CSSA 1-1-21 - THE GOLDEN CALF

Swahili

21. NDAMA YA DHAHABU

"Wakajifanyia ndama pale Horebu na wakaiabudu sanamu ya kuyeyusha"

 

Shabaha

Ni kuonyesha kwamba wale wasiotii sheria ya Mungu ni lazima waadhibiwe. Mungu aliwatoa wana wa Israeli kutoka Misri hadi mlima Sinai, aliwaita ili wawe Taifa takatifu kwake (kumb 28:9 – 10) na akawapatia amri zilizowafundisha kuwa ni lazima Mungu apate nafasi ya kwanza katika maisha yao. Watu wakakubali wakaahidi kwa hiari yao na kutii (Kutoka 24:7).Hata hivyo,haikuchukua muda mrefu wakawa wamesahau ahadi yao wakaziasi amri mbili za kwanza.Kutoka 32.

 

MUSA ANAKUWA MLIMANI SIKU AROBAINI.Kutoka 24:12 – 48

Safari zote kwa ujumla, Musa alipanda mlimani Sinai mara saba na hata kabla Mungu hajazitangaza amri kumi,Musa alikuwa ameshuka na kupanda mlimani Sinai mara tatu .Na hatimaye musa akapanda mlimani mara ya nne kumwabudu,ndipo akasikia amri za Mungu zikitangazwa.Safari yake ya tano ndipo alipopanda kileleni na kuzipokea mbao mbili za mawe ambazo ziliandikwa amri kumi zilizoandikwa kwa “kidole cha Mungu” na akawa amepewa maelekezo ya namna ya kuitengeneza maskani.Akawapatia Haruni na Huri madaraka ya kuwasikiliza yote ya kusanyiko lote la wana wa Israeli (mstari 14), akaondoka pamoja na Yoshua kama umbali wa nusu ya safari(mstari 13) akapanda mlimani na akawa huko mlimani siku arobaini mchana na usiku. Wakati musa alipokuwa huko, watu walichoka kumsubiri na hivyo wakamwasi Mungu.

 

WATU WAKATENGENEZA SANAMU NA WAKAIABUDU: Kutoka 32:1-6

 

Watu wakaanza kufikiria kuwa Musa hatarudi kamwe, ilikuwa ni kama juma la sita tangu siku waliyomwona akiingia ndani ya wingu lililokuwa limefunika mlima.Ndipo walipoanza tena kufikiria kuhusu Misri na wakayakumbuka mambo waliyoyafanya huko,Walikuwa wajinga jinsi gani kuyafikiria mawazo hayo ambapo ni juma chache zilizopita walikuwa wameahidi kumpenda Mungu tu na kuzitii amri zake. Wakamwendea Haruni, wakamwambia,“katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu” (mstari wa 1). Inatisha kama nini, wao kumsahau mapema sana BWANA,Mungu wa kweli na wa pekee, akiwa amewaonyesha ukuu wa nguvu zake dhidi ya wamisri na akawathibitishia kuwa miungu ya misri haifai kabisa.Ndipo walipozikusanya pete zao za dhahabu na wakamletea Haruni ambaye aliziweka motoni na-“akaziyeyusha na akatoka ndama huyu”(mstari 24). Watu wakaridhika sana na mungu ambaye wangeweza kumwona,lakini wakawa wamevunja amri ya kwanza:“Usiwe na miungu mingine ila mimi” (Kutoka 20:3). Wakawa pia wamevunja amri ya pili “Usijifanyie sanamu ya kuchonga”(Kutoka 20:4).Naye Haruni akawatangazia sikukuu na wakaamka mapema siku iliyofuata na wakatoa dhabihu“na watu wakaketi kula na kunywa na wakaondoka wacheze” (mstari 6)

 

MUSA ANARUDI KAMBINI:Kutoka 32:7-35

Mungu akatazama kutoka mbinguni na akayaona yale ambayo watu walikuwa wanafanya.Akakasirika sana na akamwambia Musa ashuke upesi sana na kwamba atawaangamiza watu hao waovu na afanye taifa jipya kutoka kwa Musa.Musa akamsihi sana BWANA, kwa unyenyekevu,akawaombea wana wa Israeli naye Mungu akamsikia na akakubali kutowatenda kama alivyokuwa amekusudia, kwa hiyo Musa akashuka akiwa ameshika mbao mbili za thamani zenye amri kumi za Mungu. Yoshua, mwaminifu, alikuwa bado anamsubiri na wakiwa wote sasa wakashuka mlimani. Nao walipokaribia kambi, waliweza kusikia kelele za sauti, Yoshua akahofia usalama wa wana wa Israeli.Alifikiria kwamba wameshambuliwa na maadui, lakini Musa alifahamu kuwa kelele ile haikuwa kelele ya vita ilikuwa ni kelele za watu waimbao na kucheza.

