CSSA 1-2-03 - REBELLION IN ISRAEL

Swahili

28 . UASI KATIKA ISRAELI

Nchi ikafunua kichwa chake na kuwaweza”

 

Shabaha: Kuonyesha kwamba Mungu atawaadhibu wale wasiofuata njia yake.

 

Muhtasari:

Kwa sababu walitenda uovu, na kutokuwa na Imani katika Mungu, Waisraeli hawa kuhuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi. Wakawa wamerudishwa nyuma jangwani wakahukumiwa kuzungukazunguka zaidi ya miaka 38 hadi hapo wale waliotenda dhambi juu ya BWANA watakapokuwa wamekufa (kumb. 1:35-37).

Hesabu: 16 na 17

 

KORA ANAPANGA UASI: Hesabu 16:1-14

Kora alikuwa ndugu yake mdogo wa kwanza wa Musa na Haruni, Ishari, Baba yake, na Amramu, Baba yake Musa na Haruni, hawa wote walikuwa wana wa Kohathi (Hes. 3: 19) (1Mambo ya Nyakati 6:3,18). Kwa sababu hii Kora alijiona kuwa na haki sawa ya kuwa Kiongozi au kuhani Mkuu wa Israeli. Alikuwa na marafiki kati ya Walawi, hasa aliwahitaji wengine waweze kumsaidia katika njama zake. Miongoni mwao ni katika kabila la Rubeni alipata wafuasi pia, akiwemo Dathan na Abrahamu, ambao waliungana na watu 250 waliokuwa wakuu wa mkutano (Hesa:16:2).

 

Kora alisema kuwa mkutano wote wa BWANA ni "Mtakatifu" au (Waliotengwa) na aliona hakuna sababu ya Musa na Haruni kuwekwa mbele kuliko wengine, lakini ukweli ni kuwa alikuwa na wivu kwa ajili ya nafasi zao na alikuwa anataka yeye kuwa kiongozi.

 

 

JINSI UASI ULIVYOANGAMIZWA: (Hesa: 16:15-40).

Musa alikasirika sana aliposikia maneno ya Uasi ya Kora. Aliwaita wana wa Israeli, kukusanyika mbele ya Hema ya kukutania siku iliyofuata. Alimwagiza Kora na wale wakuu 250 pia na Haruni, walete vyetezo. Vyetezo zilikuwa sahani za shaba ambazo zingewekewa moto juu ya ubani uliota harufu inayopendeza.

 

Kwa hiyo siku iliyofuata wakuu walifika pamoja na vyetezo wakasimama karibu na mlango wa Hema ya kukutania. Kora pia alifika akiwa amekutanisha watu kinyume cha Musa na Haruni.

Dathani na Abiramu na familia zao walikataa kufika kwenye Hema ya kukutania ambapo musa aliwaambia wafike.

 

Walibakia katika masikani zao. Watu walingojea mbele ya Hema ya kukutania ili kuona jibu la BWANA litakuwaje.

 

Ghafla utukufu wa BWANA ukawatokea mbele ya kusanyiko lote na sauti ikamwamuru Musa na Haruni waondoke kati ya mkutano ili wasiangamizwe. Musa naHaruni wakapomoka kifudifudi mbele za Bwana na kumsihi ili asiangamize mkutano wote kwa ajili ya waovu wachache. Mungu akasikia maombi yao akamwambia Musa awaambie mkutano waondoke penye hema za watu hao waovu; vinginevyo wataangamizwa pamoja nao. Wengi walimtii Musa na hivyo walijitenga ,hata na watoto wa Kora pia waliondoka, kuonyesha kuwa hawakubaliana na uasi wa maneno ya baba yao. Tunaambiwa hayo katika Hes 26:11 ya kwamba hawakuangamizwa pamoja na baba yao.

 

Kisha Musa akawaambia mkutano (mst 28). Kama hawa waovu wakifa kifo cha kawaida ndipo mkutano wangejua kuwa Musa hakutumwa na BWANA, lakini kama "ardhi itafunua kinywa chake na kuwameza watu wote",ndipo mkutano wangejua ulikuwa ni mkono wa MUNGU na Musa alikuwa ametumwa na BWANA.

 

Basi ilikuwa hapo Musa alipomaliza kusema, naye BWANA akatenda. Ardhi ikafunua kinywa chake na ikawameza waasi na vyombo vyote walivyokuwa navyo.

 

Wakuu 250 walikuwa viongozi katika wale waasi hawakujiepusha na hasira ya BWANA. Moto kutoka kwa BWANA uliwaangamiza wala hakuna kilichobakia isipokuwa vile vyetezo vya shaba. Na Mungu akaagiza vyetezo hivyo vifuliwe ili viwe kifuniko cha madhabahu ya kuteketezea. Huu ulikuwa "ukumbusho kwa wana wa Israeli ya kuwa Haruni na wanae ndio wanaopaswa"kumkaribia BWANA na kufukiza uvumba mbele yaBWANA (mst 40).

UASI ZAIDI : Hesabu 16: 41-60

 

Hata hivyo, wana wa Israeri hawa kupata fundisho. Mkutano wote waliendelea kukasirika na kuasi. Siku iliyofuata walimnung’unikia Musa Haruni, utukufu wa BWANA ukaonekana ukiwa umefunika Hema na Bwana akasema na Musa na Haruni, akasema alitaka awaangamize mkutano wote mara moja.

 

Ghafla Mungu akatuma tauni ya watu 14,700 wakauawa kutokana na dhambi zao. Hadi hapo Musa na Haruni walipoanza maombezi kwa niaba ya mkutano naye BWANA akazuia tauni.

