11. YAKOBO ANASAFIRI
“Sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia”
Kuonyesha jinsi Mungu alivyompenda Yakobo na kumlinda.
Maisha ya Yakobo yalitishiwa na Esau na wazazi wake wakamshauri kukimbia na kuondoka nyumbani kwake, Kwa hiyo alisafiri safari ndefu ambayo ilimchukua Eliazeri miaka mingi aliposafiri kumtafutia Isaka mwanamke. Yakobo naye pia alikwenda kutafuta mwanamke anayefaa ambaye angemsaidia katika Kweli, Isaka alimwambia kwamba hataoa mwanamke mmoja wao miongoni mwa wanawake wa Kanaani kwani hawakuwa na Mungu,walikuwa kama walivyo watu wa ulimwengu wa leo. Miaka mingi ilikuwa imepita kabla hajamwona tena Isaka, wakati huo aliishi na Labani na jamaa yake katika Harani na alifanya kazi kwa bidii kwa ajili ya maisha yake.
Kuna mambo muhimu yaliyotokea ambayo yameendelea kuwa muhimu hata kwa siku hizi, maana katika wakati huu jamaa ya Yakobo ilikuja kuwa taifa la Israeli.
Mwanzo 28: 1 – 22;29: 1 – 30; 31:1 7,24-29
NDOTO KATIKA BETHELI: Mwanzo 28:10 – 22
Yakobo aliondoka nyumbani kwake katika Beer-sheba na kusafiri kuelekea kaskazini. Jua lilipokuwa limekuchwa, alitumia mawe kama mito akalala usingizi,lakini akiwa amesinzia Mungu akasema naye katika ndoto. Katika ndoto zake Yakobo aliona ngazi au kitu cha kupandia, ikiwa imesimamishwa kutoka ardhini hadi mbinguni, na malaika wa Mungu wakiwa wanapanda na kushuka, juu yake na “tazama BWANA amesimama juu yake”. Na Mungu akarudia tena ahadi aliyomwahidi Ibrahimu na Isaka, kwamba “uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi”. Mungu akasema “tazama mimi nipo pamoja nawe mpaka hapo nitakapokufanyia hayo niliyokuambia”(v.15) Mungu alikuwa akimwambia Yakobo kuwa angekuwa pamoja naye na uzao wake mpaka hapo ahadi zitakapotimizwa, Yakobo aliamka akiwa anaogopa kuhusu maono ya ajabu aliyoyaona. Akapaita mahali hapo Betheli, akasema “Hapa si mahali pengine isipokuwa ni nyumba ya Mungu(mstari 17).Alipoamka asubuhi yake, jiwe ambalo alilitumia kama mto akalisisimamisha kama mnara na kulimwagia mafuta juu yake, aliahidi kumwabudu Mungu katika maisha yake yote na aka ahidi kumpatia sehemu ya kumi ya mali yake yote (mistari 19 – 22).
NDOA YA YAKOBO:Mwanzo 29:1-30
Siku iliyofuata Yakobo akasafari na hatimaye akafika nje ya mji wa Harani. Pale penye kisima, alikutana na Raheli akasaidia kunywesha kondoo, na akakaribishwa katika nyumba ya baba yake Labani, nduguye mama yake Yakobo, Rebeka, Labani alikuwa na binti wawili Lea ambaye alikuwa mkubwa na Raheli, mdogo wake. Raheli alikuwa mrembo na Yakobo alimpenda sana alitaka kumwoa na alikubaliana na Labani kumfanyia kazi kwa muda wa miaka saba kama mahari, na alifanya hivyo. Alimpenda sana kiasi kwamba miaka saba kama siku chache sana, lakini muda ulipowadia Labani alimdanganya na kumpatia Lea kama mke wake badala ya Raheli! Kumbuka Yakobo alivyomdanganya baba yake wakati alipomlaghai kuwa alikuwa Esau. Sasa yeye mwenyewe alidanganywa na Labani na wengine pia.Mungu alikuwa akimpa fundisho.Yakobo ilimbidi afanye kazi miaka mingine saba ili kumwoa Raheli, na kwa jinsi alivyompenda alifanya hivyo kwa hiari kabisa. Sasa Yakobo alikuwa na wake wawili baada ya kufanya kazi ngumu kwa miaka kumi na nne kwa Labani. Kila mke wake alikuwa na mjakazi, Zilpa akiwa wa Lea na Bilha wa Raheli. Wote hawa wajakazi wawili wakawa pia wakeze Yakobo na mama wa watoto wake.
