CSSA 1-2-20 - GOD REJECTS SAUL

Swahili

45. MUNGU AMKATAA SAULI:

“Kutii ni bora zaidi kuliko sadaka"

Shabaha

Kuonyesha kwamba Mungu anataka  wakati wote utii kwa amri zake.

Muhtasari

Sauli alikuwa mkulima mwenye aibu na asiyejulikana ambaye ghafla alijikuta amechaguliwa kuwa Mfalme wa kwanza kutawala watu katika Israeli (Samweli 13:8-14 na 15).

 

MFALME SAULI  ANACHUKUA WAJIBU WAKE

Haukuwa muda mrefu kwa  Sauli, kutambua kwamba  ilimpasa kuwaongoza watu wake vitani, dhidi ya adui zao na kuacha  kazi  ya baba yake ya shamba. Akiwa mkuu wa Jeshi la Israeli, Sauli alianza vyema kwa kuwaongoza watu katika ushindi. Haikuchukua muda mrefu, hata hivyo ilikuwa ilikuwa dhahiri kabisa kwamba Sauli hakuwa mtu  wa imani kama  wakuu waliotangulia kabla yake (mfano:Yoshua,Gideoni, nakadhalika). Hakuonyesha kuelewa, kwamba jeshi lake lilikuwa Jeshi la Mungu na kuwa Mungu angeleta  ushindi, iwapo tu wangemtii na kumtegemea. Wakati mmoja Samweli alimwambia Sauli kumgojea Gilgali siku saba hadi atakapofika. Ndipo Samweli angetoa dhabihu kwa Mungu kwa ajiri ya watu kabla ya kuanza vita.

 Lakini kadri Wafilisti walivyozidi kuwakaribia,Sauli alipata hofu na kutokuwa na subira kwa sababu Samweli alikuwa bado hajafika. Akatoa dhabibu  mwenyewe  na mara Samweli akatokea. Samweli alikasirika sana alipoona kwamba Sauli hakumtii."Umefanya upumbavu”.Samweli akasema “sasa ufalme wako hautadumu" (1Sam.13:13-14). Mungu angeudumisha ufalme katika nyumba ya Sauli lakini atajitafutia "mtu aupendezaye moyo wake... ili awe mkuu juu ya watu wake"(mstari wa 14). Na baadaye  hilo ndilo lililotokea .

 

 Hata hivyo Sauli aliendelea kushinda mapigano dhidi ya adui za Israeli  naye akaunda Jeshi kubwa na baraza la mfalme la kutawala sawasawa na yale ya wafalme wa mataifa yalivyofanya.

 

AMALEKI   NI   LAZIMA WAANGAMIZWE:I Sam.15:19.

Samweli aliendelea  kujaribu kumfundisha Sauli somo rahisi la kusikiliza kwa uangalifu na utii.”Bwana alinituma kukupaka mafuta uwe Mfalme juu ya watu wake, juu ya Israeli,sasa kwahiyo sikiliza sauti ya maneno ya Bwana”(mstari 1).

Karibu miaka mia nne kabla,Amaleki waliwahi kuwatendea ukatili na kuwatia woga  kwa kuwashambulia Waisraeli walipokuwa wakitaabika kuvuka jangwa  lielekealo Sinai(tazama kutoka 17:8). Mungu, hakuwahi kusahau hilo-“ninakumbuka yale Amaleki waliyowatenda  Israeli” yalikuwa maneno ya Mungu kwa Sauli “sasa nenda ukawapige Amaleki na kuwaangamiza kabisa na vyote walivyonavyo,usikiache hata kidogo"(mstari 2,3).

 

Hapa palikuwa na nafasi kwa Sauli kujionyesha kama mmoja  ambaye angeweza kutii amri ya Mungu, na kujidhibitishia kuwa mwaminifu. Lakini kama tutakavyoona, hakufanya yote ambayo Mungu alimwagiza. Sauli alianza mara moja kuwakusanya watu kwenda vitani.

 

Shambulio lilifanikiwa na  Sauli naye aliua watu kwa makali ya upanga(mstari 8) lakini- Agagi, mfalme wa Amaleki, alichukuliwa akiwa hai na kondoo wazuri,ng`ombe na wanakondoo walichukuliwa na kuwekwa na kutunzwa(mstari wa 9). Hakufaulu jaribio (Mtihani). Hakuwaangamiza kabisa Amaleki.

 

SAULI  AKOSA KUMTII MUNGU :1 Samweli 15:13-23.

