi ya kupendeza kwa kuiangalia na pia mizuri kwa chakula. Mto ukiimwagilia bustani na Adamu aliilima na kuitunza wala hapakuwa na magugu au miiba ya kuiharibu ardhi. Adamu na Hawa waliweza kufurahia vitu vyema ambavyo muumba mwenye upendo aliwapatia.Mungu aliamua kupima upendo wao waliokuwa nao kwake .Mwanzo 2:15-17;3

MTI WA KUJUA MEMA NA MABAYA MWANZO 2:15-17

Katikati ya bustani ya Edeni Mungu alikuwa amepanda aina mbili za miti maalum- “mti wa uzima” na “mti wa ujuzi wa mema na mabaya” Adamu na Hawa waliruhusiwa kula matunda ya miti mingine yote isipokuwa matunda ya mti huu wa pili. Mungu alisema, “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapo kula matunda ya mti huo utakufa hakika. Walikuwa hawaruhusiwi hata kuugusa (3:3)

Amri hii hakika ilikuwa rahisi ambayo Mungu aliwaonya kuwa ikiwa hawataizingatia watakufa hakika.Kutokutii sheria ya Mungu ni dhambi na “mshahara wa dhambi ni mauti”(Warumi 6:23)

KUTOKUWA WATIIFU KATIKA EDENI.MWANZO 3:1-6

Kwa muda mambo yaliendelea kuwa mazuri, lakini katika bustani hii ya Edeni kulikuwa na mnyama mwelevu aliyeitwa “nyoka” ,ambaye Mungu alimpa uwezo wa kusema.Mwanzo 3: 15,hueleza jinsi nyoka aivyomwambia mwanamke uongo  na mwanamke alimwamini nyoka badala ya kumwamini Mungu. Nyoka kama walivyo wanyama wengine hakuwa na ufahamu wa kupambanua mema na mabaya kwani Mungu hakumpa akili kama alivyompa mwanadamu hata hivyo aliweza kusikia maagizo ya Mungu aliyomwambia Adamu na Hawa,lakini akidhani kwamba ikiwa watakula matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, bila shaka wangekuwa na ufahamu kama malaika. Kwa hiyo nyoka alimwambia Hawa kuwa hakika “hamtakufa”.

Mara baada ya mawazo haya kumwingia Hawa akilini alianza kuushangaa mti ule. Aligundua kuwa ulikuwa  “mti unaofaa kwa chakula”,wapendeza macho, nao ni mti wa “kutamanika kwa maarifa” na kadri alivyoyangalia matunda yake ndivyo alivyozidi kutamani mti ule.Na kuwa ungemwezesha kuwa mwerevu kama malaika, kama nyoka alivyokuwa amemshawishi…

Ghafla, Hawa alinyoosha mkono wake na kuchuma tunda na kula. Hatimaye alimpatia Adamu “ambaye pia alikula”.

Hawa alidanganywa na nyoka na hakutii amri ya Mungu. Adamu alitenda dhambi kwa kuchagua kumpendeza mkewe kuliko kumpendeza Mungu.

DHAMBI HULETA AIBU NA WOGA: MWANZO 3:7-13

Mara baada ya Adamu na Hawa kula tunda walitambua kuwa wametenda dhambi.Ghafla waliona aibu na kuogopa. Kwa hiyo walishona majani ya mtini kuwa nguo za kujifunika. Walijificha katika bustani wakijua kuwa Mungu angekasirika. Hivi ndivyo hutokea kwetu pia tutendapo dhambi.  Na mara tunapotambua kuwa tumekosea njia ya Mungu tunaona aibu na kujiona kuwa tu wenye hatia kwa Mungu. Wakati Mungu alipomwita Adamu, ndipo Adamu  mwenye hatia alimlaumu Hawa na Hawa alipulizwa na Mungu naye alimlaumu nyoka. Lakini walikuwa wao wenyewe ndiyo waloijua sheria ya Mungu na ni wao walikuwa hawakuitii.

ADHABU YA MUNGU. MWANZO 3:14 – 20

Kwa Nyoka: Kwa kuwa nyoka alisema uongo na kumdanganya Hawa, Mungu alimlaani.Atakwenda kwa tumbo na kula mavumbi katika siku zote za maisha yake.

Kwa Adamu: Mungu alimwambia Adamu kwamba badala ya kuishi katika bustani nzuri ambamo kila kitu kilikuwepo kwa kusudi la Mungu, watafukuzwa katika bustani hiyo. Tangu wakati huo na kuendelea ikamlazimu kufanya kazi ngumu ili kumwezesha kupata chakula chake na Hawa. Ardhi sasa itaotesha miiba na magugu na kuifanya kazi  kuwa ngumu zaidi. Mwishowe Adamu atafariki na kurudi tena katika mavumbi ya ardhi ambayo katika hayo aliumbwa kwa maana Mungu alisema,“ kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi”(mstari 19). Kwa hiyo mtu akawa kiumbe wa kufa kwa sababu ya dhambi maana “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) na sisi sote tunatokana na ukoo wa Adamu tunashiriki pia katika namna moja ya asili na hivyo tunakufa.

Kwa Hawa: Hawa aliambiwa atakuwa na uchungu mno na kutawaliwa na mume wake.

