33. ISRAELI WANAVUKA YORDANI:
"Nini maana ya Mawe hayo"?.
Shabaha:
Ni kuonyesha kwamba Wana wa Israeli kwa kutii amri za Mungu walivuka mto
Yordani salama.
Muhtasari:
Ili kuingia katika Nchi ya Kanaani wana wa Israeli walikuwa hawana budi kuvuka mto Yordani ambao kwa wakti huo wa mwaka ulikuwa umefurika. Watu waliondoka Shitimu hadi kwenye kingo za mto na Joshua alikuwa amewaeleza kuwa baada ya siku tatu watavuka kuingia upande wa pili.
ISRAELI WANAJIANDAA - YORDANI UNAVUKIKA: Joshua: 3
Joshua anawaambia watu "jitakaseni maana kesho BWANA atatenda mambo ya ajabu kati yenu" (mst 5). Walipaswa kutupilia mbali mawazo yote ya kibinafsi na kumkabidhi mioyo yao yote na akili ili kutenda sawa na maagizo ya Mungu. Sanduku lilibebwa na Walawi ambao waliwatangulia wote nao wangewafuata baada ya umbali dhiraa 2000 (yapata Meta 800). Mungu alimwambia Yoshua; Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kukujua ya kuwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyo kuwa pamoja na Musa. (mst 7).
Yoshua aliwaamuru Walawi, walichukue sanduku la agano lililofunikwa na kitambaa cha bluu watangulie mbele. Wakilitazama, wakisubiri kuona muujiza wa kushangaza ambao Mungu alikuwa ameahidi (mist 9-13) Yordani ulikuwa umefunika kingo zote zilikuwa zimefurika. Lakini Makuhani walitembea hadi kwenye ukingo wa mto. Hata ikawa nyayo zao zilitiwa majini, "mafuriko ya mto yakarudishwa nyuma" kwa nguvu za Mungu (Zaburi 114:3-5). Hayo maji yashukayo kutoka juu yakasimama, na maji yaliyo upande wa chini yatatindika, na kuacha mahali pakavu kuwa njia ya kuvukia. Huu ulikuwa ni muujiza ulioshangaza namna gani! Ni kwa jinsi gani wana wa Israeli walivyotiwa nguvu na kusimuliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na furaha kuu, kuona kuwa yale waliyokuwa wameambiwa na Yoshua ni kweli - "Mungu aliye hai yu kati yenu" (mst10). Makuhani waliendelea mbele wakasimama wakiwa wamelibeba sanduku la Agano katikati ya mto Israeli wote walivuka katika nchi kavu.
UKUMBUSHO WA AINA MBILI: Joshua 4
Kama kumbukumbu ya tukio hili la ajabu, Mungu alimwambia Yoshua achague watu kumi na mbili, mmoja kila kabila ili wachukue mawe kumi na mbili kutoka pale makuhani walipokuwa wamesimama wayachukue hadi upande wa magharibi wa ukingo wa mto. Mawe haya yalisimamishwa Giligali, Siyo mbali kutoka Yeriko, Waisraeli walipoweka kambi yao. Joshua aliweka ukumbusho wa pili wa mawe kumi na mbili katikati ya Yordani, " mahali hapo hiyo miguu ya Makuhani walichukuao sanduku la Agano iliposimama". (mst 9)
Kumbukumbu hizi ziliwakumbusha watu jinsi Mungu wao alivyofanya miujiza ya kushangaza. Na hapo watoto wao watakapowauliza, "Ni nini maana ya mawe haya?" Walipaswa kuwaambia jinsi maji ya Yordani yalivyotindika mbele ya Sanduku la Agano la BWANA" (mst 7) na "Israeli walivuka mto huu wa Yordani kwa njia ya nchi kavu" (mst 22)
Kwa tendo hili, Mungu alionyesha nguvu yake ya uweza kwa Israeli na "watu wote wa duniani" (mst 24).
FUNDISHO KWETU
Tunaweza kujifunza kutokana na tukio la Israeli kuvuka mto Yordani. Ikiwa tutaweka tumaini kwa Mungu atatusaidia kuweza kufanya mambo mengi ambayo yasingewezekana kwetu kabisa.
Wakati mtoto wa Israeli alipotazama mawe yaliyosimamishwa kama ukumbusho na kuuliza "Ni nini maana ya mawe haya?" lilikuwa jukumu la wazazi na walimu kuwaambia muujiza wa ajabu wa kuvuka mto Yoradni. Mungu anafurahishwa ,watu wanapokuwa na ufahamu wa yale yanayopaswa kufanyika katika kumbukumbu Mungu na kuweza kujiuliza ili hata wao wenyewe wakue ili wamtumikie.
KWA UKUMBUSHO ZAIDI:
KAZI YA JOSHUA KILIKUWA KIVULI CHA KAZI ZA YESU KRISTO.
Joshua ni jina la Kiebrania lenye maana ya "BWANA MWOKOZI" na YESU ni la Kigiriki lenye maana sawa na Yoshua (matendo 7:45, Waeb4:8) Majina yote yana maana sawa ,maana watu wote hao wawili walikuwa waokozi wa watu wao. Yoshua aliwaongoza watu wake kuchukua urithi wao. Naye Yesu Kristo atafanya shughuli ya namna hii lakini kazi kubwa atakaporudi na kuimiliki dunia yote akiwa mfalme wa wafalme wa na Bwana wa mabwana (Uf 17:14) Yeye atawatumikia watu wake na kuwapa nchi aliyoahidiwa Abrahamu kuwa urithi wa milele.
MASWALI Majibu Mafupi:
- Watu walipaswa wafanye nini kabla ya kuvuka mto Yordani?
- Kulitokea nini nyayo za Makuhani zilipoingia majini?
- Ni nani waliobeba sanduku la Agano?
- Joshua alisema wajenge nini ndani ya mto na ya upande wa pili wa mto?
- Ni nini watu wangewaambia watoto wao ikiwa wangeulizwa "Nini maana ya mawe haya?".
Majibu ya Kina:
1) Eleza habari jinsi Waisraeli walivyovuka mto Yordani mpaka nchi ya Kaanani
2) Eleza jinsi unavyofahamu ukumbusho uliojengwa na wana wa Israeli baada ya kuvuka mto Yordani.
Maswali ya Nyongeza
3). Je, Yoshua aliwaambia watu nini kuhusu kumbukumbu mbili?
4). Eleza ni jinsi gani kazi za Yoshua zilivyofanana na zile za BWANA Yesu Kristo?