39. DEBORA NA BARAKA.
Kikainuka kizazi kingine nyuma yake ambacho hakikumjua BWANA.
Shabaha.
Kuonyesha kwamba matatizo yaliyowapata wanawa Isaraeli nyakati za waamuzi siyo tofauti na matatizo yanayotupata leo.
Muhtasari.
Ingawaje Waisraeli waliendelea kutokuwa waaminifu na watiifu, hata hivyo Mungu aliendelea kuwa mwenye rehema na kuwasamehe. Walipokuwa katika taabu na wakamgeukia Yeye, aliwaokoa mikononi mwa adui zao.
Waamuzi 2,4 na 5
WAKATI KILA MTU ALIPOFANYAYALIYOKUWA MEMA MACHONI PAKE MWENYEWE.
Historia ya wakati wa Waamuzi inafupishwa na mstari wa mwisho katika Kitabu cha Waamuzi : “Na katika siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli ;kila mtu alifanya yaliyokuwa ni mema machoni pake mwenyewe”
Ni wakati ambapo watu hawakujali Neno la Mungu na wakazifuata njia zao wenyewe ,mwishowe wakajiletea wenyewe taabu.Na hivyo ndivyo taabu ilivyowapata Israeli.
Siku zote za Yoshua,na siku zote za viongozi waliokuwa wamechaguliwa na Yoshua ;Israeli walimtumikia BWANA.Lakini kizazi kingine ambacho hakikuona ishara na maajabu ya BWANA,kikamwacha Mungu wa baba zao nao wakaabudu Baali na Ashtorethi,miungu ya mataifa yaliyokuwa yamewazunguka(Waamuzi 2 :7-13).Na hili lilikuwa sawa na onyo ambalo ambalo Yoshua alikuwa ameshawatahadharisha(Angalia Yoshua 23 :12-13).Hili lilimkasirisha sana Mungu.
Ikawa badala ya amani na furaha ambayo Mungu aliwaahidi kuwapatia ikiwa watamtii, wakateseka katika mikono ya watu wa Mataifa kwa sababu Mungu hakuwapigania Waisraeli.
KILICHOSABABISHA WAISRAELI WATESEKE: Waamuzi 2
Jinsi walivyoweza kusahau mapema ahadi walipokuwa na Yoshua:"Tutamtumikia BWANA, Mungu wetu na sauti yake ndiyo tutakayoitii" (Yoshua 24:24).
Wakawa wamejifunza njia za watu waovu wa nchi zile na hata na waisraeli wakawa siyo toauti watu hao kwa kutenda maovu.
Na ikawa Waisraeli walipoicha njia ya Mungu, Mungu naye akawaacha ,walijikuta "hawawezi tena kusimama mbele ya maadui zao" (mstari wa 4). Maadui wao wakazidi kuwa na nguvu juu yao, na Israeli wakawa dhaifu kwao. Wakanaani wakawatendea jeuri, na ndipo Waisraeli walipomkumbuka Mungu wao nao wakamlilia iliawaokoe. Mungu akawa mwenye rehema akawapatia waamuzi (viongozi) ambao kupitia wao Mungu aliwaokoa Waisraeli.Nawakati wa uhai wamwazi huyo ndipo waisraeli walipomtumikia Mungu na wakaokolewa kutoka kwa maadui wao lakini mwamuzi alipofariki wakarudi nyuma haraka katika matendo yao maovu .Haya yalitokea mara nyingi sana kwa sababu ya kumwacha BWANA,Mungu akasema hatawafukuza tena mataifa mbele yao,ilikwamba awathibitishe(au kuwapa mtihani ) Israeli ilikuona kama wataifuata njiayake (mistari 18-22),tukisoma kitabu chote cha waamuzi tutaona…..hili Israeli wakimtenda Mungu dhambi,na hili ndilo lililowaletea mateso juu yao,walipotubu na kumrudia Mungu,Mungu aliwaokoa kutoka katika mikono ya adui zao. .
- Dhambi huleta MATESO
- Kumtafuta Mungu huleta WOKOVU
DEBORA NABII MKE: waamuzi 4:1-9.
