CSSA 1-3-08 - ELIJAH AND THE STILL SMALL VOICE

Swahili

58. ELIYA NA SAUTI NDOGO YA UTULIVU

“Sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?”

 

Shabaha

Kuonyesha namna Eliya alivyojifunza kutokana na sauti ndogo ya utulivu kwamba Mungu bado alikuwa na kazi ya kufanya katika Israeli. Huko katika mlima wa Karmeli, Mungu alikuwa amewaonyesha Waisraeli kwa njia ya ajabu kwamba yeye ndiye alikuwa Mungu wa kweli na ya kwamba hakuna Mungu mwingine. Kwa hakika sasa wangemtumikia Mungu na kuzishika amri zake.

 

Walakini mara Ahabu alipomwambia Yezebeli yote yaliyotokea katika mlima Karmeli alikasirika sana,moyo wake ulijaa chuki, na kufikiria kwamba Eliya amediriki kuwauwa manabii wa Baali akapeleka ujumbe wa kutisha kwa Eliya kusema “kesho panapo wakati huu nisipokufanya roho yako, kama roho ya mmojawapo wa hao ” (mstari 2)

 

1Wafalme 19

 

ELIYA AKIWA AMEKATA TAMAA: 1WAFALME 19:1-4

Eliya alikuwa nabii mkubwa, mwaminifu, aliyejaa ujasiri Lakini aliposikia ule ujumbe wa kutisha wa maneno ya Yezebeli, ilikuwa ni zaidi kuliko alivyoweza kuvumilia. Akawa na hali ya kushuka moyo sana, kwa kuwa ilionekana kuwa wengi sana walikuwa kinyume naye.

 

Na na jinsi gani angepata uwezo kugeuza mioyo ya watu waachane na sanamu (vinyago) ili kumtumikia Mungu aliye hai, ambaye alimpenda? Ilikuwa imeonekana kuwa ulipatikana ushindi mkuu pale Mlima wa Karmeli, lakini bado yule Yezebeli mwovu alikuwa akitawala huko samalia. Akajihisi mpweke na mwenye kukata tamaa ya kuishi akakimbilia kusini hadi Beer-sheba akiwa pamoja na mtumishi wake. Kutoka hapo akasafiri peke yake mwendo wa siku moja jangwani na afika akaketi chini ya kimvuli cha mretemu akiwa amechoka sana na mwenye wasiwasi akatamani kama angekufa. Akasema “Yatosha” Eliya akamwomba Mungu, “sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu” (mstari 4). Kisha akajiosha akalala chini na akasinzia.

 

MUNGU ANAMPATIA NGUVU ELIYA: 1 Wafalme 19:5-8

Akiwa usingizini malaika akamgusa na akamwambia “inuka na ule” (mstari 5) akaamka na akaangalia na kwa mshangao akaona chakula kimeandaliwa mbele yake mkate mzuri ambao ungali wa moto umeokwa na ulikuwa juu ya mkaa na gudulia la maji. Ndipo akala na kunywa na akalala chini ili asinzie tena. Malaika aliyemgusa na akamwamshwa tena akamwambia, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako (mstari 7). Na Eliya akainuka, akala na kunywa, kwa chakula hicho alichopata kwa malaika, kikampa nguvu za kwendelea na safari yake.

 

Akaenda kwa nguvu za chakula hicho mwendo wa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, 'mlima wa Mungu' (mstari 8).

 

Ni hapa Horebu, miaka mingi iliyokuwa imepita ndipo Musa lipoona kichaka kikiungua. Ni hapo Mungu alipojitambulisha jina lake la ajabu kwa Musa (Kutoka 3).

 

Ni hapa katika Horebu, wana wa Isreli walipokusanyika kuzipokea amri, 'na pale palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima' (Kutoka 19:16). Tena ni hapo Horebu ambapo Mungu alimwonyesha utukufu wake Musa (Kutoka 34). Na sasa miaka mingi baadaye, Eliya nabii akapanda mlima huu na akawa anaishi ndani ya pango la mlima huu.

