CSSA 1-1-23 - THE FURNITURE OF THE TABERNACLE

Swahili

23. VIFAA VYA MASKANI

"Ni maelekezo ya vifaa vya Maskani, na mtumizii yake na mahali vilipowekwa"

 

Shabaha

 

Katika somo hili tutazingatia vifaa muhimu sita, vinne ndani ya Maskani na viwili nje ya maskani, katika Hema iliyoitwa hema ya nje, au ua wa Hema.

 

Aina sita za vifaa ni:

  1. Madhabahu ya Sadaka ya kuteketezwa

  2. Birika la shaba

  3. Kinara cha Taa cha dhahabu

  4. Meza ya mikate ya Wonyesho

  5. Madhabahu ya kufukizia uvumba na

  6. Sandukuk la Agano (Kutoka 37 na 38)

 

A: VIFAA VILIVYOKUWA NDANI YA UA WA NJE

 

MADHABAHU YA SADAKA YA KUTEKETEZWA: Kutoka 38:1-7

Upande wa Mashariki mwisho wa Hema kulikuwa kwanza na madhabahu ambayo iliitwa madhabu ya sadaka ya kuteketezwa ilitengenezwa kwa mbao za mshita,na zikafunikwa kwa shaba.Ilikuwa na wavu wa shaba uliowekwa chini ya kingo kuizunguka pande zote ukawa katikati ya hiyo madhabahu ili moto uweze kuchoma kwa urahisi zaidi na juu ya madhabahu hiyo kulikuwa na pembe nne, kila ncha juu ya madhabahu ilikuwa na pembe moja, na hizo pembe zilikuwa za kitu kimoja na zilifunikwa kwa Shaba.

 

Mnyama aliyetolewa dhabihu aliwekwa juu ya Madhabahu na kufungiwa kwenye zile pembe za madhabahu. Moto chini ya madhabahu uliwashwa na Mungu (Mambo ya Lwi 9:24) ambaye aliagiza kwamba “Moto utatunzwa daima juu ya madhabahu daima, usizimike” (Mambo ya Walawi 6:13).Kulikuwa na mfereji uliochimbwa chini ukielekea hadi madhabahu kubwa Upande wa Kusini. Pia kulikuwa na masufuria, mabakuli na uma zake, vilivyotumika kwa dhabihu za wanyama na Mashariki vyombo vyote hivi pia vilikuwa vya Shaba.

 

(A) BIRIKA LA SHABA: Kutoka 30:18-21

Katikati ya madhabahu ya kuteketezea dhabihu na mlango wa Maskani kulikuwa na Birika. Lilikuwa ni sufuria kubwa lilitengenezwa kwa shaba ambalo makuhani waliosha mikono yao na miguu yao, wakati wa utumishi wao, iwe ni katika ua wa hema au Pataktifu.

 

Kuoga katika maji ilikuwa ni muhimu sana. Mungu alitaka watumishi wake wawe safi miili yao na mawazo yao pia. Kuosha kwa maji kuna safisha miili yetu, lakini kusafisha mioyo yetu na mawazo yetu tunatakiwa tuchukue Neno la Mungu (Soma Yohana 15:3 na linganisha na Waefeso 5:26 na Zaburi 119:9).

 

(B) VIFAA NDANI YA PATAKATIFU

Kulikuwa na vitu vya aina 3 katika (chumba), hema hii iliyoitwa Patakatifu.

 

KINARA CHA TAA CHA DHAHABU:Kutoka 37:17-24

Ukishapita pazia ya pili ya Maskani upande wa kushoto wa chumba hiki kilichoitwa Patakatifu Papatakatifu kuliwa na kinara cha Taa kilichotengenezwa kwa dhahabu safi. Ilikuwa na mhimili katikati, na kilikuwa na matawi sita, matawi matatu ya kinara yalikuwa upande mmoja na matawi matatu mengine upande wa pili yaliyokuwa yamepinda kuelekea juu na tawi moja katikati na jumla zikawa taa saba. Taa hizo zilijazwa mafuta ya mzeituni safi yaliyoletwa na wana wa Israeli na zilitakiwa zijazwe mafuta jioni na asubuhi (Kutoka 27:20-21, Walawi 24:2). Chumba hiki kilikuwa na giza na mwanga wa taa hii ndiyo uliommulikia kuhani ambaye aliigia kila siku kutimiza shughuli za zamu yake.