 

Fikiria mshangao wao na hasira walipoona kwa macho yao tukio la namna hiyo la uovu. Kwa hasira kuu Musa akazitupa chini zile mbao mbili za mawe mbele ya watu na akazivunja vipande vipande.

 

Musa akamkabiri Haruni, ambaye aliachwa ili awalinde watu hao.Haruni akawalaumu wale watu, lakini Mungu akamkasirikia kila mmoja aliye husika katika uovu ule, hatimaye kwa kuwa maovu ni lazima yazuiliwe, Musa akaondoka pale penye watu na akasimama katika mlango wa kambi na akaita:Ni nani aliye upande wa BWANA? (mstari wa 26). Upesi sana kabila la Lawi likaitikia wito wake kwa amri ya Musa walichukua panga zao na wakaua watu waovu 3000 waliokuwa wamemwasi Mungu.Na ile ndama ya dhahabu ikateketezwa motoni, ikasagwa kuwa vumbi na kisha mavumbi yakatupwa ndani ya maji na watu wakalazimishwa kuyanywa maji hayo na kama vile watu walivyokufa kwa upanga, wengi wakafa kwa tauni ambayo Mungu aliituma kama adhabu. Ilikuwa ni hasara ya ajabu kwa wana wa Israeli lakini yenye kuwa na fundisho kuu.

 

FUNDISHO KWETU

Ahadi iliyowekwa lazima itimizwe, wana wa Israeli waliahidi kumpenda na kumtumikia Mungu peke yake.

 

Hawakuweza kutimiza ahadi hii, na wakaadhibiwa. Ni lazima tujifunze kutimiza ahadi tunazoweka, haijalishi ni ndogo kiasi gani, iwe ni nyumbani au kazini. Kuzitunza ahadi ni tabia nzuri ya kuanza kujizoeza wakati tunapokuwa vijana, maana tunapokuwa wazee kuna ahadi ya Mungu ambayo anataka tuitimize ya kumpenda na kumtumikia yeye katika siku za maisha yetu.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Hebu fikiria tabia ya ajabu ya Musa aliyoionyesha katika fundisho hili, alikuwa amefundishwa na Mungu akiwa mchungaji kwa miaka arobaini na sasa alikuwa anaonyesha sifa za mchungaji wa kweli ambaye anajiandaa “kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.

 

Mungu akasema atawaangamiza watu waasi kwa muda mfupi na kuliinua taifa la waaminifu kupitia Musa. Lakini Musa akawaombea kwa nguvu ya imani na msamaha. Hata akaona ni heri jina lake lifutwe kwenye Kitabu cha uzima kama Mungu hatawasamehe wao (Kutoka 33:32). Mungu akamwonyesha kuwa mtu atendaye dhambi ni lazima aadhibiwe kama ilivyo katika Wakolosai 3:23 – 25 maana adhurumaye atapata mapato ya udhalimu wake, wala hakuna upendeleo.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Musa alimwachia nani madaraka awasikilize watu wakati alipopanda kwenye kilele cha mlima?

  2. Musa alifuatana na nani mlimani?

  3. Ni kwa muda gani Musa alikuwepo kule mlimani?

  4. Musa alikwenda mlimani kupokea nini?

  5. Je,watu walifanya nini Musa alipokuwa mlimani?

  6. Ni amri zipi mbili ambazo watu walizivunja wakati Musa alipokuwa mlimani?

  7. Kwa hasira Musa alifanya nini alipouona uovu wa watu?

  8. Tunajifunza nini kutokana na fundisho hili?

 

Majibu ya Kina

 

Watu wakamsubiri Musa kushuka mlima Sinai.

1.Eleza habari ya ndama ya dhahabu

2.Ni jinsi gani Mungu alivyowaadhibu watu kutokana na uovu wao?

 

Majibu ya Nyongeza

 

3.Ni jinsi ganiukuu wa Musa unavyoonekanaalipowaombea wana wa Israeli msamaha?

4.Ni jinsi gani wana wa Lawi walivyoonyesha utayari wa kumtumikia Mungu?

 

Majibu ya Nyongeza

 

5.Ni kwanini Mungu aliwaacha watu wake wapate njaa na kiu kabla hajawapatia chakula na maji?

6.Ni nani ambaye ni mkate wa uzima?

7.Yesu,ni mfano wa Taifa la Israeli;alikuwa na njaa sana jangwani.

8.Tabia ya Yesu ilitofautianaje na ile ya wana wa Israeli?

 

Swahili Title
021 NDAMA YA DHAHABU
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type