CSSA 1-3-02 - THE WISDOM OF SOLOMON

Swahili

52. HEKIMA YA SULEMANI

“Israeli wote walimwogopa mfalme, kwani waliona kwamba hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake”

 

Shabaha

 Kuonyesha namna Sulemani alivyoanza kuwa mfalme wakati Daudi akiwa hai bado na kuanza kutawala kwa busara. Daudi sasa alikuwa mtu mzee sana. Ugumu wa maisha yake akiwa askari, aliyepigana vita vya BWANA, vilikuwa vimemdhoofisha. Ulikuwa ni wakati kwa mtu mwingine kuchukuwa mahali pake na kutawala watu wa Mungu. Daudi alielewa ni yupi angekuwa mfalme baada yake lakini ilikuwa lazima taifa litangaziwe.

 

SULEMANI ANAKUWA MFALME: 1 Wafalme 1:5 -10, 32 – 40

Daudi alikuwa mfalme kwa miaka arobaini, akatawala Yuda kutokea Hebroni kwa miaka saba na nusu na kisha katika Yerusalemu alitawala miaka thelathini na tatu juu ya Israeli wote (2 Samweli 5: 4 – 5). Alikuwa mfalme mkuu sana, lakini utawala wake haukuwa wenye amani. Tunapotazama mambo aliyoyafanya Daudi tunaweza kuona jinsi alivyokuwa akiandaa kwa ajili ya mwanawe Sulemani utawala, ambaye jila lake lina maana ya “Mtu wa amani” kwani Mungu alikuwa amemchagua kumrithi Daudi. Mungu akasema “Tazama” “utazaliwa mwana, atakayekuwa mtu wa kustarehe, nami nitamstarehesha mbele ya adui ya adui zake pande zote; kwani jina lake litakuwa Sulemani, nami nitawapa Israeli amani na utulivu katika siku zake” (1 Mambo ya Nyakati 2:9)

 

Wakati huo huo, baadhi ya wana wa Daudi walikuwa na shauku ya kuiba ufalme kwa ajili yao wenyewe, Wa kwanza alikuwa Absalomu ambaye alijaribu kumpindua baba yake, na Daudi ilimbidi kukimbia kutoka ikulu yake na kuvuka mto Yordani wengi kati ya marafiki zake waaminifu wakafuatana naye na Absalomu hatimaye aliuawa na Yoabu, mkuu wa jeshi la Daudi, mtu shujaa askari mwaminifu sana. Ndipo Daudi alipokuuwa mzee na dhaifu, Adoniya alikusanya baadhi ya wafuasi wake, akiwemo Yoabu na Abiathari, kuhani akaandaa sherehe ambako angeenda kutangaza kuwa ndiye aliyekuwa mfalme mpya.

     

Walakini, nabii mwaminifu Nathani pamoja na Bath-sheba mamaye Sulemani na Sadoki aliyekuwa Kuhani wakashauriana na Daudi.

 

Walielewa kwamba Daudi alikuwa ameahidi kuwa Sulemani angekuwa mfalme, kwa kuwa Mungu alikuwa amemchagua. Daudi alisema, “Tena katika wana wangu wote”, (kwani BWANA amenipa wana wengi), amechangua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli” (1 Mambo ya Nyakati 28:5). Ndipo Daudi akatoa maagizo ili Sulemani apakwe mafuta kuwa mfalme. “Twaeni pamoja nanyi watumishi wa bwana wenu, mkampandishe Sulemani mwanangu juu ya nyumbu mimi, mkamteleshe mpaka Giboni; kisha Sadoki, kuhani, na Nathani nabii, na wamtie mafuta huko awe mfalme juu ya Israeli” (1 Wafalme 1:33-34).

 

Hivyo wakapiga panda kwa ajili ya Yerusalemu yote ili wasikie na wakamleta Sulemani wakamketisha juu ya kiti cha enzi cha Daudi. Sadoki, kuhani, akampaka mafuta kutoka katika hema “nao wakapiga panda na watu wote wakasema, Mungu amlinde mfalme Sulemani” (1 Wafalme 1:39)

 

SELEMANI ANAANZA KUTAWALA: 1 Wafalme 3: 3- 15

Tangu utotoni Sulemani alikuwa amejifunza kumpenda Mungu. Wote wawili Daudi baba yake na Bath-sheba mama yake walikuwa wamemfundisha kumcha Mungu na kushika amri zake, hivyo mara alipofanyika mfalme kwa mara ya kwanza tunasoma kwamba Sulemani alimpenda BWANA akatembea katika maagizo ya Daudi baba yake (mist.3). Mojawapo ya vitu vya kwanza alivyofanya Sulemani alipokuwa mfalme, ni kwamba aliwakusanya wakuu wa majeshi na wakuu wote katika Israeli huko Gibea ambako madhababu ilikuwa imewekwa.Naye mbele ya watu wote akatoa juu ya meza ya shaba dhabihu ya kuteketezwa wanyama elfu kwa kuwa aliazimia kumtumikia Mungu vyema.

