CSSA 1-1-13 - JOSEPH - RULER IN EGYPT

Swahili

13. YUSUFU – MTAWALA KATIKA MISRI

Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Yusufu alivyotolewa gerezani na kuinuka kuwa mtawala wa Misri

 

Yusufu kwa uwezo wa Mungu alipotafsiri ndoto ya mnyweshaji mkuu na mwokaji,alimwomba mnyweshaji kumkumbuka mbele ya Farao,lakini mnyweshaji akasahau.Miaka miwili kamili ilipita. Yusufu akiwa gerezani hata hivyo aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu,lakini hakuweza kwenda nje ya nyumba ya gereza, kisha Mungu alichukua hatua ya kumwondoa gerezani na kumpandisha cheo kuwa mtawala wa Misri. Yote hii ilikuwa ni shabaha ya Mungu kwa Israeli.

 

Mwanzo 41 na 42

 

MNYWESHAJI ANAMKUMBUKA YUSUFU:Mwanzo 41:1 – 31

Usiku mmoja Farao,mfalme wa Misri aliota ndoto ya kushangaza,na alikuwa amesimama kando ya mto na tazama ngombe saba waliokuwa wamenona wakipanda kutoka mtoni wakalisha nyasi. Na tazama ngo’mbe wengine saba wakipanda nyuma yao kutoka mtoni wabaya wamekonda wakasimama karibu na wale ng’ombe wengine ukingoni mwa mto na kisha wale ng’ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng’ombe saba walionona, lakini wao wenyewe hawakuweza kunenepa. Farao alishangazwa sana na kustaajabu nini ilikuwa maana ya ndoto hii , usiku ule ule aliota ndoto nyingine,wakati huu aliota masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa na mazuri, ,masuke saba membamba yamekaushwa na upepo wa mashariki yakatokeza baada ya hayo. Kama ng’ombe waliokonda walivyowala wale walionona vivyo hivyo na yale masuke saba membamba yakayala masuke saba makubwa yaliyostawi lakini yenye we hayakuweza kustawi.

 

Asubuhi Farao alifadhaika kwa mawazo, aliwaita waganga na watu wanye busara katika Misri, lakini hakuwako hata mmoja ambaye angeweza kutafsiri maana ya ndoto hizo. Hii ilimfanya Farao kufadhaika zaidi.

 

Hatimaye mnyweshaji mkuu alimkumbuka Yusufu,na jinsi ndoto yake mwenyewe ilivyoelezewa Alifikiri kwamba kijana wa Kiebrania aliye gerezani angeweza kumsaidia mfalme, hakika. Alimweleza mfalme juu ya Yusufu na mara moja Yusufu alipelekwa Ikulu aliulizwa kama angeweza kutafsiri ndoto za maajabu.Yusufu alimjibu Farao “Siyo mimi,Mungu atampatia Farao jibu la amani” (mstari 16).Yusufu alieleza kuwa ndoto zote mbili zilikuwa na maana moja. Ng’ombe saba wanene na masuke saba yaliyostawi vizuri ilikuwa na maana ya miaka saba ya mavuno mazuri na chakula tele katika Misri, na wale ng’ombe saba waliokonda na yale masuke saba ilionyesha ilikuwa na maana ya miaka saba ya njaa itakayofuata.

 

YUSUFU ANAKUWA MTAWALA KATIKA MISRI:Mwanzo 41:32 – 57

Yusufu alimwonya Farao kwamba hakika hii itatokea “kwa sababu Mungu amelithibitisha neno hili” (mstari 32) alimshauri kumchagua mtu mwaminifu na mwenye hekima na kumweka katika nchi ya Misri alipendekeza kuwa mavuno yahifadhiwe katika miaka saba ya wingi wa mavuno ili yatumike wakati wa miaka saba ya njaa katika nchi.