Labani alitazamia Yakobo kuchunga mifugo yake kama sehemu ya makubaliano aliruhusiwa kubaki na kondoo dhaifu na ng’ombe.Lakini Mungu alimbariki Yakobo na “mtu huyu akazidi mno kuwa mkuu,akawa na wanyama wengi,na vijakazi,na watumwa,na ngamia,na punda”. Na kwa wakati wa miaka hiyo Yakobo alikuwa na wana wa kiume Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Dani, Naftali, Gadi, Asheri, Isakari, Zabroni na Yusefu.Pia alikuwa na bnti mmoja aliyeitwa Dina. Benyamini, mtoto wake mdogo kuliko wengine hakuzaliwa mpaka baadaye sana. Ingawa Yakobo alikuwa na wana 12 ambao walikuja kuwa baba wa makabila 12 ya Israeli. Jifunze majina yao kwa moyo.
YAKOBO ANAONDOKA KWA LABANI: Mwanzo 31:1 – 7, 24 – 29.
Hatimaye wana wa Labani walimwonea wivu Yakobo na Mungu akamwamwambia Yakobo “Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako nami nitakuwa pamoja nawe” (mstari 3).Wakati Labani hayupo akiwa amekwenda kukata manyonya ya kondoo zake, Yakobo alifunga mizigo yake na akaipandisha juu ya ngamia akaondoka pamoja na wake zake na wana wake.Baada ya siku tatu kupita,Labani alitambua kuwa Yakobo alikuwa amesha ondoka na akanza kumfuatia.
Baada ya juma moja, Labani akiwa safarini akimfuatia Yakobo, Mungu alizungumza naye katika ndoto usiku na kumwonya kuwa ajihadhari jinsi ya kuongea na Yakobo. Kwa hiyo Labani alipomkuta Yakobo, hakumdhuru lakini baada ya majadiliano juu ya jambo hilo, walifanya agano la la makubaliano. Labani akawabariki binti zakena wana wao (mistari 54 – 55) na akawaruhusu waendelee na safari yao kurejea katika nchi ya Kanaani mahali ambapo Isaka aliishi.
YAKOBO ANAJIANDAA KUKUTANA ESAU:Kutoka 32
Yakobo alimwogopa sana ndugu yake Esau kutokana na yale yaliyotendeka miaka mingi iliyopita. Sasa anajianda kukutana naye tena,alielewa kuwa msaada wa Mungu ulihitajika, na hivyo alimlilia Mungu:“Naomba uniokoe sasa na mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau maana mimi namwogopa, asije akanipiga na mama pamoja na wana” (mistari 11). Alitanguliza mbele zawadi za wanyama na vitu kwa Esau, ili kuiondo hasira ambayo huenda alikuwa bado anayo dhidi yake. Kisha usiku ule aliamka alfajiri na kuwapeleka wakeze na watoto wake kuvuka mto Yaboki kwa usalama wao na yeye alibaki peke yake kule.
YAKOBO ANASHINDANA NA MWELEKA NA MALAIKA: Mwazo 32:24 –34
Yakobo “akaa peke yake, na kule alishindana mweleka na mtu hata alfajiri” (mstari24). Huyu alikuwa ni malaika na kumbukumbu zinaelezea mapigano makubwa kati yao mpaka malaika alipomtengua paja lake Yakobo na kumfanya atembee kwa kuchechemea. Malaika alimtaka aondoke lakini hakutaka akisema “Sikuachi usiponibariki”, kisha malaika akamuuliza jina lako nani? Akajibu, “jina langu ni Yakobo” (maana yake mshika kisigino au anayechukua nafasi ya mtu mwingine(mstari 27). Kisha malaika alimwambia kuwa jina lake litabadilishwa kutoka Yakobo kuwa Israeli ikiwa na maana ya mwana wa mfalme akiwa pamoja na Mungu na akambariki palepale.
YAKOBO ANAKUTANA NA ESAU:Kutoka 33:1-11
Asubuhi aliungana na familia yake ng’ambo ya mto Yaboki na kwenda kukutana na Esau.Yakobo alipoona kuwa Esau alikuwa na watu 400, aliweka nyuma familia yake kwa usalama wao akatangulia mbele na akainama mara saba kwa ndugu yake. Kinyume na Yakobo alivyotazamia ulikuwa ni mkutano wa furaha, Esau akamkimbilia mbele na kumkumbatia ndugu yake na wote wakalia kwa pamoja.Esau alikuwa tajiri na hivyo hakuhitaji zawadi alizopelekewa na Yakobo, hata hivyo alizipokea kwa moyo wafuraha na wakawa wote wenye amani. Mungu alimlinda Yakobo na familia yake na kadri miaka ilivyosonga mbele walikuja kuwa taifa kubwa sana la Israeli ambalo kupitia kwake ahadi zitatimizwa.Na tukumbuke kwamba Mungu anatulinda kama alivyofanya kwa Yakobo ili mradi tunaonyesha upendo kwake.
