CSSA 1-2-11 - JOSHUA OVERCOMES THE CITIES OF THE SOUTH

Swahili

36. YOSHUA ANASHINDA MIJI YA KUSINI

"BWANA akampigania Israeli".

Shabaha

Kuonyesha jinsi Yoshua alivyofanikiwa kushinda miji ya kusini pale alipomwomba Mungu amwongoze.

Muhtasari

Yeriko ulipotwaliwa na kuharibiwa ;watu wa Kanaani waliamini kuwa Yoshua na jeshi lote la Israeli watawavamia na kuwaharibu wao pia. Wafalme watano wa kusini waliamua kuungana pamoja kupigana na Israeli, isipokuwa Gibeoni walifanya shauri jema.

HILA YA WAGIBEONI KWA ISRAELI. Yoshua 9

Wakati Ai ilipokuwa imeangamizwa Yoshua aliwaoongoza Waisraeli upande wa kusini. Wagibeoni walikuwa upande wa kusini wa njia iendayo Yerusalemu.

Wenyeji wa Gibeoni waliamini kuwa mji wao yamkini utakuwa ndio utakaofuata katika mpango wa kushambuliwa wa Yoshua. Kwa hiyo badala ya wao kuungana na wafalme ambao walikuwa majirani zao walifanya mpango ambao waliufikiria kuwa ungeweza kumhadaa Yoshua na wanawaisraeli kufanya mapatano.

Walitumwa baadhi yao kwenda kambi ya Gilgali, walivaa nguo zilizo kuu na zilizo chanika na walivaa viatu vilivyotoboka. Mkate ulokuwa ndani ya gunia lao ulikuwa umekauka na kuota koga magunia yao yote ni makuu kuu viriba vya divai vilikuwa vikuu kuu vilivyo raruka na kutiwa viraka .Watu hawa walifika kwa Yoshua wakamwambia sisi tumetoka nchi ya mbali sana basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi. Yoshua alikuwa amekatazwa asifanye mapatano yoyote na watu wa Kanaani. Mungu alisema "usifanye agano nao” (Kumb 7:2) kwa hiyo alipaswa kuchukuwa tahadhali. Yoshua aliwauliza wale watu wametoka wapi,nao walimwambia kuwa wametoka nchi ya mbali sana " kwa sababu ya jina la BWANA, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake na habari ya hayo yote aliyoyafanya huko Misri” (mstari wa 9).Wakamwonyesha Yoshua nguo zao zilizochanika, viatu vyao vilivyotoboka kama uthibitisho wa safari yao ndefu. Walimwonyesha mkate uliokauka ulio na koga na viriba vilivyo raruka raruka ambavyo walisema vilikuwa vipya walipoanza safari yao. Yoshua na wakuu wa Israeli walidanganyika kabisa wakafanya agano nao la amani ili waachwe hai. Hili lilikuwa kosa kubwa; hawakumwuliza kwanza Mungu lakini waliamua kwa mawazo yao wenyewe kwa kufuata yale waliyosikia kwa wale watu “wala wasitake shauri kinywani mwa BWANA” (mstari wa 14) .Waisraeli wakasafiri wakaifikia miji ya Gibeoni baada ya siku ya tatu. Ndipo walipofahamu kuwa wageni wale "waliotoka nchi ya mbali sana" hakika walikuwa ni wenyeji wa nchi ile. Waisraeli wakakasirika sana walipofahamu kuwa walidanganywa. Hata hivyo kwa kuwa walikwisha waapia wasingevunja agano. Kwa hiyo watu Wagibeoni waliachwa hai lakini walifanywa watumwa kama adhabu kwa sababu  ya kumdanganya Yoshua na waisraeli wote. Wakawa wapasua kuni na wenye kuteka maji wa mkutano wote wa Israeli. Lakini kwa kuwa maisha yao yalibbokolewa wale Wagibeoni hawakujali (mistari ya 25-27)

VITA VYA BETH- HORONI: YOSHUA 10:1-14

 