Israeli waliishi maisha ya furaha wakati wa uhai wa Ehudi aliyekuwa mmoja wa waamuzi wao,lakini alipofariki watu wakayasahau yote BWANA aliyowatendea na haraka wakazirudia njia zao mbaya.Ndipo wakati huo Mungu akawaadhibu kwa kumruhusu Mfalme wa Kanaani kuwatawala. Wakanaani walikuwa na mkuu(amiri mkuu wa jeshi mwenye akili jinalake aliitwa Sisera, lakini kilichowatisha zaidi ni kwamba alikuwa na magari ya chuma mia (kenda) tisa, Sisera " akawaonea kwa nguvu wana Waisraeli" miaka ishirini na katika taabu yao Waisraeli wakamrudia BWANA,akakisikia kilio chao na kuwapatia msaada -safari hii aliwapatia msaada kupitia kwa mwanamke. Debora,nabii mke, aliyekuwa akiishi sehemu iliyokuwa katikati ya Betheli na Rama. Neno la Mungu kupitia Debora likawajia Israeli.
Alikuwa mwanamke mwaminifu, aliyejaribu kuwaongoza watu katika njia ya haki, na wana wa Israeli walimwendea ili awaamue. Neno la Mungu lilifunuliwa kwa Debora, ya kwamba Baraka ndiye atakayeongoza waisraeli ili kumshinda Sisera. Kwa hiyo Debora alimwita Baraka na kumwambia yale ambayo Mungu alitaka Baraka afanye.
Alitakiwa aende kuelekea Mlima wa Tabori akiwa na waisraeli 10,000,kisha Sisera jeshi lake wangetiwa mikononi mwake.Ndipo Baraka akasema,"kama utakwenda pamoja na mi ndipo nitakwenda bali kama huendi pamoja nami,mimi siendi". Debora alikubali kwenda lakini alimweleza Baraka ya kuwa siyo yeye atakaye pata heshima ya ushindi, kwa kuwa Mungu "atamwuza Sisera mikononi mwa mwanamke" (mstari wa 9)
JINSI SISERA ALIVYOSHINDWA: WAAMUZI 4:10-24:5:20-22
Ndipo Debora na Baraka wakatuma ujumbe kwa makabila yote ya Israeli kuja ili kuwa jeshi moja la kupigana na Sisera. Wote kwa pamoja walikuwa wanaume 10,000 waliokusayika pamoja na wakaongozwa na Baraka kuelekea Mlima Taboli ili kukutana na jeshi la Sisera. Lakini Sisera alikuwa amekwishaonywa na mtu aliyeitwa Hebeli; kuhusu kukalibia kwa jeshi la Israeli na hivyo akafanya haraka kukusanya jeshi kubwa pamoja na magari yao yote ya chuma mia tisa.
Debora akamwambia Baraka aliongoze jeshi lake watelemke chini ya mlima, akamwambia, "Haya! Inuka maana siku hii ndiyosiku ambayo Bwana amemtia sisera katika mkono wako" (msari wa 14). Hii ilionekana kuwa ni jambo mbaya kulifanya kwa kuwa sehemu ya tambalale (nyika) chini ya mlima, ingekiwa rahisi kwa Sisera kuweza kuendesha magari yake kuwakabili Israeli, ambao wote walikuwa wakitembea kwa miguu. Kwa kweli angelikuwa na uhakika wa ushindi wa vita.
Lakini Debora alikuwa sahihi kabisa, kwa kuwa Mungu alikuwa katika Uweza wake. Alikuwa akiwapigania Waisraeli.BWANA alituma wimbi kubwa lililosababisha mto Kishoni kujaa na kumwaga mafuriko eneo lote tambalale hata farasi na magari yakazama ndani ya matope. Na hivyo wana wa Israeli wakaweza kuwashinda Wakanaani hata hakusalia "Hata mtu mmoja" ( mstari wa 16).
Hata hivyo, mtu mmoja aliweza kutoroka -Sisera aliyekuwa amiri wa jeshi lililoshindwa . Alishuka katika gari lake akakimbia kwa miguu.