FUNDISHO KWETU
Mara nyingi katika maisha tunapokea sawasawa na jinsi tunavyotenda.Yakobo alimdanganya baba yake katika kupata baraka,akijifanya kuwa mtu alikuwa mwingine.Kama alivyomdanganya baba yake, vivyo hivyo alidanganywa na Labani katika masuala ya Lea. Lakini kadri Yakobo alivyopata matatizo, alijifunza somo kubwa kuwa ni Mungu tu ambaye anaweza kutuokoa katika matatizo ya maisha-yeye asiyeweza kuonekana lakini yeye yupo tayari kutusikiliza na kutusaidia kila wakati.Katika maisha yote ya Yakobo ya kufanya kazi ngumu, alizeeka na kuwa mwenye hekima. Alimtambua Mungu kuwa ndiye tumaini lake la pekee. Alijifunza kusema na Mungu katika sala na kutambua kwamba kila tatizo jipya katika maisha yake lilikuwa bado ni fundisho lingine kwake. Tunaweza kujifunza masomo hayo hayo ambayo Mungu alimfundisha Yakobo kama tunamsikiliza Mungu na kujifunza kufanya yaliyo sahihi.Kweli, uaminifu, uvumilivu na imani katika Mungu yatampendeza baba na Mungu atatusaidia wakati wa shida.
MAELEZO YA ZIADA.
Ngazi au mpandio aliyoiona Yakobo katika maono yake, ilikuwa ni ngazi ya wakati.Ilifika wakati wa Yakobo mpaka muda wa ahadi ya uzao,ambao Bwana Yesu Kristo,atakapotawala katika ufalme wa Mungu na Ibrahimu,Isaka na Yakobo watakaporithi ahadi.Watika wote kwa muda mrefu malaika wa Mungu walimwangalia Yakobo na watoto wake, “wana wa Israeli” malaika ni wajumbe wa Mungu wanaowaongoza na kuwalinda wana wa Mungu katika maisha yao yote (soma Zaburi 34:7)
Yakobo alikuwa mwangalifu sana na matendo ya malaika katika maisha yake (soma mwanzo 48:16) na kama tulivyojifunza katika somo hili hata aliweza kupigana mweleka an malaika kwa sababu alitaka malaika abaki na ambariki.
Hatuwezi kuwaona malaika lakini wanatuchunguza ili mradi tunaenenda katika ukweli. Ni wahudumu wa Mungu au wa watumishi kwa ajili ya wale wote “watakaourithi wokovu” (Waebrania 1:14).Kama tunaendelea kujifunza neno la Mungu na kujaribu kutii amri zake,malaika wa Mungu watatulinda,ili tuweze kushiriki katika baraka za ahadi na Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
MASWALI
Majibu Mafupi:
1. Yakobo aliota ndoto gani alipokuwa amelala juu ya jiwe pale Betheli?
2. Yakobo alimwoa yupi alipokwenda kuishi kwa Labani?
3. Jumla ya wana wote wa Yakobo ni wangapi?
4. Yakobo alipoamua kuondoka kwa Labani,Mungu alimwambia kwenda wapi?
5. Ni nani aliyepigana mweleka na Yakobo pale mto Yaboki?
6. Jina laYakobo lilibadilishwa kuwa jina gani na lina maana ya jina hilo ninini?
7. Yakobo alimgeukia nani alipoogopa kukutana na Esau?
8. Yakobo aliogopa kukutana na Esau tena,lakini ni jinsi gani Esau alivyomsalia?
Majibu Ya Kina
1. Eleza juu ya ndoto ambayo Yakobo aliota wakati alipolala pale Betheli
2. Majina ya wana 12 wa Yakobo ni yapi?
3. Eleza yaliyompata Yakobo pale mto Yaboki?
Majibu ya Ziada
4.(a) Eleza kwa kirefu ndoto ya Yakobo pale mto Betheli
(b) Ndoto hii ilikuwa na maana gani?