44. MFALME KWA ISRAELI
"Mwoneni Mfalme ambaye mmemchagua"
Shabaha
Kuonyesha jinsi Waisraeli walivyotaka mfalme ili kuwa sawa na watu wa mataifa waliowazunguka badala ya kuwa na Mungu tu wa kuwatawala.
Muhtasari
Wakati Samweli alipokuwa mwamuzi, watu wa Israeli walistarehe katika sehemu walizorithi. Alitembea mwaka kwa mwaka nchi yote, akiwafundisha njia za Mungu na kuwahamasisha kumwabudu Mungu kwa mioyo yao yote. Sasa samweli alikuwa amezeeka na watoto wake hawakufaa kuchukuwa mahali pake. Watu walitaka mabadiliko, nao wakaja kwa Samweli na ombi lao . 1same. 8,9 na 10.
MUNGU ACHUKIZWA NA ISRAELI: SAMWELI 8.
Samweli aliwaamua Waisraeli kwa miaka mingi na wakati huo wote Wafilisti walikuwa wanashindwa kwa kuwa ‘‘mkono wa Mungu uliwainukia Wafilisti siku zote za Samweli’’ (1 Sam. 7:13) Wazee wa Israeli walikuja kwa Samweli huko Rama, alikoishi na kusema , ‘‘Tazama wewe umezeeka, nao wanao hawaendi katika njia zako. Sasa tufanyie mfalme wa kuamua juu yetu kama ilivyo kwa desturi ya mataifa yote’’, (mistari wa 5) walitaka mtawala mpya, sio tu kwa sababu wana wa Samweli walikuwa waovu lakini kwa kuwa waliyaona mataifa yaliyowazunguka yakiongozwa na Wafalme kwenda vitani , katikati ya sherehe na safari zenye utukufu. Walitaka kuwa kama watu wengine walisahau kwamba Mungu aliwataka wawe tofauti kwani walikuwa watu wake.
Samweli alisikitika sana. Alikuwa na uhakika halikuwa wazo jema. Hivyo alimgeukia Mungu kwa sala. Mungu alisema,’’Isikilize sauti ya watu hawa katika yote wayasemayo kwako, kwani hawa kukukataa wewe, lakini wamenikataa Mimi kwamba nisiwe Mfalme juu yao ’’. (matari wa 7) Mungu alikuwa mfalme wao akiwaongoza katika ushindi vitani na kuwalinda lakini walitaka mfalme watakayemwona ambaye watamhusudu na kuogopwa na adui zao. Mungu alimwambia Samweli, kuwaonya watu hao yatakayotokea ikiwa watapata mfalme, mfalme atachukua wana wao kuwa askari wake na watumishi wake na binti zao atawatwaa kuwa wapishi wake na waokaji mikate.Watampatia mfalme fungu la kumi(ushuru) kwa mazao na mifugo naye atatwaa mashamba yenu yenye rutuba na ardhi yenu nzuri na mizabibu.Mizabibu yenu atawapatia watumishi wake.Lakini watu walikuwa wameshaamua.Walimsikiliza Samweli kwa upole na wakasema,’’Sivyo hivyoLa,lakini tutakuwa na mfalme juu yetu ;ili kwamba sisi pia tuwe kama mataifa mengine ;na ili mfalme wetu aamue juu yetu na ,naye atoke mbele yetu na kupigana vita vyetu’’(mistari ya 19-20).
Sauli alikuwa ni aina ya mtu ambaye watu wa Israeli walimtaka kuwa mfalme, kwani alikuwa mrefu na mwenye umbo zuri kuliko wote na alikuwa wa kabila la Benjamini na jina la baba yake aliitwa kishi. Jina “Sauli”linamaanisha “kilichoombwa”, naye alikuwa hasa kile watu walichokiomba.
Kwa mara ya kwanza tunamfahamu, Sauli alipokuwa akitafuta punda za baba yake waliokuwa wamepotea.Na hakuweza hakuweza kuwapata wanyama hao, aliamua kwenda Rama kuomba apate msaada kwa nabii Samweli. Mungu alikuwa amemwambia Samweli, kwamba Sauli alikuwa anakuja na Samweli anapaswa amfanyie jambo gani.
Asubuhi iliyofuata Sauli alipowasili,Samweli alizungumza naye na kisha akachukua chupa (kiriba) cha mafuta na kumwagia Sauli kichwani Sauli. Huku kuliitwa “Kupakwa mafuta”na hili lilimaanisha kwamba Sauli alikuwa ametengwa na Mungu kuwa mfalme wa Israeli. Ndipo Samweli alipombusu Sauli na kusema,“Je,BWANA hakukutia mafuta kwamba uwe mkuu juu ya urithi wake; watu wake Israeli?”
Watumishi wote maalumu wa Mungu walitiwa mafuta. Kuhani mkuu na makuhani, na wafalme wa Israeli walitengwa kutoka kwa watu kuonyesha walikuwa na majukumu maalumu kufanya. Kijana Sauli alirejea nyumbani kwa baba yake akishangazwa na maneno ya Samweli na kwa yale ambayo yangemtokea siku za mbele.
SAULI ATAMKWA KUWA MFALME MBELE YA WATU WAKE: 1Samweli 10:17-25
Mkutano Mkuu uliitwa huko Mizipa. Samweli aliwakumbusha tena watu juu ya upumbavu wao katika kumkataa Mungu, ambaye alikuwa amewaokoa katika matatizo yao. Hata hivyo, aliyaita makabila yote kusogea, akaliteua kabila la Benjamini na kumtafuta Sauli mwana wa Kishi, lakini hakuonekana. Huyo mwenye aibu mwana asiyejulikana wa mkulima alilemewa na utukufu wa uteuzi wake kuwa mfalme wa Israeli, naye alikuwa amejificha. Hatimaye, alipatikana na kutambulishwa kwa watu “Mwoneni yeye ambaye BWANA amemchagua”, Samweli alisema (mstari wa 24) Mungu alielewa ni mtu wa aina gani waliyemhitaji na watu walifurahi wote wakapiga kelele wakisema “Mfalme na aishi”.
