CSSA 1-2-05 - MOSES

Swahili

30. MUSA

"Jicho lake halikupofuka,wala nguvu zake mwilini hazikupunguka"

 

Shabaha

Kuonyesha kuwa hatupaswi kuhuzunika wala kulalamika bali tuwe na shukrani kwa baraka tunazopewa na Mungu.

Mungu anataka tumtii na tuwe na imani na tumtumaini.

 

Muhtasari

Musa alizaliwa ili awakomboe watu wake utumwani katika Misri na kuwaleta katika Nchi ya Ahadi. Hata hivyo,tumeona katika somo lililopita kwamba Mungu hakumruhusu Musa kuwaongoza wana wa israeli kuingia katika nchi hiyo kwa sababu hakumpatia Mungu utukufu wakati maji yalipotoka katika Mwamba kule Kadeshi.

 

Ukiacha hili;Musa alikuwa mtumishi wa Mungu,mkweli na mwaminifu. "Wala hawajainuka tena katika israeli nabii aliyekuwa kama Musa"(Kumb 34:10).kwa nafsi yakehakuomba lolote,isipokuwa tu alitaka kuona ahadi za Mungu alizowaahidi Waisraeli zikitimia. Kumbukumbu la Torati 30 na 34

 

UJUMBE WA MWISHO WA MUSA KWA WANA WA ISRAELI. Kumb.29,30 na 31

Musa alikuwa na miaka 120 na Mungu akamwambia kuwa mwisho wa maisha yake umekaribia. Alimsihi BWANA ili amruhusu kuingia katika Nchi ya Ahadi,lakini aliruhusiwa tu kuiona nchi Ahadi akiwa juu ya kilele cha mlima Nebo,kilicho katika nchi ya Moabu Hes 27;12-14); kumb 32:49). Kati ya watu wote waliotoka misri(yaani, "watu wote wa vita" Hes14:29; kumb 2:16) Isipokuwa Yoshua na Kalebu wataingia katika Nchi ya Ahadi. Wengine wote walikufa jangwani. Yoshua akawaongoza watoto wao ,wakawa wamekua nao wakaimiliki (Kumb 1:34-39: 3:23-28).

 

Waisraeli wakafika mpaka wa Kanaani na Mungu akamwambia Musa afanye agano na hiki kizazi kipya kule. "Leo mmesimama nyote mbele za BWANA, Mungu wenu," Musa akasema, "ili uingie katika agano la BWANA, Mungu wako... apate kukuweka leo uwe taifa kwake naye apate kuwa Mungu kwako, kama alivyokuambia na kama alivyowaapia baba zako, Ibrahimu na Isaka, na Yakobo".(Kumb. 29:10-13).Kama wangeishi kwa kutii amri za Mungu .Mungu angewabariki, lakini kama wangemwasi laana nyingi zingewajilia."Nimekuwekea mbele yako uzima na mauti,baraka na laana". Musa akawaambia,"Basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako kumpenda BWANA Mungu wako, kuitii sauti yake" (Kumb. 30:19-20)

 

Wakiwa mkutano wote Waisraeli wamesimama pale, Musa akawaambia kwamba yeye hatavuka mto Yordani pamoja nao hata sasa Mungu hatawaacha. BWANA, Mungu angevuka mbele yao na kuwaangamiza mataifa ya Kanaani.Yoshua ndiye alikuwa kiongozi mpyaaliyechaguliwa na Mungu.Mbele ya kusanyiko lawana wa Israeli Musa alimthibitishaYoshua. "Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa nawe utawarithisha. Naye BWANA, yeye ndiye atakaye kutangulia. Hatakupungukia wala kukuacha…" (Kumb.31:1-8)

 

Musa akaandika katika kitabu cha torati aliyopewa na BWANA. Na hii ilitunzwa na Makuhani, na Makuhani waliisoma kila mwaka wa saba, wakati wa sikukukuu ya vibanda (Kumb. 31:9-13, 26). Hili liliwakumbusha agano kati yao na Mungu. Mungu akamwambia Musa kuandika wimbo na awafundishe wana wa Israeli; ili iwe rahisi kukumbuka matendo ya ajabu BWANA aliyoyatenda kwa ajili ya Taifa lao. (Kumb 31:19;32:46-47). Wana wa Israeli hawakutakiwa kusikiliza kwa bidii tu sheria ya Mungu na kutii bali pia walitakiwa kuwafundisha watoto wao kwa bidii siku zote za maisha yao, ili waweze kujifunza kumcha na kumtukuza BWANA (kumb. 6:6-7).

 

KIFO CHA MUSA - KIONGOZI MPYA ANACHAGULIWA: Kumb. 34

Kiongozi mkuu mwingine wa Israeli - Haruni Kuhani Mkuu, na Miriam, nabii mke walikuwa wamefariki katika miaka 40 ya Waisraeli katika kutanga tanga (kuzungukazunguka). Sasa, mwishoni mwa mwaka huo, muda ukawaumefika Musa kufariki pia. Wote wamelala katika makaburi yao wakisubiri kurudi kwa Bwana Yesu Kristo atakaye wafufua kutoka wafu. (Rejea kitabu cha Mwalimu wa shule ya Jumapili swali Na. 132).

 

Ingawaje Musa alikuwa na miaka 120 mwili wake haukupungua nguvu wala jicho lake halikupofoka ingawaje kazi yake ilikuwa imekwisha. Mungu akamwambia Musa apande mlima Nebo na akiwa juu ya mlima mrefu angeweza kuiona mbele yake nchi ya ahadi jinsi ilivyo.

