CSSA 1-2-16 - SAMSON

Swahili

41. SAMSONI

 

Ataanza kuwaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti.

 

Shabaha.

  Kuonyesha kwamba nguvu za samsoni zilitoka kwa Mungu.

 

Muhtasari:

Mara nyingi Mungu aliwaokoa watu wake kutoka kwa maadui wao kwa kuwainua Waamuzi kuwaongoza. Wakati wa uhai wa kila mwamuzi waisraeli walimtumikia Mungu lakini mwamuzi alipokufa kwa mara nyingine tena waligeukia kuabudu sanamu. Onyo la mwisho la Yoshua ( Yosh 213:6-7) lilikuwa limesahauliwa, na Mungu aliwaadhibu watu wake kwa kuyaruhusu mataifa mengine kuwatesa. Waamuzi 13:1-7;16

 

WAFILISTI

   Kwa miaka arobaini Waisraeli walitaabishwa na Wafilisti, walioishi katika ukanda wa nchi iliyo pwani ya  Kusini mwa Kanaani. Walikuwa ni watu wenye nguvu, waliopenda vita ambao hawakushindwa wakati Waisraeli walipoingia na kuimilki Kanaani chini ya uongozi wa Yoshua. Miji yao mikubwa ilikuwa Gaza, Gathi, Ashkeloni, Ashidodi na Ekroni. Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na mtawala wake na hawa  waliitwa  Mabwana watano wa Wafilisti, wakati walipokuwa chini ya ukandamizaji wa Wafilisti, Waisraeli hawakuweza kuunda mapanga au mikuki (1 Samweli 13:19-20).Hivyo bila  ya msaada wa Mungu hawakuwa sawa na madui zao waliowajia wakiwa na  silaha hizi.

 

Samson Anazaliwa: Waamuzi 13:1-7

Manoa na mkewe waliishi mji wa Sora katika nchi ya Wadani, ambayo ilikuwa jirani na nchi ya Wafilisti. Walikuwa Waisraeli waaminifu, lakini hawakuwa na watoto. Siku moja Mungu alimtuma malaika kwa mkewe kumwambia kuwa wangepata mtoto mwanamme!Angekuwa mtoto ni mtoto wa pekee kwani angekua na kuwa ndiye “angelianza kuwaokoa waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti”( mstari wa 5). Mama yake angechukua uangalifu wa kipekee kabla hajazaliwa.   Mama huyo asingeruhusiwa kunywa divai wala kinywaji chochote kikali, wala asile kitu chochote kilichoelezwa katika sheria za Musa hapo ndipo mimi,nitakuwa dhaifu,nitakuwa kama wanadamu wenzangu.Delila angeona kuwa wakati huu sasa  Samsoni alikuwa amemwambia mtu wa Delila.“Kitu kilichonajisi” (mstari wa 4)?

 

Mwanaye angekuwa  “mnadhiri” ( tazama Hesabu 6) inayomaanisha kwamba maisha yake yote yangetumika katika kazi ya Mungu. Kama ishara ya hilo, nywele zake hazingekatwa kamwe, asingekunywa mvinyo au kinywaji chochote kikali wala “kula chochote kilicho najisi” (mstari wa 5).

 

SAMSONI  MWAMUZI : WAAMUZI 16:1:3

Samsoni alipokua, roho ya  Mungu ilimsukuma  kujaribu kuwasaidia watu wake. Wafilisti walishaanza kumwogopa kwa sababu alikuwa na nguvu sana na katika matukio mengi aliua  wengi wao. Nguvu hizi nyingi alipewa na Mungu kwa ajili ya kazi maalumu ambayo alipaswa aifanye, ambayo ilikuwa    “kuanza kuwakoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wafilisti”

 

Samsoni alifanya ziara za kawaida ndani ya nchi ya Wafilisti. Wakati mmoja alipokuwa Gaza, wafilisti walimvizia usiku kucha penye lango la mji. Usiku wa manane lango lilikuwa limetiwa komeo (au lilikuwa limefungwa) hivyo aliung`oa mlango na makomeo yake kutoka kwenye ukuta na kuvibeba vyote mabegani mwake hadi kwenye kilima kilicho kwenye barabara iendayo Hebroni. Wafilisti walishikwa na mshangao mkuu wa  nguvu zake kubwa na kuhangaika jinsi  wangaliweza kwa yakini kumshinda

Samsoni na Delila: Waamuzi 16 :4-20

Ikawa siku zile, Samsoni alimpenda mwanamke wa kifilisti aliyeitwa Delila. Mabwana wa Wafilisti hatimaye walifikiria mpango mzuri  ili kugundua siri ya nguvu kubwa za Samsoni. Walimhonga Delila kiasi kikubwa cha fedha  ili kumshawishi Samsoni na kuona nini asili ya nguvu zake  (mstari wa 5) alikubali kuwasaidia kwani hilo lingemfanya  awe tajiri.