Alikuwa amechoka sana na alitaka ajifiche ili Baraka asimwone. Kwa hiyo alikimbia mpaka akaifikia hema ya Yaeli, mkewe Hebeli akamwuliza kama anaweza kumhifadhi katika hema yake. Alimkaribisha ndani na akampa maziwa akanywa.
Sisera kisha akalala, naye Yaeli akamfunika blanketi. Sisera akamwambia , Simama mlangoni pa hema na mtu yeyote asijue kama yupo pale. Kisha akasinzia , maana alikuwa amechoka sana.
Ingawa mmewe alikuwa rafiki wa karibu na Sisera , Yaeli aliwaonea huruma Israeli waliokuwa wakitendewa jeuri, chini ya utawala wa Waakanaani . Akitumia kigingi cha hema na nyundo, Yaeli alimwendea polepole Sisera alikuwa ameshikwa na usingizi alikitia kipingi katika kipaji chake akampiga pigo la kutisha kichwani pake lililomuuma .
Kwa hiyo adui huyu wa Israeli akawa ameondolewa na heshima ya kushinda kwake Baraka iliondelewa kwake akapewa mwanamke, kama Debora alivyokuwa ametabiri ( mstari wa 9)
WIMBO WA USHINDI WA DEBORA:Waamuzi 5
Kushindwa kwa wakanaani kulisababisha furaha kubwa sana katika Israeli na ushindi ulisherehekewa kwa maneno ya wimbo wa Debora na Baraka, msifuni BWANA ambaye aliwapigania na kuwaokoa kutoka katika mikono ya watesi wao.
Na Baada ya vita hivi, "nchi ikastasrehe miaka arobaini" (mstari wa 31)
FUNDISHO KWETU
Nyakati za waamuzi, "kila mtu alifanya yaliyokuwa mema machoni pake". Wakati watu walipofuata njia ya Mungu, mambo yote yalikwenda sawa lakini uovu na mateso yalitokea wakati Israeli walipomsahau Mungu na kufuata njia zao. Na watu katika dunia siku hizi "wanafanya yale yaliyomeme machoni pao" na hiki ndicho chanzo cha uovu na fujo nyingi kila mahali ni lazima tujitenge na haya yote na kutafuta uongozi wa Mungu, kwa kuwa tunafahamu Biblia inavyosema kwamba "ninajua ya kwamba njia ya mwanadamu haimo katika nafsi yake kuelekeza hatua zake" (Yer 10:32).
Kama tulivyojifunza kutoka katika kitabu cha waamuzi:Dhambi huleta mateso lakini
kumtafuta Mungu huleta wokovu.
MASWALI
Majibu Mafupi.
1.Ni kwa nini mabaya yaliwapata Israeli wakati wa Waamuzi?
2.Malizia Sentesi: ”Katika siku hizo hapakuwa na Mfalme katika Israeli…”
3.Wakati wa Waamuzi ni jinsi gani Mungu alivyowaadhibu Israeli?
4 Mungu alifanya nini wakati Israeli waipomlilia kumwomba msaada?
5.Debora alikuwa ni nani?
6.Ninini kilitokea kwa magari ya Sisera?
7.Ninani aliyemwua Sisera,amiri jeshi mkuu wa jeshi la Wakanaani?
8.Katika Wimbo wa Debora,ninani aliyemsifia kwa ajili ya ushindi?
Majibu ya Kina.
1 a).Baada ya Yoshua kufariki palitokea nini?
b).Mungu aliwasaidiaje,Waisraeli walipomlilia?
c).Ni jambo gani tunalokuta rikijirudiarudia tena katika Kitabu cha Waamuzi?
2.Eleza jinsi Debora na Baraka walivyosaidia kuokoa Israeli?
Majibu ya Nyongeza
3.Ni somo gani tunalojifunza kutoka katika Kitabu cha Waamuzi?
4.Ni jinsi gani Mungu alivyowaokoa Israeli walipomlilia kutoka katika mikono ya maadui zao?