Muda vita vilipokuwa vinaendelea Yoshua alifanikiwa sana, maana Kanaani ya kati yote ilikwisha kuwa mikononi mwake. Lakini wafalme watano wa kusini walioongozwa na Adon - zedeki ,Mfalme wa Yerusalemu ,alikusanya nguvu kupigana na Israeli. Kwanza,waliazimia kushambulia Wagibeoni,kwa kuwa wenyeji wa mji huo walikuwa wamefanya mapatano na Israeli.Aliongoza jeshi kubwa sana, wafalme wa Waamori walikwea na kuweka kambi yao mbele ya mji ,na Gibeoni wakatuma taarifa haraka kwa Yoshua kuomba awasaidie. Yoshua kwa wakati huo aliomba kwanza uongozi wa Mungui.“Usiwache watu hao”,Mungu alisema;"kwa kuwa mimi nimekwisha kuwatia mikononi mwako hakuna mtu awaye yote miongoni mwao atakaye simama mbele zako” (mstari wa 8) Yoshua aliamua kuwashangaza maadui. Yeye na jeshi lake walisafiri usiku kutoka Gilgali hadi Gibeoni ndipo siku ya pili mapema asubuhi ghafla wakalifikia jeshi la wale wafame watano. Jua lilipopambazuka miale ikawa mikali sana machoni mwa Waamori , hata ikawa vigumu kwao kuweza kupigana. Kitambo kidogo tu vita ikaisha na hao waliosalia hai wakiwa katika hofu wakakimbilia kilele cha  mlima kuelekea Beth-horoni.Jeshi hilo lililokuwalimetawanyika likafika hadi penye kilele cha mwamba wakiwa wanatelemka kwenda upande wa pili wakiamini kuwa wangejiponya mikononi mwa Israeli ,Mungu akawapigania watu wake.BWANA akatuma dhoruba na mawe makubwa yaliyogandamana na barafu yaliyoua watu wengi sana kuliko wale waliokuwa wameuawa katika vita. Yoshua alipoona siku inakaribia kuisha alihofia kuwa baadhi ya maadui wangepona. Hivyo aliomba jua lisimame kimya nao mwezi utulie "hata hilo Taifa lilipokuwa limekwisha jipatikiza juu ya adui zao. Kwa hiyo jua likasimama kimya katikati ya mbingu,wala halikufanyaharaka kuchwa kama muda wa siku nzima.Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake; hata kale ikawa yeye  BWANA kuisikia sauti ya binadamu;kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajii ya Israeli” (mistari ya 12 - 14). Huu ulikuwa ni muujiza wa ajabu sana na furaha  ya ushindi wa vita  wa Yoshua ambaye kwa imani na maombi aliweza kuwashinda maadui zake.

FUNDISHO KWETU
Somo hili linatufundisha kwamba mawazo yetu kila wakati yaongozwe na neno la Mungu. Mara nyingi tunaona kuwa tuwenye hekima katika macho yetu na kutohitaji msaada wa mtu yotote kwa yale tunayotaka kutenda.Ni rahisi pia kuongozwa katika kutenda mabaya kwa sababu ya kukubaliana na yale tunayoyasikia  kwa mwingine anapoyazungumza. Sulemani mtu mwenye hekima alisema "Usiwe mwenye hekima na machoni pako;mche BWANA na ujiepushe na uovu (Mithari 3:5-7)

 

MASWALI

MAJIBU MAFUPI
1. Gibeoni ilikuwa wapi?

2. Ni kwanini watu Wagibeoni walihitaji kumdanganya Yoshua?

3. Je Mungu alikuwa amesema nini kuhusu kufanya mapatano na watu wa nchi ile?

4. Ni jambo gani liliwafanya wale Wagibeoni waonekane kama watu waliotoka nchi ya mbali sana?

 5. Ni wakati gani Yoshua alipogundua kuwa wamedanganywa?

6. Je Joshua aliwapa adhabu gani Wagibeoni kwa ajili ya udanganyifu wao?

7. Ni watu gani waliokwenda wapigane na Israeli walipokuwa wamedanganywa na Wagebioni?

 8. Ni jinsi gani Mungu alivyomsaidia Yoshua kuwaangamiza Waamori?

 9. Ni muujiza gani uliotokea ili kuwaangamiza Waamori wote?

10. Ni mahali gani vita kati ya Israeli na Waamori ilifanyika?

MAJIBU YA KINA

  1. Wakati Yoshua alipowaangoza waisraeli kwenda kushinda na kumiliki Kanaani baadhi yao walianza kuogopa?

  Eleza Wagibeoni walitotumia mbinu gani hata Yoshua akawafanya mapatano nao?

 

MAJIBU YA NYONGEZA

  1. Baada ya Yoshua kufanya mapatano na watu wa Gibeoni, Waamori walikutana pamoja kupigana na Waisraeli.

 Eleza jinsi waamori walivyoshindwa pale Beth – horoni?

 

Swahili Title
036 YOSHUA ANASHINDA MIJI YA KUSINI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type