 

ELIYA ANAISIKIA SAUTI NDOGO YA UTULIVU: 1 Wafalme 19:9-21

Ndipo neno la Mungu likamjia Eliya, naye akamwambia ''Unafanya nini hapa, Eliya?(mstari 9). Eliya akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu, nao wanitafuta roho yangu, waiondoe” ( mstari 10 ).

 

Mungu alielewa jinsi Eliya alivyokuwa anajisikia na hisia zake, na wakati alipojiona kuwa katika hali hiyo ya upweke na akiwa mwenye majonzi mengi hakuwa katika hali nzuri ya kuendelea na kazi ya Mungu na Israeli. Kwa hiyo Mungu akamwambia aende asimame juu ya mlima ili aweze kuuona utukufu wa Mungu na nguvu za Mungu zipite mbele yake.

 

Eliya, aliposimama juu ya mlima ndipo ukimya ukatoweka ndipo upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, na ukaivunja-vunja miamba na vipande vyake vikatupwa chini ya mlima-lakini BWANA hakuwamo ndani ya upepo ule ( mstari 11 ).

 

Baada ya upepo likafuata tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi. Na baada ya tetemeko la nchi, kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule.

 

Na baada ya moto sauti ndogo ya utulivu ( mstari 12 ). Ilikuwa ni sauti ya utulivu sana aliyoisikia kwa masikio yake alipokuwa amejifunika uso wake kwa mavazi yake akaenda na kusimama mlangoni mwa pango ambalo alikuwemo tangu kwa ajili ya utisho wa nguvu kuu za Mungu. Ndipo neno likasema, “Unafanya nini hapa, Eliya?Na Eliya alisema kama alivyokuwa amekwisha sema kabla: “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA, Mungu wa majeshi...nami nimesalia, mimi peke yangu, nao wanitafuta roho yangu, waiondoe”.

 

Eliya alikuwa ameweza kuwaonyesha Israeli nguvu kuu za Mungu kwa kuizuia mvua na kisha kushusha moto kutoka mbinguni pale katika Mlima Karmeli. Sasa Israeli walichokuwa wanahitaji ni “sauti ndogo ya utulivu”, ili kuwafundishanjia za Mungu. Kwa hiyo ni lazima Eliya arudi tena Israeli kwa maana hakuwa yeye peke yake anayemwabudu Mungu. “Bado nimejisazia watu elfu saba katika Israeli, kila lisilomwinamia Baali” ( mstari 18 ). Waaminifu hawa ambao ni wanaume na wanawake walihitaji faraja, maana wengi wao walikuwa wamejificha hasira ya Yezebeli, pia (1 Wafalme 18:4).

 

Kwa hiyo Mungu kurudia njia yake, awarudi Israeli.

 

FUNDISHO KWETU.

Mara nyingi tunajikuta tu pekee yetu kwa kuwa tumekuwa tukijitahidi kumpendeza Mungu kuliko kujipendeza sisi wenyewe. Bwana Yesu Kristo anatuambia sisi kuwa tufurahi mambo haya yanapotupata, “kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu” ( Mathayo 5:10-12 ). Mungu kila wakati yupo pamoja na sisi. Mungu hatatuacha kabisa (Waebrania 13:5). Wapo ndugu zetu wanaume na wanawake na watoto wao, kwa maana hiyo hatupo peke yetu kamwe. Eliya menyewe alikuja kujua kuwa walikuwepo zaidi ya elfu moja katika Israeli ambao walitiwa moyo na tabia yake ya kumwamini Mungu, hata yeye pia alihitaji uaminifu wao ili aweze kutiwa moyo pia.