 

Usiku ule, Mungu alimtokea katika ndoto na akamwambia, “Omba utakalo nikupatie” (mist 5). Sulemani akatambua jinsi Mungu alivyombariki mno babaye Daudi,na sasa alikuwa amembariki na yeye pia, kumfanya yeye kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi. Hata hivyo alipofikiria iwapo angeweza kuwatawala kwa hekima.

 

Alikiri mbele za Mungu kuwa “nami ni mtoto mdogo tu. Sijui jinsi inipasavyo kutoka au kuingia” (mist.7). Alihitaji msaada wa Mungu ili kumwongoza Sulemani katika kutawala Israeli vyema. “Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabya, kwani; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?” (mstari9) Kutokana jibu hilo Mungu alikuwa amependezwa naye.Mungu akasema, “Tazama nimekupatia moyo wa hekima na wa akili” (mstari 12) Mungu alikuwa anajua kwamba ni jambo la kawaida kabisa kwa mfalme kuomba ili awe na maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako;wala hukutaka roho za adui zako. (mist.11). Lakini Sulemani hakuomba chochote katika yote haya.

 

Hivyo Mungu alipendezwa kumpatia hekima kama alivyokuwa ameomba, ikiwa ni pamoja na kumpatia mambo yale ambayo hakuwa ameyahitaji. “Na mambo yale ambayo usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari; hata hapatakuwa na mtu kafika wafalme kama wewe, siku zako zote. Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika maagizo yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi” (mistari 13, 14)

 

SULEMANI ANAONYESHA HEKIMA YAKE: 1 Wafalme 3: 16 – 28

Si muda mrefu baadaye wakati Sulemani aliporejea Yerusalemu wanawake wawili wakaja mbele yake na tatizo lililoonekana kuwa gumu sana kulitatua, hawa wanawake wawili walikuwa wakiishi katika nyumba moja na wote wakawa wamezaa watoto wa kiume usiku mmoja kati ya watoto hao alikufa. Kila mmoja wa hao wanawake sasa akadai kuwa mtoto aliye hai ndiye aliyekuwa mtoto wake. Wakabishana mbele za mfalme mwanamke mmoja akasema mtoto wa yule mwanzake alikuwa amekufa usiku na kumchukua mtoto aliye hai kutoka kwa mamaye halali wakati alipokuwa amelala usingizi na kumuweka mtoto mfu badala yake.

 

Yule mwanamke akasema, “Sivyo hivyo mtoto wako ndiye liyekufa,na mtoto wangu ndiye aliye hai” (mstari 22)

 

Ni kwa vipi mfalme angefahamu ni yupi aliyekuwa mama halisi wa mtoto aliye hai? Kwa kutafakar akasema “Nileteeni upanga” (mstari 24) Ndipo wakamletea upanga. Mfalme Sulemani akasema “mkate vipande viwili kampe huyu nusu na huyu nusu” (mstari 25). Ghafla mama halisi akalia, “Ee Bwana wangu mpe huyo mtoto aliye hai, na wala usimwue kabisa” (mistari 26). Sasa ilikuwa rahisi sasa kuona ni yupi alikuwa akisema ukweli.

 

Hakuna mama wa kweli ambaye angependa kumwumiza mtoto wake mchanga, na ndivyo Sulemani kwa hekima alivyofahamu. “Mfalme akasema”, “Mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue: maana yeye ndiye mama yake” (mstari 27) Tunaweza kuwa na uhakika kwamba kwa kweli Sulemani hakunuia kumwua mtoto yule mchanga, lakini kwa vile alikuwa na hekima, alifahamu jinsi ya kumjua mama wa kweli wa mtoto. “Na Israeli wakapata hukumu ile aliyoihukumu mfalme; wakamwogopa mfalme maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake ili afanye hukumu” (mstari 28)

 

FUNDISHO KWETU

Sulemani alikuwa amevutiwa mno na wa kuhitaji kupata hekima na hata kitabu cha Mithali, kimejaa ushauri kuwahimiza watu kuitafuta hekima kama vile kutafuata hazina iliyofichwa (2:4).

 

Haikushangaza basi kwamba Sulemani alimwomba Mungu apatiwe hekima ya kutawala watu wake, kwa kuwa alijua kwamba “Maana hekima ni bora kuliko marijani, Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo” (Mithali 8:11). Ni katika Biblia pekee, Hekima ya kweli yaweza kupatikana.

 

Hutufundisha namna ya kusema na namna ya kutenda na namna ya kufanya maamuzi sahihi katika maisha yetu. Tunaweza kujifunza hekima hiyo kama Sulemani alivyofanya, kwa kuwasikiliza kwa uangalifu mama na baba zetu jinsi wanavyotufundisha yale Mungu anayotaka sisi tuyafanye. “Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe” Daudi alimwambia mwanaye, kwa sababu hiyo siyo hekima ya kweli, ni kiburi tu na ujanja wa mwanadamu.

