38. YOSHUA ANAFARIKI
"Lakini mimi na nyuma yangu tutamtumikia BWANA"
Shabaha
Kuonyesha jinsi Yoshua kwa uaminifu aliwahimiza watu wamtumikie Mungu,lakini baada ya kufariki kwake watu walisahau kielelezo alichowachia na wakageukia kuziabudu sanamu.
Muhtasari
Hata ikiwa baada ya siku nyingi Mungu alipokuwa amekwisha kuwapa Israeli raha mbele ya maadui zao pande zote,ndipo; Yoshua alipowaita Israeli wote ili kuwapatia maonyo kabla ya kufariki. Alikuwa Mzee na mwili wake ulikuwa hauna nguvu kwa ajili ya umri hata hivyo alipenda kuwapatia Israeli maneno ya kuwatahadharisha na kuwatia moyo kwa kuwaimarisha kwa ajili ya siku za mbele.Yoshua 23 na 24.
MAONYO YA YOSHUA KWA ISRAELI: Yoshua 23.
Katika maneno yake ya mwisho kwa wana wa Israeli,Musa aliwaagiza kwamba, watakapokuwa wameingia katika nchi nilazima wawaangamize Wakanaani wote .Na wala wasifanye agano nao wala wasioane nao. (kumb 7:1-4). Musa aliwafahamisha vizuri kabisa ,kuwa mwisho wa kila mapatano kati ya Wakanaani na Israeli ni watu wa Mungu kuabudu miungu ya mataifa .
Mwishowe Israeli walikaa katika katika Nchi ya Ahadi, naye Yoshua akiwa mzee, akawakumbusha jinsi Mungu alivyowafukuza Wakanaani mbele yao; kama Mungu alivyokuwa ameahidi. Yoshua alifahamu kuwa ilikuwepo njia moja tu ya wao kuweza kujitenga na kuendelea kupokea baraka za Mungu katika nchi nzuri waliyokuwa wamepewa na Mungu. Walipaswa kufanya kama vile Yoshua alivyokuwa akifanya - Walitakiwa wasome nenola Mungu kila siku na kulitii (angalia Yoshua 1:8).
"Basi,iweni mashujaa sana kuyashika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa na kuyatenda yote , usiiache kwenda mkono wa kuume wala mkono wa kushoto;Msiingie kati ya mataifa haya, yaani haya yaliyobaki kati yenu, wala msitaje majina ya miungu yao wala kuwaapisha watu kwa majina yao, wala kuitumikia, wala kujiinamisha mbele yao; bali shikamaneni na BWANA, Mungu wenu, kama mlivyotenda hata hivi leo" (mist 6-8).
Yoshua aliwambia Israeli "kama mtashikamana na mataifa haya yaliyobaki kati yenu, na kuoana nao,jueni ya kuwa hakika BWANA Mungu hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu; bali watakuwa mtego kwenu……kisha itakuwa kama yalivyowafikilia yale mambo mema yote BWANA, Mungu aliyowaahidia ninyi. Kadhalika BWANA atawafikilizia mabaya yote, hata atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii njema, BWANA, Mungu wenu aliyowapatia" (mist 12-15).
Utii ungeweza kuleta baraka na furaha lakini uasi ungesababisha Mungu kukasirika na kuwaadhibu. Hivyo basi lilikuwa chaguo lao, kuchagua kati ya mema au mabaya.
AGANO LINAFANYWA UPYA HUKO SHEKEMU: Joshua 24
Yoshua aliwakusanya makabila yote ya Israeli na viongozi wao kule Shekemu ili waweze kusikiliza wosia wake. Maneno yake yaliwachochea kwa kuwakumbusha. Aliwakimbusha jinsi Mungu alivyo baba yao, Abrahamu , kutoka katika mji wenye sanamu wa Ur na kumleta hadi katika nchi hii; ambapo alimwabudu Mungu wa kweli mmoja tu. Aliwaambia kuhusu Isaka na Yakobo na Waebrania wote waliotoka Misri utumwani wakiongozwa na Musa.