 

Yesu akasema alikuwa ni “nuru ya Ulimwengu” na Mungu anataka sisi tuwe nuru inayoangaza, nuru iangaze matendo yetu mema yanayotoka kwa mtu anayempenda Mungu (Mathayo 5:14-16). Neno la Mungu ni taa inayotuongoza sisi. (Zaburi 119:105)

 

MEZA YA MIKATE YA WONYESHO : Kutoka 37:10-16

Hii ilikuwa ni Meza iliyotengenzwa kwa mbao ikafunikwa kwa dhabahu na kupambwa au ikafunikwa kwa dhahabu safi pande zote. Ilikuwa upande wa kulia wa chumba. Juu ya meza hii iliwekwa mikate isiyotiwa chachu kumi na mbili. Mikate hii iliitwa “Mikate ya wonyesho” ilipangwa kwa mistari miwili na juu yaliwekwa mabakuli madogo mawili yaliyojaa uvumba. Na kila juma makuhani walikula mikate ya wonyesho. Uvumba ulitumika kwenye madhabahu ya Uvumba, na mikate mipya na Uvumba viliweka tena.

 

Mikate kumi na mbili iliwakilisha kazi ya makabila kumi na mbili ya wana wa Israeli. Walikuwa wamepanda ngano, na Mungu akawa ameikuza vizuri na ilipokomaa wakaivuna na kutengeneza mikate. Mungu alikuwa amebariki kazi zao.Atatubariki na sisi pia tukifanya kazi kwa bidii katika kumtumukia,tukijitahidi kulifahamu Neno lake na kufanya bidii kuishi maisha ya uaminifu.

 

MADHABAHU YA DHAHABU YA KUFUKIZA UVUMBA: Kutoka 27:25-28

Mwisho wa Chumba cha Patakatifu pa patakatifu karibu na pazia inapotenganisha vyumba au pazia na hekalu kulikuwa na madhabahu ya dhahabu kwa ajili ya kufukizia uvumba. Ilikuwa ni ndogo sana kuliko ile madhabahu iliyokuwa ua wa maskani ilitengenezwa kwa mbao za mshita na ikafunikwa dhahabu. Ilikuwa na pembe nne na meza hiyo ikapambwa au kufunikwa dhahabu pande zote. Makuhani walichoma ubani hapa asubuhi na jioni kwa mkaa wa moto unao tolewa katika madhabahu ya kuteketezwa. Wakati uvumba ulipowekwa juu ya moto wa makaa ukatoa harufu nzuri ya kupendeza na Mungu alipendezwa na harufu hiyo ya manukato ilipopaa juu. Uvumba ulifukizwa mara mbili kwa siku, na Luka 1:8-10 anasema ulikuwa ni muda wakusali, wakati tunasali, maneno yetu yanafika mbinguni kama harufu ya manukato yanayompendeza BWANA (Zaburi 141:2).

 

(C) VIFAA NDANI YA PATAKATIFU PA PATAKATIFU

Chumba hiki kilikuwa chumba maalumu ambacho kuta zake zilifunikwa wa dhahabu. Hakuna mtu ambaye angeona chumba hiki maana pazia lilikitenga na chumba cha Patakatifu. Chumba hiki kilikuwa na vyombo vya utukukufu. Ilikuwa ni hapa ambapo Mungu alikaa na sauti yake iliposikika.

 

Ni kuhani Mkuu pekee yake aliyeruhusiwa kuingia Patakatifu Pa Patakatifu na mara moja kwa mwaka, siku ya upatanisho. Mwaandalizi maalumu yaliandaliwa kwa ajili ya siku hii maalumu ili kuhani Mkuu aweze kuingia nakuongea na Mungu.