 

Basi Samsoni alipokwenda kumtembelea alisema  “Niambie, tafadhali ni nini asili ya nguvu zako?” (mtari 6) .Samsoni alijifanya kumweleza mara tatu, na kila mara wafilisti wakaona kwamba ana nguvu kama kawaida yake. Kila siku Delila alimbembeleza  amwambie siri yake naye hatimaye alimweleza“siri ya moyoni mwake” (mstari wa 17) .Alikuwa mnadhiri tokea kuzaliwa kwake na nywele zake hazikuwahi kamwe kunyolewa, ikiwa ndiyo alama ya kutengwa kwake kuwa tofauti na  watu wengine. “Nikinyolewa alisema ndipo nguvu zangu zitanitoka”,Delila haraka aliwaita mabwana wa Wafilisti waende  na wajiandae kumchukua Samsoni. Alingojea hadi Samsoni alipokuwa usingizini naye hapo alimwambia mtu kumnyoa kichwa chake  - “na nguvu zake zikamtoka” (mistari wa 19)

 

Msifikirie kwamba nguvu kubwa za Samsoni zilikuwa kwenye nywele zake.  Nywele zake zilipobakia kuwa ndefu ilikuwa ni ishara ya utii wake wa amri  za Mungu (Waamuzi 13:5) na Mungu alimpatia nguvu hizo kwa ajili ya kazi ya  kuwapinga Wafilisti. Lakini nywele za Samsomi zilipokatwa kiapo cha mnadhiri kilivunjika; Samsoni alikuwa ameacha sheria ya Mungu na Mungu naye akaondoa nguvu zake.

 

KIFO CHA SAMSONI:WAAMUZI 16:21-31

Sasa Wafilisti ilikuwa  ni rahisi kwao kumshinda Samsoni. Walimng`oa macho yake na kumpeleka, Gaza hali wakimfunga kwa  minyororo ya shaba na kumtia katika kazi, akisaga ngano gerezani, Wakati Samsoni alipokuwa akifanyakazi gizani alikuwa akifiria juu ya mambo ya kijinga aliyokuwa ameyafanya, Mungu alikuwa amemwadhibu kwa kutotii kwake. Nywele zake zilianza kukua tena na muda ukawa umefika wa kufanya upya nadhiri yake kwa ajili ya kumtumikia Mungu.

 

Wafilisti walifikiri mungu wao alikuwa amemweka Samsoni mikononi mwao. Hivyo walikusanyika kutoa sadaka kwa Dagoni, mungu samaki, Samsoni aliletwa mahali walipokusanyika, pengine ndani ya hekalu la Dagoni mungu wao kucheza mbele zao ili wamdhihaki.

 

Alimwaomba kijana aliyemwongoza ili aziguze nguzo zilizoshika jengo lote ili aziegemee, kisha akamwomba,”Ee BWANA, Mungu unikumbuke nakuomba, unitie nguvu” (mistari wa 28). Akizishika nguzo zile akasema “achanife pamoja na wafilisti” (mistari wa 30) Alikusanya nguvu zake zote alijikaza kwenye nguzo zile nazo zikaangukia na kufanya jumba lote kuanguka. Watu wote pale wakiwamo Mabwana wa Wafilisti, wakafa. Mungu alisikia sala ya Samsoni nao aliowaua wakati wa kifo chake walikuwa wengi zaidi kuliko aliowaua katika uhai wake.(mstari wa 30)

 

Imeandikwa kwambaa Samsoni alikuwa Mwamuzi wa Waisraeli kwa miaka ishirini naye ingawaje hakuishi kila wakati  kwa kufuata njia za Mungu, alitekeleza kazi ya “kuanza kuwaokoa waisraeli kutoka mikononi mwa wafilisti”.