Samweli alipofika kwenye eneo la tukio na kuwaona wanyama ambao hawakuwa wameangamizwa, na akamtaka Sauli aeleze hilo lilimaanisha nini.Sauli alishangaa sana.Alidhani kuwa alikuwa ametenda kadri  Mungu alivyotaka. Hakika wanyama walikuwepo lakini Sauli aliwalaumu watu kwa ajiri ya hilo,watu waliacha kondoo wazuri na ng’ombe kwa ajiri ya dhabihu kwa Mungu.(mstari wa 15) hili halikuwa udhuru. Sauli hakufanya yote ambayo Mungu aliyahitaji, naye Samweli akamwambia :“Je! BWANA huzipenda sadaka  za kuteketezwa na dhabihu sawa sawa  na kuitii sauti ya BWANA? Angalia kutii ni bora kuliko dhabihu,na kusikia   kuliko mafuta ya beberu”(mstari wa 22). Mungu hataki dhabibu kwa wale wanaomwasi katika roho zao na wale wasio tii amri zake. Anataka utii wa  kweli na moyo wa uaminifu.

 

MUNGU AMKATAA SAULI: 1sam:15:35

Kutokea wakati huo  na kuendelea , Mungu hakuwa na Sauli naye Samweli hawakuwa na lolote la kufanya naye. Samweli alisikitika sana,  lakini Sauli alikuwa ametenda  lililokuwa sahihi machoni pake , Sauli hakumtii Mungu.

 

FUNDISHO   KWETU.

Mungu atoapo amri anatazamia itekelezwe kikamilifu. Kila wakati Mungu humaanisha kabisa analolisema, “angamiza kabisa usiache chochote” alimaanisha hivyo hakika.Na mara nyingi sisi huwa sawa kabisa na Sauli. Haitoshi kutii sheria kadhaa za Mungu na kufikiria nyingine siyo  muhimu. Sisi, kama Sauli nilazima tujifunze kwamba utii kamili ndiyo Mungu anaouhitaji,pamoja na uaminifu na  tabia ya  unyenyekevu.

 Ni muhimu sana kukumbuka maneno haya :“Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika BWANA”(Wakolosi 3:20). Tukijifunza kuwa watiifu kwa wazazi wetu basi, tutakapokuwa na kuwa wanaume na wanawake, tutaweza kutoa utiifu kwababa yetu wa mbinguni.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Samweli alimwambia Sauli kwamba Mungu alikuwa amemkataa kuwa mfalme(mstariwa 26). Polepole Sauli alianza kuona makosa aliyokuwa amefanya.Alitubu dhambi yake nakumbembeleza Samweli kumwabudu Mungu pamoja naye.

  Alipokuwa anafanya hilo, Sauli aliishika kanzu ya Samweli nayo ikararuka mikononi mwake. Samweli akasema kwake:“Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli,naye amempa jirani yako,aliye mwema kuliko wewe”(mstari 28). Sasa Sauli alitambua waziwazi matokeo ya kutokutii kwake, lakini badala ya kutubu na kubadili njia zake, alijionyesha kuwa mwenye wivu na muasi kwa Mungu. Alijisikitikia lakini siyo kwa toba ya kweli, au angebadili njia zake.

 Sauli alibakia kuwa mfalme kwa muda kadhaa, lakini Mungu hakuwa naye tena, Na Samweli alipelekwa Bethlehemu kumpaka mafuta Daudi,mtoto wa mwisho kuzaliwa kati ya wana wa Yese, ili  baadaye awe Mfalme wa Israeli  badala ya Sauli.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1.   Ni kwa muda gani Samweli alimwmbia Sauli kumngojea kabla hajaenda vitani?

2.   Samweli ilikuwa afanye nini akifika kwa watu hapo Gilgali?

3.   Kwanini Sauli alitoa dhabihu badala yake?

4.   Ni amri gani Mungu alimpa Sauli kuhusu Amaleki?

5.   Je jeshi la Sauli liliwashinda Amaleki?

6.   Je Sauli aliwaangamiza kabisa Amaleki kama Mungu alivyoagiza?

7.   Jina la mfalme  wa Amaleki lilikuwa lipi?

8.   Sauli aliwalaumu akinanani kwa kutunza wanyama waliotekwa kutoka kwa Amaleki?

9.   Samweli alimwambia Sauli  ni kipi “kilicho bora kuliko dhabihu?”

10.  Adhabu kwa Sauli  kutokana na kutotii kwake ilikuwa ni ?

 

Majibu ya Kina.

  1. Mungu alipomwamrisha mfalme Sauli kupigana dhidi ya Amaleki alimwagiza awaangamize kabisa.
    1. Nikwanini Mungu alimwambia Sauli  awaangamize kabisa Amaleki?
    2. b)Ni kwa njia gani Sauli hakutii amri hii?

2.Sauli alisema kwamba watu walitaka  wanyama wa Amaleki wawatoe  dhabihu.

             a)Kwanini Mungu hakulifurahia hilo?

             b)Ni fundisho gani tunajifunza kutokana na tukio hili?

Majibu ya Nyongeza

3.Sauli alipotoa sababu ya  kuwaacha wanyama wa Amaleki,Samweli alisemaje? 1Samweli:15:22

4 a)Nini kilitokea wakati Sauli alipojaribu kumsimamisha Samweli asimwache?

b)Eleza Samweli alisema nini?

c)Je maneno ya Samweli yalimfanya Sauli atubu?

 

Swahili Title
045 MUNGU AMKATAA SAULI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type