 

SANDUKU LA AGANO: Kutoka 37:1-9

Hili lilikuwa sanduku rahisi lililotengenezwa kwa mbao za mshita, lilifunikwa kwa dhahabu ndani na nje. Kulikuwa na taji juu na mfuniko wa sanduku ulitengenezwa kwa dhahabu safi na umbile la viumbe, vinavyoitwa kerubi viliwekwa pande mbili za kifuniko vilivyotengezwa kwa dhahabu safi pia. Mfuniko huu wa sanduku uliitwa “Kiti cha Rehema”. Utukufu wa ajabu wa Mungu uliangaza pale. Lakini utukufu huo aliuona Kuhani Mkuu pekee yake mara moja kwa mwaka alipoingia kule akiwa na damu ya dhabihu ambayo aliinyunyiza kwenye “Kiti cha Rehema”. Pale penye Kiti cha Rehema Mungu alinena Ikiwa ni ishara ya msamaha wa dhambi za wana wa Israeli. Kiti cha Rehema ilikuwa ni sehemu ya Mungu ya kukutania na wana wa Israeli (Kutoka 25:21-22) .

 

Mungu alimwagiza Musa kuweka vitu vifuatavyo katika Sanduku la Agano:-

 

  1. Mbao mbili za mawe zenye kuandikwa Amri Kumi.

  2. Kopo la dhahabu lenye mana zilizohifadhiwa na Mungu kwa miaka mingi kuwakumbusha wana wa Israeli ulinzi wa Mungu kwao walipokuw ajangwani.

  3. Fimbo ya Haruni iliyochipuka (Hesabu 17:10)

 

FUNDISHO KWETU

Katika maagizo yote ya Maskani na vifaa vyake kama tulivyoona kwamba Mungu aliwapatia sawa sawa jinsi ya kutengeneza na hata namna ya kuvitumia vyombo hivyo.

 

Maagizo hayo yalitakiwa kufuatwa ili Ibada ya wana wa Israeli iweze kukubaliwa na Mungu. Kwa namna moja vile vile Mungu ameeleza maagizo yaliyowazi kabisa katika Neno lake, jinsi tunavyotakiwa kumwabudu siku hizi. Na tusome Biblia kwa uangalifu sana ili tuweze kujifunza njia zake sasa, maana Yesu alisema “Wale wamwabuduo ni lazima wanamwambudu katika roho na kweli”.Yohana 4:24.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Taja vifaa viwili vilivyokuwa ua wa nje wa maskani?

  2. Mapembe ya madhabahu yalitumika kwa ajili ya nini?

  3. Birika la shaba lilitumika kwa ajili ya nini?

  4. Ni nini kinachosafisha mioyo yetu na mawazo pia?

  5. Taja vyombo 3 vilivyowekwa Patakatifu?

  6. Ni nani aliyeleta mafuta ya Kinara cha Taa?

  7. Ni nani aliyesema “Mimi ni Nuru ya Ulimwengu?”

  8. Ni mikate mingapi iliyowekwa pale?

  9. Makuhani walipata wapi moto wa kufukizia uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba?

  10. Kulikuwa na nini ndani ya Patakatifu Pa Patakatifu?

  11. Kiti cha Rehema kilikuwa cha nini?

  12. Sanduku la Agano lilitengenezwa kutokana na vitu gani?

  13. Walipokuwa wanasali walifanya nini wakati uvumba ulipokuwa unafukizwa?

  14. Ni sehemu gani katika maskani ambapo utukufu wa Mungu ulionekana?

 

Majibu ya Kina

  1. Eleza madhabahu ya kuteketezea dhabihu ilifananaje na ilitumika kwa ajili ya nini?

  2. Fafanua vifaa vitatu vya vyombo vya thamani vilivyokuwa katika Patakatifu katika maskani?

  3. Sanduku la Agano lilifananaje? Ni vitu gani vitatu vilivyokuwemo ndani ?

 

Majibu ya Nyongeza.

  1. (a) Fafanua aina tatu ya vyombo vya thamani vilivyowekwa Patakatifu ndani ya maskani?.

(b) Ni fundisho gani tunalolipata kutokana na vitu hivi vitatu?

  1. Taja aina sita za vyombo vya thamani katika ua wa ndani,Patakatifu na Patakatifu Pa Patakatifu na uchore mchoro kuonyesha kila kimoja kilipowekwa.

 

 

Swahili Title
023 VIFAA VYA MASKANI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type