MUNGU ANAWAPATIA MAVAZI. MWANZO 3:21

Adamu na Hawa walikuwa wamejifunika majani ya mtini kujaribu kuficha aibu yao, lakini jambo hili halikukubaliwa na Mungu.Badala ya majani waliyokuwa wamejifunika aliwapatia wote wawili vazi lililotengenezwa kutokana na ngozi ya mnyama. Mungu alikuwa na sababu nzuri sana kwa ajili ya hili maana liliwafundisha  Adamu na Hawa kuhusu dhambi. Kwa kuwapatia ngozi ilikuwa sharti mnyama ni lazima achinjwe na damu yake kumwagika. Yote haya yanatuelekeza mbele kwenye kifo chake Bwana Yesu Kristo ambaye kwa ajili ya kifo chake, Mungu alitutengenezea njia yetu ili dhambi zetu ziweze kufutwa au kusamehewa. Wakati mtu anapobatizwa Biblia inasema kuwa mtu huyu anakuwa “amemvaa Kristo” (Wagalatia3:27), kama vile Adamu alivyo vaa vazi alilopewa na Mungu.

KUFUKUZWA KUTOKA KATIKA BUSTANI.MWANZO 3:22-24

Baada ya Mungu kuwaambia Adamu na Hawa kuhusu adhabu watakayopata kutokana na dhambi yao, aliwafukuza kutoka katika bustani ya Edeni.“Ili wasije wakala matunda ya mti wa uzima wakaishi milele”, kwa hiyo Mungu aliwafukuza kutoka katika bustani na akawaweka makerubi upande wa mashariki ya Bustani wakiwa na upanga wa moto uliogeuka huku na huko kulinda njia ya uzima (mistari 22-24).

FUNDISHO KWETU

Nirahisi sana kujaribiwa kutenda mabaya. Kosa la kwanza la Hawa lilikuwa kusikiliza maneno ya nyoka. Ikiwa tunasikiliza ushauri wa wale wasioipeda Kweli,na sisi pia tutamkosea Mungu. Njia pekee ya kuhakikisha kuwa tunamtii Mungu ni kuyaweka maneno yake akili mwetu“moyoni mwangu nimeliweka Neno lako nisije nikakutenda dhambi”(Zaburi 119:11).

Dhambi ililetwa duniani kutokana na kosa la mtu mmoja kukosa utii,na kwa kuwa sisi ni watoto wa Adamu,ni lazima na sisi tufe pia. Lakini Mungu hataki watu wote wafe milele, kwa huruma yake ,aliweka njia ya kusamehewa dhambi zetu kupitia ubatizo katika Bwana Yesu Kristo.

Jifunze kupenda sheria za Mungu na kuziweka ndani ya moyo wako, ili uweze kukua hadi kubatizwa hatimaye kupata karama ya Mungu ya uzima wa milele (Warumi 6:23)

MAELEZO YA ZIADA

Katika Mwanzo 3:15 Mungu anasema juu ya uadui,ambo daima utakuwepo kati ya uzao wa nyoka na uzao wa Mwanamke. Uzao wa nyoka ni wale wote ambo hawajui njia za Mungu na hawapendi Kweli. Uzao wa mwanamke ni wale wote wanaosema Kweli (kama Hawa alivyofanya kwanza.Mwanzo 3:2-3).

Kuna mmoja tu ambaye ametii kwa ukamilifu kwa kuitii Kweli; naye huyo ni Bwana Yesu Kristo. Tunaambiwa kwamba uzao wa nyoka“utamponda kisigino” (Mwanzo 3:15). Hili lilitimia wakati maadui wa Kweli (wayahudi waovu na Warumi ) walipomwua msalabani. Kwa ajili ya utiifu wake mkamilifu kwa Mungu hakubaki kaburini, lakini Mungu alimfufua baada ya siku tatu.

“Mashambulizi ya” nyoka kwa Yesu yalikuwa ni “majeraha” aliyopata ambayo yalipona. Hata hivyo “Uzao wa mwanamke”  “ungeponda kichwa ”cha uzao wa nyoka (Mwa 3:15). Haya yangekuwa mashambulizi ya kifo kwa sababu Bwana Yesu Kristo alifufuka kutoka kaburini ili asife tena, dhambi na kifo vimepoteza nguvu . Ameviharibu na kufungua njia ya uzima wa milele kwa wale wote wanoipenda Kweli na kuweka tumaini katika yeye.

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Ni amri ipi moja ambayo Mungu aliwapa Adamu na Hawa?

2. Ni nani alimshawishi Hawa kuvunja amri hii?

3. Dhambi ni nini?

4. Mungu alisema jambo gani lingetokea ikiwa Adamu na Hawa watatenda dhambi ?

5. Ni jambo gani linalowatokea watu wote kwa sababu ya dhambi ya Adamu na Hawa ?

6. Ni aina gani ya vazi ambalo Mungu aliwapatia Adamu na Hawa?

7. Mungu alifanya nini baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi?

Majibu ya Kina.

1.Ni kwa jinsi gani Adamu na Hawa hawakuitii amri ya Mungu katika bustani ya Edeni?

2. Ni jinsi gani Mungu alivyowaadhibu Adamu na Hawa kutokana na kosa lao?

3.(a)Ni vazi gani kwa ajili ya dhambi ambalo Mungu aliwapatia Adamu na Hawa?

  (b)Je,tendo hili linamwonyesha nani?

Majibu ya Ziada

4.Eleza nini kilitokea baada ya Adamu na Hawa kula tunda la mti?

5.“Mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele”.

       Hii ina maana gani?

6.Eleza maana ya yafuatayo: 

      (a)Uzao wa nyoka

      (b)Uzao wa mwanamke

      (c) huo utaponda kisigino chake; na

      (d) wewe utakiponda kichwa chake

 

Swahili Title
003 KUKOSA UTIIFU KATIBU BUSTANI YA EDENI
English files
Swahili file
African text
CSSA
Translator 1
Carl Hinton
Translator 2
Jonathan Nkombe
Literature type
Sub type
Sub sub type