 

FIMBO YA HARUNI ILIYOCHIPUA

ISHARA INAONYESHA CHAGUO LA MUNGU KUHUSU KUHANI MKUU. Hesabu 17

 

Bwana alitoa ishara nyingine nyingi zaidi kuonyesha kuwa ndiye aliyemchagua Haruni kuwa KUHANI MKUU, kuwa juu ya kiongozi wa nyumba ya Waisraeli; mkuu wa kila kabila wote walitakiwa kila mmoja kuleta fimbo kwa Musa na Musa alipaswa "kuandika jina la kila mmoja katika fimbo yake; na katika fimbo ya kabila lawi aandike jina la Haruni …nawe utaziweka katika Hema ya kukutania mbele ya huo ushahidi…na itakuwa ya mtu yule nitakaye mchagua fimbo yake itachipuka" (mst 2-5). Mtu yule ambaye ni chaguo la BWANA aliweza kutambulika kwa njia muujiza -fimbo yake kwa ghafla "ingekuwa hai (kuwambichi)",kwa hiyo fimbo zote ziliwekwa katika Hema ya kukutania kama BWANA alivyo kuwa ameagiza. Sikuya pili Asubuhi Musa aliingia katika Hema ya kukutania na tazama ile fimbo ya Haruni ilikuwa imechipuka,na kutoa maua na kuzaa malozi mabivu,naye akazileta hizo fimbo zote mbele ya wana wa Israeli wote!Lakini fimbo zingine zote zilibakia vile vile zikiwa zimekufa (kavu kama mwanzo). Kwa muujiza huu BWANA aliwaonyesha wana wa Israeli kwamba Haruni ndiye kuhani wake mkuu.

 

Haruni alichaguliwa ili kufanya "kazi ya kuweka ulinzi wa patakatifu na kazi ya madhabahu".Na fimbo ile iliyochipua ilitunzwa ili "iwe ishara juu ya hawa wana wa maasi"na kisha iliwekwa ndani ya sanduku la Agano(waeb 9:4).

 

FUNDISHO KWETU

Mungu anawapenda wote wanaojitahidi kufanya vyema huduma ya Bwana,haijalishi ni kazi ndogo kiasi gani. Hawa ni wanaomfurahisha ,lakini hakuna nafasi ya roho ya wivu ya akina Kora , Dathani na Abiramu. Wale wanampenda na kumtii Mungu sasa watakuwa wafalme na makuhani katika Ufalme wake, wakati mwana wake, Yesu Kristo, atakaporudi kuitawala dunia yote.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Fimbo ile kuchipuka linatufundisha sisi ukweli kuhusu ufufuo wa wafu . Ilikuwa ni fimbo iliyokufa (iliyokauka) vile vile kama fimbo zingine,lakini Mungu aliiwezesha ghafla kupata uzima. Hili lina tuelekeza wakati wa kurudi kwa Bwana wetu Yesu Kristo hapa duniani ,wakati "tarumbeta itakapolia,nao wafu watafufuka" wakati huo, wale watakao kuwa wamefufuka kutoka wafu na wale watakaokuwa hai, wanaofahamu Injili,watahukumiwa na Bwana Yesu Kristo. Wale watakaokuwa waaminifu miongoni mwao watabadilika (1 wakor 15:52). Maana miili yao ya kufa itabadilika kuwa miiliya kutokufa, haitakufa kamwe,kama vile Yesu na malaika (Luka 20:35-36). Nitumaini la utukufu namna gani kwetu ikiwa tunakuwa waaminifu! Kwa hiyo,kilatunapouna mti wa mlozi ukiwa umetoa maua wakati wa mwisho wa majira ya baridi. Inatukumbusha kuja kwa Bwana Yesu Kristo na Ufufuo.

 

MASWALI (Majibu mafupi)

  1. Kora alikuwa nani?

  2. Kora alisema nini kuhusu Musa na Haruni?

  3. Ni akina nani walioungana na Kora aliposema kinyume na viongozi waliochagliwa na Mungu?

  4. Mungu aliwaambia Musa na Haruni wafanye nini wakati Kora,Dathani na Abiramu walipofanya uovu kinyume chao?

  5. Ni jambo gani liliwatokea Kora,Dathani na Abiramu?

  6. Ni jambo gani liliwatokea wale wakuu 250 waliokuwa wamefuata Kora,Dathani na Abiramu?

  7. Mungu alimweleza Musa avifue vyetezo vya shaba viwe nini?

  8. Kwa nini siku iliyofuata wana wa Israeli walikusanyika?

  9. Ni ishara ipi Mungu aliyotoa kumwonyesha Haruni kuwa alimchagua kuwa Kuhani Mkuu?

 

Majibu ya Kina

1.(a) Eleza ni kwa jinsi gani Kora,Dathani na Abiramu walivyoleta taabu katika kambi ya wana wa Israeli?

(b) Je,Mungu aliwaadhibuje?

2.Ni namna gani Mungu alivyoonyesha jinsi ya kumchagua Kuhani Mkuu wa Israeli walipokuwa jangwani?

3.Ni adhabu gani waliyopata waasi?

(a) Kora,Dathani na Abiramu

(b) Wakuu 250

(c) Wana wa Israeli wasiotii miongoni mwa Waisraeli?

 

Majibu ya Nyongeza.

4.Eleza maana ya fimbo ya Haruni kuchipuka

 

Swahili Title
028 UASI KATIKA ISRAELI
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type