Kwa hiyo aliwaambia Historia ya familia yao, akionyesha jinsi Mungu alivyowabariki wazazi wao wakwanza kwa kadri walivyomtumainia. Na kwa sasa amewapatia nchi nzuri , Zabibu na Mizeituni iliyositawi sana ambayo hawakuipanda wao na miji ilikuwa tayari kwa ajili yao ambayo hawakuijenga. Yote haya Mungu aliwapatia. " Halikuwapungukia hata neno moja katika mambo mema yote" ambayo Mungu awaahidi ( Yoshua 23:14). Ili kuonyesha shukurani zao kwa Mungu kwa ajili ya baraka hizi zote walitakiwa wamtumikie Mungu peke yake "Kwa unyoofu wa moyo na kwa kweli."
"Chagueni hivi leo mtakayemtumikia", Yoshua aliwaambia, "Lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA" (mist 15).
Kisha watu wote waliongozwa na maneno ya Yoshua na wakakiri kwamba hawatageukia sanamu kamwe. " Hao watu wakajibu wakasema , Hasha! Tusimwache BWANA, ili kuitumikia miungu mingine; BWANA, Mungu wetu ndiye tutakayemtumikia , na sauti yake ndiyo tutakayoitii" (mistari ya 16,24).
Basi Yoshua akafanya agano na wale watu na "akayaandika maneno haya katika kitabu cha torati ya Mungu; kisha akatwaa jiwe kubwa , akalisimamisha huko, chini ya ule mwaloni uliokua karibu na patakatifu pa BWANA"(not 26). Yoshua akawaambia watu "Tazama jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu…msije mkamkana Mungu wenu"(mstari wa 27).
Lile jiwe lilikuwa liwe ukumbusho wao wa ahadi waliyoahidi ya "kumtumikia BWANA"
KIFO CHA YOSHUA: Yoshua 24:29-30
Yoshua alikuwa amemalizakazi yake ya kuwaleta wana wa Israeli katika nchi ya ahadi.
Na sasa wakati ulikuwa umefika na yeye "kwenda njia ile waiendayo watu wote wa ulimwengu"(Yosh23:14;)Yoshua alikufa akiwa na umri wa miaka 110, alikuwa mvumilivu na hodari alifuata nyayo za Musa , na alizikwa katika urithi huko Timnath-sera.
FUNDISHO KWETU.
Kwa mfano,tunaweza tukapenda kucheza mchezo. Hili linaweza kuwa zuri, kwa ajili ya afya- lakini kupenda mchezo inawezekana kabisa ikawa ni jambo tunalolifurahia sana wakati wote. Na tusipokuwa waangalifu, tunaweza kulisukumia mbali Neno la Mungu Upesi na kuliweka nafasi ya pili katika maisha yetu.
Kujisomea Biblia, semina ya Biblia, kusaida wengine wote wale wasiku nyingi katika kweli na wachanga katika Ekklesia kwa matendo ya wema au barua za Kirafiki - haya yote ni mambo ambayo Mungu anataka sisi tuyafanye. Haya ni mambo yanayojenga tabia zetu, yakitufanya kuwa watenda mema na watumishi waaminifu kwa mfano wa Yoshua. Na kama, tutakuwa na muda wa ziada basi kila tulifanyalo ni lazima lifanyike katika njia inayompendeza Yeye kwamba ni kwa kufanya kazi au tunayoyatenda tukishirikiana na marafiki zetu.
MASWALI
Majibu Mafupi
1.Ni kwa nini Waisraeli wakupaswa kufanya mapatano yoyote na Wakanaani?.
2.Ni jambo lipi ambalo lingewasaidia kujitenga na Wakanaani?
3.Wakati Yoshua alipozeeka, aliwaita Waisraeli wakusanyikie pamoja.
Ni Sehemu gani waliyokusanyikia kusikiliza Ujumbe wake wa mwisho kwao.
4.Malizia maneno ya Yoshua - “Lakini mimi …”
5.Pale Shekemu, Waisraeli waliahidi kufanya nini ?
6.Ni kwa nini jiwe kubwa liliwekwa pale Shekemu?
Majibu ya Kina
- Yoshua aliwapatia Waisraeli onyo la kujitunza kwa kujitenga na Wakanaani. (a)Ni jinsi gani wangeweza kujilinda kwa kujitenga?
(b)Alisema ingetokea nini kama wasingefanya hivyo?
Majibu ya Nyongeza
2). Waisraeli walikuwa wameonywa kuhusu kuabudu sanamu.
a)Je, unaweza ukafikiria njia nyingine ambayo tunaweza tukaabudu sanamu siku hizi?. b)Je,badala yake tunapaswa kufanya nini?