 

Mungu akasema, "Basi nimekuonyesha kwa macho yako lakini hutovuka huko" (mist 1-4). Kwa hiyo Musa mtumishi wa BWANA, akafa huko katika nchi ya Moabu"na malaika wakamzika katika bonde lakini "hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo" (mist 5-6). Wana wa Isareli walipofahamu kuwa Musa amefariki walilia na kumwombolezea siku thelathini.

 

Musa kama wengine wengi, alikufa katika imani, wasijaipokea ahadi, bali wakaziona tokea mbali (Waeb:11:13). Ukweli ni kwamba hakukanyaga ardhi ya nchi ile, katika maisha yake halikuwa jambo la muhimu. Alikufa katika matumaini yake ya urithi ujao na wenye utukufu.

 

Mungu alimchagua Eliazeri, mtoto wa Haruni kuwa Kuhani Mkuu mpya na sasa Israeli walikuwa wakiwaangalia viongozi wao wapya, Yoshua (mst 9), awaelekeze yale wanayopaswa kuyafanya.

 

FUNDISHO KWETU:

Musa alikuwa ni mtu mpole sana na mnyenyekevu. Katika maisha yake yote alidumu katika kuyavumilia majaribu na mateso yote yaliyompata (Hes: 12:3). Maisha ya nabii mkuu yanaweza kutusaidia katika maonyo mengi.

 

Wakati wana wa Israeli, na vilele hata wale wa familia yake, wanapomuonea na kumnenea kinyume, aliyastahimili yote kwa kujizuia (isipokuwa mara moja angalia somo la 4), lakinisehemu zingine zote alisema polepole na kwa busara matatizo yake yote alimwachia Mungu. Mungu hafurahii sisi kuwa na ugomvi. Mungu anataka tuwe wenye busara na wapole, na siyo kushiriki mazungumzo na kusema maneno ambayo hatimaye tutayasikitikia. Tunapaswa kujifunza onyo la Mtume Yakobo 1:9-20.

 

KWA UKUMBUSHO ZAIDI

MUSA ALIFANANA NA YESU KRISTO KWA NAMNA NYINGI. (Kumbukumbu la Torati 34:10)

"Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa" lakini Mungu alikuwa ameshasema, "Mimi nitawaondoshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake (Kumb. 18:18). Bwana Yesu Kristo ndiye pekee aliyenenwa hapa. Mtume Petro alithibitisha hili katika (Matendo 3:20-22) Yesu alikuwa Mkuu kuliko Musa na manabii wote.

  • Musa aliwaongoza watu wa Mungu kama Mchungaji mwema, akiwatimizia  mahitaji yao yote.
  • Yesu alikuwa ndiye mchungaji mwema ambaye pia alitoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake (Yohana 10:11)
  • Musa alikuwa mtu mpole (Hes:12:3). Alifahamu kuwa hakuna mtu awezaye kuongoza watu wengi bila msaada wa Mungu.
  • Yesu alikuwa ni mpole kuliko wanadamu wote (Mat 11:29)
  • Musa alimsihi Mungu mara nyingi ili awasamehe Waisraeli (Hes 14:19).
  • Yesu alitoa uzima wake ili tupate msamaha wa dhambi milele (matendo 5:31)
  • Mungu alisema na Waisraeli kupitia Musa aliyekuwa mwalimu wao (Kutoka 24:12)
  • Mungu alisema na watu katika mwanawake (Waeb.1:2, Yohana 3:34, 14:10).

 

MASWALI:

MAJIBU MAFUPI:

  1. Je, Musa alikuwa na miaka mingapi alipowaambia watu wa Israeli maneno yake ya mwisho?.
  2. Ni kwa nini Mungu alimwambia Musa aandike wimbo na awafundishe Waisraeli?.
  3. Musa aliandika nini katika Chuo?
  4. Mara ngapi watu walisikiliza maneno yaliyoandikwa na Musa katika Chuo kabla ya kufa?.
  5. Je, Musa aliona nini alipokuwa juu ya mlima Nebo?
  6. Je, Musa alizikwa wapi?
  7. Je, lini Musa ataamka kutoka katika kaburi?.
  8. Ni nani aliyechaguliwa kuwaongoza wana wa Israeli baada ya Musa kufa?

MAJIBU YA KINA:

 

  1. Musa aliandika chuo
    1. Ni maneno gani yaliyoandikwa katika Chuo?
    2. Ni mara ngapi watu walisikia maneno ya chuo?
    3. Kwa nini ilikuwa ni muhimu wao kuwafundisha watoto wao maneno yote?
  2. Musa hakuruhusiwa kuingia Nchi ya Ahadi
    1. Ni nani alikuwa kiongozi mpya na ni jinsi gani Musa alivyomtia moyo mbele ya  watu wote?
    2. Kwa jinsi gani kifo cha Musa hakikuwa cha kawaida?
  3. Fikiria fundisho ulilojifunza kutoka maisha ya Musa. Eleza jinsi tunavyoweza kuwa sawa na mtu huyu mashuhuri?

 

Majibu ya nyongeza:

 

  1.  Musa alikuwa nabii mkuu kama Yesu Kristo.

 a) Linganisha kazi za Musa na tabia yake na yale ya Yesu Kristo.

 b) Ni kwa sababu gani imani ya Musa na utii wake itapewa thawabu na Mungu na ni lini hili litakapotokea.?

 

Swahili Title
30 MUSA
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type