 

FUNDISHO  KWETU

 

Samsoni alisalitiwa na mwanamke aliyeonekana mrembo sana, lakini aliyekuwa na  roho ya  uovu alijifanya anampenda, lakini  nia ilikuwa kumwangamiza tu. Samsoni angemtii Mungu, asingekuwa na lolote la kufanya naye, na asingeteseka na kufa kama ilivyotokea kwake.

 

Samsoni alikuwa na nguvu kwa kadri alivyotunza kiapo chake, yaani  kumtumikia Mungu, Upendo wake kwa Delila ulimpofusha hadi akatenda uovu wa kuvunja ahadi yake. Wafilisti walipomng`oa macho yake naye akawa kipofu halisi, hapo ndipo alipoweza kuona waziwazi jinsi alivyo mpumbavu.

 

Na tuwe na hekima tumtii Mungu wakati wote.

 

MAELEZO YA ZIADA:

Samsoni alikuwa  ni mfano sawa sawa  kabisa na Taifa la Waisraeli.Wakiwa Taifa walitazamiwa kujitunza  wenyewe wakijitenga  kwa ajili ya Mungu ,kama waalivyoapa kuwa  wamepa kufanya (Tazama Jushua 24:24)

 

Samsoni alikuwa mnadhiri tangu kuzaliwa kwake, lakini alivunja kiapo chake (Waamuzi 16:17)

 

Waisraeli walikatazwa kuoa au kuolewa na Wakanaani (Yosua 23:12-23) lakini walitenda hivyo, naye Samsoni alitenda hilohilo. Mungu alisema wangepotoshwa na   miungu ya mataifa yale kama wangechanganyikana nao na hivyo ndivyo ilivyotokea, kama tuonavyo mara nyingi katika kitabu cha Waamuzi (Angalia Waam 2:11-13) wakati Samsoni alipompenda Delila, alimwondolea nguvu zake kwa kumshawishi kuvunja kiapo chake. Ndipo wafilisti walifikiri mungu wao Dagoni alikuwa amepata ushindi juu ya BWANA. Hivyo Samsoni alililetea aibu kubwa jina la Mungu.

 

Alipopofushwa hatimaye aliweza kuona waziwazi akilini mwake ,ajabu iliyoje ya   kiwango cha kutisha cha uovu alioufanya! Alimlilia Mungu, kama Israeli walivyokuwa wakifanya nyakati za shida, na Mungu alisikia sala yake na kumwokoa (Tazama waamuzi 4,1,3,23:6:1,6-8,1,5). Ndipo BWANA alipoonyesha Nguvu zake kuu katika kumpatia Samsoni nguvu za kuua wafilisti wengi kiasi kile na kuangamiza hekalu la mungu wao.

 

Katika Waebrania 11:32 Samsoni anahesabiwa kati ya wenye imani yenye thamani sana. Alijifunza kushinda udhaifu wake na kumwamini Mungu mwishoni. Yapasa tujifunze kwa kupitia  maisha ya Samsoni, kwamba ni lazima tuzitii sheria za  sheria za Mungu  na ni lazima tujitenge na ulimwengu ikiwa tunataka kumpendeza Yeye.

 

MASWALI

 

Majibu Mafupi

1.Nani alikuwa baba yake Samsoni?

2.Mungu alikuwa na kazi maalumu  ya kufanywa na  Samsoni angalipokua.Je ilikuwa kazi gani hiyo?

3. Mnadhiri ni nani?

4.Kwa nini Samsoni alikuwa na nguvu hivyo?

5. Samsoni alifanya nini usiku mmoja alipofungiwa ndani ya mji wa Gaza?

6. Delila alikuwa nani?

7. Delila alitaka Samsoni amwambie nini?

8. Delila alifanya nini alipogundua siri ya Samsoni?

9. Wafilisti  walimtenda nini  Samsoni baada ya nywele zake  kunyolewa?

 

Majibu ya Kina.

1.Samsoni alichaguliwa kuishi   katika njia maalumu kwa ajili ya  Mungu.

      a)Unaweza kueleza jinsi Samsoni alivyokuwa tofauti na watu wengine?

b)Ni kazi gani  Samsoni aliyofanya  kwa ajili ya Mungu?

2. Eleza habari ya Samsoni na Delila.

 

Majibu ya Ziada.

3.Eleza yaliyomtokea Samsoni alipovunja kiapo chake kwa kuruhusu nywele zake kunyolewa na Delila.

4. Eleza jinsi Samsoni ilvyofanana na taifa la Waisraeli.

 

Swahili Title
041 SAMSONI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type