 

Hii Sauti ndogo ya utulivu ya Mungu bado inasema na sisi kutoka ktika Biblia. Tunaigeukia sauti hii tunapoomba atulinde na kutupatia nguvu, maana tusikate tamaa wakati mambo yanapokuwa magumu, lakini tuendelee na kazi ya Mungu mpaka Kristo atakaporudi (Marko 13:13)

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Kulikuwa na mambo matatu muhimu ambayo Mungu alitaka Eliya ayafanye:

  • Kwanza, alitakiwa aende Dameski ampake mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu.
  • Pili, ni lazima Eliya arudi Israeli amtafute Yehu. Ampake mfuta Yehu kuwa mfalme wa Israeli, maana Mungu ataiangamiza nyumba ya Ahabu, na mke wake mwovu Yezebeli, na wana, kwa mkono wa Yehu.
  • Tatu, Eliya ni lazima ampake mafuta mtu ambaye atachukua mahali pake awe nabii katika Israeli. Mungu alimchagua kijana wa kuchukua nafasi baada ya Eliya alikuwa ni Elisha. Hizi zilikuwa ni kazi ambazo Eliya ilikuwa ni lazima azifanye kwa ajili ya Mungu kabla ya kazi ya Eliya kuisha.

 

Kwa kweli, Mungu alikuwa ameihifadhi kazi maalumu kwa ajili ya Eliya kuitenda baada ya Yesu kurudi. Atakuwa ni Eliya ambaye atawaendea Wayahudi ambao watakuwa katika utawanyiko katika dunia yote na atawaambi kuwa Kristo amerudi, na atawaaongoza kurudi katika nchi ya Israeli.

 

Ni jinsi gani nabii Eliya alivyokuwa wa mhimu/Eliya alizipenda sana njia za Mungu na alichukia kabisa uovu wa kila namna.Na Mungu pia ndivyo alivyo, na sisi pia lazima tuwe na tabia hiyo. Kama vile mwandishi wa Zaburi alivyosema; Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu,naam,dhahabu iliyo safi Maana nayaona mausia yako yote kuwa ya adili, Kila njia ya uongo naichukia (Zaburi 119:127-128).

 

Natuhakikishe tunakuwa na tabia hiyohiyokwa dunia hii na njia zake na uovu wake, na kuyapenda sana mambo yote ya Mungu.

 

MASWALI

Majibu Mafupi.

1. Yezebeli alikusudia kufanya nini baada ya kusikia yale yaliyotendeka juu ya Mlima Karmeli?

2. Eliya alipopokea ujumbe wa Yezebeli alifanya nini?

3. Eliya aliomba nini alipokuwa amekaa chini ya mti wa mretemu?

4. Ni nani aliyemwamsha Eliya?

5. Eliya alipoamka aliona nini?

6. Safari ya Eliya ilimchukua muda gani kufika hadi Mlima Horebu?

7. Mungu alimwonyesha nguvu zake za kutisha Eliya kwa njia tatu za kuogopesha. Ninjia gani hizo?

8. Eliya alisikia nini baada ya moto?

9. Mungu alimwambia nini Eliya pale kwenye Mlima Horebu?

10. Niwaaminifu wangapii waliokuwa wamebakia katika Israeli?

11. Baada ya Mungu kuongea na Eliya pale Mlima Horebu, Mungu alitaka  Eliya afanye nini?

 

Majibu ya Kina

12. (a) Eleza ni kwa nini Eliya alikimbia kutoka Israeli

      (b) Eleza jinsi malaika walivyomtia nguvu kwenda safari ndefu mpaka Horebu.

13. (a) Eleza Eliya aliona nini na alisikianini alipokuwa pale Horebu.

      (b) Mungu alikuwa anamfundisha somo gani Eliya?

 

Majibu ya Nyongeza

14. (a) Eliya aliambiwa aende wapak mafuta watu watatu...Ni watu gani Hao?

      (b) Ni kazi gani maalumu ambayo Eliya ataifanya baada ya Yesu kurudi?

 

Swahili Title
058 ELIYA NA SAUTI NDOGO YA UTULIVU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type