FUNDISHO KWETU:
Waisraeli, waliona ugumu kuamini juu ya Mungu aliye hai; kwa sababu walikuwa hawamuoni. Tunapaswa kuwa na imani kuu zaidi kuliko ile. Yatupasa kuwa na imani sawa na Samweli ambaye daima alimwomba Mungu msaada na kuwa amwongoze. Alimjua kuwa ndiye Mungu wa kweli na aishiye ingawaje hakuweza kumwona. Ni lazima na sisi tuwe hivyo. Ni lazima tumwamini na kujifuza kuchagua njia za Mungu ambaye hatuwezi kumwona kuliko njia za wale tuwaonao wanaotuzunguka. Tukiweka imani yetu kwake na kuingojea kwa subira huruma yake atatuongoza salama ,na kwa hakika Mungu anafahamu tunachohitaji kuliko vyote. Anafahamu kilicho chema kwetu .Hata majaribu ya namna gani yajayo yakitupata mwishowe tutafikishwa kwenye ufalme mtukufu wa Mungu hapa duniani. Mungu ana tutaka tumwamini na tumtegemee.Inamaanisha sisi tujitenga kutokana na watu wanao tuzunguka kwani njia zao sio njia zake Mungu.Tunahitaji kutembea katika njia za Mungu, hivyo inatubidi kufuata yote yaliyo mema na kweli,kwa kadri tunavyojifuza kutikaBiblia.Dunia haitatuelewa lakini Mungu wa mbinguni atatuona na kupendezwa nasi.
MAELEZO YA NYONGEZA:
Mafuta yaliyotumiwa kwa kumpaka mtu yalikuwa mafuta maalumu kabisa “mafuta matakatifu ya upako”.Matayalisho yake yanapatikana katika Kutoka 30:22-33.Lakini wana Israeli walikatazwa kuyatengeneza au kuyatumia- Yalikuwa kutumika tu kwa
kuwapaka makuhani (“Haruni na na wanawe”Kutoka 30:30); na wafalme ( “makuhani walichukuwa pembe yenye mafuta kutoka kutaaaaHekaluni (madhabauni),na kumpaka Sulemani (I Wafalme 1:39) na manabii (“Elisha..utampaka mafuta awe nabii”Wafalme 19:16)
Yalikuwa mafuta matakatifu, yaliyowaweka wakfu kwa kazi maalum ya Mungu (tulijifunza mwaka jana kuwa mtakatifu au takatifu maana yake “kilichotengwa” kwa ajili ya Mungu, kwa mfano Biblia Takatifu - kitabu Mungu alichokitenga kutoka Vitabu vingine vyote kwa sababu ni maneno yake na mawazo yake).
Mafuta haya matakatifu,yaliyotengenezwa kwa maagizo ya Mungu,yalielekeza kwa Roho mtakatifu ambaye Yesu alipakwa katika ubatizo wake.“Roho Mtakatifu alishuka kutoka mbinguni katika umbo la hua juu yake, na sauti ilitoka mbinguni ikisema wewe ndiwe mwanangu, mpendwa wangu ;ninayependezwa naye”(Luka3:22).Neno “kristo” maana yake “mpakwa mafuta” katika ubatizo wake akawa Yesu Kristo. Yesu aliyepakwa mafuta na Mungu ili awe ndiye wakuwaokoa watu wote waaminio na kuitii Injili. Tutaona somo la upako wa mafuta katika somo linalofuata wakati Daudi alipochaguliwa na Mungu kuwa Mfalme mpakwa mafuta wa Mungu badala ya Sauli.
MASWALI
Majibu Mafupi.
1)Kwanini watu walitaka Mfalme awatawale?
2)Kwanini watu hawakutaka wana wa Samweli kuwa waamuzi juu yao?
3)Ninani Mungu alisema watu walimkataa walipoomba wawe na Mfalme?
4)Je Mungu aliwaruhusu watu kuwa na Mfalme?
5)Saul alikuwa akifanya nini Samweli alipompata?
6)Ninani ambaye Samweli alimpaka mafuta kuwa Mfalme?
7) Nini ni “kupakwa mafuta?”
8)Jina “Sauli maana yake?”
9)Kwanini watu walifikiri Sauli angekuwa mfalme mzuri?
10)Watu walisemaje wakati Samweli alipowaambia Sauli atakuwa mfalme?
11) Tunajifunza somo gani kutokana na habari hii ya waisrael kumwomba Samweli awapatie Mfalme?
Majibu ya Kina.
1) A)Malizia fungu lifuatalo:
a)Kamilisha sentensi ifuatayo-“Hawakukukataa wewe, bali…”
b)Ni nani alimwambia maneno haya Samweli?
c)Ni jambo gani lililosababisha Samweli kuhuzunika?
2)Watu wa Israeli waliomba wawe na Mfalme:
a)Alikuwa nani?
b)Alionekanaje?
c)Eleza jinsi Samweli alivyomtambulishal kwa watu.
Majibu ya Nyongeza
3)Samweli aliwaonya watu juu ya mambo ambayo yangetokea watakapokuwa na mfalme.
Ni mambo gani hayo?
4)Sauli alipakwa mafuta na Samweli
a)Kupakwa mafuta maana yake ninini?
b)Ni akina nani katika Israeli walipakwa mafuta?
c)Ni jinsi gani Yesu Kristo alivyopakwa mafuta?