 

Farao na washauri wake walikubaliana kabisa na ushauri huu,waliweza kutambua hekima ya mpango huo na Yusufu mwenyewe aliteuliwa kuwa mtawala wa watu wa Misri!Alipewa nguo nzuri mkufu wa dhahabu na kuvikwa shingoni na pete ya mfalme mwenyewe, alifanywa wa pili katika utwala wa Farao na kupanda katika gari la hadhi ya pili. Farao aliona jinsi mtu huyu Yusufu alivyokuwa na hekima na mcha Mungu na akawaambia watumishi wake “Je tunaweza kumpata mtu kama huyu, mtu ambaye ana roho wa Mungu y ndani yake?”(mstari 38).Katika miaka saba iliyofuata hakika Yusufu alithibitisha kuwa mtawala mwenye hekima.Yusufu “akakusanya nafaka kwa wingi kama mchanga wa bahari”(mstari 49) na kuzihifadhi kwa matumizi ya wakati wa miaka saba ya njaa. Njaa ilipowafikia kama alivyosema Yusufu wanachi walimlilifa Farao kutaka chakula,naye aliwatuma kwa Yusufu.“Enendeni kwa Yusufu,atakavyowaambia fanyeni” (mstari 55).

 

Kwa hiyo Yususfu akajulikana sana katika nchi yote ya Misri. Kwa kufanya hivyo Mungu polepole alikuwa anatimiza kusudi lake kwa wana wa Israeli.

 

NDUGU ZA YUSUFU WANAKWENDA MSRI:Mwanzo 42:1 – 6

Nchi nyingi zilizo pakana na Misri pia zilikumbwa na balaa la njaa na kuwatuma wajumbe wao katika Misri kununua chakula. Hata ikiwa Yakobo naye pia kutoka katika nchi ya Kanaani ambaye alisikia kwamba katika nchi ya Misri kulikuwa na chakual kwa hiyo akawaambia wanawe,“Angalia nimesikia ya kuwa kuna nafaka Misri shukeni huko mkatununulie chakula tupate kuishi wala tusife” (mstari 2).Hata hivyo Yakobo alimwacha nyumbani Benyamini kwa sababu alikuwa bado ana majonzi ya kupotelewa na mwana mwingine wa Raheli, Yusufu (Kumbuka jinsi Yakobo alivyodhani kuwa ameuawa na mnyama wa mwituni. Kwa hiyo wale ndugu kumi walifika kwa mtawala wa nchi “na kusujudu mbele yake” (mstari 6).Hawakujua kwamba huyo alikuwa ndugu yao Yusufu na zile ndoto alizowaambia mapema miaka mingi iliyopita ilikuwa inatimizwa; lakini “Yusufu alikumbuka ndoto alizoota” (mstari 9).Jinsi gani Yusufu alivyongojea kwa uvumilivu miaka yote,akiteseka katika mambo mengi lakini aliendelea kumwamini Mungu. Ilikuwa ni maajabu gani kwa Yusufu siyo tu kuwaona tena ndugu zake, lakini pia kutambua kwamba Mungu alikuwa anayatimiza mambo yale aliyomwonyesha katika zile ndoto.

 

WANATUHUMIWA KUWA WAPELELEZI:Mwanzo 42:7-24

Ingawa Yusufu aliwatambua ndugu zake, hapana shaka wao hawakumtambua. Alionekana kwao kama mtawala wa Misri. Aliamua kuwapima kwa maana alitaka kujua kwa miaka yote hiyo kama walibadilika au walikuwa bado hawana mioyo ya huruma.

 

Kwa hiyo Yusufu alizungumza nao kwa ukatili na kuwauliza walitoka wapi.Wakati walipomjibu kuwa walitoka Kanaani kuja kununua nafaka aliwashutumu kuwa walikuwa wapelelezi.Hawakuwa wakifikiria kwamba wangeambiwa kwa ukatili na wakamwambia yule mtu kuwa walikuwa ndugu kumi wana wa mtu mmoja, katika Kanaani ndugu yao mdogo alikuwa nyumbani pamoja na baba yao na “mmoja hayupo” (mstari 3).Yusufu aliendelea tena kuwashutumu kuwa walikuwa wapelelezi.Mmoja wao lazima abakie Misri na wengine warudi nyumbani kumleta mdogo wao.