 

 Hekima ya kweli na ufahamu ni mambo ambayo tunapaswa kuyatafuta kila siku kwa kummuomba Mungu na kulisoma neno lake lake katika Biblia. Habari tunazosoma kuhusu waaminifu wanaume na wanwake wa zamani zinatusaidia sisi pia kutembea kwa hekima mbele ya Mungu wetu.

 

MAELEZO YA ZIADA

Ndani ya masomo haya habari kuhusu historia ya siku za utukufu ya Israeli inafunuliwa siyo tu ni historia yenye kuchangamsha, lakini huchukua akili zetu mbele hadi wakati ambao “mwana mkuu wa Daudi”, Bwana Yesu Kristo (Mathayo1.1),ambapo atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika Ezekieli 37:24 anaitwa na Mungu “Mtumishi wangu, Daudi” kwani Daudi inamaanisha “anayependwa” na tunafahamu kwamna Mungu alimtamka Yesu kuwa “Mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye” (Mathayo 3:17)

 

Wakati Kristo atakaporudi atakaa katika kiti cha enzi cha Daudi (Luke 1:32) na kutokea Yerusalemu atatawala dunia yote kwani inabidi awaangamize adui zake wote kabla ya kuweza kutawala ufalme wake kwa amani.

 

Akizungumzia wakati huu, Daudi aliandika katika Zaburi “BWANA, alimwambia Bwana wangu (yaani Kristo), ukae mkono wangu wa kulia hadi niwafanyapo adui zako kiti cha kuwekea miguu yako” (Zaburi 110:1) Hivyo Mungu atamtuma Bwana Yesu Kristo kurudi kutoka mbinguni kuwashinda adui zake wote na ndipo ulimwengu wote utakapopata amani na utulivu.

 

Mambo haya yameelezwa katika Isaya 9: 6 – 7, ambapo anaitwa “Mfalme wa amani”, vile vile kama Sulemani alivyomwomba Mungu kuwa na Hekima,viyo hivyo Mungu amempa Mwanawe “Roho ya hekima na ufahamu” (Isaya 11:2 – 5) kwani atakuwa Mfalme mwenye haki, akiwatunza maskini na wahitaji (Zaburi 72:12)

 

Sasa tunaanza kuona mwanzo jinsi utawala wa Daudi na Sulemani unavyotuelekeza mbele kwenye utawala wa Kristo. Njia nyingine ya kuyasema haya ni kwamba maishani mwake Daudi alikuwa namna ya Kristo na hata Sulemani pia alikuwa ni mfano wa Kristo.

 

Twaweza kuanza kuorodhesha mifano hii.

 

DAUDI

KRISTO

Jina lake linamaanisha “anayependwa”

Mungu alimwita “mwanagu mpendwa ninayependezwa naye (Mathayo 3:17)

Mungu alimsaidia kuwaangusha adui zake wote(2 Samweli 7:9)

Atawashinda adui zake wote (Zaburi 110:1, Wakorintho15:24 – 2b)

Alikaa Yerusalemu juu ya Israeli wote (1 Samweli 5: 4 – 5)

Atakaa juu ya kiti cha enzi cha baba yake Daudi (Luka 1:32) na kutawala kutokea Yerusalemu akitawala dunia mzima (Yeremia 3:17)

SULEMANI

KRISTO

Mwana wa Daudi (2 Samweli 12:24)

Mwana wa Daudi (Mathayo 1:1)

Jina lake linamaanisha mwenye amani” (1 Mambo ya Nyakati 2:29)

Atakuwa ndiye mfalme wa amani (ISaya 9:6)

Alimwomba Mungu ampe hekima

Mungu alimpatia Roho ya hekima

(1 Mambo ya Nyakati 1:10, 1 Wafalme 3:9) ufahamu (Isaya 11:2-5)

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Daudi alitawala miaka mingapi?
  2. Ni yupi katika ya wana wa Daudi alichaguliwa na Mungu kuwa mfalme?
  3. Jina la Sulemani lina maana gani?
  4. Ni nani alikuwa mama yake Sulemani?
  5. Ni nani aliyempaka mafuta Sulemani?
  6. Kulikuwa na nini pale Gibea?
  7. Sulemani alitenda nini huko Gibea?
  8. Mungu alipomtokea Sulemani ndotoni, Sulemani aliomba nini?
  9. Ni jambo gani lingine Mungu alilomwahidi Sulemani?
  10. Sulemani alikuwa amejifunza nini kuhusu hekima?
  11. Ni sehemu gani ya pekee tunaweza kupata hekima ya kweli?

 

Majibu ya Kina

  1. Eleza jinsi Sulemani alivyofanywa mfalme kama Daudi alivyokuwa ameagiza.
  2. Eleza kilichotokea,Mungu alipomtokea Sulemani katika ndoto kule Gibea
  3. Eleza namna Sulemani alivyo hukumu kwa hekima kati ya wanawake wawili waliokuja mbele yake

 

MAJIBU YA NYONGEZA

  1. Orodhesha kuonyesha njia tatu ambavyo Daudi alikuwa ni namna ya Kristo na njia tatu ambayo Sulemani alikuwa mfano wa Kristo.

 

Swahili Title
052 HEKIMA YA SULEMANI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type