 

Walipokuwa wakizungumza wao kwa wao kutaka kujua kwa kina kuhusu yale waliyoambiwa na mtawala wayafanye, hawakujua kwamba Yusufu angeweza kufahamu lugha yao. Hali hii ilimsikitisha Yusufu na hivyo kugeukia nyuma yao ili wasione machozi yake, kisha akamfunga Simeoni na kuwarejesha Kanaani wakiwa na magunia ya chakula.Bado aliwapenda ndugu zake lakini haukuwa wakati mwafaka kujidhihirisha kwao kuwa ni nani.Ilikuwa sasa ni wakati wao kujutia walau kidogo kwa yale waliyoyatenda.

 

WANA WA YAKOBO KATIKA MASHAKA:Mwanzo 42:25-38

Kwa hiyo ndugu tisa walirudi kwa baba yao,Yakobo.Hapana shaka wakiwa njiani walizungumzIa juu ya ukatili wa mtawala wa Misri ulivyokuwa kwao.Waliweza kuwa na wasiwasi juu ya Simeoni na kuogopa sana jinsi gani Yakobo atakavyopokea habari hiyo.

 

Wakiwa njiani kurudi nyumbani, walisimama katika hoteli, na mmoja wao alifungua gunia la nafaka ili kumlisha punda wake alikuta fedha ambazo alikuwa amelipia aliponunua nafaka zikiwa zimerejeshwa katika gunia. Sasa walifadhaika na kuogopa,wakitafakari ni jambo gani litakalompata Simeoni baadaye

.

Hatimaye walipowasili nyumbani, walimhadithia Yakobo mambo yote, “mkaniletee ndugu yenu mdogo, yuke mtu ametwambia,“ndipo nitakapojua kama ninyi si wapelelezi… nami ndipo nitakapowapa ninyi ndugu yenu( yaani Simeoni)”.Kisha wakamwaga chakula kutoka katika magunia ,wakashangaa kukuta fedha ndani ya gunia la kila mmoja na “wakaogopa” (mstari 35).Lakini Yakobo hakuweza kumruhusu Benyamini aondoke “Yusufu hayuko wala Simeoni hayuko, na Benyamini sasa mnataka kumchukua naye… Mwanangu hataondoka pamoja na ninyi” (mstari 36 – 38).

 

Aidha njaa iliendelea katika nchi na Yakobo na familia yake waleweza kuishi kwa nafaka waliyoleta kutoka katika nchi ya Misri.

 

FUNDISHO KWETU

Jinsi gani Yusufu alikuwa tofauti na ndugu zake, aliweza kuona mkono wa Mungu ukifanya kazi katika maisha yake na kwa subira alimngoja Mungu aweze kutimiza mambo yale aliyokuwa amemwonyesha katika ndoto zake. Hekima yake ilijulikana kwa wote na kila mtu aliyemjua, alimheshimu.Ingawa alipata shida katika mambo mengi, hakuweza kuogopa, lakini wakati wote alimwamini Mungu.

 

Na sisi, katika maisha yetu ya kila siku tumtumikie Mungu kwa uaminifu kama Yusufu alivyofanya, wakati wote tukumbuke ahadi zake ambazo amezitoa katika Neno lake, kwa sababu hakika ataweza kuzitimiza.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Ni kwa muda gani Yusufu alikaa ndani ya gereza kabla mnyweshaji mkuu hajamkumbuka?

2. Ni miaka mingapi ya wingi wa mavuno na miaka mingapi ya njaa ilikuwa katika Misri?

3. Ni nani walitumwa na Yakobo katika Misri kutafuta chakula?

4. Ndugu zake Yusufu walifanya nini walipofika mbele ya “Mtawala wa Misri?”

5. Yusufu aliwatuhumu ndugu zake kwa jambo gani?

6. Ni nani aliyebakizwa nyuma katika Misri?

  1. Ni nani ambaye Yusufu alisema ni lazxima afike Misri?

  2. Ndugu walikikuta nini ndani ya magunia yao?

 

Majibu ya Kina

1. Eleza habari kuhusu ndoto mbili za Farao na zilikuwa na maana gani hasa?

2. Elaza jinsi Farao alivyomfanya Yusufu kuwa mtawala wa Misri.

 

Swahili Title
013 YUSUFU – MTAWALA KATIKA MISRI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type